CHADEMA bado mno Kupambana na CCM

CHADEMA bado mno Kupambana na CCM

William,

inawezekana umeandika kwa jazba au kishabiki tu au hata kwa kutojua, hiyo ndiyo siasa unaangali upenyo unaoweza kuwafanya wananchi wakuelewe na unasimamia hapo na kwa Chadema naona wanafanikiwa, kila likitokea tatizo wanawaeleza wananchi na wananchi wanauona ukweli, huwezi kuwaeleza wanachi maneno tu bila kuwapa mifano. Ufisadi wanona, ndio chanzo cha huduma duni za kijamii, wanafunzi kufeli ni kwa sababu ya uongozi bomu! na mambo mengine mengi!

Kuhusu waziri kujiuzuru huku ni kuwajibika na kwa mtu mwenye busara matokeo mabovu kabisa miaka mitatu mfululizo anaachia ngazi mwenyewe bila hata kusubiri, na hapa ndipo tungepata mahala pa kuanzia kutatua tatizo. waziri amekuwepo kwa muda sasa kwenye wizara hiyo na matokeo mabovu sana katika nchi hii yametokea kipindi chake hivyo hana mbinu za kutatua matatizo ingawa anayajua na dawa yake ni yeye kupisha mtu mwingine mwenye uwezo;

Pia nikukumbushe kwamba Chadema wanafanya uchunguzi na utafiti wa mambo mengi sana na ndio maana wanaibua uvundo mwingi sana serikalini na ndiyo sababu ya nyie kuichukia zaidi Chadema kuliko vyama vingine vyote; wanatafiti wanakuja na tafiti makini bungeni mnazizima! wakienda kuwaeleza wananchi wenye nchi yao mnatumia polisi kuwazima, sasa unataka watumie mbunu zipi!?

Tusiwe Majuha jamani nchi yetu nzuri inateketea chini ya utawala wa ccm na sisi tumekaa kimya tu tukiangalia! kisa mimi ninapata kila kitu sina tatizo! huu ni ubinafsi tu! mamilioni ya watanzania wanaishi kwa shida na taabu wakati nchi yao tajiri sana, nchi inashindwa kutoa huduma bora za kijamii kwa wananchi wake! tukataeni mambo haya ndugu zangu! msikubali kutumiwa na hawa wafujaji wa mali za umma! hivi umeshaona hawa watu wanavyofuja mali za nchi hii! na hapa hatuongelei hao waliojuu tu hata waliochini ni tatizo, 60% ya fedha za serikali zinatumiwa kwa mambo ya hovyo kabisa kwa sababu hakuna mfumo mzuri wa kusimamia fedha na hakuna uwajibikaji, kila kitu ni chini ya kiwango, hatuko makini kuhakikisha fedha yetu inafanya kazi kwa tija na kwa viwango! tunafanya mizaha tu! kila mtu anapiga dili tu! tutabaki nyuma sana!

TUSIWE WABINAFSI TUAMKE TUTETEE JIMII NZIMA YA WATANZANIA.

ujumbe mzuri Je unamfikiaje na mtu asiyejua Jamii folumu na asiyehudhuria mikutano ya hadhara akiamini siasa ni ulongo.
Mbinu duni za kujieneza hizi
 
ujumbe mzuri Je unamfikiaje na mtu asiyejua Jamii folumu na asiyehudhuria mikutano ya hadhara akiamini siasa ni ulongo.
Mbinu duni za kujieneza hizi

Wewe na mimi tunatakiwa kuifanya kazi hii, mimi kila ninapokuwa huwa najitahidi kuwaelimisha wale wasielewa umuhimu wa kufanya mabadiliko na huwa nafanikiwa kubadili mitazamo ya watu! waeleze jinsi ya umuhimu wa kura na kupiga kura! waelimishe wale waliokariri hata tukiwapa chadema mambo ni yaleyale! wabadili mtizamo huo, hujachelewa anza leo elimisha watu watano tu kila siku sehemu yeyote uwapo, anza na nyumbani kwako, ndugu wako, jirani wako, shangazi na wajomba wako vijijini, utakuwa unanza kufanya mageuzi ya kifikra na kupelekea mageuzi ya kisiasa na baadae yatuletee mageuzi kiuchumi! anza sasa anza leo! usiogope!
 
yule mwizi wa meno ya tembo kaenda kuleta wezi waue tembo wetu
 
OMG; Un-commissioned freelance consultants bwana!!!! we acha tu!
 
Ndugu yangu hiki chama uwa hakikosolewi na chama cha Mitume.
45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka 2010 mkoani Arusha � Arusha mjini
 
Ndugu yangu hiki chama uwa hakikosolewi na chama cha Mitume.

Natamani ndg huyu anayejiita Ritz awe anatafuta walau hoja za msingi na kuzizungumzia au atoe hoja za kibinafsi zenye mashiko. Naona kazi yake ni kutetea tu CCM na kubeza CDM hapa jukwaani. Najua unaweza kuwa na mawazo mazuri sana yenye kujenga iwapo utatoka kwenye biases ulizo nazo. Kama ni huyo ninayefikiri kuwa ndiye, basi niko disappointed sana! Kama ni Ritz mwingine yeyote sina tatizo kubwa sana
 
William Mshumbusi,badala ya kuilaumu CHADEMA hebu jifikirie umeifanyia nini nchi yako kulingana na maelezo yako.Inawezekana hata kelele hupigi basi nafuu hata CHADEMA wanapiga kelele kumuamsha mwenye nyumba usingizini.

Unaweza ukadhani kelele zipigwazo na CHADEMA hazina msingi lakini isingekuwa kelele hizo basi hata wewe usingekasirika na kutoa ujumbe wako ili tuujadili.

Kwangu mimi upinzani unaweza ukajengwa na kuamua kwa dhati kabisa kwamba tupunguze nguvu ya serikali kwa kubana nafasi za wabunge nyingi ziende kwa upinzani ili ule ujinga wa serikali wa waliokubali wameshinda utakwisha na yote ya ubadhirifu wa mali ya umma utapungua sababu mhimili mmoja wa kuibana serikali utakuwa na nguvu.Lakini kwenye hili vyama vyote vinapigania vipate rais hatutafika kule tunakoenda.

Sisi sote watanzania( mimi,wewe na yule) bila kujali itikadi ya vyama tunajukumu la kuiwezesha nchi yetu kutowachagua wale wote tunaowaona hawafai kuwa viongozi kwa sababu za wizi wa mali ya umma,udini,uwongo,unyanyasaji.na mengineyo.

hapo kwenye red, upo sahihi, kila mtanzania na ajiulize hilo swali! tutapiga hatua badala ya porojo za kila siku!
 
hapo kwenye red, upo sahihi, kila mtanzania na ajiulize hilo swali! tutapiga hatua badala ya porojo za kila siku!
All in all, mbinu za kuneneza chama siyo effective. Viongozi wasikwepe jukumu kwa kusema eti 'kila mtanzania ajiulize kaifanyia nini nchi' vinginevyo hatuna haja ya kuwa na viongozi. Mikutano ya hadhara sawa ila siyo mwarobaini pekee wa kueneza chama.
 
William Mshumbusi

mkuu mbona nassari alitaka kuwasilisha hoja binafsi kuhusu elimu bungeni mkamzuia?????????
 
Last edited by a moderator:
mmetuchosha sasa always cdm, cdm.vyama vya siasa vipo 20 na zaidi why cdm, cdm kila mda aaaahhhhhhhhh
Chukulia mfano: watu 20 mnamfukuza mwizi, mmoja wenu ana mbio na uwezo wa kumkamata yule mwizi lakin kila akikaribia kumkamata mwizi anapunguza mwendo badala yake anazidisha kelele mwizi, mwizi, mwizi...! Katika hali hiyo ni rahisi kuhisi kuwa huyo na anayemfukuza mwizi na yule mwizi mwenyewe lao moja!
 
kweli vyama uvielewi,una chama sawa,lakini na ww pia ujielewi,umepoteza dira ujui mbele ni wapi na nyuma ni wapi,nchi hii ina vyama zaidi ya 17 ila ww mbaya wako ni chadema tu?bahati mbaya ata hiyo tread yako aijakaa sawa ni vizuri nawe pia ufanye utafiti kabla ya kuleta pumba zako

Kaka mtoa thread mbona amechanganua kitaalam kabisa au hujamuelewa? au hutaki kukubali ukweli? au na wewe ni mbumbumbu. Mbona hata wewe hujasema chochote kuhusu thread hiyo? anachosema mtoa mada ni upembuzi yakinifu wa mambo ya kitaifa ili tuwaone CHADEMA kama chama chenye muelekeo na uelewa wa mambo yanayolisumbua taifa. Tatizo ndio hilo la kukurupukia tu leo kuna matokeo mabaya mnashinikiza waziri ajiuzulu. mkumbuke waziri kakaa wizarani si zaidi ya miaka 3. Structural problems zilikuwepo pale wizarani miaka nenda rudi. yeye si malaika na hana uwezo wa ki mungu wa kutatua matatizo ya wizara OVERNIGHT kama unavyotaka kuaminisha Watanzania. Ndipo hapo tunaposema upeo wa CHADEMA katika kuyaendea mambo ya kitaifa ni mdogo. Na hii inanipa shaka juu ya maandalizi yao ya kwenda Ikulu, kwani watu wengi sasa mmewafumbua macho kwamba CHADEMA ni weupe sana katika uelewa ikiwa mwenendo ndio huu. Jitokezeni kama watu waelewa na mjenge hoja mukadam kabisa vinginevyo CHADEMA itakuwa ni chama cha Matukio tu.
 
Msimlaumu hayo ni mawazo yake. Siku zote mvivu ni mtu mwepesi kupokeas jambo lolote ili mradi tu lisimfikirishe sana. Hata Mkapa ni CCM ileile ndio maana ni lazima chama kibadilike. Tusubiri kidogo tu Tutaenda kuomba ushauri Rwanda jinsi ya kuiendeleza nchi yetu. Aibu!!!!
 
Nchi hii imejaa mapoyoyo kweli kweli. Unakiambia chama ambacho kiliuza sera za ilani yake na kuporwa ushindi ndo kifanye utafiti ili Maccm wao wabaki wasafirisha meno ya tembo tu!!

Mawazo Mgando, hujui kama utafiti unalindwa kisheria na hatimiliki yake? Poyoyo wa kwanza ni wewe inaelekea kama umekwenda shule basi ulifanya mtihani wa multiple choice na bahati ilikuwa yako ukabahatisha. Kura ziliporwa wapi? mbona proportion ya Wabunge ndio indicator mzuri kwa siasa za Tanzania? Tulizana jiulize mko poyoyos wangapi?
 
unashangaza kweli badala ya kuwa na hasira na chama chako ambacho ndo kimefanya upuuzi huo, unakuwa na hasira na chadema ambayo inasema ukweli wa kilichotokea.

Kama unasema elimu ilianza kushuka tokea tokea mkapa, ila kilichotokea sasa ni udhibiti wa wizi wa mitihani....unataka kutuaminisha kuwa udhibiti ulukuwa unaongezeka kwa asilimia kadhaa kila mwaka tokea aingie kikwete maana pia ufaulu nao ulikuwa unashuka kila mwaka tokea aingie Kikwete.
usiandike mambo kwa sababu ya hasira zako na chadema, andika kwa sababu una sababu.
 
Watanzania tukubali kukosolewa na kukosoana.

Hili suala la elimu limeshasemwa miaka mingi na kulalamikiwa hata kwa data lakini bahati mbaya hakuna anayesikiliza. Kwa sababu ya mfumo wetu hakuna anayeshituka wala kuwajibika. Wahusika wakiambiwa wanadharau tena wakati mwingine kwa kejeli na matusi. Na siyo eneo hili la elimu tu angalia hata eneo la afya si siku nyingi zilizopita wadau walitoa malalamiko Yao kwa kueleza kwa kina matatizo yaliyo katika sekta hiyo.

Wenye akili walielewa lakini tena mfumo wetu ukainigiza siasa na badala ya kutatua tatizo wakatupa lawama kwa wadau nasi tukashangilia. Bahati nzuri au mbaya huko hakuna kufeli kutakakoonekana Bali watu wanakufa na tunasema 'mapenzi ya mungu'. Siku zinaenda.

Ninashangaa watu wanaposema eti tufanye utafiti! Ni utafiti gani ambao haujafanyika mpaka kuna vyama vya siasa katika Ilani zao walisjasema wanataka kufumua mfumo mzima wa elimu (CUF na CHADEMA). Hatutaweza kuendelea Kama hatutabadilisha jinsi tunavyofanya mambo yetu na pia watu kuwajibika katika maeneo Yao. Watu wanakufa katika eneo Lako kwa uzembe unaambiwa kuwajibika unasema siwezi kuwajibika kwa sababu sikuwaua Mimi! Ungekuwa umewaua wewe tungekupeleka jela lakini tunakuomba tu uwajibike ili kuonyesha kujali.
 
William Mshumbusi

Sijui ni muhaya kweli au wa kuchonga umeandika kwamba wafanye utafiti kabla tukio halijatokea,watafanyaje utafiti wakati ofisi imekaliwa na watu zaidi ya miaka 50 sasa utaingiaje kwanza kuanza huo utafiti? Zaidi ya miaka hiyo nchi haina mitaala ya kufundishia wakiambiwa wanazomea,madhara ya kuzomea Mungu kawaonyesha nusu ya watoto wamefeli,badala ya kuwekeza kqenye elimu wao kia siku safari kwenda kukopa wakati tunauwezo wa kujitosheleza kwa raslimali tullizzonazo,

Nashangaa mtu unapotoa mawazo duni kama hayo na tayari unahukumu kwamba ni chama dhaifu kwani wamepewa dola wakashindwa kurekebisha hali hiyo? Wameng'ang'ania nchi lakini wanashindwa kila siku wanalalamika tu kulalamika si suluhisho la kutatua matatizo uliyo nayo,wanaona mikutano wanalalamika wamechanganyikiwa hatimae upinzani utachukua nchi hii hata kama urais utachukuliwa na Ccm ila wajiandae kuwa chama cha upinzani bungeni 2015
 
Last edited by a moderator:
Na mimi pia sina chama, chama changu kutafuta ukweli.

CHADEMA ina mapungufu mengi tu, mengi nimeyasema humu.

Hata leo nimehoji kauli zinazoripotiwa kutoka kwa Tundu Lissu, one of the best legal minds CHADEMA has, kuhusu lawama za uongozi wa mkoa.This was tacky and immature in my view.

Nimeuliza policy strategy ya CHADEMA kuukabili mfumuko wa bei sijapata mpaka leo.

Nasema haya ili usifikiri kwamba mimi ni mkereketwa wa CHADEMA mwenye bias.

Lakini swali langu ni.

Unaposema.

Na wakati huo wote huja na jibu rahisi tu: Fulani ajiuzuru! Kana kwamba yeye ndiye kaja na mkosi huo.

Unawatendea haki kweli? Au una dumb down the narrative even further?

Hivi kweli CHADEMA wote habari yao yoote ndo inaishia hapo kwenye kutaka watu wajiuzulu tu?

Angalia katika kutaka kuwafanya CHADEMA wakose credibility usipoteze credibility wewe mwenyewe.
 
Mwongoza njia ni form vi leaver unategemea nini. Hayo ndo maarifa ya form VI mwongoza njia aliyewafanya vijana wasomi humo Chapman kuwa mandondocha wake
 
chadema inapigia kelele matatizo yaliyoibuliwa tayari hivyo nahofia uwezo wake wa kufanya kazi kisayansi na uchunguzi.
Nataka wabaini vyanzo vya matatizo

R,Mushumbusi masalia au masabuni naomba unijibu swali hili
Nini maana ya upinzani,ukishaelewa maana ya upinzani ndipo utakapojijibu hayo maswali yasiyo na miguu lakini kama haujui maana ya upinzani hauqezi kuelewa make kama umesoma ni chini ya mti
Chadema kupigia kelele tafiti ambazo zimeshaibuliwa inawezekana maana hizt tafiti zimetumia pesa za walala hoi ni haki ya upinzani kupigia kelele wewe unataka watulie ni upumbavu usiopimika haujui unachokiandika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom