Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,888
- 141,534
It’s now not even debatable that CCM know how to play the game of politics better than anybody.
They have an indescribable svengali type of hold on the rest of the opposition parties that renders them [the opposition] functionally ineffective.
For the life of me, somebody explain it to me. Make it make sense;
1. Unakamatwa na kufungwa bila kosa/ makosa.
2. Unafunguliwa mashitaka ya uongo/ kizushi ambayo hayana dhamana [ili usote mahabusu].
3. Tunaambiwa eti wewe ni gaidi na ushahidi upo unaothibitisha hilo [licha ya kwamba mtu yeyote mwenye akili anajua wewe siyo gaidi].
4. Kesi inaendeshwa kwa mwendo wa konokono kwa makusudi tu ili uendelee kutaabika jela.
5. Kwa vile mashitaka ni ya uongo/ kizushi, kesi inadhihirika kuwa kituko baada ya mashahidi kuanza kutoa ushuhuda wao.
6. Baada ya miezi takriban minane [8], mwendesha mashitaka ananena kuwa hana nia ya kuendelea na kesi.
7. Sijui hiyo nia ya kutotaka kuendelea na kesi imemjia lini? Labda alioteshwa usiku 🤣.
8. Mashitaka yanatupiliwa mbali. Unaachiwa huru baada ya kusota lupango kwa muda wote huo.
9. Wamekupotezea muda kwa mambo ya kizushi. Wamekutesa. Wamekunyanyasa. Wamekuvunjia heshima. Wamekuzushia mambo ya ajabu.
10. Licha ya yote hayo ambayo ni dhahiri shahiri waliyafanya kwa makusudi tu ili unyanyasike, hutopewa fidia yoyote ile.
11. Ulichoambulia ni kualikwa ikulu kwenda kukutana na mtu aliyesababisha madhila yote hayo dhidi yako. Kwenye picha nilizoziona, sikuona bilauri za juisi kama tulivyowahi kuziona hapo zamani mlipoitwa ikulu baada ya kupigwa virungu na kumwagiwa maji ya upupu. Safari hata juisi ya Sayona hukupewa! Au ulikunywa?
12. Unatoka jela, badala ya kukutana na kuongea na watu waliosimama na wewe muda wote huo ambao uliporwa uhuru wako, wewe unaenda moja kwa moja kuonana na kucheka cheka na mtu aliyekusababishia madhila yote hayo uliyoyapitia katika hizo siku 200 na kitu.
13. Umekosea sana aisee. Yeye ndo alipaswa aje kwako kukuona. Yeye na serikali yake ndo wanapaswa kukuomba radhi kwa usumbufu waliokuletea wewe pamoja na familia yako. Wao ndo wanapaswa kukufidia vyote ulivyopoteza pindi walipokuwa wamekufunga.
14. Umeonyesha udhaifu mkubwa sana ambao CCM wataendelea kuutumia kuwapumbaza na kuwahadaa kwa siku, miaka, na miongo ijayo.
15. CCM wataendelea kuwapiga, kuwanyanyasa, kuwatendea vibaya, na mwisho wa siku watawaalikeni ikulu muende kupiga picha, kunywa juisi, na kula biskuti halafu mnasahau kabisa mabaya yote mliyotendewa. Mko wepesi mno wa kusamehe na kusahau.
Sioni kabisa CCM ikitoka madarakani kwa upinzani huu tulionao. Hata kwenye katiba mpya, kama ikija kupatikana, mtahadaiwa na kurubuniwa tu. Na mtalia weee hadi mtachoka na kunyamaza.
16. Wapinzani wa Tanzania wakiongozwa na CHADEMA, hamna kabisa uti wa mgongo.
Just a bunch of weak weasels.