CHADEMA & CCM Jiangalieni! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA & CCM Jiangalieni!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by W. J. Malecela, May 20, 2012.

 1. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #1
  May 20, 2012
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  - Matukio ya hivi karibuni kati ya Wabunge Nassari na Shibuda, yanaleta maswali magumu sana kuliko majibu yake. Ninasema hivi CCM wasipuuze maneno ya Nassari na pia Chadema wasipuuze maneno ya Shibuda wayatafakari na kuyafanyia kazi, mifano ipo mingi sana kwa mfano kuna wakati hatukutaka kuongelea katiba wala Muungano, lakini sasa wakati umefika ambapo ukweli upo wazi kwamba tungenongea haya kule nyuma, saa hizi tungekwua mbali sana.

  - So Chadema na CCM, wasiwapuuze Nassari na Shibuda, kwa sababu reading between the lines kuna ujumbe mzito wa kisiasa kwenye maneno yao.


  William.
   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Shibuda ameongea lipi la maana?
   
 3. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #3
  May 20, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Si dhani kama ni vyema kutumia muda kuanza kuangalia Shibuda au Nassari alichoongea kama ni ujumbe walitaka kuufikisha umefika, hivyo ni kupanga kukabiliana nao. Sitarajii watu kuacha kujadili masuala muhimu ya kujenga na kuanza kumjadilia Shibuda ambaye kwa vyovyote kauli yake ile ni ya kuganga njaa.

  Tutumie majukwaa ya siasa kujadili mawazo ya kujenga nchi yetu na siyo nani kasema nini, hizi ni siasa za maji taka kwa wakati huu. Tena kwa mtu kama shibuda ni bora kukaa kimya tu ili ajione mwenyewe alichikifanya hakina maana.
   
 4. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #4
  May 20, 2012
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  - Hapana kuna ujumbe mzito sana kwenye maneno yao, ni waste of time kuwajadili wao kama walivyo, ila hoja zao hazikwepeki!


  William.
   
 5. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #5
  May 20, 2012
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,616
  Likes Received: 1,908
  Trophy Points: 280
  - In the big picture Shibuda ana tatizo na establishment na njia inayotumiuka kumtafuta mgombea wa urais huko!

  William.
   
 6. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #6
  May 20, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Bora Aliyosema Nassari kuhusu utawala wa majimbo kuliko kujadili mtu anayeshobokea urais kupitia CDM lakini anaenda kutangazia kwenye Mikutano ya magamba ha! ha ha
   
 7. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #7
  May 20, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tukumbuke kuwa ni Shibuda huyo huyo aliyekuwa na tatizo na establishment ya CCM kuhusu jinsi ya kupata wagombea wa Ubunge na ndicho kilichompeleka CDM. Labda tujiulize tatizo ni CCM, CDM or Shibuda? Nani hapa ni common denominator (main tatizo?)
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  May 20, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,573
  Likes Received: 3,873
  Trophy Points: 280
  kote tu si CCM si Chadema........kubisha hapa ni kufunika uovu
   
 9. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #9
  May 20, 2012
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unafahamu njia inayotumika kumtafuta mgombea urais "huko"?
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  May 20, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,820
  Trophy Points: 280
  Kibudu... I mean Shibuda hastahili kupewa hata dakika chache za kumjadili. Tangu aingie CDM ameshafanya mengi ya kukidhalilisha chama hicho mbele ya wapiga kura hivyo anachostahili ni kufukuzwa chamani tu na siyo kumjadili....na aliyoyasema Nassari ni kweli tupu pamoja na magamba kutaka kumtisha eti aombe radhi.....aombe radhi kwa kusema kweli!?
   
 11. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #11
  May 20, 2012
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na hoja yako 100%
  Mara nyingi wapuuzaji hujikuta kuwa ni wapuuzi wao wenyewe. Mfano CCM ilivyopuuza hoja ya Mtikila ya mgombea binafsi. Sijui walimaliza shilingi ngapi kupinga hiyo hoja mahakamani, na sasa wamegundua nini!!!!
   
 12. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #12
  May 20, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  naona una pumba nyingine leo kama kawaida yako
   
 13. W

  Wakurogwa JF-Expert Member

  #13
  May 20, 2012
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuna watu humu jamvini yani ukizungumzia mtu yeyote anayetoka au mwanachama,mbunge wa chadema yan wanadiscourage hoja hata kama ina ujumbe."Utasikia tusipoteze muda kumjadili"Mi nakubaliana nawe Willy ipo haja ya kuangalia kauli zao kwa jicho la tatu.Kwani hoja zao walizotoa huyo Nassari na Shibuda pamoja na majibu yanayotolewa na wahusika siyo mazuri kabisa wengine wanapenda kushabikia hoja zenye ukakasi.Mi nasema ingawa hoja ya Nassari inachunguzwa lakini haikuwa nzuri pia hata majibu ya hoja za Shibuda za kuutaka Urais kupitia CDM na majibu aliyopata kutoka BAVICHA hayakuwa mazuri kwani inaonekana ukitaka kugombana na vigogo wa chadema basi we sema unautaka urais utashambuliwa sana lakini wakati huo huo hawasemi nani wanamtaka katika nafasi hiyo angalia alivyoshambuliwa Mh.Zitto tena kwa maneno meusi kabisa.Mi naogopa sana kusemea ukanda,ukabila au udini kwani naamini nikiamini hivyo nitakuwa mvivu wa kufikiri ni vema hizi kauli zikaangaliwa kwa kina kwani zina madhara na madhara yake hayaonekani hapo hapo ni kwa baadaye.
   
 14. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #14
  May 20, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  "CHADEMA started as a docile NGO" - Kitila Mkumbo. Sasa jiulize ni lini CHADEMA iliacha kuwa NGO? Vile vi element ambavyo vilimfanya msomi Kitila kuiona CHADEMA kama NGO vimeisha? Labda Shibuda na mtu mwingine anayetaka kupata "umuhimu" ndani ya CHADEMA anachopaswa kufanya ni kumuona Kitila kwa ushauri. By the way, Kitila ndio consultant wa sera za CHADEMA.
   
 15. CHIETH

  CHIETH Senior Member

  #15
  May 20, 2012
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimependa Jibu lako kwa Mtoto wa Malecela. Unajua Wiliam hataki kuweka wazi tatizo la shibuda na badala yake anaona tatizo la CDM tu. CCM kuna matatizo mengi lakini kwake yeye haoni anaona tu ya CDM. This is not a good analysis especially to him(Wiliam) who I think is well educated outside Tanznia.
   
 16. F

  FredKavishe Verified User

  #16
  May 20, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,090
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nilikua naimani sana CDM lakini sasa imani inaanza kupungua kwao sidhani kama wamejipanga kuchukua nadhani hawako tayari kuchukua nchi 2015 wamekua wasemaji sana kutokutekeleza.

  Ilani ya CDM mwaka 2015 ilikua na sera za majimbo nilitegemea baada ya kukosa uraisi utendaji wa chama ungegawanya kimajimbo tuone ufanisi wa hili jambo lakini wameendelea na mfumo wa CCM wakuwa na wenyekiti wa Mkoa kama mnahubiri majimbo simamieni sera yenu ya majimbo sasa mpaka sasa ni Miaka Miwili na Nusu inabaki mingine jk amalize muda wake.
  Mmefanye Mikutano mingapi kuhubiri hii sera ya majimbo hakika nawaambia CCM wataitumia hii sera yenu kwamba mnataka kuvunja amani kwa sababu hawamuonyeshi nia kuitekeleza mmekua wasemaji kama CCM kuliko watendaji.
  Toka tumemaliza Uchaguzi wa mwaka 2010 CDM nahisi mmefanya mikutano si chini ya 100 je wapi mliongolea hii sera majimbo kama sio Nyimbo zile zile za kila siku.
  Muda wa kufanya siasa za kisasa sasa si kila siku kupita njia za CCM wanazopita boresheni siasa zenu ziwe za kisasa jielezeni nyie mtafanya nn kipya baada ya Sytem ya CCM kufail.

  CDM wanapinga matumizi makubwa ya CCM je niambie hapa uchaguzi wa Arumeru tulitumia Sh ngapi?tunadanganya watu au vipi tunapita njia zile zile za CCM lakini nyuma ya pazia.

  Wanawake ndo wapiga kura wakubwa tuna wabunge wa viti maalumu zaidi ya 20 wamefanya nn kuongoza imani ya wanawake kwa CDM.nilisikia Tamko moja tu la umoja wa wanawake Mwenyekiti wao kama hayupo hivi mnashindwa kupita mavyuoni kuitisha mikutano na wanakina dada mavyuoni mmelala sana wanawake CDM.
  Jingine kulikua na umuhimu gani cecial pareso sijui kupokea na maandamano makubwa na kuaanza kujisifia sijui atasomesha wangapi ndani ya jimbo la karatu mnaitumia Mikutano hiyo baada ya kujenga chama mnabomoa tu.

  Suala la shibuda sasa kulikua na haja gani heche kumjibu Shibuda angekaa kimya angefanya nn o angipungikiwa nn sasa Shibuda ameanza kuwachimba.Mengine mnajitakiwa wenyewe hakika nawaambia Shibuda asifukuzwe kwenye chama abaki CDM tena muanze kumtumia mnamtenga sana mumtumie kuimaliza CCM.

  Mikatano mingi ya CDM now mnajikita kutambulisha watu kutoka CCM hii inamaliza muda tu jikiteni kwenye sera hao kina ole millya sijui watambulishwe kwenye media tu kwa kikao basi sasa hadi mambo ya kimla mnafanya jukaani hii ni kupoteza muda jikiteni kwenye hoja na sera zenu tuelezeni jinsi mtakavyoboresha uchumi hayo mambo ya kimla si maala pake hapo.

  Kuna jambo jingine baya sana siku hizi watu wanaokaa kwenye Jukwaa kuu wote wanataka wazungumze ndo yale ya nassari yanakuja watu hawajiandaa kuzungumza kwahiyo wanafikiria chochote kitakachotoka Mdomoni.
  Sasa kwenye vikao kila mtu anataka kuzungumza tujipange watu wa 4 ndo wawe wanatoa hoja.

  Shime Chadema ijigawe kimajimbo sasa tukielekea uchaguzi wa serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu.

  Majanikv
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  May 20, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kwenye Ilani ya CDM ya 2010-2015 ni wapi inaelezea sera ya majimbo au kuweka ahadi kuwa ingeunda majimbo kama ingeshinda?
   
 18. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #18
  May 20, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hivi ni kweli 95% ya wabunge wa kupendelewa wa chadema ni kutoka kanda ya kaskazini?

  Kama kweli, ni vipi utawafananisha na CCM? hiyo si ndio majimbo and kanda at its best?
   
 19. F

  FredKavishe Verified User

  #19
  May 20, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,090
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mkuu lakini najua CDM wana sera ya majimbo wangeanza kuiapply now mbona wanachelewa utekelezaji ina maana mfumo wao wa uongozi ungebadilika na kuwa wa majimbo
   
 20. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #20
  May 20, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  po mkuu umesomeka.
  na jingine juzi nilikuwa katika kata ya kimochi kijiji cha mdawi kulikuwa na mkutano wa kata kuhamia chadema ila nilichokiona ni kama chadema haijajipanga vya kutosha,msoma risala sijui hata darasa la saba kama kamaliza anasomakama anajifunza aeiou,
  chadema ijipange kwa sasa ndilo tumaini pekee kwa watanzania na kama haitabadilika watanzania wataangalia pengine.
   
Loading...