Chadema acheni kutuchezea... nendeni mahakamani tu...!

Fahamu kuwa kuiacha mahakama wakati una ushahidi wa dhuluma ni kuhalalisha dhuluma.................Ipe nafasi mahakama kuondoa dhuluma na ishindwapo basi unakuwa na sababu kubwa zaidi ya kudai marekebisho hata ya muundo wa kimahamakama.............

Ruta.. Mimi naomba tu kujua kwamba kama mahakama ikiletewa kesi ya kwamba NEC haikutangaza matokea halisi na ukakubaliana na ushahidi iliotolewa ina maana itakuwaje...

1. Je uchaguzi urudiwe?
2. Je NEC watakubali kubatilisha uamuzi wao na kusema kwamba Kikwete hakushinda na kwamba yalikuwepo makosa ya kiufundi...
3. Ni nini hatma ya kipengele kinacho sema kwaqmba NEC wakitangaza mshindi hakuna anayeweza kuhoji ushindi huo?

4. Je kipengele hicho ni unconstitutional na kinachomnyima binadamu haki yake ya kikatiba ya kuchagua na kimchagua anayemtaka ?

5. Ni nini itakuwa hatma ya NEC kama mahakama ikukubali kupokea kesi ya kwamba NEC hawakufuata utaratibu wa kutangaza matokea?

6. Ni ibara gani inayosema lazima NEC wafuate utaratibu fulani katika kutangaza matokea au watumie software gani/fulani na ni nani ameihakiki hiyo software kuwa ni tamper proof wakati na kabla ya uchaguzi?

Majibu ya maswali haya nafikitri yamekwisha patiwa majibu kwamba NEC Haiwezi kulazimisha kufuata utaratibu wa namna Vyama vinavyotaka katika kutangaza au kupokea matokea .. vinginrvyo kutakuwa na chaos katika zoezi zima la ychaguzi..
Pia kwamba kama mahakama itakubali hiyo kesi ni wazi kwamba NEC itakuwa imeondolea mamlaka yake ya kuendesha uchaguzi maana kinachotangazwa katika uraisi kinaweza kuhojiwa kwa njia nyingine ya process na kile kilichotangazwa kuwa batili..

majibu mengine utayatoa hapa..
 
Chadema hawana jema wala hawana cha kuibiwa kura. Wameona wameshindwa kwa kishindo, kwani wao walikuwa na uhakika kabisa wa kushinda, sasa roho zinawauma wanatafuta mbinu za kupakaza, hatujaona ushahidi wowote walioueleza au kufikisha suala hili mahakamani. Wanachofanya ni kuburuzwa tu na Mbowe, wabunge wa Chadema wengine, wenye muono, wameona ni upuuzi na wakasusa hata kuingia Bungeni.
 
Jambo usilolijua ni sawasawa na usiku wa giza
 
What we asking from Chadema is leadership but not a bunch of endless complaints

The constitution of the United Republic of Tanzania of 1977

POWER AND PRIVILEGES OF PARLIAMENT
Freedom and immunity from proceedings Act No.15 of 1984,s.14.

100.-(1) There shall be freedom of opinion and debate in the National Assembly, and that freedom shall not breached or questioned by any organ in the United Republic or any other court or elsewhere outside the National Assembly.

(2) Subject to this Constitution or to the provision of any other relevant law, a Member of any relevant law, a Member of Parliament shall not be prosecuted and no civil proceedings may be instituted against him in a court in relation to anything which he has said or done in the National Assembly or has submitted to the National Assembly by way of petition, bill, motion or otherwise.
 
CHADEMA wamesusia hotuba ya Rais ambayo ni kumuaibisha tu na kutuma ujumbe wa uchakachuaji wa kura hawajakataa kuwatumikia wananchi. Napata wasiwasi kama wewe kweli public policy analyst.
 
Jambo ambalo ningependa ufahamu ni kuwa Rev. Mtikila ni kweli alishinda hiyo kesi na hata mahakama ya Rufaa ilikiri katika hitimisho lake kuwa mgombea binafsi ni haki ya kimsingi na serikali ni lazima ilishughulikie kwa sababu nchi hii yaendeshwa kwa misingi ya kidemokrasia................Rev. Mtikila kama hangekwenda mahakamani hayo maangalizo ya kimahakama yasingelikuwepo...............Jaji Mkuu alichokifanya pale ni kumsaidia JK kusiwepo wagombea binafsi katika uchaguzi huu wa 2010 lakini kwa uchaguzi wa 2015 wagombea binafsi watakuwepo........................na hata Rev. Mtikila anawashauri Chadema waende mahakamani na wasipofanya hivyo watakuwa wameliangusha taifa zima........
Ni vyema tusikie mahakama itasema nini kuhusu hiyo Ibara inayokataza matokeo ya Uraisi yaliyotangazwa na NEC inakitafsiri vipi...............hususani kama kuna ushahidi NEC haikufuata sheria katika kumtangaza JK kuwa Raisi wa JMT kwa kujitungia matokeo ya kura waliyoyataka wenyewe..........

Kila kesi ina mazingira yake na siyo vyema kutoa maangalizo ya kiujumla kuwa ni lazima yatajitokeza katika kila kesi ya kisiasa............ni vyema wakaenda huko na tujue walikwama wapi..........................na hasa tukiamini safari ushahidi wanao tofauti na kesi za uchaguzi za miaka iliyopita............

Chadema wajifunze kutoka kwa Besigye wa Uganda ambaye amekuwa wakipata ushindi mwingi dhidi wa Yoweri Museveni ambo unachangia kuweka chaguzi za huko kuwa na hafueni ya uhuru na haki zaidi..........Hii ni mbali ya ukweli kuwa mahakama zipo chini ya himaya ya Museveni kama hapa.........

Huko bado kutakuwa ni kumpigia mbuzi gitaa, hakuna MAHAKAMA kubwa zaidi ya NGUVU YA UMMA!.

Sasa hivi tuko kwenye mgogoro wa ki-KATIBA na CCM washaonyesha kuwa peke yao hawana uwezo wa kuhimili mikiki-mikiki yake.

Kitendo kidogo tu cha wabunge kususia hotuba ya Mkwere tayari wameshaanza kubabaika, yale yatakayofuatia baadaye ndio itakuwa mtaji kwa CHADEMA kufungua ukurasa mpya wa demokrasia ya kweli.

Amini usiamini safari hii WANANCHI watahamisika ili kubadili KATIBA na hakuna mahakama yeyote itakayopinga maamuzi yao...
 
Chadema tumewachagua kutuwakilisha bungeni na wala siyo vinginevyo......wasipokwenda bungeni kwa visingizio vyovyote vile hapo watakuwa wanamkomoa mpigakura na wasifikiri tutawachagua tena........................next time tutakaa nyumbani na wacha hao CCM waendelee kututesa maana yawezekana kabisa taifa hili Mwenyezi Mungu kalilaani................

Kama Chadema wana ushahidi wa ya kuwa kura za vituoni zinatofautiana na zile ambazo NEC ilizitangaza sasa ni nini kinawazuia kulalamika mahakamani? Hicho kiji-Ibara cha katiba cha kuzuia matokeo ya kura za Uraisi yaliyotangazwa na NEC kuhojiwa mahakamani msikisome kijuu juu tu........Hakizuii hoja za kimsingi kusikilizwa na mahakama zetu na huo ni msimamo wao wa tangu mwaka 1995........Kumbukeni kazi ya kutafsiri sheria ni ya mahakama......nendeni huko mkadai haki yenu na kama mahakama ikikataa kuwasikiliza sasa ndiyo mrudi kwetu na hapo tutajua ya kuwa hata mahakama zinadi ukarafati mzito..

Katiba yetu iliweka dhana ya kuwa matokeo yaliyotangazwa na NEC kulingana na taratibu za kisheria ndiyo tu ambayo mahakama haiwezi kuyahoji lakini katiba yetu haikukusudia ya kuwa NEC wavunje sheria za uchaguzi katika kuyatangaza matokeo hayo na mahakama zinapolalamikiwa zikae kimya........................la hasha.................siyo hivyo hata kidogo........

Madai ya chadema kama yana ushahidi ni lazima yafikishwe mahakamani na hoja ya muhimu ni kuwa NEC haikufuata sheria ya uchaguzi na taratibu zake kwa kuyadharau matokeo ya kura kama zilivyopigwa na wananchi na wao kujitangazia matokeo wayatakayo tu wenyewe.........................Mahakama ikipata ushahidi wa kutosha na kuridhika itayatengua matokeo ya Uraisi kwa sababu hayakuheshimu ridhaa ya wapigakura.....................

Nje ya kuufuata utaratibu huu wa kisheria Chadema nasema acheni kutuchezea watu wazima na nendeni bungeni mkafanye kazi tuliyowatuma kama hamtaki semeni na chaguzi za majimbo mliyoshinda zirudiwe na wanaotaka kutuhudumia hata kama ni kutudhulumu wache wafanikiwe kwenye malengo yao.....................

What we asking from Chadema is leadership but not a bunch of endless complaints

Utumbo tu unaandika mrefu namna hiyo!!! Je, ukiandika mambo ya maana si tutasoma mwaka mzima!!.
 
Rutashubanyuma we utachangia shilingi ngapi kesi ikienda mahakamani au wakili yupi utamlipa asimamie kesi unayojua majibu yake dhahiri.
 
Katika historia ya nchi hatujawahi kupata changamoto kama hii ya Chadema na itakuwa ni makosa ya kihistoria kama Chadema wataihukumu mahakama bila ya kuwapa nafasi ya kuyatolea maamuzi malalamiko yao..............Ushahidi wa kimsingi wote wanao...........sasa wasizihukumu mahakama zetu kwa njia hiyo.....................hii kesi itaiweka mahakama nayo kizimbani.........raia tutapenda kuona kama mahakama zaweza kutenda haki na zikishindwa hiyo ni hoja nyingine ya kuzirekebisha mahakama hizo...............Let us test our judicial system before we pass an adverse judgment against them.................

UMEISOMA HII IBARA YA 41(7) au unaandika tu? nakuwekea hapa kwa faida yako na wengine kama wewe

41 (7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi
kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi
hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya​
kuchunguza kuchaguliwa kwake.
 
CCM bwana walidhani wanaweza kufanya haya mambo wao tu ? Pale hakuna kuchakachua wala FFU sasa labda kumtumia Makinda ambaye najua atavuruga Bunge kweli na wote mtashangaa .Watu kumsusa JK naona CCM inawaumiza walizoea kueleza Dunia kwamba ni TZ ni kisiwa cha amani nk na sasa joto linawakabili wanalia lia wacha wabanwe tuone .
 
Katika historia ya nchi hatujawahi kupata changamoto kama hii ya Chadema na itakuwa ni makosa ya kihistoria kama Chadema wataihukumu mahakama bila ya kuwapa nafasi ya kuyatolea maamuzi malalamiko yao..............Ushahidi wa kimsingi wote wanao...........sasa wasizihukumu mahakama zetu kwa njia hiyo.....................hii kesi itaiweka mahakama nayo kizimbani.........raia tutapenda kuona kama mahakama zaweza kutenda haki na zikishindwa hiyo ni hoja nyingine ya kuzirekebisha mahakama hizo...............Let us test our judicial system before we pass an adverse judgment against them.................

Judicial system itestiwe mara ngapi, kama ingekuwa strong Mgombe huru si tungekuwa nae, ua kesi ya yule Muhindi alie supply Vifaru Jeshini ambaye mahakama iliamua in his fever kwamba alipwe na Serikali imetekelezwa, acha pumba bwana, CHADEMA wameonyesha njia zaidi ya mara mbili na zimefanyakazi, kumbuka walivyo mfukuza Zitto bungeni chadema walitumia nguvu ya uma Operation Sangara, na Mkutano wa mwembe yanga ambao Mafisadi walitajwa hadharani, ndipo tulipoona akina kilango na Mwakyembe wanakigeuka chama chao na kuzungumzia masuala yenye maslahi ya nchi, au hukuwepo tukukumbushe. CHADEMA wamekomaa, wabunifu jaribu kuwa na subira utaona matokeo. CHADEMA PEOPLES POWER!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Ruta,

Vipi umepata supu au chai na kitafunwa asubuhi ya leo? maana naona ghafla umebadilika na kuanza kuongea kama mtu aliyekata tamaa!!:target:

Tambua hawa viongozi wa CDM wanaelewa fika matatizo ya mahakama zetu mfano, Rev. Mtikila alishinda kesi ya mgombea binafsi lakini hadi leo jamaa wanacheza delay tacs, unakumbuka mapendekezo ya Judge Nyalali juu ya vifungu kama 50 hivi vya katiba vinavyotakiwa kubadilishwa lakini hadi leo jamaa wanacheza delay tacs.

CCM wanapenda sana pale vyama vya upinzani vinapoenda mahakamani maana inakuwa ni rahisi kwa wao kuchezea maamuzi ya mahakama. Suluhisho la matatizo tuliyonayo kwa sasa kamwe halitapatikana mahakamani bali ni kwa kupitia njia mubadala!

Kutosikiliza hotuba ya Mkwere ni mwanzo tu lakini nina hakika kuna mengi yako jikoni yanapikwa, (kwanza hata mimi ningekuwa mbunge wa Ki-Jani siku ile either ningesinzia kwa makusudi au ningemwomba Spika ruksa ya kutoka kiana kusingizia ka-ugonjwa hotuba ya Mkwere ilikuwa ina-bore!).

Tatizo ninaloliona hapa Jamvini ni kwa sisi wanajamvi kukosa uvumilivu ama kutaka kuchanganua na kutolea maamuzi kila kitu bila kujali timing yake...

Duh! Nilidhani peka yangu, kwani Hotuba ile imefanana kabisa na ya mwaka 2005 ambayo nilimskiliza na nipata matumaini kweli na ndio maana baada ya dakika 15 tuu niligundua sio Hotuba mpya bali anasoma ya Mwaka 2005.
 
Chadema tumewachagua kutuwakilisha bungeni na wala siyo vinginevyo......wasipokwenda bungeni kwa visingizio vyovyote vile hapo watakuwa wanamkomoa mpigakura na wasifikiri tutawachagua tena........................next time tutakaa nyumbani na wacha hao CCM waendelee kututesa maana yawezekana kabisa taifa hili Mwenyezi Mungu kalilaani................

Kama Chadema wana ushahidi wa ya kuwa kura za vituoni zinatofautiana na zile ambazo NEC ilizitangaza sasa ni nini kinawazuia kulalamika mahakamani? Hicho kiji-Ibara cha katiba cha kuzuia matokeo ya kura za Uraisi yaliyotangazwa na NEC kuhojiwa mahakamani msikisome kijuu juu tu........Hakizuii hoja za kimsingi kusikilizwa na mahakama zetu na huo ni msimamo wao wa tangu mwaka 1995........Kumbukeni kazi ya kutafsiri sheria ni ya mahakama......nendeni huko mkadai haki yenu na kama mahakama ikikataa kuwasikiliza sasa ndiyo mrudi kwetu na hapo tutajua ya kuwa hata mahakama zinadi ukarafati mzito..

Katiba yetu iliweka dhana ya kuwa matokeo yaliyotangazwa na NEC kulingana na taratibu za kisheria ndiyo tu ambayo mahakama haiwezi kuyahoji lakini katiba yetu haikukusudia ya kuwa NEC wavunje sheria za uchaguzi katika kuyatangaza matokeo hayo na mahakama zinapolalamikiwa zikae kimya........................la hasha.................siyo hivyo hata kidogo........

Madai ya chadema kama yana ushahidi ni lazima yafikishwe mahakamani na hoja ya muhimu ni kuwa NEC haikufuata sheria ya uchaguzi na taratibu zake kwa kuyadharau matokeo ya kura kama zilivyopigwa na wananchi na wao kujitangazia matokeo wayatakayo tu wenyewe.........................Mahakama ikipata ushahidi wa kutosha na kuridhika itayatengua matokeo ya Uraisi kwa sababu hayakuheshimu ridhaa ya wapigakura.....................

Nje ya kuufuata utaratibu huu wa kisheria Chadema nasema acheni kutuchezea watu wazima na nendeni bungeni mkafanye kazi tuliyowatuma kama hamtaki semeni na chaguzi za majimbo mliyoshinda zirudiwe na wanaotaka kutuhudumia hata kama ni kutudhulumu wache wafanikiwe kwenye malengo yao.....................

What we asking from Chadema is leadership but not a bunch of endless complaints
SOMA HAPA ALAFU MUOMBE INVIZIBO AFUTE THREAD YAKO, Kwa kuwa ni ya HOVYO.

Katiba Ya Jamuhuri ibara =41(7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi (NEC) kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake.

Hapa sio KUPINGA MATOKEO TU ya URAIS. Katiba inakataza HATA KUCHUNGUZA, Kuchunguza tu NI UMEKIUKA KATIBA, Ni kosa.

Mtoa hoja nawe ni kilaza,

Unapoishitaki NEC, MAHAMANI KUHUSU KUCHEZEA MATOKEO YA URAIS, ina maana katika kupeleka USHAHIDI MAHAKAMANI unahusisha UCHUNGUZI!!!

Hakuna ushahidi usio na UCHUNGUZI. wakati huo KESI iliyopo mahakamani ni kuishitaki NEC, kwa kuchezea KURA ZA WANANCHI kwa upande wa RAisi.(kumbuka hadi sasa CHADEMA wao ni ishu ya Matokeo ya Urasi, sio ubunge wala udiwani)

Huyo jaji anaesikiliza HIYO kesi utakayofungua(maana CDM hawawezi kupoteza muda wakati njia zingine zipo) AMETEULIWA NA NANI? Labda nifafanulie na hapa.

Kama ni huyo ndugu yako Augostino Ramadhani, alishajishushia heshima kwenye kesi ya Mgombea binafsi zamaaaaaani, yeye na wenziwe.

Kwa kusoma hapo palipopigiwa msitali HOJA YAKO ni UPUUZI MTUPU, Go Chadema GO....
 
Crapppp!!!!! It does not hold water, simple as that...the good thing is, you too know to be so.

When you you have no reasoning ability this is what we get.................................no reasons but gushing anger.........and frustrations but can not explain why.......................................The cost of ignorance is always visible to the knower...........
 
SOMA HAPA ALAFU MUOMBE INVIZIBO AFUTE THREAD YAKO, Kwa kuwa ni ya HOVYO.

Katiba Ya Jamuhuri ibara =41(7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi (NEC) kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake.

Hapa sio KUPINGA MATOKEO TU ya URAIS. Katiba inakataza HATA KUCHUNGUZA, Kuchunguza tu NI UMEKIUKA KATIBA, Ni kosa.

Mtoa hoja nawe ni kilaza,

Unapoishitaki NEC, MAHAMANI KUHUSU KUCHEZEA MATOKEO YA URAIS, ina maana katika kupeleka USHAHIDI MAHAKAMANI unahusisha UCHUNGUZI!!!

Hakuna ushahidi usio na UCHUNGUZI. wakati huo KESI iliyopo mahakamani ni kuishitaki NEC, kwa kuchezea KURA ZA WANANCHI kwa upande wa RAisi.(kumbuka hadi sasa CHADEMA wao ni ishu ya Matokeo ya Urasi, sio ubunge wala udiwani)

Huyo jaji anaesikiliza HIYO kesi utakayofungua(maana CDM hawawezi kupoteza muda wakati njia zingine zipo) AMETEULIWA NA NANI? Labda nifafanulie na hapa.

Kama ni huyo ndugu yako Augostino Ramadhani, alishajishushia heshima kwenye kesi ya Mgombea binafsi zamaaaaaani, yeye na wenziwe.

Tatizo lako hapa wewe unajifanya ni mahakama na wakati siyo maswali yako haya yote yalikwisha kujibiwa kwenye kesi ya kupinga matokeo ya Uraisi mwaka 1995..........yaani I am amazed by your vacuous confidence...........kuzuiwa kuchunguza matokeo ni kitu tofauti na kuhoji kama NEC ilifuata sheria ya uchaguzi katika kuyatangaza matokeo hayo ........hilo hakuna kifungu kinachokataza kuhoji NEC kama ilifuata sheria sasa.........what are you talking about?.........Huku unanisaga huku unaniomba ufafanuzi ......where do you stand my friend?.....either you give me a credit as a professional or you just ignore me,.you cannot have both ways........Wewe kwa upeo wako mdogo wa kisheria unavyosoma hiyo Ibara usifikiri tafsiri yake ni hiyo uionavyo........Neno moja kwenye sheria lina tofauti kibao na laweza kumaanisha vitu viwili au hata zaidi tofauti...........Mahakama ilikwisha kusema wao ndiyo kimbilio la mwisho la raia na hakuna sheria ambayo itawakataza kuchunguza haki iliyotolewa na sheria inapopindishwa na bado haki hiyo ikiwa haijaondolewa kwenye vifungu vya sheria..............................

Unapofananisha na hukumu ya mgombea binafsi unanithibitishia jinsi ambavyo huelewi Mahakama ya Rufaa ilisema nini...............ninakushauri ukasome post yangu iliyopo kwenye Jukwaa la sheria ili uelewe tofauti zake za migogoro hii miwili...................

Kwa kifupi tu hukumu ya mgombea binafsi imeongezea sauti juu ya hili suala kusikilizwa na mahakama hii pale waliposema ....vifungu vyo vyote vya kikatiba lazima utungwaji wake uzingatie sheria na kama kuna malalamiko kuwa kifungu kiliondolewa au kuongezwa bila ya kufuata sheria mahakama zitachunguza na kutoa maamuzi stahili.................Hoja hapo ni kama sheria zimepindishwa mahakama ina wajibu wa kuhakikisha dosari hizo zinarekebishwa...............

Ipo sheria ya uchaguzi ambayo NEC hawakuifuata na mahakama inayohaki kama ikiombwa kuchunguza jambo hili...........................ushauri wangu kwako kama kitu hujakifanyia kazi kama mimi nilivyohangaika na hili suala ni vyema ukauliza badala ya kujitutumua wakati hufahamu juu ya mapambano ya hoja za kisheria yaliyopo mbele yetu.................Ninarudia usitumie hukumu ya mgombea binafsi hapa kwa sababu hata wanasheria wa upande wa Mtikila kwa kweli walichemsha kwa kutohoji masuala fulani fulani ambayo yangelisaidia katika kutenda haki.........lakini mjadala huo nisingependa kuurudia kwa sababu kazi hiyo nilikwisha kuifanya huko nyuma...................
 
UMEISOMA HII IBARA YA 41(7) au unaandika tu? nakuwekea hapa kwa faida yako na wengine kama wewe

41 (7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi
kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi
hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya​
kuchunguza kuchaguliwa kwake.
Hoja ambayo huioni ni kuwa JK alichaguliwa au alisimikwa na NEC na je wanayo mamlaka ya kufanya hivyo? Mgogoro huu ninaouelezea mimi siyo kuhoji kuchaguliwa kwake kwa sababu hatukumchagua sisi sasa mahakama itachunguzaje mtu ambaye hatukumchagua na vielelezo vya ushahidi vipo...........................ila mahakama inao uwezo wa kuchunguza kama NEC inayo mamlaka ya kutofuata sheria za uchaguzi na kujifanyia shughuli zake watakavyo.............na ninakuhakishia haya maswali yataharakisha kuvunjwa kwa NEC kuliko hizo jitihada zinazofanyika nje ya sheria hizi zilizopo hata kama zina mapungufu.........jamani this is too obvious to me..........but now I have to appreciate what is common sense to me may not always be common to everybody....................

Suala hili siyo jepesi kama mnavyolitafakari wengi wenu humu.......................think deep on what I have said and you may be able to dissect the message......please do not rush to adjudge without being backed with a pertinent hindsight......................
 
Rutashubanyuma we utachangia shilingi ngapi kesi ikienda mahakamani au wakili yupi utamlipa asimamie kesi unayojua majibu yake dhahiri.

swali la msingi ni kuona uhaja wa kuitumia sheria zilizopo kudai haki na wengi tutajifunza mengi hapo........hata hukumu hiyo ya mgombea binafsi usifikiri Mtikila alitoka patupu..maelekezo ya mahakama ya Rufaa yameweka wazi kuwa hiyo ni haki ya msingi na serikali iwe sikivu...............kama mtikila angelikuwa na mawazo mgando wa kuibeza mahakama hiyo kauli tungeliipata wapi?

kubwa hapa ni kuona umuhimu wa kufuata sheria na mengine yanawezekana......who said democracy is cheap.even nyerere had to make personal sacrifice and the nation will always do the same ...........it is not an individual or personal responsibility......
 
One of us mimi au huyo mtoa mada has 'LOST THE PLOT" hivi hujui kwamba raisi akishatangazwa na Tume huwezi ukapinga mahakamani So wande mahakamani kumtembelea Judge au..... Come on Guys Lets Me Serious.... Njia waliotumia is perfect wamepata media coverage nzuri... so now they can carry on as normal
 
Back
Top Bottom