Chadema acheni kutuchezea... nendeni mahakamani tu...! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chadema acheni kutuchezea... nendeni mahakamani tu...!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Nov 21, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  Chadema tumewachagua kutuwakilisha bungeni na wala siyo vinginevyo......wasipokwenda bungeni kwa visingizio vyovyote vile hapo watakuwa wanamkomoa mpigakura na wasifikiri tutawachagua tena........................next time tutakaa nyumbani na wacha hao CCM waendelee kututesa maana yawezekana kabisa taifa hili Mwenyezi Mungu kalilaani................

  Kama Chadema wana ushahidi wa ya kuwa kura za vituoni zinatofautiana na zile ambazo NEC ilizitangaza sasa ni nini kinawazuia kulalamika mahakamani? Hicho kiji-Ibara cha katiba cha kuzuia matokeo ya kura za Uraisi yaliyotangazwa na NEC kuhojiwa mahakamani msikisome kijuu juu tu........Hakizuii hoja za kimsingi kusikilizwa na mahakama zetu na huo ni msimamo wao wa tangu mwaka 1995........Kumbukeni kazi ya kutafsiri sheria ni ya mahakama......nendeni huko mkadai haki yenu na kama mahakama ikikataa kuwasikiliza sasa ndiyo mrudi kwetu na hapo tutajua ya kuwa hata mahakama zinadi ukarafati mzito..

  Katiba yetu iliweka dhana ya kuwa matokeo yaliyotangazwa na NEC kulingana na taratibu za kisheria ndiyo tu ambayo mahakama haiwezi kuyahoji lakini katiba yetu haikukusudia ya kuwa NEC wavunje sheria za uchaguzi katika kuyatangaza matokeo hayo na mahakama zinapolalamikiwa zikae kimya........................la hasha.................siyo hivyo hata kidogo........

  Madai ya chadema kama yana ushahidi ni lazima yafikishwe mahakamani na hoja ya muhimu ni kuwa NEC haikufuata sheria ya uchaguzi na taratibu zake kwa kuyadharau matokeo ya kura kama zilivyopigwa na wananchi na wao kujitangazia matokeo wayatakayo tu wenyewe.........................Mahakama ikipata ushahidi wa kutosha na kuridhika itayatengua matokeo ya Uraisi kwa sababu hayakuheshimu ridhaa ya wapigakura.....................

  Nje ya kuufuata utaratibu huu wa kisheria Chadema nasema acheni kutuchezea watu wazima na nendeni bungeni mkafanye kazi tuliyowatuma kama hamtaki semeni na chaguzi za majimbo mliyoshinda zirudiwe na wanaotaka kutuhudumia hata kama ni kutudhulumu wache wafanikiwe kwenye malengo yao.....................

  What we asking from Chadema is leadership but not a bunch of endless complaints
   
 2. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,423
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Umeweka fikra nzito na umeona mbali! Kuishitaki NEC kwa kutofuata sheria, kwa kudharau maoni ya wapiga kura sio sawa na kukataa au kupinga kutwawazwa JK! Safi sana! Lakini usikate tamaa kiasi hicho. Najua wanasiasa wanapinda pinda njia hadi wafike wanakotaka! Vuta subira!

  Mimi nasubiri kwa hamu kesi za kupinga matokeo ya ubunge kama kule Moshi Vijijini, Njombe Magharibi, Geita nk, lakini sioni kinachoendelea, CHADEMA angalieni msije mkatupelekesha kwingine!
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  Tatizo ninaliona kwa baadhi ya viongozi wa Chadema wanafikiri jazba na mabavu ndiyo suluhisho lakini hapana......................wasikate tamaa hivyo............na wapaswa kuonyesha mfano wa uongozi bora...........................ya kumkataa JK yameeleweka sasa ni mahakamani kutafuta ufumbuzi wa kudumu na wala siyo kulihusisha bunge kwa kulisusia..........................Bungeni wapeleke miswada ya marekebisho ya katiba na NEC halafu ikikatailiwa warudi kwetu tutawaenzi kwa sababu watakuwa na mifano hai jinsi bunge ambalo CCM wamelihodhi lilivyowawanyapaa......
   
 4. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2010
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  CCM ni mabingwa wa kucheza Danadana Mahakamani.

  Wao wakituhumiwa hawaendi mahakamani huishia kutoa maneno matupu majukwaani.

  CHADEMA wakienda mahakamani hukumu ya haki inaweza kutolewa, lakini je serikali itakuwa tayari kutekeleza hukumu hiyo??


  Ni kitu gani kitawasukuma kutekleza hukumu juu ya Wizi wa NEC wakati kwa miaka zaidi ya 10 sasa bado wananajisi Maamuzi ya Mahakama juu ya kesi ya Mgombea Binafsi katika chaguzi zote za kisiasa??

  Serikali ya CCM haiheshimu Mahakama pia haiheshimu wananchi.
  Serikali ya CCM inacheza na HAKI za WaTanzania.

  Kimsingi wewe na watu wengine wa aina yako ndo mnakubali kuchewa ili hali nyie ni watu wazima na akili zenu. Sijui mwenzetu unfaidika nini na Ubabe wa Serikali ya CCM kutia kiburi kutekeleza hukumu za Mahakama??

  Kazi amabayo Wabunge wa CHADEMA walitumwa na wananchi kuifanya,watafanya kwa asilimia 100%.

  Kusikiliza Hotuba ya Rais si moja ya kazi walizotumwa kufanya na wananchi Bungeni. Hotuba ya Rais bungeni ni symbol tu haina meno pale Bungeni wala si Muswada. Rais anaweza kutekeleza kazi yake akiwa Ikulu na wabunge wanaweza kutekleza kazi yao wakiwa Bungeni bila kumtegemea Rais hata 0.1% ya ushauri wa Rais.

  Iwapo serikali itatekeleza Hukumu ilotolewa kuruhusu Mgombea Binafsi katika ngazi zote za chaguzi za kisiasa maneno yako yanaweza kuwa na ujasiri hapa JF, kinyume chake unajikonga nafsi yako tu.

  Rais akija tena kuhutubia Bunge, nawaombeni wabunge wa CHADEMA kuendeleza utaratibu wenu mzuri wa kuichinia hotuba yake. ujumbe mlioutuma umesikika vyema, umeeleweka vizuri na pande zote mbili, Nia na kusudio lake limetia.

  Zile dakika chache mlizo andamana pale bungeni zimepeleka ujumbe wa nguvu zaidi kuliko Mandamano ya Watanzania 7,000,000. Zaidi mmeepusha mabomu ya machozi Virungu vya polisi na hata umwagaji damu usio wa lazima endapo wananchi wangeingia mtaani na ujumbe kama wenu.

  Hongera sana CHAEMA msisikilize maneno ya akina ZAZU.
   
 5. b

  bojuka Senior Member

  #5
  Nov 21, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaa ukijua hiyo nec imewekwa na ccm na mahakama imewekwa na serikali ya ccm hivyo hakuna jipya.
   
 6. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,423
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Hivyo hivyo tutakula nao sahani moja! Hoja ikiwa nzito, inaweza ikasambaratisha hao waliopandikizwa kwenye vyombo hivi. Ni kwa ajili hiyo tuliweza kuwapata kina Mwakyembe, Sita nk
   
 7. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #7
  Nov 21, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  Hapo sasa hatua hizi ambazo Chadema wanataka kuzitumia za mass action zitaeleweka kwa wapigakura kama maamuzi ya mahakama yatakataliwa kutekelezwa.......................
   
 8. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #8
  Nov 21, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Well Done CHADEMA! Ujumbe umefika! Mara zote kumfunga paka kengere ni shughuli-nyie kweli ni wapiganaji, haki haiji kilelemama na mchezomchezo, nchi nyingine wanatafuta haki kwa damu kumwagika-sembuse ss kwa amani! Kazi ndy kwanza inaanza, hakikisheni kabla ya uchaguzi 2015 katiba mpya na tume huru vnapatikana. Anayesema mmegoma kuingia bungeni ni kibaraka wa CCM-Kiao kijacho wakiona mnachoma ndani na hoja za msingi watakuja na vichwa vya habari vingine. SISI WAPIGA KURA WENU TUNAOELEWA NINI MNAPIGANIA TUKO NYUMA YENU!
   
 9. tartoo

  tartoo Senior Member

  #9
  Nov 21, 2010
  Joined: Jul 2, 2010
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Crappp!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Nov 21, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  Katika historia ya nchi hatujawahi kupata changamoto kama hii ya Chadema na itakuwa ni makosa ya kihistoria kama Chadema wataihukumu mahakama bila ya kuwapa nafasi ya kuyatolea maamuzi malalamiko yao..............Ushahidi wa kimsingi wote wanao...........sasa wasizihukumu mahakama zetu kwa njia hiyo.....................hii kesi itaiweka mahakama nayo kizimbani.........raia tutapenda kuona kama mahakama zaweza kutenda haki na zikishindwa hiyo ni hoja nyingine ya kuzirekebisha mahakama hizo...............Let us test our judicial system before we pass an adverse judgment against them.................
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Nov 21, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  I fully subscribe to this view............................
   
 12. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #12
  Nov 21, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,682
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Ruta,

  Vipi umepata supu au chai na kitafunwa asubuhi ya leo? maana naona ghafla umebadilika na kuanza kuongea kama mtu aliyekata tamaa!!:target:

  Tambua hawa viongozi wa CDM wanaelewa fika matatizo ya mahakama zetu mfano, Rev. Mtikila alishinda kesi ya mgombea binafsi lakini hadi leo jamaa wanacheza delay tacs, unakumbuka mapendekezo ya Judge Nyalali juu ya vifungu kama 50 hivi vya katiba vinavyotakiwa kubadilishwa lakini hadi leo jamaa wanacheza delay tacs.

  CCM wanapenda sana pale vyama vya upinzani vinapoenda mahakamani maana inakuwa ni rahisi kwa wao kuchezea maamuzi ya mahakama. Suluhisho la matatizo tuliyonayo kwa sasa kamwe halitapatikana mahakamani bali ni kwa kupitia njia mubadala!

  Kutosikiliza hotuba ya Mkwere ni mwanzo tu lakini nina hakika kuna mengi yako jikoni yanapikwa, (kwanza hata mimi ningekuwa mbunge wa Ki-Jani siku ile either ningesinzia kwa makusudi au ningemwomba Spika ruksa ya kutoka kiana kusingizia ka-ugonjwa hotuba ya Mkwere ilikuwa ina-bore!).

  Tatizo ninaloliona hapa Jamvini ni kwa sisi wanajamvi kukosa uvumilivu ama kutaka kuchanganua na kutolea maamuzi kila kitu bila kujali timing yake...
   
 13. i

  ifolako Member

  #13
  Nov 21, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Slaa Raisi Wangu.Nitamtii na nitapiga saluti zote anazostahili! Hima Himaaaaaa......Tanzaniaaaaaa!

  Ni kweli Slaa ni Raisi wako lakini Rais wa watanzania ni Jakaya M.Kikwete.
   
 14. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #14
  Nov 21, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  Toa sababu vinginevyo.........................hujui unaloliongea au linaloongelewa...................
   
 15. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #15
  Nov 21, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  Jambo ambalo ningependa ufahamu ni kuwa Rev. Mtikila ni kweli alishinda hiyo kesi na hata mahakama ya Rufaa ilikiri katika hitimisho lake kuwa mgombea binafsi ni haki ya kimsingi na serikali ni lazima ilishughulikie kwa sababu nchi hii yaendeshwa kwa misingi ya kidemokrasia................Rev. Mtikila kama hangekwenda mahakamani hayo maangalizo ya kimahakama yasingelikuwepo...............Jaji Mkuu alichokifanya pale ni kumsaidia JK kusiwepo wagombea binafsi katika uchaguzi huu wa 2010 lakini kwa uchaguzi wa 2015 wagombea binafsi watakuwepo........................na hata Rev. Mtikila anawashauri Chadema waende mahakamani na wasipofanya hivyo watakuwa wameliangusha taifa zima........
  Ni vyema tusikie mahakama itasema nini kuhusu hiyo Ibara inayokataza matokeo ya Uraisi yaliyotangazwa na NEC inakitafsiri vipi...............hususani kama kuna ushahidi NEC haikufuata sheria katika kumtangaza JK kuwa Raisi wa JMT kwa kujitungia matokeo ya kura waliyoyataka wenyewe..........

  Kila kesi ina mazingira yake na siyo vyema kutoa maangalizo ya kiujumla kuwa ni lazima yatajitokeza katika kila kesi ya kisiasa............ni vyema wakaenda huko na tujue walikwama wapi..........................na hasa tukiamini safari ushahidi wanao tofauti na kesi za uchaguzi za miaka iliyopita............

  Chadema wajifunze kutoka kwa Besigye wa Uganda ambaye amekuwa wakipata ushindi mwingi dhidi wa Yoweri Museveni ambo unachangia kuweka chaguzi za huko kuwa na hafueni ya uhuru na haki zaidi..........Hii ni mbali ya ukweli kuwa mahakama zipo chini ya himaya ya Museveni kama hapa.........
   
 16. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #16
  Nov 21, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Unajuwa bwana ruta,haya mambo soyo ya kuyakimbilia tu hawa wabunge wa chadema wengi wao wanaelewa sheria,na ukumbuke kuwa wao wanachosema wamekubali kuwa jk ni raisi na hawana uwezo wa kutenguwa hilo,ila lengo lao lilikuwa ni kufikisha ujumbe kwa jamii na dunia kwa ujumla na wamefanikiwa kwa hilo,then mambo mengine ya kisiasa mjengoni yataendelea,nadhani na hilo la kutoka nje pia ni uwakilishi wa wapigakura ama mna udifine vipi uwakilishi?


  Mapinduziiiiii daimaaaaaa
   
 17. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #17
  Nov 21, 2010
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Katiba haiwaruhusu kwenda Mahakamani kupinga jambo lolote kuhusu ushindi wa rais uliotangazwa na NEC.

  Kitendo cha kwenda Mahakamani kupinga matokeo ni uvunjaji wa katiba.

  Kesi wawezayo kuifungua Chadema ni ile ya kupinga Kifungu cha katiba kinachowazuia kupinga matokeo ya Urais.

  Kesi ya namna hiyo ikifunguliwa leo haiwezi kuhusisha wizi wa kura zilizo muweka Kikwete ikulu bali itabidi hoja nyingine zijengwe kuipa nguvu kesi hiyo.
  Let us say CHADEMA wameshinda kesi hii dhidi ya kifungu cha katiba.

  Nikirejea swali langu la msingi kwako.
  Je ni msukumo gani utaifanya serikali ya CCM kutekeleza hukumu hii mpyya wakati kuna kigonela cha hukumu ya mgombea binafsi ambayo Serikali ya CCM bado inanajisi utekelezaji wake bila aibu hadi dakika hii niandikapo?
   
 18. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #18
  Nov 21, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  Fahamu kuwa kuiacha mahakama wakati una ushahidi wa dhuluma ni kuhalalisha dhuluma.................Ipe nafasi mahakama kuondoa dhuluma na ishindwapo basi unakuwa na sababu kubwa zaidi ya kudai marekebisho hata ya muundo wa kimahamakama.............
   
 19. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #19
  Nov 21, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Sitakuwa nimeitendea haki jamii yangu ya kitanzania kwa kukosa kusifia kitendo cha kijasiri kilichofanywa na wapiganaji wa CHADEMA kwani ndio njia pekee ya kuonyesha kwamba hata uvumilivu una mwisho. si mara moja wala mbili sisiem wamekuwa wanaona sawa tu kukalia utashi wa watu bila kuzingatia madhara wanayo yaleta kwenye jamii.

  Kwa walichofanya CHADEMA inatosha sasa kuwaonyesha hawa watawala uchwara kwamba tunapaswa kuwa na hofu ya pamoja katika kushughulikia na kujali haki ya watu.

  Ni upambavu ujinga na matumizi mabaya ya mali na rasilimali mbali mbali za nchi hii katika kutekeleza demokrasia halafu wananchi wanachagua viongozi wao halafu wao wanatangaza wanavyotaka hii sio haki na ujumbe lazima utumwe katika kukemea suala hili.

  Ni bora kusema usisikilizwe kuliko kutosema kabisa, tuko pamoja CHADEMA kilio chenu ni kilio cha Mungu kwani uhayawani wa watanzania kunyamazia kila kitu hata pale ambapo haki zao zinachezewa unaelekea mwisho. Inaelekea staili iliyotumika kupata uhuru wetu imetufanya tumekuwa wazembe hata kwenye kudai haki na hii ndio inayowafanya hawa warithi wa utawala kufanya watakavyo.

  Watake wasitake yana mwisho haya, tumeona falme zilizokuwa na nguvu lakini mwisho wake hatimaye ulifika. Utawala kama wa Mabutu ambao uliwekwa madarakani na dola zenye nguvu duniani (US) na kusababisha wanamapinduzi wa Zairi kuuawa lakini mwisho ulifika hatimaye sembuse sisiem, nabashiri kwamba mwisho wao hauko mbali na dhuluma waliyofanya katika uchaguzi huu ni laana ambayo haitawaacha hivihivi tusubiri tuone!
   
 20. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #20
  Nov 21, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,209
  Likes Received: 414,657
  Trophy Points: 280
  Mwaka 1995 akina Mrema na wenzie walienda mahakamani kuhoji matokeo ya Uraisi yaliyotangazwa na NEC na mahakama ilisema ya kuwa inao uwezo wa kuichunguza NEC kama katika kuyatangaza matokeo hayo ilifuata sheria ya uchaguzi na ya kuwa mahakama kamwe haitafumbia macho kama sheria hazifuatwi......................kwa hiyo tafsiri ya hicho kipengere mahakama ilikwisha kitolea misimamo na sisi huku mtaani siyo wafuatiliaji wa maamuzi ya mahakama...........................kwa hiyo kwenda mahakamani siyo kweli unavunja katiba hata kidogo.............

  Ukiwa mahakamani unaweza kuchanganya yote mawili ya kuomba Ibara onevu ifutwe ili kuipa mahakama uhuru zaidi wa kuchunguza maamuzi ya NEC kama yalizingatia sheria.........na yote haya yawezekana kabisa..............

  Kwa kumalizia mahakama inao uwezo wa kuyafuta matokeo yaliyotangazwa na NEC kama ikithibitika hayakuzingatia sheria na kuamuru uchaguzi urudiwe upya ila haina uwezo wa kumtangaza Dr. Slaa mshindi hata kama ikiona ndiye aliyepaswa kutangazwa kidedea kwa sababu kwa kufaya hivyo mahakama itakuwa imeingilia majukumu ya kikatiba ya NEC..........
   
Loading...