Mpevu,
Asante kwa swali lako kuhusu "Inclusivity". Mimi nadhani mtu yeyote mwenye Busara atapenda kwanza kusolve puzzle ifuatayo kabla hajashauri kuundwa kwa Kambi ya Upinzani inayoshirikisha vyama vyote:
i) Kwa mazingira ya 2010 ambapo CUF ipo tayari Serikalini na Katibu wake Mkuu ndiye Makamu wa Kwanza wa Rais ( pamoja na kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano haitambui cheo hiki na kimsingi Katiba imevunjwa). CUF ipo kwenye Serikali ya Chama cha Mapinduzi na Chama hicho ndicho kinachounda Serikali Bara. Hivyo Serikali zote mbili ni za Chama kimoja. Ni kuna uwezekano gani wa CUF hiyo hiyo iliyoko Serikalini kuwa kwenye Kambi ya Upinzani kwa Upande wa Bara? Tungependa kabla kutushauri kuunda Kambi ya Pamoja mtushauri hii Puzzle, hii Chemistry na utendaji wake utakuwaje? Je Watanzania( Bara) wanahitaji kuwe na Chama kimmoja Bungeni yaani CCM/CUF +Chadema =Hakuna Upinzani au inashauri nini. Chemistry hii ikijibiwa tunaweza kujadiliana kwenda mbele. Kwa Taarifa yenyewe ninazo zaidi ya SMS 2000 baada ya Mdahalo wa Jana kutoka kwa Watanzania, tena wakiwemo wa Zanzibar ( ambao wanaona kwa kitendo cha CUF kuingia Serikalini Zanzibar imekuwa nchi ya Chama kimoja (Bungeni japo De facto one party state haijatangazwa kama ilivyokuwa mwaka 1962. We may be on the way in Zanzibar atleast kama hatutakuwa makini.
ii) Mpevu umetumia mfano wa 2005. Nadhani Hamad hakuwa mkweli kilichotokea 2005. a) CUF waliunda Kambi ya Upinzani peke yao bila kushirikisha Vyama Vingine. Kama unavyofahamu CUF wote walikuwa wanatoka Pemba, ambayo kimsingi population yake haifiki nusu ya population ya Jimbo la Uchaguzi ya Ubungo. Hivyo, Wabunge wa Upinzani kutoka Bara tulikataa kuwa Upinzani (ambao pia wanawawakilisha Bungeni mamilioni ya Watanzania waliokerwa na CCM) hauwezi kuwakilishwa na Wabunge wanaotoka kwenye "Kitongoji". Kauli hiyo ilileta ugomvi sana wakati huo, lakini ndio ukweli kwani Mawaziri Vivuli wote walitoka Pemba. b) Zanzibar kama nchi inayo Bunge lake kamili (Baraza la Wawakilishi) inayo Baraza lake la Mawaziri, inayo Mahakama zake ( isipokuwa mahakama ya Rufaa). Ndani ya Baraza la Wawakilishi CUF nao walikuwa wanawakilishwana hivyo maslahi ya Zanzibar yalikuwa yamelindwa. Hivyo, ilikuwa si halali kwa Tanzania Bara yote kuwakilishwa na tulichokiita wakati huo Wabunge kutoka kitongoji kimoja. Watanzania nao wanahitaji kuwakilishwa ndani ya Bunge na Watu watakaokuwa wanawasemea tofauti na Wabunge wa Chama Tawala ambao kimsingi walikuwa wakiunga Serikali yao kwa kila kitu hata kama haikuwa na maslahi kwa wananchi. c) Kilio hicho kikasikilizwa na mamlaka ya Bunge, na Tukaambiwa tutengeneze Fomula itakayokubalika. Hivyo Fomula tuliyotengeneza ili tusiwatenge wenzetu ilikuwa Chama kinachounda Kambi ya Upinzani kiwe kimefikisha asilimia 12.5 ya Wabunge wote. Baada ya Fomula hiyo kukubalika na Bunge ndio tukaanza mjadala na Hamad Rashid ambaye wakati huo alikuwa tayari kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani. Tukakubaliana na Fomula hiyo ili Chama chochote kisipate nafasi ya kuchezea Kanuni na kuunda Kambi ya Upinzani bila kuzingatia maslahi ya Wananchi. Kambi ya Upinzani haipo kwa ajili ya Maslahi ya Wapinzani bali ya Wananchi, na hivyo lazima kujenga kinga ndani ya Kanuni ili watu wasije wakaunda tu Kambi kwa kuwa wana wabunge wengi kuliko wenzao kama ilivyotokea. d) Kwa kuwa CUF walikuwa "hawajafikia" asilima 12.5 Kanuni inasema, iwapo Vyama kwa pamoja vimefikia asilimia 10 ya Wabunge wote, (Kanuni ya 14(1) basi " Kambi ya Upinzani itaundwa na Wabunge wote wa Kambi ya Upinzani. Hivyo si kweli kuwa CUF walikubali kutushirikisha kwa hiari yao. Historical Facts must be respected. Hii ni historia na Historia haifutiki. e) Baada ya Kukubaliana kuunda Kambi ya Upinzani itakayoshirikisha Vyama Vyote, na kwa kuwa CUF ilikuwa na Wabunge wengi, Kiongozi wa Upinzani akatoka CUF na Hamad Rashid akaendelea kuwa Kiongozi wa Upinzani kwa kauli ya Wabunge wote. Kwa vile Chadema ilikuwa ya pili kuwa na Wabunge wengi kufuatia CUF (Wabunge 11 na UDP alikuwa 1) hivyo Dr. Slaa ambaye wakati huo alikuwa Mwenyekiti wa Wabunge wa Chadema (ieleweke Wabunge wa Chadema na siyo Kambi) akateuliwa kwa kauli mmoja kuwa Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani. Kuhusu kutoa Nafasi, naomba ieleweke kuwa mimi sikupewa nafasi na CUF kwa upendeleo. Nimekuwa Mbunge wa Bunge la SADC toka mwaka 1997 (nilishiriki kuaianzisha kwa kuandika Katiba) hivyo kauli ya Hamad siyo ya kweli. Kutokana nafasi yangu ndani ya SADC ambapo kwa muda mrefu nimekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Interparliamentary Cooperation and Cooperation Committee) Bunge la Tanzania limekuwa likinichagua kaiwakilisha siyo kwa upendeleo wa CUF. Hapa kilichokuwa kinaangaliwa ni maslahi ya Nchi na nani anaweza kuiwakilisha vizuri zaidi nchi si upendeleo kama ilivyotaka kueleweka). Vivyo hivyo kwa nafasi ya LAAC ambayo nilikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu. Lakini Hamad naye angelieleza nafasi za juu alizokuwa nazo yeye na kwanini hakuteua wabunge wengine wa CUF kwenye nafasi hiyo ilihali yeye ndiye Kiongozi wa Kambi ya Upinzani. Nadhani hoja ililenga ku polarize na kwa bahati mbaya Mhe. Mbowe hakuwa anajua intrigues za 2005 kwa kuwa hakuweko Bungeni wakati huo na asingeliweza kujibu kitu ambacho hakifahamu. Hivyo si kweli kuwa Kambi ya 2005 iliundwa kwa msingi tu wa kuunda mshikamano bali mazingira ya 2005 yalihitaji hivyo. Mazingira ya 2010 yanahitaji kwanza Chemistry iliyoko ijibiwe kabla hatua yeyote ya kuzungumzia mshikamano kuzungumziwa na kutotambua mazingira tofuati ni kutokuwa wa kweli kuwa Hali ya Siasa ni tofauti sana. Wananchi unaowasema, ndio ambao kama nilivyokuambia wanataka tusiungane na CUF sasa kama kuna msingi mwingie wa Kisayansi mtujulishe ili tuyajadili kwa kina maoni yaliyoko kwa maslahi ya Taifa na si kwa maslahi ya ushabiki.
Ninapenda kuuliza pia Chemistry ya pili, Hivi i) Lyatonga alipompigia Kampeni JK na leo anaingia kwenye Kambi ya Upinzani Chemistry hiyo itafananaje? Ndio maana iwapo ataingia kwenye Kambi ni lazima kwanza Kanuni zinazoongoza Kambi ya Upinzani zitazamwe upya na wote waiweke saini upya. Lakini haiji tu kwa kuwa mtu ameingia Bungeni kwa Msingi wa Upinzani na hivyo lazima aingie kwenye Kambi kwa kuwa tu kuna watu wanataka kuona Umoja. Hoja ni Umoja uko kwa kuwa watu wanataka kuona umoja au Umoja uko kwa kuwa kuna malengo tunataka kuyafikia. Je kwa Chemistry iliyoko malengo hayo yanaweza kufikika. Kama hatutapima kwa malengo basi kuna tatizo kubwa kwa kuwa tutakuwa hatukuwa tuna elewa Lengo na Madhumuni ya Kambi ya Upinzani kuwepo Bungeni na malengo yake ya Msingi ni yapi.
Mpevu, nadhani hoja yeyote inayoanzia kuwa " kuna kutoelewana kati ya viongozi ni potofu" na haitatufikisha katika kujenga Kambi imara ya Upinzani. Kitakachotufikisha kwenye Kambi imara ya Upinzani ni Chemistry ipi ya Kambi ya Upinzani itatufikisha kwenye Malengo ya uwepo wa Kambi ya Upinzani. Ninaogopa sana mtu anapotumia kauli " sisi wananchi" hawa wananchi unaowasema wanataka ni kina nani na wako wapi na maoni yao wametoa kwa njia gani na ni asilimia ngapi ya Watanzania. Haya mambo ni ya msingi sana na amini hayatapuuziwa katika mjadala kama huu.