Cement yazidi kupanda bei mkoani Mwanza

livafan

JF-Expert Member
Oct 20, 2016
2,925
5,528
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza apo juu, Bei ya Mfuko wa cement Mwanza unazidi kupaa, awali mfuko wa cement apa Mwanza ulikuwa ukiuzwa kwa 18000/= Tsh lakini kuanzia wiki hii cement kwa mfuko inauzwa kwa 18500/= hadi 19000/= ,

Hatujui sababu kuu ni nini haswa, sijui ndio kupanda kwa bei ya malighafi!! binafsi sifahamu, yawezekana labda gharama za usafirishaji zimeongezeka!! , binafsi sifahamu pia japo nasikia bei ya mafuta imezidi kushuka, yawezekana uzalishaji wa cement umepungua labda nani ajuae?? Mwanza kunaniii .

Agents wa cements sijui ndio wanaopanga hizi bei, kusema ukweli si rafiki kwa mtumiaji wa Mwisho maana ndie aumiae.
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza apo juu, Bei ya Mfuko wa cement Mwanza unazidi kupaa , awali mfuko wa cement apa mwanza ulikuwa ukiuzwa kwa 18000/= tsh lkn kuanzia wiki hii cement kwa mfuko inauzwa kwa 18500/= hadi 19000/= ,

Hatujui sababu kuu ni nini haswa , sijui ndo kupanda kwa bei ya malighafi !! binafsi sifahamu, yawezekana labda gharama za usafirishaji zimeongezeka !! ,binafsi sifahamu pia japo nasikia bei ya mafuta imezidi kushuka , yawezekana uzalishaji wa cement umepungua labda nani ajuae ?? , Mwanza kunaniii .

Agents wa cements sijui ndo wanaopanga hizi bei, kusema ukweli si rafiki kwa mtumiaji wa Mwisho maana ndie aumiae;.
"Kumbuka pia huu ni mwaka wa uchaguzi"
 
Afadhali hata huko ipo ila bei ya juu. Arusha maduka yote ya hardware hadi leo hayakuwa na cement kabisa. Naamini lakini wiki hii itakuwepo ya twiga badala ya simba ambayo kiwanda chake sijui imekuwaje kwa sababu ndio tunatumia simenti yao na hawajaleta kwa maduka ya jumla wala rejareja.
 
Bado najiuliza kwanini Cement inatoka Pakistan inafika Tanzania with all logistics lakini bei iko either chini au sawa na hii ya hapa kwetu?

Kama Pakistan production cost iko chini kwanini tusilazimishe viwanda vifuate mfumo wa uzarishaji kama Pakistan ili bei ziwe chini watu wetu wanufaike?..

Kwanini Tusiruhusu Cement kutoka nje iingie ili ilete ushindani kwenye viwanda vya ndani nao waangalie uwezekano wa kushusha bei?..

Kwanini serikali isiangalie uwezekano wa baadhi ya viwanda vya cement kujengwa kanda ya ziwa na nyanda za juu kusika ili kurahisisha upatikanaji wa cement huko, kama materials hakuna kwanini zisijengwe mills tu na clinker ikasafirishwa na train to Mwanza pale au Isaka dry port na kanda nyingine wakapata cement kwa bei ya Dar..

Ujenzi ni gharama sana TZ hebu wakubwa angalieni namna bora ya kushusha gharama za ujenzi kuanzia viwanja na vifaa ili watu waishi kwenye makazi bora...
 
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza apo juu, Bei ya Mfuko wa cement Mwanza unazidi kupaa , awali mfuko wa cement apa mwanza ulikuwa ukiuzwa kwa 18000/= tsh lkn kuanzia wiki hii cement kwa mfuko inauzwa kwa 18500/= hadi 19000/= ,

Hatujui sababu kuu ni nini haswa , sijui ndo kupanda kwa bei ya malighafi !! binafsi sifahamu, yawezekana labda gharama za usafirishaji zimeongezeka !! ,binafsi sifahamu pia japo nasikia bei ya mafuta imezidi kushuka , yawezekana uzalishaji wa cement umepungua labda nani ajuae ?? , Mwanza kunaniii .

Agents wa cements sijui ndo wanaopanga hizi bei, kusema ukweli si rafiki kwa mtumiaji wa Mwisho maana ndie aumiae;.
Jana kulikuwa na MATAGA, anasema eti uboreshaji wa reli umesaidia kupungiza gharama za usafirishaji sana, nikamwambia bei ya bidhaa inapanda kutokana na mambo mengi sana sio usafirishaji tu. Tatizo kubwa ni gharama za uzarishaji pamoja na kodi.
 
Ndio mzidi kupiga maombi SGR ikamilike ili gharama za usafirishaji zipungue.
Sgr haitakuwa na uwezo wa kufata mzigo wa cement kutoka twiga au dangote itabidi kuwe na feeder trucks ,
Sgr pia haitwweza kudeliver kwa mlaji wa mwisho hapa nazungumzia Mimi na wewe, itabidi kuwe na delivery trucks
Tatizo la Bei ghali za cement kuwa juu linaanzia kwenye Kodi lukuki kuanzia malighafi Hadi uzalishaji
 
Ni kweli, ila gharama haiwezi kuwa sawa na ya kusafirisha mzigo kwa truck hadi Mwanza
 
Dar kwenye viwanda vya cement bei imepanda pia.
Kuna kitu cha ziada viwandani.

Hii kitu imenigharim sana. Hata kwa Dar cement imepanda bei na kuadimika kwa baadhi ya mawakala.

Nimeulizia nikaambia ujenzi wa miundombinu unaoendelwa unahitaji kiasi kikubwa sana cha cement, wakala magari yao yanasubiria sana hadi yapate nafasi ya kupakia mzigo. Ndio maana wakiipata bei iko juu. Sijui hilo lina ukweli kiasi gani ila cement inazidi kuwa bidhaa adimu au ghali.

Zanzibar wanaingiza kutoka nje (uarabuni) na bei iko rafiki.
 
bro unajua kweli bei ya mafuta???,

Hapo cha maana Ni muwekezaji kuweka kiwanda kanda ya ziwa, maana huko hakuna kiwanda lazika bei iwe juu.
Ile style ya kadri cement iendapo mbali na kiwanda huko haiapply..

Safari hii mambo sivyo. Dangote alipo ongeza bei toka June co. Zingine hazijaongeza bei . mawakala ununuzi dangote umepungua ma-co. Mengine yameelemewa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom