kambagasa
JF-Expert Member
- Aug 18, 2014
- 2,241
- 1,749
Kikao cha kumfuta uanachama Balozi Karume kimefanyika saa saba usiku wa kuamkia leo Jumamosi Julai 8, 2023 chini ya Katibu wa Mkoa wa CCM, Amina Mnacho.
Taarifa ya kumuondosha kwenye chama hicho ilitolewa na Katibu Mwenezi wa Mkoa huo, Ali Timamu Haji.
Hatua hiyo inakuja baada ya chama hicho kumpa onyo kutoka na kauli zake zake akidaiwa kukidhalilisha chama na kuwatukana viongzi wakuu hadharani.
Kutokana na matamshi ambayo Balozi Ali Kalume amekuwa akiyasema likiwemo la CCM Zanzibar haijawahi kushinda uchaguzi na hujuma za kutwaa ardhi ya familia yao zinazofanywa katika Serikali ya Raisi Mwinyi, kikao cha CCM kilichokaa jana usiku huko Zanzibar kimemfuta uanachama Balozi Karume.
Ikumbukwe pia kumekuwa na kutokuelewana kwa muda sasa kati ya Raisi Mwinyi na Balozi Karume kwa kile ambacho Balozi Karume amekuwa akipinga hadharani sera za Mwinyi kuuza visiwa mbalimbali vilivyoko Zanzibar.
Pia soma: