Kitendo cha APR kuingia nusu fainali si habari nzuri hata kidogo kwa wana Yanga. Mechi itakuwa ngumu sana kwa vile timu hizi zilishacheza katika hatua ya makundi. APR siyo timu mbovu hata kidogo na itataka kulipa kisasi kwa Yanga, bahati mbaya hatua hii ni mtoano, ikiwa hivyo basi wana Yanga tutakuwa tumepata msiba wa mwaka. Nakumbuka mwaka 1993 kule Nakivubo stadium, Yanga ililala kwa 3-1 kwa SC Villa ya Uganda katika hatua ya makundi, timu hizi zilikutana fainali, mechi ilikuwa ngumu ajabu lakini mwisho Yanga waliibuka na kikombe katika nchi ya ugeni.
Nashauri benchi la ufundi la Yanga liweke mikakati maalum kuiong'oa APR, vinginevyo msiba unanukia.