Chad: Serikali Yapinduliwa!!!

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,187
671
Habari Zilizoenea Ni Kuwa Waasi Wa Serikali Ya Chad Wakitokea Magharib Mwa Sudan Wameingia Mji Mkuu Wa Chad Ndjamena Na Wanaelekea Ikulu Na Rais Wa Nchi Hiyo Idris Deby Ameshakimbia Nchi.

Habari Hizi Nimezipata Kwenye Bbc.

Jamani Afrika Tunaelekea Wapi?

Jee Mheshimiwa Kikwete Ataweza Kusaidia Kutatua Hali Hii Wakati Kenya Bado Maji Hayajakauka Haya Mengine Yanamwaika?

Afrika Tuwe Pole, Halafu Nijuavyo Serikali Ya Chad Ina Mkataba Na Ufaransa Wa Ulinzi Sasa Hawa Wafaransa Wako Wapi?
 
Hio coup ya chad mimi naisapoti kabisa maana Debby amefanya nchi ni kama yake binafsi!!!! Yes many people have died, and very sorry to their families lakini ndio hivyo maybe that is the only close alternative that is around!!!!!!!!!!
 
Huyo Debbi naye sii alitoka mstuni 13 years akaangusha serikali???

Mwaka juzi amebadili katiba aendelee kutawala without limit- tamaa ya madaraka!

Kwani Debbi, M7, Jammie wote sii waliingia madarakani kwa mtutu wa bunduki? Na walipoingia wamekataa kuondoka?

JK ana kazi kubwa- crises in DRC, Chad, Sudan, Commoro, Kenya, I Coast, Burundi!!

Crises kila siku -hivi Afrika itakuwa stable lini?
 
Pundit

Nenda Bbc Wameiweka Kwa Ufupi Utikuta Pale, Ila Serikali Wanakanusha Kuwa Rais Kakimbia, Pia Wanasema Wanawadhibiti Waaasi Na Waasi Na Wao Wanajitapa

Kazi Si Ndogo Tufatilieni Hii Habari
 
Labda wakuu wakati wanakula na kuishi kwenye mabangalow, wanajeshi hawalipwi etc etc;

DSC04397.JPG


Picha kwa hisani ya Jiji La Dar Blog;

DSC04388.JPG


Hizi nchi za kiaafrika kuangushwa ni bei rahisi ukilinganisha na eventual returns. Sema wote wezi wanaokua kwenye madaraka wanakuwa wachoyo na hawajui kuwalipa watu wao wanaoweza kuleta mapinduzi. Na wazungu wanasapoti upande wowote wenye kuwafaidisha.

So, hamna cha ajabu hapo. Same old same old story!! Na itaendelea kutokea Afrika......Every dog has its day.
 
kama hii taarifa ni kweli, je haiwezekani wafaransa wameipa
"nod" baada ya ile kesi ya jamaa waliofungwa kwa kosa la
kufanya biashara ya watoto?
 
1. JK amatoa msimamo wa AU kuwa kama rebels wakichukua madaraka basi they will be expelled from AU!

Taabu madiktator Afrika wamekuwa wengi sana- halafu hawataki kuachia ngazi!

Halafu unafiki wa AU kulindana!

2. Kafara
France hawakufurahia wale wazungu kuhukumiwa Chad- may be wamemgeuka Debbi. Taabu ya France are known to cause instability in Afrika- angalia Ivory Coast, Rwanda 1994, na sasa Chad!

Leo Sakoz amefunga ndoa rasmi Paris na yule Ex- Model! Watu 20 tu ndo waliohudhuria!
 
Tatizo serikali zetu nyingi zinakosa legitimacy. Hivyo lazima watawala wetu wakikutana Addis ajenda inakuwa ni kujilinda kwa kutoruhusu mapinduzi. Lakini kwa suala la Debbi hata kama Chad itakuwa epelled from Addis haitakuwa na maana, kwani kuweko kwa Debbi madarakani hakukuwa na tofauti na mafisadi tulionao. Wanapoona issue nyeti wanakimbilia USA huku wakiacha maagizo ya hakuna cha kujadiliwa mpaka watakaporudi.
 
Habari Zilizoenea Ni Kuwa Waasi Wa Serikali Ya Chad Wakitokea Magharib Mwa Sudan Wameingia Mji Mkuu Wa Chad Ndjamena Na Wanaelekea Ikulu Na Rais Wa Nchi Hiyo Idris Deby Ameshakimbia Nchi.

Kwa hiyo Mtu wa Pwani bado unapiga ramli, kwani kama unavyosea ndio wanakaribia Ikulu.
 
mvts za rebels zipo www.cnn.com kwa takribani siku tatu sasa........lakini kuna updated report(about 10:22 AM EST) ya kina!!!! kana unataka tinga hapo cnn.com
 
Habari hizi ni kweli ila haijulikani Rais yuko wapi . Hakuna mapigano kule na hadi sasa waasi wanaendesha magari maeneo ya Ikulu na maeneo mengine nyeti bila ya Upinzani. More news to follow . Au JK karuki kusema hawatatambua lakini wanajisahau kwamba haya ni matokeo ya watu kukata tamaa kama mambo ya BoT
 
mvts za rebels zipo www.cnn.com kwa takribani siku tatu sasa........lakini kuna updated report(about 10:22 AM EST) ya kina!!!! kana unataka tinga hapo cnn.com

Jamaa wamekatiza jangwa na mapick up yao wakitokea Sudan, baadhi ya witnesses walioko Hotel Le Meridien wanasema baadhi ya wananchi waliwakaribisha rebels kwa shangwe, sasa I guess baadhi ya wananchi washachoka na utawala wa Deby.
 
Jamaa wamekatiza jangwa na mapick up yao wakitokea Sudan, baadhi ya witnesses walioko Hotel Le Meridien wanasema baadhi ya wananchi waliwakaribisha rebels kwa shangwe, sasa I guess baadhi ya wananchi washachoka na utawala wa Deby.400 rebels wako mjini na hawataki mchezo . Wacha tuangalie . Ama kweli watawala wa Africa sijui wana laana gani . Yaani wanasoma Ulaya na kuishi huko ila wakirudi huwa hawajui ama wanasahau yale waliyo yaona ugenini .Balozi wao sasa anawaita wale ni Terrorists baada ya kumwaga mabovu nyumba ya Balozi wa Saudi Arabia . Nadhani Saudi Arabia watakuwa wameshiriki uozo so wana wamwagia nyongo na tindikali .
 
400 rebels wako mjini na hawataki mchezo . Wacha tuangalie . Ama kweli watawala wa Africa sijui wana laana gani . Yaani wanasoma Ulaya na kuishi huko ila wakirudi huwa hawajui ama wanasahau yale waliyo yaona ugenini .Balozi wao sasa anawaita wale ni Terrorists baada ya kumwaga mabovu nyumba ya Balozi wa Saudi Arabia . Nadhani Saudi Arabia watakuwa wameshiriki uozo so wana wamwagia nyongo na tindikali .

Sasa jiulize jeshi la nchi linawapiganaji wangapi mpaka wakashindwa kuwaround them up, au wanajeshi nao wameingia kwenye mgomo baridi kupigana?
 
20080202134121idriss_deby203.jpg


Wapiganaji nchini Chad wameingia mji mkuu Ndjamena na kuiteka Ikulu ya rais huku taarifa zikisema kumekuwa na makabiliano makali kati ya waasi na majeshi. Walioshuhudia wamezungumzia kuona magari ya majeshi yakiteketea barabarani.

Hata hivyo Waziri wa maswala ya kigeni wa nchi hiyo amesema Rais Deby yu salama na hali katika mji huo imedhibitiwa. Mwenzake wa Ufaransa ambayo imekuwa ikiunga mkono upande wa serikali ameshutumu hatua hiyo ya waasi kujaribu kutwaa mamlaka.

Alidai kwamba kuna mwingilio wa kijeshi kutoka nje.
Muungano wa Afrika. Inaaminika wapiganaji hao walianzia maasi yao katika mpaka wa Chad wa mashariki ulio karibu na Sudan mapema juma hili. Serikali ya Chad imekuwa ikilaumu Sudan kwa kuunga mkono wapiganaji hao na Sudan nayo ikiishutumu Chad kwa kuunga mkono waasi huko Darfur.

Ufaransa imewataka raia wake wote walioko Chad kutotoka nje.
Muungano wa Afrika umetaka waasi hao wasitishe harakati zao na kuonya kwamba iwapo waasi watatwaa mamlaka Chad itafukuzwa kutoka kwa muungano huo.
 
Historia ya Chad has been marred by instability tangu Uhuru!

Sasa kama Wanajeshi wako wanashangilia rebels badala ya kupigana nao- wewe ukiwa raisi utafanyaje? Tukumbuke pia Amini 1971 alishangiliwa pia na Waganda alipochukua nchi!

Wapi hawa rebels abot 10,000 wanapata silaha? Naskia ni msafara wa magari 300 ya Kijapani!

Muhimu conflicts Afrika kuchangiwa na forces za nje- France, US wana interest Chad baada ya kuwa Oil Exporting Country!

Naskia Debbie amekimbilia Gabon!
 
Si ndo maana SISIEMU hapa nchini wanajiwahi kwa kuwapa Maafande Ukuu wa wilaya Mikoa na kazi nyingine nyingi nyeti.

Kazi hizo wakipewa hawaziwezi na wanapwaya kishenzi kaa wamevaa kiatu size 24 wakati miguu yao ni size 8.

Tutaendelea kupinduana mpaka kieleweke.

Kama usemi kwamba "kutesa kwa zamu" ni usemi wa uhakika, sasa ni zamu ya watu wengine kutesa huko Chad.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom