CHADEMA bado mno Kupambana na CCM

Nimejaribu kufuatilia malumbano yaliyopo kati ya Chadema na vyama vingine SIO CCM. Nime gundua CHADEMA bado haijafiliwa kiwango cha kuongoza nchi. Hii ni pamoja na mambo yafuatayo:-
1. Haija jiimarisha katika mikoa mingi hapa nchini wakati wenzao CCM wana office karibia kila kijiji hapa nchini.
2. Wanaleta mkanganyiko kwenye hoja ya Muungano. pia hawana nguvu yoyote Zanzibar.
3. Hawana muda wa kufundisha viongozi. viongozi waliochadema wote wanamafundisho kutoka CCM. na hii inakiathili sana chama hiki. kwasababu mtu akitoka chama kingine anaingia moja kwa moja kwenye uongozi.
4. Wanafuatilia ugomvi mdogo mdogo ambao hauna tija. mfano kuita NCCR kuwa ni CCM B. hii haina tija yoyote kwa watu wenye mpango wa kuongoza nchi.
 
Eti unatumia kigezo cha CCM kuwa na ofisi kila kijiji kwaajili ya kuidhohofisha CHADEMA, wewe unaijua CCM ilikoanzia?

CCM imekaa kutawala kipindi cha mfumo wa chama kimoja, TAA ilizaa TANU afu ndo ikazaliwa CCM sasa unataka kusema nini hapo, CCM haiwez kujilinganisha na CHADEMA hata mara moja.

CHADEMA wamepiga hatua kubwa sana kwa siasa za hapa Tz huwez kuilinganisha CHADEMA na CCM iliyoshika dola miaka zaidi ya 50.
 
Eti ofisi' ama kweli we pimbi, wewe unaijug CCM ilikoanzia? CCM imekaa kutawala kipindi cha mfumo wa chama kimoja, TAA ilizaa TANU afu ndo ikazaliwa CCM sasa unataka kusema nini hapo, CCM haiwez kujilinganisha na CHADEMA hata mara moja. CDM wamepiga hatua kubwa sana kwa siasa za hapa Tz huwez kuilinganisha CDM na CCM iliyoshika dola miaka zaidi ya 50 afu ukajiona unazo akili.
 
watanzania wa leo ni tofauti na wa jana hivyo ccm isitegemee kushinda kirasi kama unavyofikiria wewe. wananchi wa vijijini unaowasema ni waelewa mno.
 
Hizi ndizo kauli za wasichana wanaobishana sokoni kuhusu mvulana yupi ni mzuri. Na ccm imeishaujua ujinga wa watanzania na ndio maana inawatongoza na inapowapata inawatumia ipasavyo.

Ccm inawahadaa watanzania mithili ya mvulana anayemtafuta msichana!!! Inawatongoza kwa vitisheti vya njano na vikofia vya kijani; Inawapa lifti; inawalisha wali kuku; inawatumbuiza kwa taarabu; inawaahidi maisha bora na kisha inawahonga elfu tano!! Kwa ulaini wananchi wanakubali kufanya mapenzi na ccm. Wanapewa mimba. Wanazaa ufukara na kisha ccm inawatelekeza kwa maisha duni!

Nionavyo mimi:
Watanzania wakiteseka na mazingaombwe ya ugumu wa maisha ni sawa tu!! Ni haki yao!! Waendelee tu kutaabika kwa kuwa dhiki, mahangaiko na ufukara wanavitaka wenyewe!!

Ukweli ndio unaomuweka mtu huru. Mimi sio Muumini wa chama chochote. Lakini kusema kweli CHADEMA bado ni chama kichanga. CCM wame boronga mambo mengi lakini mpaka leo hii hakuna chama kilichokomaa kiasi cha kushika nchi. So hatuna option yoyote isipokuwa bado CCM kiasi fulani ina sifa. Au mnasemaje?
 
Ni kama akili yako haina akili vile! Baki na mawazo hayo hayo mpaka safina itakapofungwa lango, kutakuwa na kilio cha kusaga MENO. Endelea na dharau zako, tuache tunaomwamini Nuhu kuwa ameagizwa na Mungu.
 

Kumbuka chadema inaitaji ushindi wa 80% kuchukua nchi wakati CCM inaitaji 30% tu. Yani chadema bado sana

Ningekubaliana na wewe kama ungesema wewe binafsi hutaki CDM ichukue nchi 2012. Takwimu zako hazina viwango, angalau maelezo ya utangulizi juu ya takwimu zako yangetia uziro hoja yako
 
Mbinu za CHADEMA kujieneza haziridhishi na inaonekana wazi hakifanyii utafiti matatizo yaliyopo nchini na matatizo makubwa yaliyofichika.

Bali kuja kushinikiza maamuzi juu matokeo ya matokeo ya tafiti au taarifa zinazotolewa na vyombo vya selikali zinazoonesha madhaifu ya sekta fulani mifano:

1. Matokeo mabaya darasa la saba na form four
2. Taarifa za mkaguzi na mzibiti wa fedha
3. Migao ya umeme
4. Migomo ya wafanyakazi
5. Migogoro ya kidini inayoendelea

Na wakati huo wote huja na jibu rahisi tu: Fulani ajiuzuru! Kana kwamba yeye ndiye kaja na mkosi huo.

Mimi sina chama kwani vyote sivielewielewi.

Swali:
Je, CHADEMA kwanini isifanye tafiti. Action reserch kujua matazizo kwenye sekta hizo kabla madhara hayajatokea na kushinikiza mabadiliko ya kisela mfanö- Elimu, kunawizi mkubwa wa mitihani ya darasa la saba wa wazi na usiofichika ambao unadumaza wanafunzi sana na kilichotokea mwaka jana ni kudhibiti wizi tu ila elimu ni mbooovu toka enzi za Mkapa.

Mabadiliko ya mtaala yaliyoacha walimu nyuma na kutofahamu si tu dhana hata maana ya neno muhamo wa luwaza.

Upungufu mkubwa wa vitabu na vitabu dhaifu.
Vyuo vya ualimu binafsi na vyuo vikuu vinavyotoa walimu wasio na sifa
Kufutwa kwa mitihani
Muamko duni wa elimu kwa wazazi na walezi
Usimamizi na uongozi mbaya wa sekta zote za uma na si ualimu pekee
Kupuuzwa kwa madai na haki za walimu
Ukosefu wa vitabu na vifaa vya kufundisha na kujifunzia
Mazingira duni ya kufundishia
Njaa na umasikini
Posho kubwa za wabunge na wanasiasa ufisadi na matumizi mabaya ya fedha za uma na miradi zinavyoshusha uzalendo kwa raia wa kawaida kama mwalimu askari nesi na mahakimu
Ukosefu wa semina na makongamano ya kutatua na kushugulikia changamoto za kielimu na kubadilishana uzoefu
Umeme...

Yapo kama tisini hivi, ila ntawachosha. Je, kwanini wasije na tafiti za kina sio kuparamia ripoti zilizoandaliwa tayari.

Nina hasira mie basi tu ila sawa CHADEMA ni Chama dhaifu saana ila kwa Tanzania ni bora kwani "KWENYE VIPOFU MWENYE JICHO MMOJA MFALME"
 
Ndugu yangu hiki chama uwa hakikosolewi na chama cha Mitume.
 
Kwa kweli hilo la semina inabidi viongozi kaangalia. Bila semina chama hakitaendelea. Kwa hiyo Mbowe na Slaa muuangalie hilo swala la semina kwa viongozi.
 
Unamaanisha kwamba CCM ambayo ni Chama Tawala haiwezi lolote hivyo Chadema ndio wanaweza kufanya hizo kazi au?Kama Ndivo hivo safi Kabisa 2015 Ichague hayo yote yataisha.Magamba ziiiiiiiiiiigh ziiiiiiiiiigh oooooooohhhhhhh.
 
kweli vyama uvielewi,una chama sawa,lakini na ww pia ujielewi,umepoteza dira ujui mbele ni wapi na nyuma ni wapi,nchi hii ina vyama zaidi ya 17 ila ww mbaya wako ni chadema tu?bahati mbaya ata hiyo tread yako aijakaa sawa ni vizuri nawe pia ufanye utafiti kabla ya kuleta pumba zako
 
Kama hakutakuwa na uwajibishwaji kwa mawaziri, usitegemee ufanisi wa hayo matatizo yote uliyoyaorodhesha.watachapa tuu usingizi na kubakia kutengeneza tuu madili ya hela tuu.
 
Nchi hii imejaa mapoyoyo kweli kweli. Unakiambia chama ambacho kiliuza sera za ilani yake na kuporwa ushindi ndo kifanye utafiti ili Maccm wao wabaki wasafirisha meno ya tembo tu!!
 
Back
Top Bottom