CHADEMA Haiko na Raila, please...

CHADEMA Haiko na Raila, please...

Mambo yameanza kunuka. Hata Yesu aligeukwa na baadhi ya wafuasi wake kwa matamanio ya kidunia. Yaani pamoja na ushahidi wote wa CHADEMA kupeleka magari, baadhi ya wabunge na kutoa michango ya kifedha kwa ODM, leo wanageuka? hatari. Na huo ufafanuzi mbona hawajatoa viongozi wa CDM kwenye vyombo vya habari? maana ninavyowafahamu kwa kupenda sifa wangeitisha press conference.

halafu, hayo madai si ya leo au jana. yalikuwepo hata kabla ya uchaguzi haujafanyika. leo mmeona maji yameanza kuwafika shingoni na ni siku moja tu kabla ya matokeo ya mwisho kutangazwa hapo tarehe 8.3.2013 asubuhi mnaanza kuwakana ODM na kusingizia kuwa CCM ndiyo wana ushirika na ODM. Hivi inaingia akilini?

halafu barua yenyewe ina utata;
- kama ulikuwa ni mwaliko wa kichama, ingepaswa uandikiwe uongozi wa chama cha mapinduzi. halafu kwa kawaida barua za organizations hazimlengi mtu. hivyo kwa kitendo cha kumuandikia mtu tena kwa kumtaja, Waziri wa Ujenzi, John Pombe Magufuli, bila shaka ni mpango ambao umeandaliwa na watu ambao upeo wao katika barua za kiofisi ni finyu na ninaamini kuwa hao ni viongozi wa CHADEMA ambao hawatumii hata chembe ya akili yao kufikiria.

- inawezekana vipi Mkutano ufanyike tarehe 7/12/2012 halafu barua ya mwaliko iandikwe tarehe 5/12/2012. kwa maoni ya haraka, barua hiyo kama ingekuwa ni ya kweli ingewafikia walengwa baada ya tukio. hata kama utatumia fax, lazima kuna taratibu za kiofisi mpaka barua kufikia mlengwa na kufanyiwa kazi kwa wakati.

-udhaifu mwingine wa barua hiyo ni kuwa maudhui ya barua yenyewe haieleweki.je ilikuwa ni kukialika chama cha mapinduzi kuimarisha nguvu za ODM au ilikuwa ni nini?

-halafu utata mwingine ni kitendo cha barua kukosa kumbukumbu namba. hata kwa watu waliosoma hadi darasa la saba tu bila shaka wana uelewa kuwa barua ya kiofisi tena ya chama ambacho kipo madarakani lazima iwe na Kumbukumbu Namba. kwa hiyo barua iliyotolewa inakosa hadhi na ndipo tunapoamini kuwa imeandaliwa na wafuasi wa CHADEMA ambao wengi wao uelewa wao ni mdogo katioka mambo ya kiofisi na huenda ni hawa waliopata alama 0 kwenye mitihani ya kidato cha nne au wale waliochora zombi na messi:amen:

kwa ujumla nimeona kichefuchefu baada ya kuiona hiyo barua na kitendo cha kujinasibisha kuwa imeandikwa na ODM


......

Mkuu mfa maji haachi kutapa tapa!
 
Sioni Matizo kwa Odinga ama ODM kuwa na marafiki na vyama ama wanavyama wa ccm and cdm kwa nyakati tofauti ama wakati mmoja kwa maslahi yafananayo ama tofauti. Kuanza kukana uhusiano kwa vile swahiba anazama siyo utu wala uungwana. Ninyi ni wa Tanzania, mlitamani Odinga awe raisi wa Kenya kwa Vigezo na vipaumbele vyake na vyenu wakati matokeo yanaonyesha kwamba vigezo na vipaumbele vyenu si vya wa Kenya na hamna uwezo wa kuwalazimisha wafuate hayo maruwe ruwe yenu wakati wana ya kwao.

CCM na CDM lazima mpate somo hapa. Kupanda na kushuka, kupata na kukosa yote ni matokeo yanayowezekana kwa mtu yeyote.

Ni vizuri kujifunza uhalisia wa maisha. Kama Raila ama uhuru ni rafiki ya yeyote, usimkatae eit kwa vile anasindwa. Kaa naye ujifunze wapi alikosea ili wewe usifanye ile kosa na yeye kesho aisrudie kosa lile. Yako ya ndani ya chama, yako ya mgombea na yako ya jamii. Yatathminini ya hao na mtengeneze kwenu.

Lakini sioni kwa nini muanze kukosa usingizi ajili ya wakenya ambao wanaenda kasi ya maendeleo kuliko sisi ma pompompo Bozolala.

La kufanya kwa CDm ni kuhakikisha ubozolala wa watz unakwisha kabla ya uchaguzi ili wafanya uchaguzi sahihi na kudhibiti wizi na udhurumati wa ccm ili mshindi sahihi apatikane.

MSIPOTEZE MUDA NA NGUVU KUJIPENDEKEZA AMA KULUMBANA KWA MAMBO YA WAKENYA AMBAYO HAYATUHUSU MOJA KWA MOJA. LAKINI RAFIKI YAKO AKIZIDIWA USIMKIMBIE. MSHIKE MKONO NA UWE NAYE HADI APATE NGUVU TENA. MNAVYOFANYA SASA MNATIA SHAKA KAMA KWELI MNAWEZA KUWA RAFIKI WA KWELI WA WA HATA WATZ KATIKA RAHA NA TABU
 
Mi na mtu wa karibu wa CHADEMA alianiambia kabisa kwamba wametoa na magari kwenda kupimgia kampeni.Ila hayo magari yamebadilishwa rangi na namba
 
Waandaye maandamano kumsaidia ODINGA kupinga matokeo , maji wakiyavulia nguo hawana budi wayaoge.

we subiri tu. si walimshinikiza kalonzo musyoka akatae kura kuhesabiwa kwa njia ya mashine, hilo wamefanikiwa na sasa ni mannual counting. lakini bado uhuru yuko juu. sasa wamekuja na hoja nyingine ya kutaka kurudia kuhesabu kuanzia kwenye vituo vya kupigia kura. hilo limekataliwa. na sasa wanashauriana na CHADEMA kuitisha maandamano nchini kenya kupinga uhuru kushinda. Si unajua baadhi ya wabunge vijana wa CHADEMA wamekataa kwenda JKT? UNAJUA KWA SASA WAPO WAPI? wapo Nairobi wanaandaa maandamano
 
Nimegundua kuwa kumbe kwenye chama cha siasa kuna wanachama, wafuasi na washabiki. Hii thread ni kwa ajili ya washabiki tu
 
Mbona mnabishanis mambo ya kipumbavu, masuala ya kenya yanawasaidia nini nyinyi kama watanzania?
Wewe huoni unafiki unaojitokeza?
Backing a losing horse, halafu baadaye anapokata roho anaambiwa farasi huyo si wangu bali wa kwako!!
 
Naona kuna upotoshaji mkubwa sana wa baadhi ya members humu JF........THIS IS FOR THE RECORD!

attachment.php


[FONT=Arial, Tahoma, Helvetica, FreeSans, sans-serif]Picha za kampeni za mwisho mwisho chini ya Kamanda MBOWE. msitufanye wajinga[/FONT]






 
Tumekata mzizi wa fitina maana haya manyang'au masisiem yanaropoka tu kila siku....
 
Na hii? Halafu punguza hasira unapojibu hoja.......haikusaidii hata kidogo

cAHutCJl.jpg



........

Wewe ni wa wapi? mbona husomeki. Hiyo ni ni individual letter ni mtu kamuandikia mkubwa wake.

Hata wewe kama umeajiriwa na unaandika barua kuexpress issues zako ziwe kustaafu kwa hiari, kuomba uhamisho, kuomba kupandishwa cheo utaandika bila ya reference number.

Au hujui matumizi ya kumbukumbu namba? kifupi ni kurahisisha utafutaji wa barua inapohitajika kwa vile zipo nyingi.

Sasa wewe unayeandika una mafaili nyumbani kwako? ila yeye atakapojibiwa lazima kuwe na reference. kama unayo aliyojibiwa itundike hapo ndipo utakapoamini ninachukueleza
.
 
we safari ni safari bora usepe tu maana umechokoza mada unashindwa kuidefend
 
Kayataka Mwenyewe, wenyewe walikimbilia kuleta mada ya kuonesha hisia zao kwa ODINGA sasa wanaruka ruka nini, wavumilie tu.

Nasikia EZEKIEL WENJE kapiga kura Migori, magari ya M4C yako huko


.......

Tusubiri matokeo jamani mbona mnaleta uchuro wakati mchakato bado unaeendelea.tusubiri tuone.
 
Wewe ni wa wapi? mbona husomeki. hiyo ni ni individual letter. ni mtu kamuandikia mkubwa wake.

Hata wewe kama umeajiriwa na unaandika barua kuexpress issues zako ziwe kustaafu kwa hiari, kuomba uhamisho, kuomba kupandishwa cheo utaandika bila ya reference number.

Au hujui matumizi ya kumbukumbu namba? kifupi ni kurahisisha utafutaji wa barua inapohitajika kwa vile zipo nyingi.

Sasa wewe unayeandika una mafaili nyumbani kwako? ila yeye atakapojibiwa lazima kuwe na reference. kama unayo aliyojibiwa itundike hapo ndipo utakapoamini ninachukueleza
.

......

Aisee wewe ni wa zamani sana..........pole wenzako hayo mabo ya kumbukumbu numbers tumeshasahau kitambo....yaani hata barua ya kujiuzulu Hillary unasema sio official? Kweli?

2.+barua.jpg
 
Wewe umeelewaje hiyo barua?
Mimi mtanzania mwelewa si mtanzania wa kuuliswa swali nami nikauliza swali badala ya kujibu kwanza, kama mada imekushinda nenda kwenye blogs za akina AMINA KOPA, ASHA BARAKA na MZEE ysufu huko uta-enjoy kwa upeo wako huo.
 
from this thread and the comments wana CCM utawajua na wana CHADEMA utawajua......i cant wait for 2015,, anyways lets learn from the KENYAN electiion mistakes na sio kuvurigiana.....
 
Siku zote tunawaambia Yeriko Nyerere na Ben wanauma na kupuliza Chadema ona sasa wameitia doa Chadema kwani thread ya kusema Chadema ina support ODM na Odinga imeletwa hapa JF na Yeriko Nyerere ambaye ni mtu wa jikoni kabisa pale Chadema sasa Raila na OdM yake wameinamishwa na kijana wa mujini Uhuru mnakuja na kuanza kukanusha kuwa hamko upande huo hahahhhaaaaaaaaaaaaaaaaa
Hii barua ya kutengeneza tu. Tangu mwanzo mliandika wenyewe CHADEMA(RAILA) vs CCM(UHURU) yamewafika shingoni sasa, haya ogeleeni tuone kama mtafika ng'anmbo
 
Mi na mtu wa karibu wa CHADEMA alianiambia kabisa kwamba wametoa na magari kwenda kupimgia kampeni.Ila hayo magari yamebadilishwa rangi na namba

......

Sasa kama umeambiwa? ni dhambi CDM ikimsaidia Raila? magari yenyewe mnayopigia kelele mawili, nyie mmelipa ticket ngapi za ndege kwenda kuchakachua matokeo yao?
 
Back
Top Bottom