ZeMarcopolo
JF-Expert Member
- May 11, 2008
- 14,011
- 7,192
Kuna kundi la wafuasi wa CHADEMA ambao wamehadaika kuwa kuna mkakati wa ndani unafanywa na viongozi wa chama hicho baada ya kutoridhika na kushindwa uchaguzi.
Hata hivyo, ukifuatilia mijadala inayoendeshwa na viongozi wa CHADEMA, utagundua kuwa hivi sasa wanajihusisha zaidi na masuala ya bunge. Aliyekuwa mgombea wa urais naye "ameingia mitini".
Wote tunajua kuwa aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, hapendi kuchelewesha mambo. Ndio maana alitaka matokeo uchaguzi toka sehemu mbalimbali nchini yatangazwe bila kucheleweshwa. Kitendo cha yeye kuchelewa kutoa vidhibiti au kauli yoyote ni ishara tosha kuwa aidha vidhibiti hivyo havipo au "amekubali yaishe".
Ushauri ninaowapa wafuasi wa CHADEMA wanaongoja mkakati wowote kuhusiana na uchaguzi mkuu uliopita ni kwamba, endeleeni na shughuli zenu za kila siku. Hakuna mkakati wowote ndani ya chama. Viongozi wanajadili kugombea uongozi wa upinzani bungeni n.k.
Kwa viongozi wa CHADEMA. Wapeni mwongozo wafuasi wenu. Maamuzi yoyote mnayoyafikia ni vyema mkayatoa kwao hata kama mnahisi ni maamuzi DHAIFU. huo ndio uongozi. Mkishindwa kabisa waambieni, wategemee nini na lini.
Wangu kwenu ni ushauri tu!