Chadema acheni kutuchezea... nendeni mahakamani tu...!

Umeweka fikra nzito na umeona mbali! Kuishitaki NEC kwa kutofuata sheria, kwa kudharau maoni ya wapiga kura sio sawa na kukataa au kupinga kutwawazwa JK! Safi sana! Lakini usikate tamaa kiasi hicho. Najua wanasiasa wanapinda pinda njia hadi wafike wanakotaka! Vuta subira!

Mimi nasubiri kwa hamu kesi za kupinga matokeo ya ubunge kama kule Moshi Vijijini, Njombe Magharibi, Geita nk, lakini sioni kinachoendelea, CHADEMA angalieni msije mkatupelekesha kwingine!

Hakuna kitu yaelekea huyo Ruta sio mwanasheria... Kwenye mahakama sio urobot pale lazma utashindwa maana kila wakili anajua sheria sasa huko ni kupoteza kesi kirahisi.. Hata mimi ningepewa hiyo kesi siwezi maana hiyo sheria ya mwaka 1992 iliyoko ibara ya 41(7).. Huwezi kuifuta au kumzuia mwenzio kuitaja mahakamani.. Cha msingi mahakamani ni lazma uwe na kesi ya msingi lakini hiyo ibara inailinda hata NEC.. Na lazima mwenzio umweke kwenye mazingira ya kujibu kesi(shitaka) kama sivyo huwezi kufika mbali zaidi utaabika... Sisi wanasheria tunajua hilo... Waacheni CHADEMA waendelee na hilo ili CCM wakiloga wakaenda mahakamani kwa kesi ya kikatiba sasa hapo kazi itakuwa rahisi sana....
 
Chadema tumewachagua kutuwakilisha bungeni na wala siyo vinginevyo......wasipokwenda bungeni kwa visingizio vyovyote vile hapo watakuwa wanamkomoa mpigakura na wasifikiri tutawachagua tena........................next time tutakaa nyumbani na wacha hao CCM waendelee kututesa maana yawezekana kabisa taifa hili Mwenyezi Mungu kalilaani................

Kama Chadema wana ushahidi wa ya kuwa kura za vituoni zinatofautiana na zile ambazo NEC ilizitangaza sasa ni nini kinawazuia kulalamika mahakamani? Hicho kiji-Ibara cha katiba cha kuzuia matokeo ya kura za Uraisi yaliyotangazwa na NEC kuhojiwa mahakamani msikisome kijuu juu tu........Hakizuii hoja za kimsingi kusikilizwa na mahakama zetu na huo ni msimamo wao wa tangu mwaka 1995........Kumbukeni kazi ya kutafsiri sheria ni ya mahakama......nendeni huko mkadai haki yenu na kama mahakama ikikataa kuwasikiliza sasa ndiyo mrudi kwetu na hapo tutajua ya kuwa hata mahakama zinadi ukarafati mzito..

Katiba yetu iliweka dhana ya kuwa matokeo yaliyotangazwa na NEC kulingana na taratibu za kisheria ndiyo tu ambayo mahakama haiwezi kuyahoji lakini katiba yetu haikukusudia ya kuwa NEC wavunje sheria za uchaguzi katika kuyatangaza matokeo hayo na mahakama zinapolalamikiwa zikae kimya........................la hasha.................siyo hivyo hata kidogo........

Madai ya chadema kama yana ushahidi ni lazima yafikishwe mahakamani na hoja ya muhimu ni kuwa NEC haikufuata sheria ya uchaguzi na taratibu zake kwa kuyadharau matokeo ya kura kama zilivyopigwa na wananchi na wao kujitangazia matokeo wayatakayo tu wenyewe.........................Mahakama ikipata ushahidi wa kutosha na kuridhika itayatengua matokeo ya Uraisi kwa sababu hayakuheshimu ridhaa ya wapigakura.....................

Nje ya kuufuata utaratibu huu wa kisheria Chadema nasema acheni kutuchezea watu wazima na nendeni bungeni mkafanye kazi tuliyowatuma kama hamtaki semeni na chaguzi za majimbo mliyoshinda zirudiwe na wanaotaka kutuhudumia hata kama ni kutudhulumu wache wafanikiwe kwenye malengo yao.....................

What we asking from Chadema is leadership but not a bunch of endless complaints

Hakuna kitu yaelekea wewe Ruta sio mwanasheria... Kwenye mahakama sio urobot pale lazma utashindwa maana kila wakili anajua sheria sasa huko ni kupoteza kesi kirahisi.. Hata mimi ningepewa hiyo kesi siwezi maana hiyo sheria ya mwaka 1992 iliyoko ibara ya 41(7).. Huwezi kuifuta au kumzuia mwenzio kuitaja mahakamani.. Cha msingi mahakamani ni lazma uwe na kesi ya msingi lakini hiyo ibara inailinda hata NEC.. Na lazima mwenzio umweke kwenye mazingira ya kujibu kesi(shitaka) kama sivyo huwezi kufika mbali zaidi utaabika... Sisi wanasheria tunajua hilo... Waacheni CHADEMA waendelee na hilo ili CCM wakiloga wakaenda mahakamani kwa kesi ya kikatiba sasa hapo kazi itakuwa rahisi sana....
 
Tatizo wakienda mahakamani kesi zitapigwa dana dana na wao hawawezi kuongelea tena jambo ambalo liko mahakamani wao washitaki kwa wananchi tuu
 
Utumbo tu unaandika mrefu namna hiyo!!! Je, ukiandika mambo ya maana si tutasoma mwaka mzima!!.
Ni vyema ukabainisha kama kusisitiza kufuata sheria ni utumbo...je kutofuata sheria na kuleta vurugu ni nini? You will never gain from chaos.........the incumbent will just get stronger.........while you will be struggling to make ends meet...............patience and following the law is a key here..............Nyerere mwaka 1958 alikutana na changamoto kama hizi hizi........mkoloni aliweka upigaji kura wa tatu mzungu, mbili kwa mhindi na moja kwa mwafrika.........................Nyerere aliposema tukubali kuiheshimu hii sheria dhalimu wapo waliomtukana kwa sababu hawakuona mbali na ndiyo Nyerere aliyekuwa na kiona mbali nchi ataendela kuwa yeye tu....................watu wanafikiri kuna majibu mepesi ya hili suala.......ukweli ni kuwa hakuna ila unafuu upo kwa kufuata sheria zilizopo na hata kama zina mapungufu....................Kama mahakama zingelikuwa hazitendi kiujumla haki hivi mara tatu mbona zimesema Dr. Slaa kuchaguliwa kwake hakukuwa na dosari kama mbunge wa karatu? Hivi kwani hatujui anayewateua hao majaji? Yapo masuala ambayo ni wazi kama hili la NEC kuboronga na mahakama haiwezi kufumbia macho hata kidogo..........Kama Chadema wakiwaomba kufanya hivyo....
 
Hakuna kitu yaelekea wewe Ruta sio mwanasheria... Kwenye mahakama sio urobot pale lazma utashindwa maana kila wakili anajua sheria sasa huko ni kupoteza kesi kirahisi.. Hata mimi ningepewa hiyo kesi siwezi maana hiyo sheria ya mwaka 1992 iliyoko ibara ya 41(7).. Huwezi kuifuta au kumzuia mwenzio kuitaja mahakamani.. Cha msingi mahakamani ni lazma uwe na kesi ya msingi lakini hiyo ibara inailinda hata NEC.. Na lazima mwenzio umweke kwenye mazingira ya kujibu kesi(shitaka) kama sivyo huwezi kufika mbali zaidi utaabika... Sisi wanasheria tunajua hilo... Waacheni CHADEMA waendelee na hilo ili CCM wakiloga wakaenda mahakamani kwa kesi ya kikatiba sasa hapo kazi itakuwa rahisi sana....

Maana CHADEMA watawasilisha ushahidi halafu dunia nzima itaamini waliibiwa... Mahakama haiwezi kumtoa raisi aliyeko madarakani lakini aibu ni zaidi ya kishindo cha tetemeko.. Mwili utakufa ganzi kwa simanzi:A S crown-1:
 
CCM ni mabingwa wa kucheza Danadana Mahakamani.

Wao wakituhumiwa hawaendi mahakamani huishia kutoa maneno matupu majukwaani.

CHADEMA wakienda mahakamani hukumu ya haki inaweza kutolewa, lakini je serikali itakuwa tayari kutekeleza hukumu hiyo??

Ni kitu gani kitawasukuma kutekleza hukumu juu ya Wizi wa NEC wakati kwa miaka zaidi ya 10 sasa bado wananajisi Maamuzi ya Mahakama juu ya kesi ya Mgombea Binafsi katika chaguzi zote za kisiasa??

Serikali ya CCM haiheshimu Mahakama pia haiheshimu wananchi.
Serikali ya CCM inacheza na HAKI za WaTanzania.

Kimsingi wewe na watu wengine wa aina yako ndo mnakubali kuchewa ili hali nyie ni watu wazima na akili zenu. Sijui mwenzetu unfaidika nini na Ubabe wa Serikali ya CCM kutia kiburi kutekeleza hukumu za Mahakama??

Kazi amabayo Wabunge wa CHADEMA walitumwa na wananchi kuifanya,watafanya kwa asilimia 100%.

Kusikiliza Hotuba ya Rais si moja ya kazi walizotumwa kufanya na wananchi Bungeni. Hotuba ya Rais bungeni ni symbol tu haina meno pale Bungeni wala si Muswada. Rais anaweza kutekeleza kazi yake akiwa Ikulu na wabunge wanaweza kutekleza kazi yao wakiwa Bungeni bila kumtegemea Rais hata 0.1% ya ushauri wa Rais.

Iwapo serikali itatekeleza Hukumu ilotolewa kuruhusu Mgombea Binafsi katika ngazi zote za chaguzi za kisiasa maneno yako yanaweza kuwa na ujasiri hapa JF, kinyume chake unajikonga nafsi yako tu.

Rais akija tena kuhutubia Bunge, nawaombeni wabunge wa CHADEMA kuendeleza utaratibu wenu mzuri wa kuichinia hotuba yake. ujumbe mlioutuma umesikika vyema, umeeleweka vizuri na pande zote mbili, Nia na kusudio lake limetia.

Zile dakika chache mlizo andamana pale bungeni zimepeleka ujumbe wa nguvu zaidi kuliko Mandamano ya Watanzania 7,000,000. Zaidi mmeepusha mabomu ya machozi Virungu vya polisi na hata umwagaji damu usio wa lazima endapo wananchi wangeingia mtaani na ujumbe kama wenu.

Hongera sana CHAEMA msisikilize maneno ya akina ZAZU.

BIG UP MZEEE!!!!! Hapa JF tunataka hoja kama hii, imekaa kisomi zaidi. Yani imetulia.
 
Huko bado kutakuwa ni kumpigia mbuzi gitaa, hakuna MAHAKAMA kubwa zaidi ya NGUVU YA UMMA!.

Sasa hivi tuko kwenye mgogoro wa ki-KATIBA na CCM washaonyesha kuwa peke yao hawana uwezo wa kuhimili mikiki-mikiki yake.

Kitendo kidogo tu cha wabunge kususia hotuba ya Mkwere tayari wameshaanza kubabaika, yale yatakayofuatia baadaye ndio itakuwa mtaji kwa CHADEMA kufungua ukurasa mpya wa demokrasia ya kweli.

Amini usiamini safari hii WANANCHI watahamisika ili kubadili KATIBA na hakuna mahakama yeyote itakayopinga maamuzi yao...
The beauty of human life is hope..........so I encourage you to keep hoping for the best....................................Good luck as I have a sneaky feeling you will need it........all the way.......
 
Ni kweli kaka, kuna kila sababu ya kupigana pande zote, waende mahakamani na wakati huohuo harakati nyingine zinaendelea.

Ninashukuru......finally someone has understood me..........................attack the problem from all directions..........do not limit your horizon by picking on flimsy excuses...........................
 
Katiba haiwaruhusu kwenda Mahakamani kupinga jambo lolote kuhusu ushindi wa rais uliotangazwa na NEC.

Kitendo cha kwenda Mahakamani kupinga matokeo ni uvunjaji wa katiba.

Kesi wawezayo kuifungua Chadema ni ile ya kupinga Kifungu cha katiba kinachowazuia kupinga matokeo ya Urais.

Kesi ya namna hiyo ikifunguliwa leo haiwezi kuhusisha wizi wa kura zilizo muweka Kikwete ikulu bali itabidi hoja nyingine zijengwe kuipa nguvu kesi hiyo.
Let us say CHADEMA wameshinda kesi hii dhidi ya kifungu cha katiba.

Nikirejea swali langu la msingi kwako.
Je ni msukumo gani utaifanya serikali ya CCM kutekeleza hukumu hii mpyya wakati kuna kigonela cha hukumu ya mgombea binafsi ambayo Serikali ya CCM bado inanajisi utekelezaji wake bila aibu hadi dakika hii niandikapo?

MM:

Hiyo ni katiba gani inayozuia? Haya ndio matatizo ya watanzania wengi kutoelewa haki zao za kikatiba na kisheria. Kama kweli kipo hicho kipengere au ibara naomba utuonyeshe.

Hili mahakama iendeshe shughuli zake ni lazima KESI IFUNGULIWE. Mpaka sasa CHADEMA hawajafungua kesi na katiba haikatazi kufungua. Hivyo basi ibara yoyote katika katiba haikatazi ufunguaji wa kesi mahakamani.

Pili kipengere cha katiba kinachoonyesha kuwa NEC ikishatangaza matokeo, hakuna mahakama itakayochunguza matokeo hayo kina utata mkubwa. Sio kazi ya mahakama kuchunguza. Kazi ya mahakama ni kutoa hukumu yanayohusiana na mambo ya kisheria.

(7) Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais kwa mujibu wa ibara hii, basi hakuna Mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka ya kuchunguza kuchaguliwa kwake.

Tatu, kama kuna kasoro zozote basi kutakuwa na watu waliovunja sheria kwa makusudi. Wasimamizi wa ngazi zote za uchaguzi walilipwa na waliapa kufanya kazi zao kwa kufuata taratibu. Hivyo mahakama inaweza kutokuwa na uwezo wa kubadilisha matokeo lakini ina haki ya kusikiliza na kutoa hukumu kwa waliovunja taratibu za uchaguzi.

Nne, ni muhimu kwa CHADEMA kufungua kesi. Katika marekebisho ya katiba, hukumu za mahakama zinachukua uzito. Hivyo sio lazima CHADEMA wafungue ya kutengua matokeo ya urais. Lakini wanaweza kufungua kesi zitakazofanya marekebisho ya katiba.
 
Ninashukuru......finally someone has understood me..........................attack the problem from all directions..........do not limit your horizon by picking on flimsy excuses...........................

ACHENI KUJAZA UPUUUUZI KWENYE MASWALA YA MSINGI NA SENSITIVE KAMA MAHAKAMA...Ni kosa kubwa sana kuongelea kesi iliyo mahakamani nje ya mahakama... Tena ni dhambi kubwa ya kukupeleka jela zaidi ya miaka mi3 nadhani... Kama jambo ni la jukwaaa basi jukwaani vinginevyo mahakama na ukae kimya... Sheria ni msumeno.. Lakini CHADEMA wane Tundu Lissu nakumbuka ndie alikuwa best student pale UDSM... He is smart and He knows how to jump within the Law...
 
MM:

Hiyo ni katiba gani inayozuia? Haya ndio matatizo ya watanzania wengi kutoelewa haki zao za kikatiba na kisheria. Kama kweli kipo hicho kipengere au ibara naomba utuonyeshe.

Hili mahakama iendeshe shughuli zake ni lazima KESI IFUNGULIWE. Mpaka sasa CHADEMA hawajafungua kesi na katiba haikatazi kufungua. Hivyo basi ibara yoyote katika katiba haikatazi ufunguaji wa kesi mahakamani.

Pili kipengere cha katiba kinachoonyesha kuwa NEC ikishatangaza matokeo, hakuna mahakama itakayochunguza matokeo hayo kina utata mkubwa. Sio kazi ya mahakama kuchunguza. Kazi ya mahakama ni kutoa hukumu yanayohusiana na mambo ya kisheria.

Tatu, kama kuna kasoro zozote basi kutakuwa na watu waliovunja sheria kwa makusudi. Wasimamizi wa ngazi zote za uchaguzi walilipwa na waliapa kufanya kazi zao kwa kufuata taratibu. Hivyo mahakama inaweza kutokuwa na uwezo wa kubadilisha matokeo lakini ina haki ya kusikiliza na kutoa hukumu kwa waliovunja taratibu za uchaguzi.

Nne, ni muhimu kwa CHADEMA kufungua kesi. Katika marekebisho ya katiba, hukumu za mahakama zinachukua uzito. Hivyo sio lazima CHADEMA wafungue ya kutengua matokeo ya urais. Lakini wanaweza kufungua kesi zitakazofanya marekebisho ya katiba.

Isome sheria hii vizuri kwa kiingereza... Kutafuta suluhu ni lazma Jaji ataomba vielelezo kutoka NEC na hiyo tuu inatosha ku-define investgation
 
Isome sheria hii vizuri kwa kiingereza... Kutafuta suluhu ni lazma Jaji ataomba vielelezo kutoka NEC na hiyo tuu inatosha ku-define investgation

Huoni kuwa unakanyaga. Unasema kutafuta suluhu ni lazima Jaji ataomba vielelezo kutoka NEC. Sio lazima Jaji aombe vielelezo. Anatoa hukumu kutokana na vielelezo vya pande vinazopingana. Hiyo ni deliberation na sio investigation.

Na kwa kiingereza:

(7) When a candidate is declared by the Electoral Commission to have been duly elected in accordance with this Article, then no court of law shall have any power to inquire into the election of that candidate.

Vilevile ni kazi ya mahakama kusema kuwa kesi imefungwa kwa sababu kipengere cha katiba kinawazuia kufanya hivyo.
 
Chadema tumewachagua kutuwakilisha bungeni na wala siyo vinginevyo......wasipokwenda bungeni kwa visingizio vyovyote vile hapo watakuwa wanamkomoa mpigakura na wasifikiri tutawachagua tena........................next time tutakaa nyumbani na wacha hao CCM waendelee kututesa maana yawezekana kabisa taifa hili Mwenyezi Mungu kalilaani................

Kama Chadema wana ushahidi wa ya kuwa kura za vituoni zinatofautiana na zile ambazo NEC ilizitangaza sasa ni nini kinawazuia kulalamika mahakamani? Hicho kiji-Ibara cha katiba cha kuzuia matokeo ya kura za Uraisi yaliyotangazwa na NEC kuhojiwa mahakamani msikisome kijuu juu tu........Hakizuii hoja za kimsingi kusikilizwa na mahakama zetu na huo ni msimamo wao wa tangu mwaka 1995........Kumbukeni kazi ya kutafsiri sheria ni ya mahakama......nendeni huko mkadai haki yenu na kama mahakama ikikataa kuwasikiliza sasa ndiyo mrudi kwetu na hapo tutajua ya kuwa hata mahakama zinadi ukarafati mzito..

Katiba yetu iliweka dhana ya kuwa matokeo yaliyotangazwa na NEC kulingana na taratibu za kisheria ndiyo tu ambayo mahakama haiwezi kuyahoji lakini katiba yetu haikukusudia ya kuwa NEC wavunje sheria za uchaguzi katika kuyatangaza matokeo hayo na mahakama zinapolalamikiwa zikae kimya........................la hasha.................siyo hivyo hata kidogo........

Madai ya chadema kama yana ushahidi ni lazima yafikishwe mahakamani na hoja ya muhimu ni kuwa NEC haikufuata sheria ya uchaguzi na taratibu zake kwa kuyadharau matokeo ya kura kama zilivyopigwa na wananchi na wao kujitangazia matokeo wayatakayo tu wenyewe.........................Mahakama ikipata ushahidi wa kutosha na kuridhika itayatengua matokeo ya Uraisi kwa sababu hayakuheshimu ridhaa ya wapigakura.....................

Nje ya kuufuata utaratibu huu wa kisheria Chadema nasema acheni kutuchezea watu wazima na nendeni bungeni mkafanye kazi tuliyowatuma kama hamtaki semeni na chaguzi za majimbo mliyoshinda zirudiwe na wanaotaka kutuhudumia hata kama ni kutudhulumu wache wafanikiwe kwenye malengo yao.....................

What we asking from Chadema is leadership but not a bunch of endless complaints

- Simply a great thinking, saafi sana mkuu tufike mahali tuachane na kufikiri kwa mafungu na tuwe huru kama Mheshimiwa Zitto.

William.
 
Sitakuwa nimeitendea haki jamii yangu ya kitanzania kwa kukosa kusifia kitendo cha kijasiri kilichofanywa na wapiganaji wa CHADEMA kwani ndio njia pekee ya kuonyesha kwamba hata uvumilivu una mwisho. si mara moja wala mbili sisiem wamekuwa wanaona sawa tu kukalia utashi wa watu bila kuzingatia madhara wanayo yaleta kwenye jamii.

Kwa walichofanya CHADEMA inatosha sasa kuwaonyesha hawa watawala uchwara kwamba tunapaswa kuwa na hofu ya pamoja katika kushughulikia na kujali haki ya watu.

Ni upambavu ujinga na matumizi mabaya ya mali na rasilimali mbali mbali za nchi hii katika kutekeleza demokrasia halafu wananchi wanachagua viongozi wao halafu wao wanatangaza wanavyotaka hii sio haki na ujumbe lazima utumwe katika kukemea suala hili.

Ni bora kusema usisikilizwe kuliko kutosema kabisa, tuko pamoja CHADEMA kilio chenu ni kilio cha Mungu kwani uhayawani wa watanzania kunyamazia kila kitu hata pale ambapo haki zao zinachezewa unaelekea mwisho. Inaelekea staili iliyotumika kupata uhuru wetu imetufanya tumekuwa wazembe hata kwenye kudai haki na hii ndio inayowafanya hawa warithi wa utawala kufanya watakavyo.
Watake wasitake yana mwisho haya, tumeona falme zilizokuwa na nguvu lakini mwisho wake hatimaye ulifika. Utawala kama wa Mabutu ambao uliwekwa madarakani na dola zenye nguvu duniani (US) na kusababisha wanamapinduzi wa Zairi kuuawa lakini mwisho ulifika hatimaye sembuse sisiem, nabashiri kwamba mwisho wao hauko mbali na dhuluma waliyofanya katika uchaguzi huu ni laana ambayo haitawaacha hivihivi tusubiri tuone!
Asante Jayfour. Tatizo la watanzania wengi linafanana na lile la wabunge waliochaguliwa kwa tiketi ya CCM ambao sasa wamebatizwa kuwa mavuvuzela wa Makamba na Kikwete yaani hushangilia kila jambo linalotoka kwa mtu waliyeelekezwa kutetea CCM kama wanavyofanya sasa, yaani wanapiga meza na kushangilia hata Spika "mtiifu wa CCM" anapopiga chafya au kuropoka utumbo!
Hakuna anayejishughulisha kujua CHADEMA wamevunja sheria ipi bali wameng'ang'ania eti "wamevunja sheria". Ukweli utabaki palepale; yaani kitendo kilichofanywa na wabunge majasiri hawa kimeingia kwenye historia; yaani wamekataa kuketi na kumsikiliza mtuhumiwa wa uhaini JK ambaye kwa kushirikiana na vyombo vilivyotarajiwa kuzuia uhaini kutokea kama Usalama wa Taifa, Polisi na Jeshi amepindua mamlaka halali iliyochaguliwa na wananchi na kuipora nafasi ya "Urais". Kosa la uhaini ni kubwa, linalodai adhabu kubwa, lakini sasa limezoeleka kwa viongozi wa kiafrika wanochakachua kura na kisha kuamua kuunda serikali za mseto kwa "presha" za viongozi wachakachuaji wenzao.
Imetokea hivyo Kenya, Zimbabwe na sasa wanataka iwe hivyo visiwa vya Bikini ambako baada ya chama tawala "kuchakachua" kura na kuwaudhi wapiga kura walioandamana na kuiondoa serikali ya kitapeli kwa nguvu, viongozi wa kiafrika; wengi wao wachakachuaji wanahaha kuirudisha serikali ya "mwenzao" angalau katika mfumo wa "mseto". Hakuna sheria ya nchi hii inayolazimisha mbunge au mtu yeyote kumsikiliza rais anapolihutubia Bunge, awe ameingia madarakani kwa kura za halali kama alizopata Kikwete 2005, au kwa njia ya ulaghai kama hii ya 2010!
Hebu tafakari kama si ulaghai, mgombea urais mmojawapo alilalamikia makosa katika utangazaji matokeo ya kura za urais; ambapo kwa mshangao mkubwa tume iliharakisha kumtangaza Kikwete mshindi na kumwapisha "chapchap". Mi naafiki na wanaosema Kikwete ni rais wa NEC lakini si wa nyoyo za watanzania. NEC ilifanya hivyo hivyo ikijua fika kwamba katiba ya "kubumba" tunayoitumia sasa hairuhusu mahakama kuhoji utaratibu au makosa ya namna rais alivyotangazwa mshindi. Njia pekee zinazobaki kufanya hivyo ni au kuandamana na kuidai haki hyo kwa nguvu kama ilivyofanyika kule Bikini au kutumia njia za amani kama walizotumia CHADEMA.
 
Chadema hawana jema wala hawana cha kuibiwa kura. Wameona wameshindwa kwa kishindo, kwani wao walikuwa na uhakika kabisa wa kushinda, sasa roho zinawauma wanatafuta mbinu za kupakaza, hatujaona ushahidi wowote walioueleza au kufikisha suala hili mahakamani. Wanachofanya ni kuburuzwa tu na Mbowe, wabunge wa Chadema wengine, wenye muono, wameona ni upuuzi na wakasusa hata kuingia Bungeni.

Duu! Kwa stahili hii wabongo bado tunasafari ndefu.:angry:
 
Ninashukuru......finally someone has understood me..........................attack the problem from all directions..........do not limit your horizon by picking on flimsy excuses...........................

Ruta:

Tatizo la wanasiasa wengi ni kutaka power. Lakini kama wanataka mabadiliko kuna njia nyingi sana.
 
Hivi nilisikia neno MAHAKAMA?????????????????????

Mahakama gani hiyo, ile ya kawaida au ya wananchi??? Kama ni zile mahakama za kawaida tunazozifahamu siku zote basi ni maelekezo mazuri kwa sababu kama ambavyo nyumba za ibada siku zote huwa ni nyumbani kwao na 'AMANI' na 'UPENDO' nako Mahakama hutarajiwa kuwa na nembo ya kuwa'HURU' kwa maamuzi yake na kuhakikisha 'HAKI' sawa kwa wote wakati wowote ule. Nahodha mkuu mwenye kukabidhiwa duka hilo anatajwa kuwa ni 'JAJI'.

Sasa, tunapofika kwenye kwake huyu msimamizi wa duka maarufu wa kutoa haki ndipo ninaposita kukuunga mkono ushauri kwa CHADEMA japo ina nia njema sana. Shida yangu yote hapo ni kujiuliza kwamba hasa ni kitu gani kitakachomfanya Mtunza duka mwingine aone kasoro katika jambo ambalo mtunza duka mkuu, Jaji Mstaafu Makame????? Au CHADEMA wakajaribu tu kupita njia hiyo licha ya KATIBA kufunga rasmi njia zote za kimahakama?????????????????????????????????????
 
...Katika nchi zenye kuheshimu haki na utawala wa sheria, mahakama ni kimbilio la watu wenye kutafuta haki. Nina wasiwasi na mahakama zetu... kama NEC wameshindwa kutenda haki, kwanini mahakama zilizopatikana kwa taratibu zilezile zitende haki kwa shauri hili? Labda kuna kitu nakikosa... Tunategemea kupata nini huko mahakamani kwa shauri hili?
Kwenye kesi ya mgombea binafsi hakuna hata mtu mmoja wa CCM aliyehamaki na kutikisika, na matokeo yake tumeyaona. Hili la CDM kususia hotuba, kila mmoja amehamaki; na wamehamanika kwelikweli. Big up CDM!!
 
Back
Top Bottom