Umejaribu kuandika ukweli mdogo sana lakini umeupamba na uongo mwingi sana na hivyo umeharibu kila kitu katika hoja yako.
Kwa mfano:
1/Ni kweli kuna haja ya CHADEMA kujieneza kwa njia mbali mbali lakini si kweli kuwa wanachokifanya CHADEMA kwa sasa hakina Faida. Why? Matunda yake yanaonekana wazi wazi tena sasa na wakati huo huo CCM wanahaha usiku na mchana tena bila mafanikio kutaka kuithibiti CHADEMA lakini wapi. Too late!!!
2/Mpaka sasa sijaona watu ndani ya CCM wenye uwezo wa kupambana na hoja za CHADEMA. Secretarieti mpya ya CCM ya sasa ambayo ndio timu ya CCM 2015 ina watu dhaifu sana kisiasa(Wachovu, wachafu, waoga, wapuuzi), kwa mfano watu kama Kinana, Mwigulu, Migiro, Nape, Khatibu, Meghji, Mangula, Kikwete nk. Ni nani katika hao ana ubavu na uhalali wa kwenda kuwaambia wananchi waendelee kuiamini CCM?
3/Si kweli hata kidogo kuwa wananchi hawatakuwa na Imani na CHADEMA 2015.
Ni juzi tu uchaguzi wa kata 22 za udiwani umefanyika, kampeni zake na matokeo yake yanaweza kutumika kama 'Pilot Study' ya 2015, swali kwanini CHADEMA wamekuwa na matokeo mazuri ya kiujumla kama hawaaminiwi na watanzania?
4/Japokuwa ni kweli kuna haja ya CHADEMA kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa wakina mama na wazee, Why? Ni wapiga kura wazuri sana kwenye uchaguzi.
Lakini bado ukweli unabaki pale pale kuwa uchaguzi mkuu 2015 utaamuliwa na vijana. Why? Ndio waliokuwa wengi katika jamii na hivyo ndio wenye uchawishi mkubwa. But good thing kwa CHADEMA ni kwamba vijana wengi ni wapenzi wakubwa sana wa CHADEMA.