CHADEMA, anzisheni TV/Radio Station!

CHADEMA, anzisheni TV/Radio Station!

Viongozi CDM msiogope kutuchangisha. Naamini Peoples power TV itapendwa kuliko vituo vingine. Mi nipo tayari kuchangia laki tano kwa maendeleo ya nchi yangu.
 
Nikuuleze wewe, je umetumwa na CCM kupinga mabadiliko Tanzania ? je, hujui mjenga nchi ni mwananchi, na mvunja nchi ni mwana nchi ?

Sasa nikwambia tu ukweli : Hii ni mara ya mwisho kukujibu kwani asiyeelewa maana ya Utaifa na umuhimu wa kuwa na misingi bora ya sheria na zinazolinda rasilimali za taifa kwa manufaa wananchi wake, ni sawa na mamluki.


Najua MAFISADI ndani ya CCM wanapata presha sana kuona CDM inakemea ulaji wao. [/QUOTE
mwana nchi (Viongozi wa CCM)
 
Nenda kanunue sabuni na hiyo hela yako, watanzania wanalia shida wewe unaleta mawazo ya kuchangia chama.

nyie si mnawahonga malaya viti maalumu bungeni? sisi CDM tunafungua TV
 
Mie naona ni wazo zuri wale wote wenye fikra positive watakuwa tayari kujitolea ili TV na radio viwe hewani mapema iwezekanavyo, hao ccm wanavyo maana hata ile TBC sasa ni C(ccm)BC
 
CHADEMA Kuanzisha Televison, Radio au hata Gazeti ni kupoteza mwelekeo na kuijongezea mzigo.?

Waacheni waasisi au wanachama waazishe haya mambo binafsi kama ilivyo gazeti la Tanzania Daima lakini msiazishe kama Chama.

Hi ni njia moja ya kuua vyombo vya habari na ni rahisi sana kuukiuka a maadili ya uandishi wa habari. Chadema isingie kwenye mtego huu.
 
watumie hela zao kurekebisha mambo majimboni mwao , wao walifikiri ubunge ni kucheza sindimba?
 
Heshima mbele Wakuu!!!
Tafadhali Mods Naomba msihamishe hii Topic.


Leo nimeamua niweke maelezo ya kutosha juu ya kuanzisha radio kwa hapa Tanzania, bila kuwa na lugha ya kibiashara badala yake niweke ukweli wote ili mtu aone kabisa mwanzo au mwisho gharama zake zikoje.

Kwanza kabisa kuna makundi matatu ya radio:-


1. Commercial Radio. (Za kibiashara)
2. Public Radio (Radio za watu wenye lengo/dhumuni maalum, kama vile makanisa, mashirika, asasi n.k)
3. Community Radio (Radio za jamii, zinazowekwa kwa manufaa ya jamii, mara nyingi hazitengenezi faida japo imo ndani kwa ndani)

Unaweza kuamua wewe binafsi juu ya radio gani ungependa kuanzisha, inategemeana na wito wako. Gharama juu ya kila kundi la radio zinaweza kutofautiana kulingana na ubora, mfano radio ya jamii inaweza kuwa ya kawaida sana vifaa vya kawaida, lakini ya biashara inahitaji uwe na vifaa vizuri ili uweze kuingia kwenye ushindani. Nisiende mbali sana na lengo wacha nijielekeze kwenye pointi husika:-
Haya ni mambo muhimu kwanza ya kuzingatia unapotaka kufungua au kuanzisha kituo cha radio:-

1. Fanya uchunguzi wa masoko (Ni wapi radio yako uweke, mfano mkoani, wilayani, je kuna ushindani gani kwenye maeneo hayo, je maeneo unayoweka radio yanaweza kuvuta wadhamini wakubwa kama makampuni ya simu na wakaja kudhamini?)

2. Ukishapata eneo. Andika Pusiness Plan+Feasibility Study kwa ajili ya mradi wako. Katika Feasibility Study unatakiwa kuwasiliana na TCRA ili upewe fomu za kuombea leseni ambazo ndizo zinavipengele vizuri vya Feasibility Study utakavyovijana na baada ya hapo unaweza kusubmit hiyo moja kwa moja kama application. Moja na vipengele muhimu katika Feasibility Study ni:-
A: Specific ya vifaa vya radio yako vyote.
B: Memorundum/katiba ya kampuni yako na leseni yake ya usajili.
C: Structure ya uongozi ya radio unayotaka kuianzisha.
D: Financial Statement ya miaka 5 (hii ni muhimu zaidi)
E: Line up ya vipindi vya radio unayotaka kuanzisha.
E: Policy zote za radio.
N.k
3. Kuomba leseni TCRA.
4. Ununuaji wa Vifaa. (Kuna vifa vingine ni mpaka uwasiliane na TCRA ili upewe specification mf. kama STL)
5. Utengenezaji wa Studio.
6. Installations ya vifaa vya studio na transmission site.
7. Mafunzo
8. subiri TCRA wakupe leseni kisha uanze kurusha matangazo ya majaribio ya mieizi 3-6.


Gharama halisi za Radio inayoweza kusikika kuanzia KM 100-150.

1. Transmitter ya Watts 1500 Tshs 12,051,960/=
2. Antena Zake 2dipole Tshs 5,869,200/=
3. STL (Studio to Transmitter Link) Tshs 9,648,000/=
4. Vifaa vyote vya studio 2. (full set) Tshs 25,808,400/=
5. Freight Fee Tshs 3,296,400/=
6. Usajili TCRA Tshs 5,000,000/= na gharama zote zingine zitakazohitajika.
7. Kutengeneza studio Tshs 4,000,000/= (milango, accoustic materialsn.k)
8. Kuendesha mafunzo Tshs 4,000,000/= (kila kitu)
9. Kuandika Feasibility Study Tshs 3,000,000/=
10. Installations ya vifaa vyote na consultancy fee Tshs 7,000,000/=
Jumla Kuu ya vifaa bila local custom charge+mafunzo+TCRA Tshs 79, 673, 960/=

Gharama za uendeshaji kwa mwezi:-

1. Mshahara wa Meneja Tshs 700,000/= kwa kuanzia unamlipia nyumba.
2. Mshahara wafanyakazi 5@250,000/= Tshs 1,250,000/=
3. umeme Tshs 150,000/=
4. Maji 20,000/=
5. Mawasiliano na Internet 100,000/=
6. Usafiri/Mafuta Tshs 200,000/=
7. Stationaries Tshs 100,000/=
8. Pango la nyumba Tshs 250,000/=
9. Ziada Tshs 300,000/=

Jumla Tshs 3,270,000/= makadirio ya wastani.

hivyo jumla kuu ukitaka kuanzisha na kuendesha radio station kwa mwezi 1, inayoenda umbali wa Km 100-150
ni Tshs 82, 943, 960/= bila VAT+customs charge wakati wa kuingiza vifaa nchini.


Faida(Kipato) ya biashara ya Radio.

Utafaidikaje sasa na investiment hii kubwa:

1. Matangazo madogomadogo na muda wa hewani kwa wanaohitaji unaweza kukuingizia mpaka Tshs 10,000,000/= kwa mwezi hasa kama upo mkoani, hapa tayari utakuwa umepata gharama za kuendeshea radio.
2. ukipata wadhamni wakubwa kama makampuni ya simu, mfano ukapata makampuni matatu, kila kampuni kwa mwezi ikakulipa Tshs 3,000,000X3=9,000,000/=
3. Kuna mashirika huwa yanaendesha vipindi na matangazo kwa mwezi minimum Tshs 5,000,000/=

So kama radio yako imepata wadhamini wa hatua zote tatu hizo unaweza kupata mpaka Tshs 24,000,000/= kwa mwezi haya ni makadirio tu, uhalisia unaweza kupunguza au kuongeza mapato haya.

bei ya vifaa vya kurushia matangazo, bei hii ni FOB.

1. Transmitter:TX1000 FM Transmitter (240V only) 25-1100 watts (adjustable) RF output powerTX1000 FM Transmitter (240V only) 25-1100 watts (adjustable) RF output power

Bei yake ni Tshs: 9,639,960/=
Ikifungwa vizuri eneo zuri lisilozungukwa na miinuko inaweza kurusha matangazo kati ya Kilomita 100 mpaka 200.

2. Transmitter: Sielco 2000Watts inauzwa Tshs 18,331,200/= inauwezo wa kurusha matngazo kati ya kilomita 200 mpaka 400 kutegemeana na eneo lilivyo.


3. 2KW 4x114FM antenna with power divider and interconnecting c ables 50m low loss cable. Hii ni antena ya radio yenye antena 4 ya 4 dipole, inauzwa Tshs 9,648,000/=

4. STL (Studio Transmitter Link) STL 398 – 399.9 MHz with 2x9dB yagi antenna and 2x 50m low loss cables antenna clamps and cable clamps (mitambo ya kurusha matangazo kutoka studio mpaka ulipo mnara wako.)

Inauzwa Tshs 9,648,000/=

Bidhaa zote hufika ndani ya wiki 2, ni kutoka Australia na UK.

Tuwasiliane: PM

Kwa maelezo ya kina juu ya kuanzisha radio station fungua hapa: Kuanzisha Radio Station: Gharama halisi za Kuanzisha Radio kwa TZ.

Na mwisho unaweza kuwa unaomba grant kupitia radio yako.

Jaman niishie hapa kwa kusema kwamba, mtu anaweza kukuambia kuanzisha radio kwa Tshs 20,000,000/= kila kitu lakini ukweli zitaongezeka tu ukiweka na gharama zingine, eidha gharama hizi zinaweza kupungua ukiamua kuweka radio ndogo zaidi. niishie hapa, kwa chochote au lolote ni PM kwa details zaidi. Au unaweza kutuandikia email: consultancy@radiotz.com

by Radio Producer: JamiiForum Member
 
Kupiga domo ni kazi rahisi sana kuliko kutenda, Chadema inaishia kilometer 150? tupe hesabu ya coverage ya nchi nzima.
 
Kupiga domo ni kazi rahisi sana kuliko kutenda, Chadema inaishia kilometer 150? tupe hesabu ya coverage ya nchi nzima.
Mpaka sasa wamekufa wangapi kwenye ajari ya gorofo... huku mkandalasi ni mpiga domo wa lumumba.
 
Garama za kampeni za dr slaa za uraisi mwaka jana ilikuwa Biliön 1.8
hapo lazima ujue chadema kinavyodumazwa redio hoi ata kagazeti
 
mkaodarasi kumbe na kutoka kile chama cha yule jamaa anaetengeneza dawa feki za ukimwi? kweli hili ni janga.
 
Ukizoea kula nyama ya mtu hauwezi kuacha,mkandarasi aliona ajifiche kwenye kichaka cha wahuni,mafisadi,wezi wakugushi vyeti akagombea udiwani ili apate ukandarasi,hatimaye ameuwa watu zaidi ya 31.munamshitaki kwakosalipi au mungoje upepo upite basi? maana huyu pia nimwenzenu!
 
Back
Top Bottom