CHADEMA: Hatima ya Shibuda leo..

Nyie CDM hamna ubavu wa kumfukuza Shibuda; maana mlipomchukua mlifikiri mmefanikiwa; lakini sasa akiwa ndani au nje ya CDM atawamaliza maana mmemeza ndoano. Hahaha! Tusubiri maana ndoa sasa imekuwa ndoano.
CCM ndo huwaomba manyang'au wajiuzuru, CHADEMA huwa inawatimua na mfano mzuri ni Kafulila na wenzake...
 
Labda wananchi wawe vilaza, mataahila, mtindio wa ubongo au mazezeta ndo watamchagua huyu kilaza anayetetea tumbo lake badala ya hao wananchi waliomchagua lakini vinginevyo ujue akitimliwa huu ndio mwisho wake na hata yeye anatambua hilo
 
Haya ndio matatizo ya siasa zetu, sijasikia kwingine kokote Mbunge akijadiliwa kuwa na msimamo tofauti na wengine katika chama chake. Shibuda, huko ni matatizo tu, hiyo ni kampuni na ni usultani tu huko, si kama chama cha siasa cha kawaida, kama ulikuwa hujui sasa ndio utajuwa.

Badala ya watu kujadili strategies wanakwenda kumjadili mtu.
Naona una ushauri mzuri ungewapa kina Nape mapema wala Rostam yasingemkuta.
 
kama hyo ilikua ilani ya cdm, kwa nini zito alikua anawakilisha kama hoja yake?
akawapa kazi ngumu akina mbowe kutangaza kuwa ni mpango wa cdm sio ya mtu mmoja, naona sasa cdm wanazidiwa na power strugle
endeeni kumalizana tu ccm hamitoi kwa style hii
 
Labda wananchi wawe vilaza, mataahila, mtindio wa ubongo au mazezeta ndo watamchagua huyu kilaza anayetetea tumbo lake badala ya hao wananchi waliomchagua lakini vinginevyo ujue akitimliwa huu ndio mwisho wake na hata yeye anatambua hilo

naomba ufafanuzi kuhusu posho walizozikataa wazee wa magwanda, mbona zinaendelea kuzama kwenye account zao tu na hatuoni kelele tena? cheza na wanafiki wewe, au kama hujui wanapokea posho kaa kimya! siku magamba watawalipua magwanda utatafuta chaka la kujificha
 
tena naona Chadema mmechelewa sana kufanya maamuzi...alipaswa awe keshafungashiwa virago vyake mapemaaaaa..... Wataondoka wengi wapuluzi kama Shibuda na chama kitasimama....mwanachama hapaswi kujitia maarufu kuliko chama.
 
Shibuda kutimuliwa serves him right, kwanza aliingia tu CDM kwa vile alitolewa na SSM kwenye kura za maoni so alichofuata CDM ni cheo tu na sio mapenzi mema na chama
 
mmmmmh!patamu hapa na kama alibahatika kuyajua mengi ya CDM basi atabwabwaja pindi atakapo timuliwa.Nadhani anaweza kufanya kama Kafulila.
kafurila alitoka akasiliba sana lakini bado wabunge waliongezeka.sembuse huyu ambaye hana hata mwaka chadema!.asepe tu.mia
 
Afadhali tumfukuze huyo magamba manake naona bado ana zile fikra za kimagamba hatufai huyu jamani tumteme fasta
 
Sifahamu sana taratibu na Katiba ya cdm zinavyosema lakini mimi ninamtazamo tofauti kidogo na wengi wa wachangiaji waliotangulia. Kwenye wengi pana mengi na kutofautiana mitazamo ni kawaida. Kosa la Shibuda ni kwenda kinyume na makubaliano/msimamo. Tunaruhusiwa kutofautiana ila tukishakubaliana lazima tuwe na msimamo mmoja. Na hapo ndipo alipokosea Shibuda. Chama kijadili na kitoe adhabu kulingana na taratibu/katiba yake
Tofauti yangu na wachangiaji wengi ni kuhusu tolerance/uvumilivu. Cdm inajijenga kwa gharama kubwa ikiwa ni pa1 na kushawishi wananchi wajiunge nacho. Itakuwa ni ajabu sana kama hawataweza kuvumiliana na kurudishana kwenye mstari pale mwanachama anapopotoka na badala yake ni kutimuana na kutupiana maneno ya kashfa. Chama ni Imani na wanaweza kuwa na imani inayofanana lakini hawawezi kuwa na approach/ mtazamo unaofanana. Nilazima wavumiliane na kukumbushana misingi ya chama hadi kufikia malengo.
Kwa mtazamo huo basi, nashauri Shibuda apewe ONYO tu, akirudia wampe adhabu!
 
Huyu Shibuda ni liability kwa chama chochote kile cha kisiasa. Watu kama yeye wangefaa sana kuwa wagombea binafsi wasiofungamana na chama chochote.

Sasa akitimuliwa toka CHADEMA sijui ataenda wapi? Labda atarudi CCM....who knows.
 
Sifahamu sana taratibu na Katiba ya cdm zinavyosema lakini mimi ninamtazamo tofauti kidogo na wengi wa wachangiaji waliotangulia. Kwenye wengi pana mengi na kutofautiana mitazamo ni kawaida. Kosa la Shibuda ni kwenda kinyume na makubaliano/msimamo. Tunaruhusiwa kutofautiana ila tukishakubaliana lazima tuwe na msimamo mmoja. Na hapo ndipo alipokosea Shibuda. Chama kijadili na kitoe adhabu kulingana na taratibu/katiba yake
Tofauti yangu na wachangiaji wengi ni kuhusu tolerance/uvumilivu. Cdm inajijenga kwa gharama kubwa ikiwa ni pa1 na kushawishi wananchi wajiunge nacho. Itakuwa ni ajabu sana kama hawataweza kuvumiliana na kurudishana kwenye mstari pale mwanachama anapopotoka na badala yake ni kutimuana na kutupiana maneno ya kashfa. Chama ni Imani na wanaweza kuwa na imani inayofanana lakini hawawezi kuwa na approach/ mtazamo unaofanana. Nilazima wavumiliane na kukumbushana misingi ya chama hadi kufikia malengo.
Kwa mtazamo huo basi, nashauri Shibuda apewe ONYO tu, akirudia wampe adhabu!

Adhabu gani?
hata kufukizwa ni adhabu pia,...
akirudia tena na tena je?
 
kutofautiana ni healthy. zito anasema shibuda afukuzwe, mbona yeye hakufukuzwa kwa kutofautiana na chama?
 
Nimesoma mwananchi uk wa 4 nashangaa zitto anasema shibuda afukuzwe kwa kutofautiana na chama. mimi naona tofauti za mawazo ni kawaida. kama basi ni kosa la kufukuzwa zitto awe wa kwanza maana alizungumza na waandishi kupinga msimamo wa chama wakati shibuda alizungumza bungeni anakolindwa na sheria. zitto anataka chadema ianguke nimwonavyo
 
Wanasiasa aina ya Shibuda ni mzigo mkubwa kwa ustawi wa Taifa.

Umepotoka na kinyume chake ni sahihi...

Tunahitaji wanasiasa wenye mawazo huru wengi zaidi ili tutoke hapa tulipo kama taifa, ule wakati wa fikra sahihi kwa jina la chama umekwisha...
 
Nadhani kazi ya kufukuza mtu upewe mkutano mkuu uamue kwa kura ili kuondoa lawama
 
Back
Top Bottom