Kwa kufahamu kuwa Madaraka si haki yake,bali ni Jukumu la kila Mmoja,Dr Slaa ametangaza hadharani kwamba atakuwa Rais kwa kipindi kimoja tu (miaka mitano).Dr Slaa ameuonyesha Umma wa Watanzania kwamba,kila mtu anawajibika kuongoza Nchi,ikiwa tu atatimiza masharti na akikubaliwa kwa njia ya Uchaguzi (Demokrasia).Katika kipindi chote cha kampeini zake ameonyesha Uvumilivu,Uuungwana na Ustaarabu wa kutodharau au Uchochezi wa namna yoyote.Leo Mimi binafsi nautumia uhuru wangu wa kikatiba kutamka hadharani kwamba kura yangu ya NDIO nitampigia Dr.Slaa.
Dr Slaa keshaweza kutushawishi kwa maelezo kwenye kampeini zake kwamba ni Kiongozi Mahiri...Tumpe nafasi ili tumuone kwa vitendo,Kipindi chake cha miaka 15 aliyokaa Bungeni kimethibitisha kwamba ni Kiongozi mzuri,ameweza kusimamia kwa dhati kile alichoamini.Chadema leo ina uhakika wa majimbo mapya mengi kutokana na Kampeni wanazofanya Nchi nzima.Mabadiliko hayaji usiku mmoja,Chama kimejengeka zaidi....Tumpe ushirikiano Dr ili ashinde Uchaguzi Oktoba/31.Mabadiliko ya kweli yanamuhitaji kila Mtanzania...Tukianzia na juhudi ya mtu mmoja mmoja na baadaye kundi kubwa la Watu.
Sisi katika umoja wetu hapa JF tumsaidie Dr. kwa kuwashauri wale undecided voters,ambao kwa mtazamo wangu bado wapo wengi.Mimi binafsi nimewashauri ndugu zangu 20 na nina uhakika kuwa watampigia kura Dr.Slaa.Katika ndugu hawa 12 ni new voters lakini 8 walimpigia kura Kikwete katika Uchaguzi wa 2005.Nimefarijika kwa sababu hata Mama Mzazi mwaka huu atampigia kura Dr.Slaa,Mama kama Wazee wengine alikuwa anasema Wapinzani wataleta machafuko.......najisikia raha zaidi na kujiona ni mmoja wa wapenda mageuzi baada ya mmoja wa Ndugu zangu na Mgombea Ubunge kwa CCM kunithibitishia kwamba atampigia kura ya Urais Dr.Slaa.Ndugu huyu ameniasa Mimi na wapenda mageuzi wengine tuwe macho katika usafirishaji na uhesabuji kura,Matokeo huchakachuliwa ktk uhesabuji wa kura.....Hivyo kila mmoja atakayepiga kura awe mlinzi wa kura yake,Tuwepo vituoni kwa amani mpaka matokeo yatangazwe...Tujihadhari kuvaa nguo zenye viashiria vya ushabiki wa Vyama,tuwe watulivu na kuhakiki kila nyendo ktk maeneo yetu ya upigaji kura.Siku ya tarehe 31 iwe maalumu kwa ajili ya zoezi la uchaguzi tu.
Ndugu zanguni naomba kila usiku kuanzia leo, kabla ya kulala uwapigie simu au kuwa-textia ndugu zako wa karibu,na kuwakumbusha ku-vote tarehe 31 na waambie wampigie kura ya NDIO Dr.Slaa...Lugha ya Kejeli,Uchochezi na Matusi isitumiwe katika Text hizo.Kipindi hichi cha wiki moja,ni lazima tufanye kampeini ya mtu kwa mtu.Kila mtu akumbuke kuwa matokeo ya siku moja yatakuwa na impact mwa miaka 5 na kuendelea na pengine kubadili kabisa Historia ya siasa za Tanzania.Tuepuke namna yoyote ya Uchochezi na Fujo...Kwa asili watanzania ni wastaarabu na wakarimu,tuuendeleze utamaduni huu katika kipindi hichi tete cha uchaguzi.Tukishindwa tukubali Matokeo,mwisho wa siku sisi sote ni wamoja,Umoja wetu hautenganishwi na Itikadi za vyama.
"Mwenyezi Mungu Ibariki Tanzania na Uwabariki watu wake"