The Emils
JF-Expert Member
- Apr 16, 2011
- 568
- 124
- Thread starter
- #81
Ben hapa kweli nakuunga mkono kupata maoni ya wengi kuwa wanamtaka au hawamtaki lakini unaona wewe mwenyewe mfano hapa JF wengi tunataka Shibuda aondoke kabisa ili iwe fundisho kwa wale wote wanaoenda kinyume na msimamo wa chama, any way najua CDM viongozi wetu ni watu makini sana tunaamini watafanya maamuzi sahihi..Mkuu nakubaliana na yote uliyosema hapo juu.Tatizo tulilo nalo ni kwamba vyama vya siasa ni lazima tuangalie katiba zetu na kanuni ili kukidhi matakwa halali ya kidemokrasia kwa maana ya kuzingatia demokrasia na falsafa iliyosimama nyuma yake.Hapa chini ni baadhi ya conditions amabzao zinaweza kutoa mwanya na nguvu kwa chadema kumfukuza mbunge yeyote ingawa sitaenda deep kwa sasa kwa sababu maalumu
Kwanza kabisa kuna wajibu kama huu kwa mwanachama:
5.3.4 Kushirikiana na wanachama na viongozi wengine wote katika kutekeleza sera na mipango ya Chama.
.3 MAADILI
Maadili ya Chama ndiyo yatakayoainisha sifa, nidhamu, utii, uwajibikaji na dhamira yawanaChama, watendaji na viongozi wa Chama katika ngazi zote. Maadili haya yanajumuisha uongozi wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee.
2.4 ITIFAKI
CHADEMA kama Chama kinachokua na kupanuka kwa kasi kitaifa na chenye nia yakuchukua dola wakati wowote hakina budi kujiwekea taratibu mbalimbali ambazo zitakisaidia Chama kuendesha shughuli zake za Chama katika mtiririko wa aina fulanibila kuonyesha utofauti kati ya viongozi na ngazi mbalimbali za Chama. Nia ya kuwekataratibu hizi ni kuleta umoja na mshikamano ndani ya Chama na kukitambulisha
CHADEMA kama Chama kimoja. Kwa hiyo itifaki ya Chama inajumuisha pia uongozi wa Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee ambayo ni sehemu tu ya muundo na uongozi wa chama.
Kufukuzwa Uanachama:
5.4.3 Kuachishwa ama kufukuzwa na tawi lake ama ngazi nyingine ya Chama, kwa mujibu wa katiba kwa kukosa sifa za kuendelea kuwa mwanachama ama kuwa na mwenendo usioendana na Itikadi, falsafa, madhumuni, kanuni, maadili na sera za Chama.
5.4.4 Bila kuathiri kifungu 5.4.3 cha katiba, Kamati Kuu inaweza kumwachisha amakumfukuza mwanachama yeyote kwa utaratibu utakaopangwa na kanuni za Chama.
Hizo ndiyo leaning walls/tables,
Sasa vipi kama tukitoa pendekezo la kutumia mbinu ya kisasa na ya kidemokrasia kwa mapana kwa kuitisha kura ya maoni jimboni ili kujua msimamo wa wanachama na wapiga kura wa jimbo la Maswa kuhuu tabia na mwenendo wa mbunge wao na pia kupata maoni yao juu ya adhabu itakayofaa/chukuliwa dhidi ya Mh.Shibuda
Sijui kama Collin Powel angekuwa mwanachama wa chama cha siasa Tanzania angekuwa nadni ya chama hicho baada ya kumpigia kampeni mgombea wa chama kingine.Je huu si usaliti kwa ideology na sera za chama husika?mwaka jana kwenye kampeni,tujiulize swali ambalo hatutaki au tumesahau kujiuliza,je kuna mgombea yoyote aliyempigia kampeni mgombea wa chama kingine?Tafsiri yake ni nini katika sera,philosophy and ideology of the party?
Julius Malema Mwenyekiti wa vijana wa ANC aliimba pamoja na wafuasi wake wimbo wa 'Kill the boers' ambao unaenda kinyume na falsafa ya sasa ya ANC na serikali yake ya kuponya majeraha ya kibaguzi,na hakufukuzwa lakini waliona fursa ya kum-shape psychologically ili awe fit na balozi mzuri wa kuponyesha majeraha na kujenga taifa moja kwa kutumia fursa komavu za kidemokrasia.
Tujiulize mbona ODM ya kenya hawakumfukuza Willium Ruto na akina Sally kosgei pamoja na sarakasi zote ndani ya chama chao,tuangalie faida waliyoipata as a serious political entity na hasara waliyoipata as a serious & weak political Entity.