RealMan:
Hivi inamake sense, Kufanya Conclusion halafu ndo uombe uchunguzi ufanyike?. So far msimamo wa Chadema ni kwamba uchaguzi raisi wa mwaka 2010 ulichakachuliwa kwa hiyo ni uchaguzi batili.
na ili kuthibitisha Msimamo wa viongozi wakuu wa Chadema katika hilo:
(1) Dokta Slaa hakutokea siku ya kumwapisha JK, ili kutuma ujumbe wa kutokuridhika na matokeo
(2)Wabunge wa Chadema walisusia Hotuba ya Raisi ili kutuma ujumbe wa kutoridhika na mchakato wa uchaguzi wake.
Sasa hii ina maana gani?, maana yake ni kwamba Chadema wanaushahidi wa kuonyesha kwamba uchaguzi ule wa raisi uliharibiwa na kuhujumiwa ili kumfeva mgombea wa CCM.
Sasa kama wana Ushahidi haina haja ya kuundwa tume. kwa maoni yangu wanaweza kwenda mahakamani kuwashitaki wale ambao wana ushahidi wa kutosha waliovuruga uchaguzi(siyo kupinga kutangazwa kwa raisi).
Iwapo hawana nia ya kufanya hivyo, na so far mpaka sasa hawajaitangaza nia hiyo, option ya nguvu ni kwenda kwa wananchi kuwaeleza ni nini kilichotokea. kama miaka kadhaa iliyopita waliondoa hoja bungeni kwa kuhofia kuzimwa, na kisha kuja kuwashitaki wanaoitwa mafisadi kwa wananchi wananshindwa nini kuja kuwaelezea wananchi kinagaubaga kilichotokea katika uchaguzi wa mwaka huu?. kwa mtizamo wangu ni dhahiri kwamba kuiba uchaguzi nao ni ufisadi. ikumbukwe pia kwamba ahadi ya kutoa ushahidi wa kuhujumiwa kwa uchaguzi wa mwaka huu ilitolewa na Dokta Slaa.
Haitoshi kusema kwamba wameiandikia NEC kuonyesha kutoridhishwa na mchakato wa uchaguzi, na kwamba ushahidi wamepewa NEC, sasa haya ni majibu ya kushangaza, NEC ndiyo mtuhumiwa halafu unampa ushahidi ili afanyeje?, akiri kwamba ni kweli ndiyo ameharibu uchaguzi?, hili linawezekana?. yaani unamtuhumu mtu kwamba umeiba unampa na ushahidi halafu unamwambia kwamba jihukumu?.
Na kwa mtizamo wangu ni kwamba wakati huu ni wakati muafaka kabisa kutuelezea kile kilichojiri katika uchaguzi wa mwaka huu. hoja wanayoitumia ni kwamba huenda kukatokea uvunjifu wa amani kwa baadhi ya wananchi kuingia mtaani na kuleta vurugu. hoja hii ilikuwa na nguvu mara baada ya matokeo kuwa yametangazwa, lakini kwa sasa serikali ishaundwa, na iko under full control, halafu kitu kingine ni kwamba iwapo Chadema watatoa ushahidi huku wakiwaelimisha na kuwaelewesha wananchi kwamba vurugu siyo option nzuri, kiufupi Chadema wakidiscourage vurugu, bila shaka wananchi wataelewa na Chadema itazidi kujijengea heshima zaidi mbele ya Wananchi.
Kiufupi ni kwamba Chadema inabidi watuambie Watanzania.
(1) Je wanamtambua Raisi halali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba ni mheshimiwa Jakaya Kikwete?
(2) Je Uchaguzi Uliibiwa?, Ulichakachuliwa?, ulivurugwa?, wapi?, na nani?
(3) Dokta Slaa alipata kura ngapi za haki?, ambayo ni asilimia ngapi ya kura zote?
Wakisha fanya hivyo, then waendelee kutuletea ajenda ya NEC huru, kwa sababu so far ajenda yao ya kudai NEC huru hatuwezi kuielewa kama hawatatuelewesha kwa ushahidi wa kutosha Ubaya wa NEC
.
Nakushauri ukawaulize NEC na Kikwete unayedhani amedhalilishwa kama kweli NEC ushahidi iliyoupokea toka Chadema ni feki au si feki.
Ukipata jibu ndiyo uje hapa jamvini kutuletea hoja,nje ya hapo kaa kimya na ukawapepee hao MAFISADI