DUH WEWE NI KM MAMA POROJO VILE, KELELE NYINGI BILA USHAHIDI, SKU NYINGINE TUTAKUNYOA NYUSI ILI UFANANE VIZURi NA WAMBEA
Nimemsaidaia kuleta huo ushaidi, joseph makene alikiri kuwa wana msapoti Odinga! Mbona mnaanza kumkataa wakati hapo mwanzo mlikuwa mnamshabikia??
Chadema yambeba Odinga
By :
Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Kilimtumia magari, wasanii kuzunguka nchi nzima
WAKATI wananchi wa Kenya leo wanatarajia kupiga kura kumchagua rais wa nchi hiyo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeonekana kumbeba mgombea urais kupitia Chama cha ODM ambacho kimo ndani ya Muungano wa CORD, Raila Odinga, kwa kupeleka magari na timu ya wasanii kumsaidia wakati wote wa kampeni zake.
Chadema ambao wanadaiwa kuwa rafiki mkubwa wa Odinga, kilituma magari mawili aina ya Fuso kwa ajili ya kumpigia kampeni ambazo zimedumu kwa mwezi mmoja.
Mbali ya kutuma magari hayo, Chadema walituma kikundi cha wasanii kikiongozwa na mwimbaji maarufu wa chama hicho, Fulgance Mapunda 'Mwanakotide.
Mbali ya chama hicho, Watanzania wengi ambao wanadaiwa kumuunga mkono Odinga na wamekuwa wakitajwa mara kwa mara ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli na Rostam Aziz.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Habari wa Chadema, Boniphace Makene alikiri chama chake kupeleka magari hayo na wasanii kwa ajili ya kumsaidia Odinga na timu yake kuendesha kampeni zake kwa ufanisi.
Ni kweli kwa kipindi cha miezi mitatu sasa, timu ya Chadema imekuwa ikizunguka katika miji mbalimbali nchini Kenya, kwa ajili ya kumsaidia mgombea wa Muungano wa CORD kupiga kampeni, kumekuwa na mafanikio makubwa mno.
Tuliruhusu magari yetu mawili aina ya fuso, ambayo yalikuwa na vifaa vya kisasa kwa ajili ya muziki na wasanii wawili, Mwanakotide na Pepe ambao kwa kweli wamefanya kazi kubwa, tunaamini mchango umeonekana, alisema Makene.
Alisema magari hayo, yalitumiwa na Odinga katika mikutano yote ya kampeni, ambazo zilihitimishwa juzi katika Uwanja wa Nyayo mjini Nairobi.
Kama ulifanikiwa kuangalia televisheni, juzi kwenye Uwanja wa Nyayo, magari yale yalikuwa kivutio kikubwa sana, yalikuwa yamepambwa picha nyingi za Odinga na Kalonzo Musyoka, ambaye ni mgombea mwenza wake, alisema Makene.
Kwa upande wake, Mwanakotide alipoulizwa alisema wamekuwa Kenya kwa kipindi cha miezi mitatu kusaidia ODM, kutokana na kuwa na uhusiano mzuri na chama chao.
Tumekuwa na mafanikio makubwa, kazi yetu ilikuwa kuhubiri amani na kuwataka Wakenya kuachana na mambo ya ukabila na chuki, tunaamini wametuelewa
unajua wale ni jamaa zetu, lazima tuwasaidie, alisema Mwanakotide.
KWA HISANI YA GAZETI LA MTANZANIA.