CHADEMA hawana mkakati, endeleeni na shughuli zenu

Kuna kundi la wafuasi wa CHADEMA ambao wamehadaika kuwa kuna mkakati wa ndani unafanywa na viongozi wa chama hicho baada ya kutoridhika na kushindwa uchaguzi.

Hata hivyo, ukifuatilia mijadala inayoendeshwa na viongozi wa CHADEMA, utagundua kuwa hivi sasa wanajihusisha zaidi na masuala ya bunge. Aliyekuwa mgombea wa urais naye "ameingia mitini".

Wote tunajua kuwa aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, hapendi kuchelewesha mambo. Ndio maana alitaka matokeo uchaguzi toka sehemu mbalimbali nchini yatangazwe bila kucheleweshwa. Kitendo cha yeye kuchelewa kutoa vidhibiti au kauli yoyote ni ishara tosha kuwa aidha vidhibiti hivyo havipo au "amekubali yaishe".

Ushauri ninaowapa wafuasi wa CHADEMA wanaongoja mkakati wowote kuhusiana na uchaguzi mkuu uliopita ni kwamba, endeleeni na shughuli zenu za kila siku. Hakuna mkakati wowote ndani ya chama. Viongozi wanajadili kugombea uongozi wa upinzani bungeni n.k.

Kwa viongozi wa CHADEMA. Wapeni mwongozo wafuasi wenu. Maamuzi yoyote mnayoyafikia ni vyema mkayatoa kwao hata kama mnahisi ni maamuzi dhaifu. huo ndio uongozi. Mkishindwa kabisa waambieni, wategemee nini na lini.

Wangu kwenu ni ushauri tu!

lazima serikali ikae vizuri baada ya kuunda cabinet, sasa hivi hata wakitangaza matokeo haitakuwa na mantiki yoyote. subiri na kaa chonjo kwa maandamano ya kudai katiba mpya
 
ZeMarcopolo,

Asante kwa post yako. Hata hivyo:

1.
i) Mgombea Urais wa CHADEMA ndiye pia Katibu Mkuu wa CHADEMA. Katibu Mkuu wa Chama na kwa maana hii, ndiye mpishi Mkuu wa Mikakati ya Chama. Inashangaza kuona mtu asiyefahamu kinachoendelea Chama kutangaza hadharani kuwa hakuna mkakati unaoendelea na kuwa wanachadema wamahadaika. Ninatoa Mwito kwa Wanachadema halisi kukataa upotoshaji huu wa makusudi, kwa malengo ya kuindoa Chadema kwenye mikakati yake. Napenda kumjulisha mhusika na wote wenye fikra hizo kuwa wamepotea njia na wasubiri. Kama anayeandika ni mwanachadema, basi ni vizuri aandike jina lake la kweli ili tumjue na tujue anajua nini, au anapindisha nini na kwa lengo gani. Wanachama ninawaomba watulie tuli kwa kuwa Viongozi wao ni makini, na meli inayoongozwa na viongozi wao makini haitayumbishwa hata tone na force au mtu mwingine yeyote popote alipo na kwa nia yoyote aliyo nayo.
ii) Chadema inafanya kazi zake kwa mujibu wa Katiba yake, Kanuni yake na maadili yake. Haifanyi kazi kwa pressure za nje. Haifanyi kazi hata kwa pressure za wanachama wake kwa vile Wanachama ndani ya Chadema wana wajibu wao, majukumu yao na haki zao. Viongozi wana wajibu wao, majukumu yao na haki zao. Siyo kila mwanachama kwa kila kitu anaweza kufahamu kila hatua ya utekelezaji au ya mipango. Hata nyumbani mama anapopika jikoni siyo wote waliokaa sebuleni wanajua kinachoendelea jikoni. Subira pekee ndio itakayoeleza ni nini kilikuwa kinapikwa, labda wakisie tu kutokana na harafu harufu inayonukia.
iii) Kwa msingi huo ukifuatilia para ya kwanza kuwa kuna wafuasi wa chadema wamehadaika, mtoa ataarifa, japo haelezi yeye ni nani, source ya information yake ni nini jambo ambalo kwa dhahiri lingeliweza kuwatoa mashaka wanachadema anaowaita "wamehadaika". Ningemshauri kama ana nia njema ajitambulishe kwa hao anaowashauri yeye ni nani kama ni mwanachadema cheo chake ni nini na kama siyo mwanachadema amepata wapi taarifa yake kiasi cha kutaka kuwadanganya na kuwapotosha siyo tu wanachadema lakini Watanzania wengi walioipigia Kura. Hakuna maficho kuwa mamilioni ya Watanzania waliipigia kura Chadema na wao ndio hasa wenye kuongojea hatima ya kura zao kuliko wanachadema. Inalekea ZeMarcopolo siyo mdadisi, mtafiti wa kutosha kujua centre of conflict iko wapi. Napenda kumfahimisha kuwa Centre of Conflict haiko chadema bali kwa Watanzania maelfu kila kona ya nchi ambao kura zao zilichakachuliwa na wao ndio mashahidi wa awali wa uchakachuaji huo. Kama lengo la mwandishi ni kupotosha umma huo, basi amepotoka, na hilo halitatokea kwa kuwa kama mgombea Urais na Katibu Mkuu wa Chadema nina mawasiliano ya karibu sana na Watanzania hao wala siyo wana Chadema tu. Watanzania watapenda kujua kama ZeMarcopolo atakuwa jasiri na kujitambulisha kwa jina lake halisi na kwa cheo chake ili tuweze kuthamini ushauri wake. Atakuwa mtanzania wa karne ya 47 atakayesikiliza ushauri wa mtu asiye na ujasiri wa hata kuonyesha jina lake halisi. Ndio maana Dr. Slaa niko hapa kwa jina langu bila maficho, na wako humu jamvini wapambanaji ambao hawajifichi wako kwa majina yao, na wanaposimamia jambo kila mmoja anajua ujasiri wao.

2) ZeMarcopolo unasema kuwa 'shughuli za chadema zimeelekezwa kwenye shughuli za kibunge'. Chadema imepewa kura hata baada ya uchakachuaji zaidi ya 2 Millioni. Sasa ulitaka wafanye nini walale na kustarehe na hizo kura? Watanzania wengi wanaiona Chadema ndio matumaini yao pekee ya kuwakomboa kwenye makucha ya CCM na umaskini uliosababishwa na CCM. Hivyo ni dhahiri, pamoja na mikakakati yake mingine Chadema inashughulikia maswala ya kuimarisha Wabunge wake ( wabunge wanajua mipango na mikakati iliyoko kuwaimarisha), ipo kwenye mipango ya kuunda Baraza lake la Mawaziri kivuli (baada ya Serikali kuundwa-wengi hawaelewi tafsiri ya hili baada ya msimamo wa Chadema kukataa kutambua Matokeo ya Uchaguzi ningeliwashauri wawasiliane na Wanasheria wao ili kujua tafsiri halisi ya Hatua hiyo). Hiyo nayo ni shughuli za Bunge na Watanzania wengi wanahamu ya kujua Baraza Kivuli litakuwa na sura gani na itatendaji kazi zake kwa maslahi yao na Taifa kwa ujumla. Ni mtu asiyejua tu anaweza kutoa kauli kama ya ZeMarcopolo. Chadema haina kazi mmoja tu wala mkakati mmoja tu katika ukombozi wa Taifa hili. Aliyefunga akili yake kwa malengo anayofahamu tu ndiyo anaweza kutoa kauli na ushauri wa aina hiyo.

3) ZeMarcopolo ni vema akajua kuwa Chadema inaendeshwa kwa katiba, Kanuni, Maadili na Itafaki inayojulikana. Chadema siyo Brief case political party kama anavyofikiri. Kama ni mtafiti angelijua hilo au kama hana nia na lengo lilifichika pia angelikuwa na njia nyingi za kujua hilo. Hivyo, ni vyema akajua kuwa Chadema katika utekelezaji wa majukumu yake haisukumwi na mtu yeyote wala wanachama wa kawaida ( wanachama wanaelimishwa na wakielimishwa wanaridhika kama tulivyofanya kwa wale waliotaka kujua nini kinaendelea). Wanachama ndani ya Chadema wana haki zao, majukumu na wajibu wao, na viongozi nao wana majukumu, haki na wajibu wao. Hivyo katika utekelezaji wa majukumu hatusukumwi na pressure ya mtu awaye yeyote, wa ndani au wa nje kwa vile tunasukumwa tu na Katiba, Kanuni, Maadili na Itifaki ya chama. Mchakato unaoendelea utakapopitia kwenye vyombo vyote vya maamuzi utatolewa hadharani na si kabla ya hapo. Pamoja na hilo, ni vyema ZeMarcopolo akaelewa kuwa walaio chakachuliwa kura ni watanzania na wao wanamawasiliano kwa njia mbalimbali na Chama na wanaridhika na hatua tunazochukua. Kama yuko ambaye haridhiki ana lake jambo, na kwa vyovyote vile si rahisi kumridhisha kila mtu mmoja mmoja japo tunajitahidi. Ndio maana naandika kwa kina ili ZeMarcopolo aelewe kuwa kazi na hasa maswala magumu kama haya hayafanywi kwa emotions, wala kukurupuka. Yeye mwenyewe anajua uwezo wa Dr. Slaa kufanya utafiti, na kuwa hatoi kauli mpaka utafiti umefika mahali pake. Ningependa pia ZeMarcopolo aelewe kuwa vidhibiti ni watanzania wenyewe waliochakachuliwa kura zao, na Dr.Slaa ni conduit tu ya kukataa matokeo hayo. Kama haamini haya atashangaa wakati mwafaka utakapofika.

4) ZeMarcopolo anatoa ushauri kwa wafuasi wa CHADEMA kuwa waendelee na kazi zao. Hapa kuna jambo. Sijui ZeMarcopolo lini amekuwa msemaji wa Chadema kiasi cha kuwataka Wanachadema "waendelee na kazi zao" Nadhani mwenye macho haambiwi kutazama na nipende tu kumwambia ZeMarcopolo kuwa Watanzania wa 2010 siyo mwaka 47 wanaweza kuchambua pumba na mchele. Nadhani wanafahamu kabisa malengo ya ushauri huu, na ni kwa manufaa ya nani. Tumekusoma ZeMarcopolo. Hata Kauli kuwa "viongozi wanagombea uongozi wa Kambi ya Upinzani ni wa upotoshaji". Ah, nani anagombea. Kambi imeisha kuundwa, tayari kuna Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani, kuna Mnadhimu Mkuu wa Kambi (Chief Whip) na kuna Deputy Leader. Sasa nafasi zipi zinagombaniwa na viongozi. Kwa kauli hii tu unaweza pia kumsoma lengo lake ni nini ZeMarcopolo.

5) ZeMarcopolo anatoa ushauri kuwa tuwape Mwongozo wafuasi wetu. Nataka kumjulisha kuwa Tumeisha kutoa mwongozo siyo tu kwa Wafuasi wa Chadema bali kwa Watanzania walioibiwa na kuchakuliwa kura zao. Kimsingi licha ya miongozo mingine ya ndani, kuwa " Tumekataa kutambua matokeo na kumtambua Rais aliyepatikana kwa matokeo haya ( issue hapa ni UHALALI WA RAIS NA SI UWEPO wa kisheria wa Rais mtu asipoelewa au kutaka kutambua tofauti kati ya maneno haya mafupi ya kisheria atateseka daima). Huu ni mwongozo kwa Watanzania wategemee nini. Matokeo ya jambo la kutegemewa limekwisha kuonekana kwa matendo "Kususia shughuli anazofanya Rais" kuna mwongozo gani zaidi ya huu. Wabunge wametoka nje ya Bunge na Chadema imepongezwa na wote wenye nia njema na Taifa hili, na kitendo cha kutoka nje ya Bunge Duniani kote ni kitendo cha kawaida kwenye Mabunge. Kuna mwongozo gani zaidi ya huu. Au ZeMarcopolo anataka tumwage hadharani na mengine ambayo yako Jikoni? Naomba avute subira atayaona, kama siyo kwa matendo basi kwa kauli.

Chadema inapenda na inakaribisha Ushauri. Lakini Upotoshaji wa aina yeyote ile utajibiwa papo hapo ili Malengo yetu yasivurugwe na wasioitakia mema, na pia kulinda Watanzania tuliowaahidi kuwa tutawatumikia bila maslahi yeyote binafsi.

Kuna kundi la wafuasi wa CHADEMA ambao wamehadaika kuwa kuna mkakati wa ndani unafanywa na viongozi wa chama hicho baada ya kutoridhika na kushindwa uchaguzi.

Hata hivyo, ukifuatilia mijadala inayoendeshwa na viongozi wa CHADEMA, utagundua kuwa hivi sasa wanajihusisha zaidi na masuala ya bunge. Aliyekuwa mgombea wa urais naye "ameingia mitini".

Wote tunajua kuwa aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, hapendi kuchelewesha mambo. Ndio maana alitaka matokeo uchaguzi toka sehemu mbalimbali nchini yatangazwe bila kucheleweshwa. Kitendo cha yeye kuchelewa kutoa vidhibiti au kauli yoyote ni ishara tosha kuwa aidha vidhibiti hivyo havipo au "amekubali yaishe".

Ushauri ninaowapa wafuasi wa CHADEMA wanaongoja mkakati wowote kuhusiana na uchaguzi mkuu uliopita ni kwamba, endeleeni na shughuli zenu za kila siku. Hakuna mkakati wowote ndani ya chama. Viongozi wanajadili kugombea uongozi wa upinzani bungeni n.k.

Kwa viongozi wa CHADEMA. Wapeni mwongozo wafuasi wenu. Maamuzi yoyote mnayoyafikia ni vyema mkayatoa kwao hata kama mnahisi ni maamuzi dhaifu. huo ndio uongozi. Mkishindwa kabisa waambieni, wategemee nini na lini.

Wangu kwenu ni ushauri tu!
 
Mpevu,
Asante kwa swali lako kuhusu "Inclusivity". Mimi nadhani mtu yeyote mwenye Busara atapenda kwanza kusolve puzzle ifuatayo kabla hajashauri kuundwa kwa Kambi ya Upinzani inayoshirikisha vyama vyote:
i) Kwa mazingira ya 2010 ambapo CUF ipo tayari Serikalini na Katibu wake Mkuu ndiye Makamu wa Kwanza wa Rais ( pamoja na kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano haitambui cheo hiki na kimsingi Katiba imevunjwa). CUF ipo kwenye Serikali ya Chama cha Mapinduzi na Chama hicho ndicho kinachounda Serikali Bara. Hivyo Serikali zote mbili ni za Chama kimoja. Ni kuna uwezekano gani wa CUF hiyo hiyo iliyoko Serikalini kuwa kwenye Kambi ya Upinzani kwa Upande wa Bara? Tungependa kabla kutushauri kuunda Kambi ya Pamoja mtushauri hii Puzzle, hii Chemistry na utendaji wake utakuwaje? Je Watanzania( Bara) wanahitaji kuwe na Chama kimmoja Bungeni yaani CCM/CUF +Chadema =Hakuna Upinzani au inashauri nini. Chemistry hii ikijibiwa tunaweza kujadiliana kwenda mbele. Kwa Taarifa yenyewe ninazo zaidi ya SMS 2000 baada ya Mdahalo wa Jana kutoka kwa Watanzania, tena wakiwemo wa Zanzibar ( ambao wanaona kwa kitendo cha CUF kuingia Serikalini Zanzibar imekuwa nchi ya Chama kimoja (Bungeni japo De facto one party state haijatangazwa kama ilivyokuwa mwaka 1962. We may be on the way in Zanzibar atleast kama hatutakuwa makini.
ii) Mpevu umetumia mfano wa 2005. Nadhani Hamad hakuwa mkweli kilichotokea 2005. a) CUF waliunda Kambi ya Upinzani peke yao bila kushirikisha Vyama Vingine. Kama unavyofahamu CUF wote walikuwa wanatoka Pemba, ambayo kimsingi population yake haifiki nusu ya population ya Jimbo la Uchaguzi ya Ubungo. Hivyo, Wabunge wa Upinzani kutoka Bara tulikataa kuwa Upinzani (ambao pia wanawawakilisha Bungeni mamilioni ya Watanzania waliokerwa na CCM) hauwezi kuwakilishwa na Wabunge wanaotoka kwenye "Kitongoji". Kauli hiyo ilileta ugomvi sana wakati huo, lakini ndio ukweli kwani Mawaziri Vivuli wote walitoka Pemba. b) Zanzibar kama nchi inayo Bunge lake kamili (Baraza la Wawakilishi) inayo Baraza lake la Mawaziri, inayo Mahakama zake ( isipokuwa mahakama ya Rufaa). Ndani ya Baraza la Wawakilishi CUF nao walikuwa wanawakilishwana hivyo maslahi ya Zanzibar yalikuwa yamelindwa. Hivyo, ilikuwa si halali kwa Tanzania Bara yote kuwakilishwa na tulichokiita wakati huo Wabunge kutoka kitongoji kimoja. Watanzania nao wanahitaji kuwakilishwa ndani ya Bunge na Watu watakaokuwa wanawasemea tofauti na Wabunge wa Chama Tawala ambao kimsingi walikuwa wakiunga Serikali yao kwa kila kitu hata kama haikuwa na maslahi kwa wananchi. c) Kilio hicho kikasikilizwa na mamlaka ya Bunge, na Tukaambiwa tutengeneze Fomula itakayokubalika. Hivyo Fomula tuliyotengeneza ili tusiwatenge wenzetu ilikuwa Chama kinachounda Kambi ya Upinzani kiwe kimefikisha asilimia 12.5 ya Wabunge wote. Baada ya Fomula hiyo kukubalika na Bunge ndio tukaanza mjadala na Hamad Rashid ambaye wakati huo alikuwa tayari kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani. Tukakubaliana na Fomula hiyo ili Chama chochote kisipate nafasi ya kuchezea Kanuni na kuunda Kambi ya Upinzani bila kuzingatia maslahi ya Wananchi. Kambi ya Upinzani haipo kwa ajili ya Maslahi ya Wapinzani bali ya Wananchi, na hivyo lazima kujenga kinga ndani ya Kanuni ili watu wasije wakaunda tu Kambi kwa kuwa wana wabunge wengi kuliko wenzao kama ilivyotokea. d) Kwa kuwa CUF walikuwa "hawajafikia" asilima 12.5 Kanuni inasema, iwapo Vyama kwa pamoja vimefikia asilimia 10 ya Wabunge wote, (Kanuni ya 14(1) basi " Kambi ya Upinzani itaundwa na Wabunge wote wa Kambi ya Upinzani. Hivyo si kweli kuwa CUF walikubali kutushirikisha kwa hiari yao. Historical Facts must be respected. Hii ni historia na Historia haifutiki. e) Baada ya Kukubaliana kuunda Kambi ya Upinzani itakayoshirikisha Vyama Vyote, na kwa kuwa CUF ilikuwa na Wabunge wengi, Kiongozi wa Upinzani akatoka CUF na Hamad Rashid akaendelea kuwa Kiongozi wa Upinzani kwa kauli ya Wabunge wote. Kwa vile Chadema ilikuwa ya pili kuwa na Wabunge wengi kufuatia CUF (Wabunge 11 na UDP alikuwa 1) hivyo Dr. Slaa ambaye wakati huo alikuwa Mwenyekiti wa Wabunge wa Chadema (ieleweke Wabunge wa Chadema na siyo Kambi) akateuliwa kwa kauli mmoja kuwa Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani. Kuhusu kutoa Nafasi, naomba ieleweke kuwa mimi sikupewa nafasi na CUF kwa upendeleo. Nimekuwa Mbunge wa Bunge la SADC toka mwaka 1997 (nilishiriki kuaianzisha kwa kuandika Katiba) hivyo kauli ya Hamad siyo ya kweli. Kutokana nafasi yangu ndani ya SADC ambapo kwa muda mrefu nimekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Interparliamentary Cooperation and Cooperation Committee) Bunge la Tanzania limekuwa likinichagua kaiwakilisha siyo kwa upendeleo wa CUF. Hapa kilichokuwa kinaangaliwa ni maslahi ya Nchi na nani anaweza kuiwakilisha vizuri zaidi nchi si upendeleo kama ilivyotaka kueleweka). Vivyo hivyo kwa nafasi ya LAAC ambayo nilikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu. Lakini Hamad naye angelieleza nafasi za juu alizokuwa nazo yeye na kwanini hakuteua wabunge wengine wa CUF kwenye nafasi hiyo ilihali yeye ndiye Kiongozi wa Kambi ya Upinzani. Nadhani hoja ililenga ku polarize na kwa bahati mbaya Mhe. Mbowe hakuwa anajua intrigues za 2005 kwa kuwa hakuweko Bungeni wakati huo na asingeliweza kujibu kitu ambacho hakifahamu. Hivyo si kweli kuwa Kambi ya 2005 iliundwa kwa msingi tu wa kuunda mshikamano bali mazingira ya 2005 yalihitaji hivyo. Mazingira ya 2010 yanahitaji kwanza Chemistry iliyoko ijibiwe kabla hatua yeyote ya kuzungumzia mshikamano kuzungumziwa na kutotambua mazingira tofuati ni kutokuwa wa kweli kuwa Hali ya Siasa ni tofauti sana. Wananchi unaowasema, ndio ambao kama nilivyokuambia wanataka tusiungane na CUF sasa kama kuna msingi mwingie wa Kisayansi mtujulishe ili tuyajadili kwa kina maoni yaliyoko kwa maslahi ya Taifa na si kwa maslahi ya ushabiki.
Ninapenda kuuliza pia Chemistry ya pili, Hivi i) Lyatonga alipompigia Kampeni JK na leo anaingia kwenye Kambi ya Upinzani Chemistry hiyo itafananaje? Ndio maana iwapo ataingia kwenye Kambi ni lazima kwanza Kanuni zinazoongoza Kambi ya Upinzani zitazamwe upya na wote waiweke saini upya. Lakini haiji tu kwa kuwa mtu ameingia Bungeni kwa Msingi wa Upinzani na hivyo lazima aingie kwenye Kambi kwa kuwa tu kuna watu wanataka kuona Umoja. Hoja ni Umoja uko kwa kuwa watu wanataka kuona umoja au Umoja uko kwa kuwa kuna malengo tunataka kuyafikia. Je kwa Chemistry iliyoko malengo hayo yanaweza kufikika. Kama hatutapima kwa malengo basi kuna tatizo kubwa kwa kuwa tutakuwa hatukuwa tuna elewa Lengo na Madhumuni ya Kambi ya Upinzani kuwepo Bungeni na malengo yake ya Msingi ni yapi.
Mpevu, nadhani hoja yeyote inayoanzia kuwa " kuna kutoelewana kati ya viongozi ni potofu" na haitatufikisha katika kujenga Kambi imara ya Upinzani. Kitakachotufikisha kwenye Kambi imara ya Upinzani ni Chemistry ipi ya Kambi ya Upinzani itatufikisha kwenye Malengo ya uwepo wa Kambi ya Upinzani. Ninaogopa sana mtu anapotumia kauli " sisi wananchi" hawa wananchi unaowasema wanataka ni kina nani na wako wapi na maoni yao wametoa kwa njia gani na ni asilimia ngapi ya Watanzania. Haya mambo ni ya msingi sana na amini hayatapuuziwa katika mjadala kama huu.

Nakuunga hapo mkuu, you are truly and very firm on issues.
Naomba niende nje kidogo ya mada, kwako dr. SLAA: Nawaombeni mtazame kwa mapana juu ya kushirikisha hivi vyama vilivyopo bungeni muwe kitu kimoja kwa manufaa ya watanzania NO MATTER IN WHICH POLITICAL PARTY RECOGNISES JK. Nikirejea maelezo ya HR jana, alisema katika zile idara za uongozi (kambi ya upinzani bunge lililopita) yeye akiwa ndio leader...alitoa nafasi muhimu zote kwa other opponents ukiwamo wewe, Zitto na wengine ambapo chama kilichokuwa kikiongoza hakikuchukua nafasi yoyote katika kuweka na kuleta uwiamo/ushirikiano wa kambi ya upinzani bungeni. Naimani huu ni mfano mzuri wa wa mshikamamo, JE HAMUONI HII NI POLITICAL ISOLATION na inawagusa moja kwa moja wananchi kwa kutoona ushirikiano wenu bungeni?
Nawaombeni mtujenge ki-umoja, ninyi tunawaangalieni kwa macho yote, shirikianeni na hata kama kuna kutoelewana basi yawe ni internal issues na zisivuje bali jamii ielewe kuwa mna umoja jamani...mtatusumbua kuamua sisi wananchi in future.
 
ZeMarcopolo,
Unajua sipendi uwongo. Toa quotation ambako Dr. Slaa amesema atatoa Majina ya Usalama wa Taifa. Jamani kama hamjui uchambuzi ni vema mkaacha. Jibu langu kwa Naibu Mkurugenzi ilikuwa Waende Mahakamani majina yatatolewa mahakamani. Nikawashangaa wapi mmesikia Ushahidi unapelekwa usalama wa Taifa? Tatizo watu hawajui taratibu, hawafanyi utafiti, hawazingatii kauli ya watu. Haya ndio matokeo yake. ZeMarcopolo ninakuheshimu sana, lakini ningeweze kusema u mwongo kwa hili la usalama wa Taifa. Pili inaelekea hujui kinachozungumziwa. mara ngapi nimesema "at this stage issue siyo kushinda au kushindwa" issue ni Ushahidi wa Uchakachuaji" kama unakiri Geita ilichakachuliwa sasa unakataa nini. Kama imefanyika Geita na kwingineko unakataa nini kama Tunasema imechakachuliwa? Ni lazima tukupe ushahidi, na tukupe kama nani? Follow procedures and all will be well na nchi itakombolewa ikiwa ni pamoja na ZeMarcopolo.
 
Jenifa,
Tatizo ni kutokujua tofauti kati ya kuwa aliyetangazwa kisheria yupo na kwa kutomtambua hutabadilisha hali hiyo na hivyo mtu huyo yupo kwenye nafasi hiyo, na mtu huyo kuwa kwenye nafasi hiyo Visivyo halali. Ndio maana nikakushauri uwaone Wanasheria wako watakusaidia kuliko kung'ang'ania jambo usilolielewa. Hakuna Tofauti kati ya Kauli ya Mbowe na ya Slaa, na slaa anatumia "Rais" kuonyesha kuwa hayuko kihalali. Full stopo. Usipotambua na kuelewa vionjo hivi mtaendelea kuhangaika sana na kutukana sana. Wengine tumeumbwa schock Absobers. Tukana itamezwa tu.
 
Dar-Es-Salaam.
Ni mwenyewe kwani unamwogopa kwenye box la ushahidi. Dont Worry Dr. Slaa, hana ugomvi na mtu hata ukimbambikizia kwa sababu amefundishwa kuyameza yote. Kwanini mtu mwingine atumie ID yangu. Leo nimeamua kukaa hapa, ili twende sambamba na upotoshaji unaotaka kufanyika. Ndio maana sikuficha ID yangu toka mwanzo.

Huyu ndie Dr.W.Slaa mwenyewe au kuna mtu anatumia ID yake?
 
Mpevu,
Asante kwa swali lako kuhusu "Inclusivity". Mimi nadhani mtu yeyote mwenye Busara atapenda kwanza kusolve puzzle ifuatayo kabla hajashauri kuundwa kwa Kambi ya Upinzani inayoshirikisha vyama vyote:
i) Kwa mazingira ya 2010 ambapo CUF ipo tayari Serikalini na Katibu wake Mkuu ndiye Makamu wa Kwanza wa Rais ( pamoja na kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano haitambui cheo hiki na kimsingi Katiba imevunjwa). CUF ipo kwenye Serikali ya Chama cha Mapinduzi na Chama hicho ndicho kinachounda Serikali Bara. Hivyo Serikali zote mbili ni za Chama kimoja. Ni kuna uwezekano gani wa CUF hiyo hiyo iliyoko Serikalini kuwa kwenye Kambi ya Upinzani kwa Upande wa Bara? Tungependa kabla kutushauri kuunda Kambi ya Pamoja mtushauri hii Puzzle, hii Chemistry na utendaji wake utakuwaje? Je Watanzania( Bara) wanahitaji kuwe na Chama kimmoja Bungeni yaani CCM/CUF +Chadema =Hakuna Upinzani au inashauri nini. Chemistry hii ikijibiwa tunaweza kujadiliana kwenda mbele. Kwa Taarifa yenyewe ninazo zaidi ya SMS 2000 baada ya Mdahalo wa Jana kutoka kwa Watanzania, tena wakiwemo wa Zanzibar ( ambao wanaona kwa kitendo cha CUF kuingia Serikalini Zanzibar imekuwa nchi ya Chama kimoja (Bungeni japo De facto one party state haijatangazwa kama ilivyokuwa mwaka 1962. We may be on the way in Zanzibar atleast kama hatutakuwa makini.
ii) Mpevu umetumia mfano wa 2005. Nadhani Hamad hakuwa mkweli kilichotokea 2005. a) CUF waliunda Kambi ya Upinzani peke yao bila kushirikisha Vyama Vingine. Kama unavyofahamu CUF wote walikuwa wanatoka Pemba, ambayo kimsingi population yake haifiki nusu ya population ya Jimbo la Uchaguzi ya Ubungo. Hivyo, Wabunge wa Upinzani kutoka Bara tulikataa kuwa Upinzani (ambao pia wanawawakilisha Bungeni mamilioni ya Watanzania waliokerwa na CCM) hauwezi kuwakilishwa na Wabunge wanaotoka kwenye "Kitongoji". Kauli hiyo ilileta ugomvi sana wakati huo, lakini ndio ukweli kwani Mawaziri Vivuli wote walitoka Pemba. b) Zanzibar kama nchi inayo Bunge lake kamili (Baraza la Wawakilishi) inayo Baraza lake la Mawaziri, inayo Mahakama zake ( isipokuwa mahakama ya Rufaa). Ndani ya Baraza la Wawakilishi CUF nao walikuwa wanawakilishwana hivyo maslahi ya Zanzibar yalikuwa yamelindwa. Hivyo, ilikuwa si halali kwa Tanzania Bara yote kuwakilishwa na tulichokiita wakati huo Wabunge kutoka kitongoji kimoja. Watanzania nao wanahitaji kuwakilishwa ndani ya Bunge na Watu watakaokuwa wanawasemea tofauti na Wabunge wa Chama Tawala ambao kimsingi walikuwa wakiunga Serikali yao kwa kila kitu hata kama haikuwa na maslahi kwa wananchi. c) Kilio hicho kikasikilizwa na mamlaka ya Bunge, na Tukaambiwa tutengeneze Fomula itakayokubalika. Hivyo Fomula tuliyotengeneza ili tusiwatenge wenzetu ilikuwa Chama kinachounda Kambi ya Upinzani kiwe kimefikisha asilimia 12.5 ya Wabunge wote. Baada ya Fomula hiyo kukubalika na Bunge ndio tukaanza mjadala na Hamad Rashid ambaye wakati huo alikuwa tayari kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani. Tukakubaliana na Fomula hiyo ili Chama chochote kisipate nafasi ya kuchezea Kanuni na kuunda Kambi ya Upinzani bila kuzingatia maslahi ya Wananchi. Kambi ya Upinzani haipo kwa ajili ya Maslahi ya Wapinzani bali ya Wananchi, na hivyo lazima kujenga kinga ndani ya Kanuni ili watu wasije wakaunda tu Kambi kwa kuwa wana wabunge wengi kuliko wenzao kama ilivyotokea. d) Kwa kuwa CUF walikuwa "hawajafikia" asilima 12.5 Kanuni inasema, iwapo Vyama kwa pamoja vimefikia asilimia 10 ya Wabunge wote, (Kanuni ya 14(1) basi " Kambi ya Upinzani itaundwa na Wabunge wote wa Kambi ya Upinzani. Hivyo si kweli kuwa CUF walikubali kutushirikisha kwa hiari yao. Historical Facts must be respected. Hii ni historia na Historia haifutiki. e) Baada ya Kukubaliana kuunda Kambi ya Upinzani itakayoshirikisha Vyama Vyote, na kwa kuwa CUF ilikuwa na Wabunge wengi, Kiongozi wa Upinzani akatoka CUF na Hamad Rashid akaendelea kuwa Kiongozi wa Upinzani kwa kauli ya Wabunge wote. Kwa vile Chadema ilikuwa ya pili kuwa na Wabunge wengi kufuatia CUF (Wabunge 11 na UDP alikuwa 1) hivyo Dr. Slaa ambaye wakati huo alikuwa Mwenyekiti wa Wabunge wa Chadema (ieleweke Wabunge wa Chadema na siyo Kambi) akateuliwa kwa kauli mmoja kuwa Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani. Kuhusu kutoa Nafasi, naomba ieleweke kuwa mimi sikupewa nafasi na CUF kwa upendeleo. Nimekuwa Mbunge wa Bunge la SADC toka mwaka 1997 (nilishiriki kuaianzisha kwa kuandika Katiba) hivyo kauli ya Hamad siyo ya kweli. Kutokana nafasi yangu ndani ya SADC ambapo kwa muda mrefu nimekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Interparliamentary Cooperation and Cooperation Committee) Bunge la Tanzania limekuwa likinichagua kaiwakilisha siyo kwa upendeleo wa CUF. Hapa kilichokuwa kinaangaliwa ni maslahi ya Nchi na nani anaweza kuiwakilisha vizuri zaidi nchi si upendeleo kama ilivyotaka kueleweka). Vivyo hivyo kwa nafasi ya LAAC ambayo nilikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu. Lakini Hamad naye angelieleza nafasi za juu alizokuwa nazo yeye na kwanini hakuteua wabunge wengine wa CUF kwenye nafasi hiyo ilihali yeye ndiye Kiongozi wa Kambi ya Upinzani. Nadhani hoja ililenga ku polarize na kwa bahati mbaya Mhe. Mbowe hakuwa anajua intrigues za 2005 kwa kuwa hakuweko Bungeni wakati huo na asingeliweza kujibu kitu ambacho hakifahamu. Hivyo si kweli kuwa Kambi ya 2005 iliundwa kwa msingi tu wa kuunda mshikamano bali mazingira ya 2005 yalihitaji hivyo. Mazingira ya 2010 yanahitaji kwanza Chemistry iliyoko ijibiwe kabla hatua yeyote ya kuzungumzia mshikamano kuzungumziwa na kutotambua mazingira tofuati ni kutokuwa wa kweli kuwa Hali ya Siasa ni tofauti sana. Wananchi unaowasema, ndio ambao kama nilivyokuambia wanataka tusiungane na CUF sasa kama kuna msingi mwingie wa Kisayansi mtujulishe ili tuyajadili kwa kina maoni yaliyoko kwa maslahi ya Taifa na si kwa maslahi ya ushabiki.
Ninapenda kuuliza pia Chemistry ya pili, Hivi i) Lyatonga alipompigia Kampeni JK na leo anaingia kwenye Kambi ya Upinzani Chemistry hiyo itafananaje? Ndio maana iwapo ataingia kwenye Kambi ni lazima kwanza Kanuni zinazoongoza Kambi ya Upinzani zitazamwe upya na wote waiweke saini upya. Lakini haiji tu kwa kuwa mtu ameingia Bungeni kwa Msingi wa Upinzani na hivyo lazima aingie kwenye Kambi kwa kuwa tu kuna watu wanataka kuona Umoja. Hoja ni Umoja uko kwa kuwa watu wanataka kuona umoja au Umoja uko kwa kuwa kuna malengo tunataka kuyafikia. Je kwa Chemistry iliyoko malengo hayo yanaweza kufikika. Kama hatutapima kwa malengo basi kuna tatizo kubwa kwa kuwa tutakuwa hatukuwa tuna elewa Lengo na Madhumuni ya Kambi ya Upinzani kuwepo Bungeni na malengo yake ya Msingi ni yapi.
Mpevu, nadhani hoja yeyote inayoanzia kuwa " kuna kutoelewana kati ya viongozi ni potofu" na haitatufikisha katika kujenga Kambi imara ya Upinzani. Kitakachotufikisha kwenye Kambi imara ya Upinzani ni Chemistry ipi ya Kambi ya Upinzani itatufikisha kwenye Malengo ya uwepo wa Kambi ya Upinzani. Ninaogopa sana mtu anapotumia kauli " sisi wananchi" hawa wananchi unaowasema wanataka ni kina nani na wako wapi na maoni yao wametoa kwa njia gani na ni asilimia ngapi ya Watanzania. Haya mambo ni ya msingi sana na amini hayatapuuziwa katika mjadala kama huu.

You said it all mkuu, hasa katika hiyo para ya (ii) with is sub-paras. Mimi binafsi bado ninaamini kuwa huu muungano unasababisha conflicts za interest nyingi sana na wakati mwengine hata kuhinder process muhimu katika mabadiliko. Hakuhitaji akili ya ziada kujua kuwa CUF ni chama tawala sasa wanapoomba kuwa chama cha upinzani mimi naona wanataka kudilute efforts za CHADEMA amacho ni chama kikuu cha upinzani.

Hamad jana alionyesha ni jinsi gani walivyo na aim ya madaraka tu
 
Mi ntaendelea kulia tuu na huyu maalim Seif ambaye tulikua tunamheshimu sana kisiasa. Tangu 1995 amekua anashinda lakini ananyimwa ushindi. Namshangaa suluhisho lake kwa demokrasia ni kukubali kujiunga na CCM. Iyo hatua imerudisha nyuma demokrasia, na kwa mantiki haya CUF haitakaa ishinde Zanzibar tena. Mwaka 2015, huyu Seif atagombea kama kiongozi wa serikali, je ataathubutu kumsema vibaya bosi wake Shein? Na kama akimsifia Shein, wazanzibar watamchagua Shein. Je, huyu Seif atashiriki uchaguzi ili ashinde au ashindwe kuhalallisha nafasi yake ya makamu wa rais. Je, si itakua tuu uchaguzi wa kupanga matokeo kama timu ya mpira. Demokrasia Zanzibar imezikwa kwa tamaa za Seif kutaka madaraka. Wapo wapi hao wote waliopoteza maisha tangu 1995, wakitaka demokrasia ya kweli ya mshindi wa kweli apewe ushindi, je wote hao walijitoa mhanga ili Seif awe makamu wa rais? Chadema lazima ionyeshe kwa vitendo upinzani maana yake nini na si tamaa ya madaraka tuu
 
Tatizo la CUF linaeleweka sana, kama CUF inategemea kushinda Pemba tuu, je itatoaje upinzani wa kweli. Huu utaratibu wa kutaka chama chenye wabunge wengi kiunde upinzani unatumiwa vibaya na CUF. Kama CUF inashinda jimbo moja bara, na majimbo 24 Zanzibar, wakati kwa Zanzibar kura zake zote ni ndogo kuliko jimbo moja la bara, inabidi pawe na utaratibu mwingine. Pemba isije ikatawala bunge la muungano kwa kuwa inashinda, na mbunge anapata kura 4000 huku ameshinda, wakati bara mtu anapata kura 60000 na anakua ameshindwa. Katiba mpya iwe jibu la kweli la huu utata
 
Jenifa,
Tatizo ni kutokujua tofauti kati ya kuwa aliyetangazwa kisheria yupo na kwa kutomtambua hutabadilisha hali hiyo na hivyo mtu huyo yupo kwenye nafasi hiyo, na mtu huyo kuwa kwenye nafasi hiyo Visivyo halali. Ndio maana nikakushauri uwaone Wanasheria wako watakusaidia kuliko kung'ang'ania jambo usilolielewa. Hakuna Tofauti kati ya Kauli ya Mbowe na ya Slaa, na slaa anatumia "Rais" kuonyesha kuwa hayuko kihalali. Full stopo. Usipotambua na kuelewa vionjo hivi mtaendelea kuhangaika sana na kutukana sana. Wengine tumeumbwa schock Absobers. Tukana itamezwa tu.

Dr. Slaa,
Kubali tu kuwa mnachokiongea hakina mantiki. Hivi unadhani watanzania wangapi wana wanasheria wa kuwaelewesha hili? Jifunzeni kutumia lugha rahisi inayoeleweka na watu wa uwezo mbalimbali wa kuelewa.
Ukiona watu wanapata shida kuelewa maelezo mnayoyatoa, inapaswa ujiulize; labda hujayatoa kwa mtiririko unaweza kueleweka (if at all there is any substance).
 
ZeMarcopolo,
Unajua sipendi uwongo. Toa quotation ambako Dr. Slaa amesema atatoa Majina ya Usalama wa Taifa. Jamani kama hamjui uchambuzi ni vema mkaacha. Jibu langu kwa Naibu Mkurugenzi ilikuwa Waende Mahakamani majina yatatolewa mahakamani. Nikawashangaa wapi mmesikia Ushahidi unapelekwa usalama wa Taifa? Tatizo watu hawajui taratibu, hawafanyi utafiti, hawazingatii kauli ya watu. Haya ndio matokeo yake. ZeMarcopolo ninakuheshimu sana, lakini ningeweze kusema u mwongo kwa hili la usalama wa Taifa. Pili inaelekea hujui kinachozungumziwa. mara ngapi nimesema "at this stage issue siyo kushinda au kushindwa" issue ni Ushahidi wa Uchakachuaji" kama unakiri Geita ilichakachuliwa sasa unakataa nini. Kama imefanyika Geita na kwingineko unakataa nini kama Tunasema imechakachuliwa? Ni lazima tukupe ushahidi, na tukupe kama nani? Follow procedures and all will be well na nchi itakombolewa ikiwa ni pamoja na ZeMarcopolo.

Rafiki yangu Wilbroad,
Yaani wewe umeibiwa, halafu unaomba "aliyekuibia" aende akakushtaki mahakamani. Am sorry lakini huu ni utani.
Kubali tu kuwa huna ushahidi wowote unaobeba uzito wa ushahidi, ndio maana ulitumia barua feki ya La Cairo.
 
Kama hata Mtikila ameona uchaguzi umeibwa, sijui mnataka ushaidi gani zaidi? Wako wapi watu milioni 20 waliojiandikisha kupiga kura? Je, waliokosa kuona majina yao na kushindwa kupiga kura ukijumuuisha na waliouza shahada zao za kupiga kura.
 
hivi ni dr slaa kweli au matapeli wa kwenye jf?

na mbona makamba hatumwoni humu.... uwezo wake ni kama wako akili kama nyumba ya msonge... hufikia mwisho kwenye ncha ya fukuto...be constructive au nenda kwenye mtandao wa kina Majimarefu na Sh. yhy
 
Rafiki yangu Wilbroad,
Yaani wewe umeibiwa, halafu unaomba "aliyekuibia" aende akakushtaki mahakamani. Am sorry lakini huu ni utani.
Kubali tu kuwa huna ushahidi wowote unaobeba uzito wa ushahidi, ndio maana ulitumia barua feki ya La Cairo.

Dr Silaa, Kuna watu wanaohitaji kujibiwa na kuna wasiostahili kujibiwa kwa sababu ni wagumju kuelewa na wepesi kusahau. Huyu anaejiita ZeMarcopolo, na Malaria sugu wako katika kundi hili na huenda wametumwa na CCM kujaribu kupotosha mikakati ya Chaadema. Tupo wengi sana wenye mapenzi mema na Chadema ingawa sio wanachama na tunafurahishwa na kukubaliana na hatua zinazochukuliwa na Chama katika kuwakomboa watanzania kwa sababu ndio chama kilicho na uchungu wa kweli na maendeleo ya watanzania.

Kwa vile nchi hii ni kubwa, lazima kutakuwa na vichwa ngumu na mamluki wengi wanaotumiwa na CCM kujaribu ku distabilize Chadema kwa kauli zao na vitendo. Hata hivyo tuwasamehe tu kwa sababu siku moja wataumbuka siku kitakapoeleweka.

DR Silaa,tunakuunga Mkono, Tuko pamoja na wewe na tunakutakieni mafanikio katika kuendesha hili gurudumu la mabadiliko kwa mahufaa ya watanzania wote. Nakuomba uendelee na moyo huo huo kutuhabarisha wapenda mabadiliko wa kweli Tanzania.
 
Rafiki yangu Wilbroad,
Yaani wewe umeibiwa, halafu unaomba "aliyekuibia" aende akakushtaki mahakamani. Am sorry lakini huu ni utani.
Kubali tu kuwa huna ushahidi wowote unaobeba uzito wa ushahidi, ndio maana ulitumia barua feki ya La Cairo.
Bwana Macropolo tafsiri ya sheria ina technicalities ambazo haziwezi kufananishwa na mifano kama hiyo! kumbuka UWT ni institution na kinachoweza kufanyika ni kutoa dukuduku la maovu ila si ushahidi sheria haziruhusu kutolewa kiholela holela!
 
Back
Top Bottom