CHADEMA bado mno Kupambana na CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CHADEMA bado mno Kupambana na CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by William Mshumbusi, Jun 7, 2012.

 1. William Mshumbusi

  William Mshumbusi JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 874
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Siwezi kupinga kuwa CHADEMA sasa ndio chama chenye wanasiasa wazalendo na uwezo mkubwa.

  Pia ni chama kilipata nguvu sana kwa makundi ya Wasomi, Vyuoni na Vijana wa mjini wasomi na Watumishi wa uma.

  Ila kuchukua nchi 2015 kwa kasi hii bado sana kwa CCM. Wakati wote wanachadema wanajipa moyo ila safari kasi haitoshi.

  CCM Mbali na kujivunia tume ya uchaguzi, Polisi na sasa mahakama kuhakikisha wanashinda bado wanakundi kubwa linalowaunga mkono.

  1.'WAJINGA' wasiojua kusoma. Waliko vijijini. Nilisimamia uchaguzi 2010 hawa ni zaidi 39% Tabora vijijini hii ni amini usiamini. Kila asiyejua kusoma ni CCM.

  2. Kundi la wenye elimu ndogo ya kusoma na kuandika tu. Wepesi kurubunika na nyimbo nzuri za komba. Amani na utulivu na waoga wa mabadiliko

  3. Kundi la wanawake ambao mantiki yao ya kupenda CCM ama woga wa mabadiliko. Au huruma ya kumtoa kiongozi aliyopo au Wakiamini wanasiasa wote waongo tu. Kama wanaume wanavyowadanganya kilasiku na kuwachezea tu. Watu hawa wanatakiwa kuanza kujihurumia wao kwanza na si viongozi wenye magari mazuri.

  4.wasijiojiamini ambao hawaamini karatasi zinaweza kuondoa selikali madarakani. Watu hawa wako CCM kwa woga na ni wengi mno na wengi huwa hawapigi kura.

  Pili CCM Kutumia wanamziki maarufu kama Chege, Diamond, Bushoke, Ngwea na Marlow huwa kunawaongezea kura za mabinti.

  Umasikini na Njaa bado ni donda linawafanya watanzania wahongeke kirahisi. Kama mitambo ya Dowansi sasa Simbion imewashwa na inaizua Tanesco umeme kwa bei ghali sipati picha Rostamu na Rowasa atakuwa na tririon kumi na ngapi mwaka 2015. Na watashindwaje kuchukua nchi na kutupangia wabunge wawatakao.

  Kwa ujumla CHADEMA Wanakazi kwelikweli. Ila ushauri wangu kwao Inabidi wazindue kampeni za mtu na mtu mtaa kwa mtaa. Tena waanze ufunguzi na uimalishaji matawi vyuovikuu. Mbona CCM wanayo. Wawaandae wasomi hawa kugombea udiwani kwani ni kiungo muhimu kwa madaraka. Kwani halmashauri zinafedha zinaibwa tu na wakuu wa idara. Diwani anaweza kulipwa mpaka laki 6 kwa mwezi tukidhamilia. Pili naamini kutakuwa na muhitimu wa chuo kikuu kila kata hivyo udiwani kuwa ajira kwani vyuo ni vingi na hakuna ongezeko kubwa la nafasi za ajira'

  Walimu wa sekondari hasa za kata watumie ata sekunde 5 kwenye kipindi kuweka hisia zao za madiliko kwa wanafunzi ata kwa kuonesha vidole 2, kuisifu chadema kwa neno moja tu au kuwapa machungu jinsi nchi ilivyowatenga

  Kumbuka chadema inaitaji ushindi wa 80% kuchukua nchi wakati CCM inaitaji 30% tu. Yani chadema bado sana
   
 2. escober

  escober JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 391
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  so what?ina maana gani serikali kutumia hela ya wananchi kugharamia uchaguzi ambao tayari mshindi anafahamika kwa hiyo kwa mtazamo wako inabidi CCM itangazwe mtawala wa kudumu wa Tanzania
   
 3. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  nimekusomaaaa ukasomeka bana...

  kinachofanyika sasa na chama ndicho hasa unachokipendekeza hapa...operation hizi za sasa lengo kuu ni kukishusha chama toka kinondoni mpaka vijijini kule waliko wananchi wa kawaida na sio kampaneni

  CCM hili linawaumiza sana kwani ujinga wa wanachi ndo imekua LOOPE HOLE yao...
  kwa sasa CHADEMA kimejikita zaidi katika kueneza elimu ya umma na kushusha chama kwa levo ya matawi na nina imani matokeo yatakua mazuri sana
   
 4. m

  mamajack JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Sio sababu za msingi any more, wewe kama ulisimamia uchaguzu, nasikia mlipewa 60000 kukibeba cha cha ccm, wasiojia kusoma wote mlikuwa mkiwaelekeza kuchagua rangi ya kijani, ila madhara mmeyaona.

  Kunawatu wengu sana wanajuta kwa makosa hayo, na ndo kwanza mwaka wa oili huu mambo yako hivi, wote mlioshirikwa kwa namna moja au nyingine kuleta ushindi wa nyinyiemu na ambao hamkupiga kira, ndio mmetufanya tuwe hapa tulipo.

  Maisha ni magumu sana, watu wanagawana mali za umma bila uoga wowte, huduma za jamii zimekuwa ovyo,kosa la siku moja nimeg'halimu watu wengi na wakati mwingine hata kupoteza maisha ya wapendwa wetu sababu ya kukosa huduma.

  Hiyo 60000 ilisaidia nini,au hizo kanga kaofa na skafu.

  Tujifunze kutokana na makosa.
   
 5. K

  Kipimbwe JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2012
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Imeandikwa asamehewe hajui atendalo,no difference with his fellow Shibu..
   
 6. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  We si ndo Yule wa Uzi wa DR. Slaa na Lema kuwania Uraisi, baada ya kutopata ulichotaka katika Uzi huo umekuja kivingine. Tatizo uwezo mdogo wa kujenga hoja unazinyima mashiko propaganda zako. Kajipange tena.
   
 7. Chaimaharage

  Chaimaharage JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Haloo! unajua unacho kiandika, au umekurupuka usingizini na kutuletea thread zisizo na mantiki. Utafiti gani uliofanya au umefanywa na nani kuthibitisha unayo yasema? Habari za wasio jua kusoma kuwa ni wanachama wa magamba hiyo ilikuwa 2010. Mwamko watu walionao kipindi chote baada ya hapo unaujua?

  Nakushauri rudi tena ufanye utafiti uje na data mbadala zisizo pungua miezi 6 iliyopita.Huna ushauri wowote wa kuwapa CDM, vichwa vilivyoko pale wana fikiria mile 1000 mbele yako. Hayo mawazo ya kimazoea ya magamba kwamba mwisho wa siku wajinga watawapigia kura subiri 2015.

  KANU walikuwa na fikra kama zako na magamba wakijipa matumaini. Yaliyo wakuta hata wewe uliye poor informed unajua. Kibaya wao walikufa lakini bado wapo..ninyi magamba mtakufa na hata dalili za kama mlikuwepo hazito kuwepo. Najua huamini na utapinga vikali but time will tell.
   
 8. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hayo ni mawazo yako inaonekana unatamani wewe iwe hivyo lakini sio kweli kwamba ndo hivyo ilivyo
   
 9. M

  Mazoea Member

  #9
  Jun 7, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtoa maada inaonekana upo mbali na uchunguzi wako kwa taarifa yako watu wamebadilika na wamechoka na udanganyifu wa magamba kila cku maisha bora wakati huko vijijini watu wanapata taabu hata,shule hakuna na kama zipo walimu na vitu vingine hakuna,hospitali hakuna maji ndo hivyo taabu sasa hata na kutokujua kusoma hata kuona hawaoni.Mimi binasfi nimeshangaa kuona bendela za CHADEMA huko vijijini kwa hiyo hiyo ni dalili za mabadiliko.
   
 10. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #10
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mushumbusi, mchango wako kuelekea mabadiliko 2015 ni upi? Ukishajua kazi iliyo mbele na udhaifu wa wananchi kuhusu mabadiliko basi unayo kazi rahisi, play your part Mushumbusi.
   
 11. F

  Froida JF-Expert Member

  #11
  Jun 7, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Juzi maeneo tisa uchaguzi umefanyika ,upinzani ukazoa maeneo matano CCM manne,vijiji gani unazungumza,Igunga ambako CDM haikuweko 2010 vijijini ndani kabisa walipata kura nyingi tuu ,Arumeru kula nyingi tuu huko chato kati ya vijiji 18 CDM 15 CCM 3,huko Mbeya vijiji 11 CDM 9 CCM 2 unazungumza vijiji vya kuzimuni lakini vya Tanzania wamebadilika zamani au huoni kwenye TV wananchi wanawafungia wenyeviti wao ofisi ,Soma alama za nyakati usiwe Toma
   
 12. William Mshumbusi

  William Mshumbusi JF-Expert Member

  #12
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 874
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Nimeandika huu uzi kuona kilamwanachadema amefanyanini kuimalisha chama. Kwenye Jamii F. Mko vizuri ni hamasa tupu. Je na mtaani kwako ni hivyo? Kumbukeni Walioko JF NI Wengi waelewa. Hawa mbumbumbu wa kitaa mnawasaidiaje?

  Kumbuka mwenye afya hamuhitaji daktari!
   
 13. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #13
  Jun 7, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kama ana akili amakusoma tayari
   
 14. W

  Wakuti JF-Expert Member

  #14
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 379
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Asante kwa kukiri ila naomba ufafanue CHADEMA kuhitaji 80% na CCM 30%? usikate tamaa mapema CCM chama kubwa
   
 15. s

  sawabho JF-Expert Member

  #15
  Jun 7, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Hata Mwndawazimu akiongea msikilize tu, unaweza chukua neno moja na kulifanyia kazi.
   
 16. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #16
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Hii thread inatafutia watu ban ngoja nitimke
   
 17. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #17
  Jun 7, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  nimesema wanajamba maputo post imefutwa why?
   
 18. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #18
  Jun 7, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  na bado wanaendelea kujamba maputo
   
 19. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #19
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Ina maana kule Igunga waliwazidi CDM kwa asilimia 36%. Uongo mbaya sana, na njia ya muong ni fupi sana. Wadanganyeni hao nyinyiem, mnafanya kazi nzuri.
   
 20. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #20
  Jun 7, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Mosi, Hawa wanamziki hakika watatokomea mbali, tulishajadili hoja ya aina hii kuhusu wanamziki wanatumika kipumbavu huku wakilalamika serikali haiupi kipaumbele mziki na hatimiliki.

  Pili, Waliochoka na maisha haya sio wasomi tu, niwauzaa dagaa, wakulima, wamachinga, madalali, wanawake na wanaume; kuchoka uelewe maana yake hakuhiji elimu, hakuna mjinga wala msomi inapofika suala la kuchoka na CCM, wanaohama CCM vijijini unadhani ni maprofesa??? wanachia udiwani vijijini, wanaachia madaraka wilayani ni wananchi wa kawaida wala sio wasomi.

  Tatu, CHADEMA sio kundi la wananchama wa chadema, kwa siasa za tz chadema ni wananchi wa TZ, amini nakwambia.

  Nne, ufahamu namna polisi wanafanya kazi, jifunze sehemu yoyote ambapo mapinduzi yametokea. Kwani polisi wao ndo wameridhika na umasikini? kwani polisi hawana familia na ndugu? kwa wanajeshi hawana ndgu?? wote hao ni kaka na dada zetu, watoto wetu, mama na baba zetu. wao pia wamechoka kuiba kura.
   
Loading...