Chad na Jamhuri ya Afrika ya kati (CAR) watoa wito kwa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika (AU) kuchunguza kuuawa kwa wanajeshi

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
634
1,000
Pande hizo mbili zinatambua uzito wa hali hiyo na zinasisitiza dharura ya kufafanua mazingira ambayo shambulizi hili lilifanyika, mawaziri wa mambo ya nje wa Chad na CAR walisema katika taarifa ya pamoja Jumanne jioni.

Chad na Jamhuri ya Afrika ya kati (CAR) wanatoa wito kwa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika (AU) kuchunguza tukio katika eneo la mpaka ambapo angalau wanajeshi sita wa Chad na raia watatu wa Russia waliokuwepo kwenye kazi za kijeshi kuisaidia CAR waliuawa. Kulingana na shirika la habari la Reuters.

Ujumbe kutoka CAR ulikutana na Rais wa muda wa Chad, Mahamat Idriss Deby, siku ya Jumanne kujibu tukio hilo ambalo linatishia kuwepo uhusiano mbaya wa kidiplomasia.

Pande hizo mbili zinatambua uzito wa hali hiyo na zinasisitiza dharura ya kufafanua mazingira ambayo shambulizi hili lilifanyika, mawaziri wa mambo ya nje wa Chad na CAR walisema katika taarifa ya pamoja Jumanne jioni.

Wizara ya ulinzi ya Chad, Jumapili ilisema wanajeshi wa Afrika ya kati walishambulia kituo cha jeshi la Chad ambapo walimuua mwanajeshi mmoja na waliwateka pamoja na kuwaua wengine watano, vitendo ambavyo walisema vilikuwa uhalifu wa vita.

Mamlaka ya CAR ilisema mapigano ya risasi yalitokea kwa makosa wakati wanajeshi wao walipofuatilia kundi la waasi karibu na mpaka wa Chad na kusababisha vifo vya wanajeshi wa pande zote mbili. Hawakuelezea ni wanajeshi wangapi wa Afrika ya kati waliokufa

Shirika la habari la RIA la Russia, liliripoti wanajeshi watatu wa Russia, sehemu ya ujumbe wa kusaidia jeshi la CAR pia waliuawa wakati wa operesheni ambayo ilipelekea mlipuko wa mgodi.

Msemaji wa jeshi la Chad aliliambia shirika la habari la Reuters hapo Jumanne kwamba wanajeshi wengi walipelekwa mpakani kujibu tukio hilo.

Wanajeshi wa Chad walikuwa katikati ya ujumbe wa kulinda amani wa Afrika uliopelekwa CAR baada ya uasi wa mwaka 2013 ambao ulimuondoa madarakani rais. Chad iliondoa vikosi vyake mwaka uliofuata baada ya kushtumiwa na watu huko CAR kwa kuunga mkono waasi hasa waislam, katika mzozo wao na wanamgambo wengi wakiwa wakristo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom