Nimepata kuwa na mjadala na Ruta (mweka thread hii) juu ya katiba na suala la kupinga mahakamani maamuzi ya NEC. Jamani, nashangaa suala hili bado linazidi kuchanganya tu watu. KATBA YETU HAIRUHUSU KWENDA MAHAKAMANI KUPINGA KILE NEC ILICHOFANYA. MI SIELEWI TATIZO LIKO WAPI. SIELEWI. TUTAISHIA KUWALAUMU CHADEMA BURE. MTU AKITAKA KWENDA MAHAKAMNI ATAISHITAKI NEC AU JK AU CCM? KATIBA INASEMAJE? SOMENI KATIBA JAMANI............!!!!!
Pole sana kasome Ibara Na 41(5) ya Katiba ambayo yasema NEC ni lazima iheshimu taratibu za kisheria za sheria ya uchaguzi zilizowekwa katika kumpata Raisi..........................na baada ya hapo rudia kusoma Ibara Na. 41(7) ambayo imeweka bayana kuwa matokeo ya Uraisi hayatahojiwa na chombo cho chote kama yalipatikana kulingana na maelekezo ya Ibara hii ya 41......................
Swali ambalo unapaswa kujiuliza hivi NEC walizingatia Ibara 41(5) ya katiba katika kumtangaza JK kuwa ni Raisi? Jibu ni hapana.........sasa kama ni hapana maangalizo yaliyotolewa na katiba ya aina gani ya matokeo ya Uraisi ambayo mahakama haiwezi kuyahoji imetimizwa? Jibu ni hapana............Sasa hoja ya kuwa Ibara 41(7) imekataza mahakama kuingilia NEC inatoka wapi?
Labda kwa manufaa ya ambao hawajui Ibara hii ya 41(5) ninainakili hapa:-
"
All the other matters concerning to the procedures for the election of the President, shall be as provided for in law enacted by Parliament in that behalf,..............................
Sasa Ibara ya
41(7) ambayo wengi humu wanaikimbilia kutetea ututusa uliomo ndani ya Chadema ni hii hapa:-
"When a candidate is declared by the Electoral Commission
to have been duly elected in accordance with this Article, then no court of law of law shall any power to inquire into the election of that candidate."
Maeneo niliyoyawekea alama nyekundu ndiyo ambayo mahakama itabidi iyachunguze ya kuwa je NEC iliheshimu Ibara ndogo
41(5) kabla ya kumtangaza JK kuwa Raisi wetu na hivyo kuinyima mahakama uhuru wa kuchunguza matokeo hayo? Na matokeo ambayo mahakama haiwezi kuyachunguza ni yale tu ambayo mahakama itajithibitishia ya kuwa hayakukiuka Ibara yote ya
41 kama angalizo hili lisemalo.................................."...........
to have been duly elected in accordance with this Article....................."
Acheni kutetea ututusa wa kishera ndani ya Chadema na hii siyo mara yao ya kwanza...................Kumbuka katika chaguzi ndogo ya kule Mbeya waligoma kwenda mahakamani wakidai chaguzi kuu ilikuwa karibu...........What a nonsense!!!........Hii ilitokana na NEC kuliondoa jina la mgombea wake wa Chadema kwa visingizio hakuweka sahihi na mhuri wa hakimu kama sheria ndogo ya uchaguzi inavyoelekeza............mzimu huo wa kutokwenda mahakamani umewasababishia Chadema madhara ya wagombea wake wengi kwenye chaguzi kuu waliokuwa wakidai wanaisubiria na hivyo kuenguliwa kwa tatizo ambalo mahakama ingekuwa imelifuta siku nyingi la kukataza sheria ndogo ndogo kuwanyima wapigakura haki ya kimsingi ya kikatiba ya kuchagua viongozi wao.........Dosari ndogo ndogo za sheria za uchaguzi zilipaswa kutumika kuwapa waliokosea angalau nafasi moja ya kwenda kuzirekebisha badala ya utaratibu wa hivi sasa kuwa ni nyundo ya kuwanyang'anya wapigakura haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wao wawapendao.