Watanzania kuna kitu tunakosa, hasa sisi tunaojiita wapenzi na wachambuzi wa soka; Kagame Cup inaendelea na timu nzuri kutoka Nchi shiriki kama vile Uganda, Kenya, Congo, Rwanda, Djibout, Zanzibar na Sudan ziko hapa nchini kwa ajili ya mtanange:
Concern yangu ni kwamba, wachambuzi wa soka kupitia JF wanakua wagumu kujitokeza kuongelea kwa kina kinachokua kinaendelea Uwanjani wakati timu kutoka nje ya nchi zinapokuwa zinacheza; uchambuzi unaanza pale tu Yanga na Simba zikiwa uwanjani, inasikitisha kwakweli. ni vyema kuwa karibu na haya mambo vinginevyo tukikalia Yanga na Simba tu tunapotea.