Kwa saa 24 nilitafakari nikidhani kuna kitu sielewi, baada ya kuliona bandiko wasi wasi umenitoka.
1. Wanopinga hoja za
Nyani Ngabu sizioni hoja zao.
Kusema ana chuki tu bila kujibu hoja ni kukosa hoja.
2. Mbowe (FAM) hakupaswa kwenda Ikulu jana.
Sababu alizotoa NN ni za kweli na naongezea, kwamba, Mbowe aliomba kuonana na Rais SSH kabla ya kukamatwa ,barua haikuwahi kujibiwa.
Ni kwa mantiki gani anakwenda Ikulu kabla ya kuonana na waliompigania akiwa gerezani!
3. Kuna hoja kwamba '' watu walitaka FAM afanye nini''. Well, hakutakiwa kwenda Ikulu katika muda mfupi bila kujua mazingira ya nchi. Sijui kama alikutana na kamati kuu ya CDM.
4. ''Kwamba Mbowe hataki kulipa kisasi'' hakuna anayemtaka alipe kisasi, kujipa muda wa kutathmini si kulipa kisasi ni kujijenga kifikra baada ya mateso ya miezi 8.
5. Kwamba ''alijipa muda na kwenda nyumbani'', si kweli , aliwaambia watu hataongea hadi muda utakapofika, ilikuwaje muda wa kuonana na Rais SSH ulipatikana?
Kwa waliofuatilia kesi, kulikuwa na 'presha' kutoka ndani na nje ya nchi.
Mahakama ilikuwa ma wakati mgumu achilia mbali ilivyovurunda mwenendo wa kesi.
Rais SSH kukutana na viongozi wa dini ilikuwa njia tu ya 'kutokea''
Kwa hali yoyote CDM na Mbowe walikuwa na 'upper hand''. CCM, wakati mgumu.
Mbinu iliyotumiwa na CCM inamwacha FAM na swali '' kwanini alikwenda''
Rais SSH alijua Mbowe naungwa mkono, kitendo cha kutoka tu kinatosha kuongeza ari ya Chadema na Wananchi kudai haki ikiwemo katiba. FAM alikuwa na ''leverage' na ni wazi ame squander
Mbinu iliyotumiwa kwa Masheikh wakitoka wakae kimya haikufanya kazi kwa Mbowe.
Mbinu mpya ni kumwita 'kumtia adabu'' tunaweza kukuweka ndani na kukutoa!
Je hilo mnaliona sawa?
Mbinu ya kupiga picha na kutoa hotuba za maridhiano ni ''kumfunga Mbowe mdomo'' .
Mbinu ya kumwita ni kumlazimisha 'akiri kwamba amesamehewa''
Ukitaka kujua mbinu ya 'kusamehewa' imetumikaje, siku Mbowe anakwenda Ikulu ni siku hiyo hiyo vijana wa JKT wanasamehewa. Kwa maana kwamba Rais SSH ni mtu wa kusamehe.
Je, Mbowe alihitaji kusamehewa? Kwa kosa gani? Lilithibitishwa wapi? Je alipewa kujitetea?
CCM wanasema hizo ndizo siasa safi! kwamba wanamwambia Mbowe atulie , siasa chafu zitamrudisha kule, si ugaidi ni siasa ! hilo ndilo Mbowe alitesekea?
Kwa namna yoyote ile Chadema na uongozi chini ya Tundu Lissu wana la kueleza Wanachama wao likuwaje wakamwacha ''mfungwa'' akakimbilia Ikulu bila kumpa taarifa za chama na bila kumpa muda wa kutafakari!!!
''Mashtaka ya NN'' yana mashiko! kuna ''hoja za kujibu''
JokaKuu Pascal Mayalla