CHADEMA: Hatima ya Shibuda leo.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA: Hatima ya Shibuda leo..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Emils, Jul 17, 2011.

 1. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  WAKATI Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ikikutana leo jijini Dar es Salaam kumjadili Mbunge Maswa Magharibi, John Shibuda, mbunge huyo amesema hana taarifa za kikao hicho.

  Kikao hicho kitakachofanyika kinatarajiwa kumjadili mbunge huyo ambaye alihamia Chadema akitoka CCM siku chache kabla ya kuanza kwa kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.

  Kwa mujibu wa habari, kikao hicho tafanyika kwenye ukumbi wa Mbezi Garden. Shibuda aliiambia Mwananchi Jumapili jana kuwa hajapatiwa barua yoyote na chama hicho inayomtaka ajieleze kwanini aliisaliti kambi ya upinzani Bungeni kuhusu posho wakati akichangia hotuba ya makadirio ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

  Lakini, kumekuwapo habari kuwa Chadema inafikiria kumchukulia hatua za kinidhamu. Tuhuma zinazomkabili Shibuda ni kutoa matamshi yanayopinga na msimamo wa kambi yake inayoongozwa na Chadema pale alipowapiga vijembe wabunge wale wanaopinga posho zinazotolewa kwao na watumishi wengine wa umma nchini. Hata hivyo, Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema tangu Shibuda atoe kauli hizo Bungeni hakuna hatua yoyote aliyochukuliwa. Alisema kuwa kikao cha kamati kuu kitakachoketi leo pamoja na mambo mengine kitamjadili mbunge huyo. ’’Kesho (leo) atajadiliwa, ila hatua gani zinatachuliwa hilo sijui, pia suala la nidhamu ndani ya chama litakuwa moja ya ajenda za kikao hicho,’’ alisema Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai. Awali, Mnadhimu Mkuu wa Kambi hiyo, Tundu Lissu alilieleza gazeti hili kwamba kitendo cha Shibuda kupingana msimamo wa kambi ya upinzani ambao ni kukataa kulipwa posho za vikao, kimewadhalilisha na kwamba lazima mhusika (Shibuda) atoe maelezo kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa dhidi yake.

  "Kutokana na tukio la kudhalilisha uamuzi ya vikao vya kambi, kuna aina mbili za kumchukulia hatua Shibuda, kwanza ni kwa upande wa kambi ya upinzani na pili kumshitaki Chadema,”alisema Lissu na kuongeza:

  “Mbunge anapokiuka uamuzi ya kambi anastahili kuchukuliwa hatua za kinidhamu na kupewa adhabu, na adhabu kubwa anayoweza kupewa na kambi hii kwa kanuni zetu ni kumtenga katika kambi na kumtangaza hadharani kuwa huyu ametengwa na kambi kwa sababu amefanya makosa kadhaa".

  Kwa mujibu wa Lissu ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Shibuda mbali na kosa hilo, pia amekuwa akitoa matamshi ya kudhalilisha kambi ya upinzani na Chadema, pamoja na kuwadhalilisha viongozi wao.
  Akizungumzia matamshi ya kudhalilisha kambi ya upinzani na Chadema yanayotolewa na Shibuda, Mbowe aliliambia Mwananchi Jumapili, kwamba kila mtu ana haki ya kuzungumza anachokitaka, lakini kama ni masuala ya chama anatakiwa kufuata utaratibu. ‘’Kama anaona hajakosea huo ni mtizamo wake, unajua chama kina taratibu zake, chama sio kundi la watu ambalo halina kitu kimoja (katiba na kanuni) ambazo wamekubaliana kuzifuata kama njia ya kuwaongoza katika maamuzi yao,’’ alisema Mbowe. Alisema kiongozi si yule anayesimamia fikra zake binafsi, bali ni yule ambaye anaafikiana na chama chake kwa kila jambo kwa kufuata katiba, kanuni na sera za chama. ‘’Kama chama hakifuati katiba hakina umuhimu wa kuwapo, Chadema sio kundi la watu, ni chama ambacho kina malengo..., malengo hayo ndio yaliyotuunganisha pamoja,’’ alisema Mbowe. Alisema maamuzi ya Kamati Kuu yatatolewa kulingana na Katiba ya Chadema inavyoeleza. ‘’Unaweza kumuudhi Mbowe.., Lakini unapoanza kukishutumu chama pamoja na viongozi wake ni jambo jingine, katika hilo lazima itizamwe katiba ya chama inasemaje,’’ alisema Mbowe. Alisisitiza kuwa tangu kuibuke kwa mvutano hio, ni mara ya kwanza kwa Kamati Kuu kukutana na kuongeza kuwa ripoti mbalimbali pia zitajadiliwa katika kikao hicho ambacho kinaonekana kuwa kitatoa picha halisi ya maamuzi mwelekeo wa Shibuda ndani ya Chadema. Kauli ya Zitto

  Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini juzi alilieleza gazeti hili kuwa msimamo wa kumfukuza Shibuda upo pale pale, kwani kambi hiyo wala Chadema hawawezi kumwacha mbunge anayekiuka sera na kuwadhalilisha viongozi hadharani.

  "Shibuda hatafukuzwa kinyemela, lazima taratibu zifuatwe kwa Mnadhimu Mkuu wa kambi yetu kumwandikia barua ya kumweleza makosa yake na yeye kupata fursa yakujibu shutuma hizo, pili ataitwa katika Kamati Kuu ya chama chetu (Chadema), nao watatoa uamuzi wao,"alisema Zitto na kuongeza:

  “ Chadema si chama cha kihuni kwamba tutakurupuka ni lazima haki itendeke na mimi sipendi mtu aonewe, Shibuda atapata haki zake zote kama mwanachama. Mbunge yeyote wa Chadema anapaswa kujua akienda kinyume na sera ya chama atafukuzwa”.

  Alisema suala la posho lipo kwenye Ilani ya uchaguzi wa 2010 kwa hiyo ni sera, na kwamba anayepinga atafukuzwa tu na kwamba Chadema wataanza na Shibuda.

  Zitto alisema, "Shibuda anajua mie humtetea sana, lakini anapokwenda kinyume na sera ya chama tutamfukuza, aniite majina yoyote tu akienda kinyume na sera nitakuwa wa kwanza kumfukuza."

  "Kuna masuala ya nidhamu kwenye Bunge na wabunge wa chama fulani inaitwa’ three line whip, masuala ya msimamo wa kitendaji mfano tulipokaidi kwenda Bungeni kutoka nje ya ukumbi wakati Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akihutubia bunge (walk out), haya ni ya kawaida na hayana adhabu kali, lakini likiwa la sera adhabu ni kufukuzwa, Shibuda asipaparike," alisema Zitto.


  Msimamo wa Shibuda
  Akizungumza na Mwananchi Jumapili, Shibuda alisema kwa kifupi kuwa hajui lolote kuhusiana na kikao hicho huku akisisitiza kuwa yeye ni mwanasiasa adimu na kwamba akizungumza jambo anakuwa ameshalifanyia kazi. Alipoulizwa kama atakubaliana na maamuzi yatakayotolewa na Kamati Kuu, Shibuda alisema, “Siwezi kujua utamu wa mboga wakati sijui viungo vyake vitakavyonunuliwa,’’. Wakati akichangia makadirio ya matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka 2011/2012, Shibuda alitoa mpya pale alipopingana na misimamo wa Chadema huku akilikokotoa neno ‘posho’ kuwa maana yake halisi ni ujira wa mwia.

  Alisema mwia (sasa posho) ni malipo anayopewa mtu kwa kazi anayoifanya ili kumwongezea hamasa ya kuendelea kuifanya kazi hiyo. Kwa mujibu Shibuda, kama maana ya posho ni ‘ujira wa mwia’ kama ilivyokuwa ikitumika na wakoloni, haina sababu kuifuta kwa kuwa ndiyo hamasa kwa wabunge na watumishi wengine wa umma kuendelea kufanya kazi yao.

  Shibuda alilitahadharisha Bunge kuwa mjadala wa posho umetokana nalo kuwa na aina mbili ya wabunge; wabunge maslahi jamii na wabunge maslahi binafsi.
  My take: Tujikumbushie kauli zifuatazo zilizowahi kutolewa na hawa viongozi:
  1.Akizungumza na mwandishi wa TBC, Lissu amesema Shibuda amepewa siku Saba tangu atakapopokea barua hiyo awe ameijibu.

  2.Aidha Katibu Mstaafu wa Bunge George Mlawa akizungumza katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachotangazwa na TBC1 amesema kanuni za bunge zinamlinda mbunge dhidi ya kauli yoyote anayokuwa ameitoa ndani ya bunge.

  3.Shibuda anasema anahama CCM kutokana na chama hicho kupoteza dira ya maendeleo na uadilifu kwa kugubikwa na rushwa kiasi cha kusaliti dhamana kilichokabidhiwa na wananchi ya kulinda na kuendeleza demokrasia, haki na utawala bora. Raia mwema toleo namba 147 tarehe 18 august 2010

  4.“NDANI ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuna viongozi wanaoilewa vema misingi na maadili ya chama, lakini wapo wanachama wasiojua chochote kuhusu chama chao. Ni wale waliovunwa kwa njia ya ufisadi na uanachama wa papo kwa papo. Hawa ndio wanaokivuruga chama chetu.

  “Ni unafiki wa wazi kabisa kusema CCM bado ipo katika mstari wake uleule wa awali. Nikiwa kada ninayekijua vizuri chama hiki, siwezi kusema CCM ipo imara na imebaki katika mstari wake uleule ulioasisiwa na viongozi wetu. Siwezi kuwa mnafiki…”

  Hiyo ni kauli ya mwanasiasa John Magale Shibuda (58), mbunge wa Maswa (CCM), Shinyanga, mwenyekiti wa zamani wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM mkoani humo, Mjumbe wa zamani wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

  Shibuda ni mmoja wa wanachama wa CCM waliojitosa katika kinyang’anyiro cha urais ndani ya chama hicho mwaka 2005.

  Katika mahojiano yake na MwanaHALISI wiki iliyopita mjini Dar es Salaam, Shibuda anasema ndani ya chama chake kuna ombwe la uongozi linalotokana na chama hicho kuacha mwelekeo wake wa asili. mwanahalisi tarehe 8 septemba 2009

  Kwa kauli kama hizo ambazo zilishawahi kutolewa na John Magale Shibuda tutegemee nini kutoka kwake kama atatimuliwa na CHADEMA?
   
 2. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2011
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  CHADEMA ninawapongezeza sana kwani kweli kurunzi yenu inamulika mbali..Sasa kwa wasio na macho ya kuona mbali wasipoweza tena kuona na kuelewa basi inatosha kwao.
  SASA MAAMUZI YOTE YA CHAMA NI LAZIMA KUWA MAKINI SANA NA KUFANYA UTAFITI WA HALI YA JUU..NI KWELI AKIKOSA MTU APEWE ADHABU NA IWE YA KIPIMO PASIPO KOSA JINGINE KUIBUKA NDANI YA ADHABU.....iI LOVE CHANGES AND I LOVE CHADEMA
   
 3. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mtoeni fasta. Sijui huwa anawazaga nini yule.
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kumbe alikwenda CHADEMA kutetea posho zake?
   
 5. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hizo ndio fikra za shibuda..alijua labda CDM kuna mila kama zile alizoziacha kule magamba za kupindisha maamuzi kumbe akakutana na makamanda wanaoweka kwanza maslahi ya taifa mbele then mambo mengine baadae sasa leo sijui kama atapona huyu kilaza..
   
 6. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  mmmmmh!patamu hapa na kama alibahatika kuyajua mengi ya CDM basi atabwabwaja pindi atakapo timuliwa.Nadhani anaweza kufanya kama Kafulila.
   
 7. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Nasubiri kwa hamu
   
 8. m

  mtimbaru Member

  #8
  Jul 17, 2011
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 74
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  huyu shibuda ni mamluki na alijiunga cdm kwa ajili ya kukipasua ,haiwezekani ukawa cdm na hapo hapo unapinga sera za chama ,hii haikubaliki. kamati kuu shughulikieni suala hili na ikibidi shibuda afukuzwe chama
   
 9. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #9
  Jul 17, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  Naheshimu maamuzi ya CDM, pia natamani afukuzwe akale matapishi yake kule alikotoka. Shibuda ni mzigo kwa chadema. Hana mawazo mapya zaidi ya kufikiria tumbo. Ndiyo maana ccm walimtosa.
   
 10. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Abwabwaje baada ya kutimuliwa? ataonekana mwehu tu

   
 11. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #11
  Jul 17, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kafulila alibwabwaja hadi akafulia CDM iko pale pale na ndio ina excel sembuse huyu aliyejichokea kabla hajaanza.
   
 12. S

  SwaiMosha Member

  #12
  Jul 17, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Nyie CDM hamna ubavu wa kumfukuza Shibuda; maana mlipomchukua mlifikiri mmefanikiwa; lakini sasa akiwa ndani au nje ya CDM atawamaliza maana mmemeza ndoano. Hahaha! Tusubiri maana ndoa sasa imekuwa ndoano.
   
 13. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Makao makuu CDM mnamiliki maamuzi ya kumfukuza au kutokumfukuza, ama Shibuda ana miliki wapiga kura ambao kwao yeye ndiye jembe lao la ukweli wako tayari kufa nae hata ahame chama chenu. Shibuda ataenda kwa Cheyo na bado atakuwa na vote kubwa sana.
   
 14. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #14
  Jul 17, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Aliondoka Kabouru katibu wa mkuu atakuwa Shibudu.
   
 15. kichomi

  kichomi JF-Expert Member

  #15
  Jul 17, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Misimamo kama hiyo ndio tunaitaka sasa,hakuna kuremba mamluki lazima watimuliwe.
   
 16. Keynes

  Keynes JF-Expert Member

  #16
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 499
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  huyu ndugu zangu mtoeni fasta hana tofauti na mwanamke ma.l.ya.
  Tunahitaji watu wanaoweza kuzungumzia mstakabali wa nchi yetu na kusimamia yale wanayo yazungumza.

  Huyu hafai tena kwenye chama chochote maana ni vuguvugu....hasomeki ni baridi au wa moto!!!
   
 17. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #17
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Haya ndio matatizo ya siasa zetu, sijasikia kwingine kokote Mbunge akijadiliwa kuwa na msimamo tofauti na wengine katika chama chake. Shibuda, huko ni matatizo tu, hiyo ni kampuni na ni usultani tu huko, si kama chama cha siasa cha kawaida, kama ulikuwa hujui sasa ndio utajuwa.

  Badala ya watu kujadili strategies wanakwenda kumjadili mtu.
   
 18. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #18
  Jul 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Huyu hastahili kuendelea kubaki, atimuliwe!
   
 19. The Emils

  The Emils JF-Expert Member

  #19
  Jul 17, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nani kakudanganya wewe kwamba Shibuda anamiliki wapiga kura..mbona unadhalilisha wapiga kura wewe? Weka hiyo hati miliki ya Shibuda kwa wapiga kura..ahaa kumbe na wewe ndio walewale wa Posho kwanza maslahi ya wananchi baadae..wapiga kura wote wameyasikia aliyoyasema huyu posho kwanza sasa subiri hutaamini kitakachotokea..
   
 20. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #20
  Jul 17, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  CDM ilikuwepo kabla ya Shibuda na itaendelea kuwepo. Chadema ni ya wananchi na wakiamua hawamtaki basi hawamtaki. Hata kama ni kukosa jimbo.
   
Loading...