johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 84,035
- 142,145
Cecil Mwambe: Mbowe msalaba umemuelemea na mimi ndiye Simoni Mkirene nipo tayari kubeba msalaba huo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, mgombea wa uenyekiti CHADEMA taifa Cecil Mwambe amedai kwamba kwa hali ilivyo sasa Mh. Mbowe ameelemewa sana na msalaba wa kuongoza CHADEMA hivyo anahitaji mtu wa kumtua na kumsaidia msalaba huo.
Cecil Mwambe amefafanua kwamba yeye ndiye mtu pekee anayeweza kumpokea Mbowe msalaba huo wa uenyekiti taifa kwani kwa sasa Mbowe ameprove failure katika kuongoza CHADEMA kama mwenyekiti taifa.
Cecil Mwambe amefikia hatua ya kujifananisha na Simoni Mkirene yule mpita njia aliyekuwa akitoka mashamba ambaye baadaye alibeba msalaba wa Yesu ambaye Yesu kwa kipindi hicho alikuwa ameelemewa na msalaba huo.
Cecil Mwambe amesisitiza kwamba lazima CHADEMA wajue kwamba mabadiliko ya kuongozi ndani ya chama yanahitajika sana kipindi hiki kwani Mbowe ameshaelemewa hivyo hakuna namna lazima aje mtu wa kumsaidia ambaye ndiye yeye Cecil Mwambe.
Pia Cecil Mwambe amewaonya wale waliopanga kumnyima fomu ya kugombea uenyekiti na pia amewaonya waliopanga kugoma kupokea fomu yake kipindi anairejesha ikiwa imeshajazwa. Kwani kuchukua fomu na kuirejesha ni haki yake ya kikatiba ndani ya chama.
Cecil Mwambe ameahidi kuboresha chama na kuleta mabadiliko makubwa sana endepo atashinda na kuwa mwenyekiti CHADEMA taifa.
Source: online TV.
Mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chadema mh Cecil Mwambe amesema haitaji watu wa kumchukulia fomu kwani zoezi hilo atalifanya yeye mwenyewe kwa kuwa anajiamini.
Mwambe amesema anachoomba ni ushirikiano kutoka kwa wale wote wenye mapenzi mema na Chadema ili kwa pamoja waweze kushinda.
Source Global tv
My take; Nakubaliana na Mwambe mambo ya kuchukuliana fomu ni mbinu za kizamani zilixotumiwa na akina rip Bamchawi pale Simba SC!
Kwani kuna dhambi kuwanukuu wahusika?..........siasa siyo uadui!Wee Jo ni kigeugeu kinyonga kasingiziwa
Hahahaaa....... hahahaaa....... Wasomi wa jalalani bhana!Hapo anauzungumzia Uenyekiti wa Kanda ya Kusini. Sidhani kama inawezekana kwake kugombea Uenyekiti wa Kanda na wa Taifa.
Punguza kulazimisha mada za kitoto kama hizi. Uwe unafuatilia mambo na kuyajua kabla ya kukurupuka na kuanzisha mada humu.
Uione: johnthebaptist
Umemsikia Mwambe lakini?!CCM mnamuogopa sana mbowe, mnataka kuweka mapandikizi yenu
Si afadhali sisi wa jalalani kuliko wewe tapeli wa mtaroni? Kutwa nzima ni kutuhamishia humu vihabari vyako vya kizushi. Acha hayo mambo yako binti. Jifunze kujenga hoja!Hahahaaa....... hahahaaa....... Wasomi wa jalalani bhana!
Pandikizi lenu hiloUmemsikia Mwambe lakini?!
Kwani ana nini cha ajabu?!Atamweza mbowe?
Mimi sijasoma bhana kama nyie wanasheria nguli mnaosota jalalani.Si afadhali sisi wa jalalani kuliko wewe tapeli wa mtaroni? Kutwa nzima ni kutuhamishia humu vihabari vyako vya kizushi. Acha hayo mambo yako binti. Jifunze kujenga hoja!
Haya. Kumbuka kula na kunywa na upumzike.Mimi sijasoma bhana kama nyie wanasheria nguli mnaosota jalalani.
Mimi na mdogo wangu Mbowe " tulizungusha" form six na safari yetu ya jalalani iliishia pale.......ndio maana Freeman anakulaani hadi kesho kwa kumdanganya aruke dhamana akasota keko miezi mitatu ilhali wewe ni msomi uliyetukuka from jalalani!