CCM yamweka chini ya Uangalizi Balozi Karume

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimemuweka chini ya uangalizi wa miezi mitatu kada wake Balozi Ali Abeid Karume kutokana na kauli zake za kukidhalilisha chama na viongozi wake.

Hatua hiyo inatokana na onyo alilopewa na kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Jimbo la Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja iliyokutana Juni 15, 2023.

Karume aliitwa kuhojiwa na kamati ya maadili ya jimbo hilo kutokana na kauli zake alizozitoa kwenye mitandao ya kijamii akikituhumu chama kuwa hakijawahi kushinda kihalali kisiwani humo na kumkosoa hadharani Rais Hussein Mwinyi kuhusu sera zake za kukodisha visiwa.

Pia alipinga utaratibu wa wananchi wa Kilimani kuondolewa kujenga ukumbi wa kimataifa na ujenzi wa uwanja wa Amani akidai vinakiuka utaratibu.

Juni 11, katika moja ya mikutano yake, Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar, Hussein Mwinyi aliiagiza kamati ya maadili kuwashughulikia makada wanaokwenda kinyume na taratibu huku akihoji kwanini bado wako ndani ya chama.

“Wakati umefika kwa kamati ya maadili kufanya kazi yake, una sababu gani ya kubaki kwenye chama hiki, ikiwa hupendi chama ondoka! Nenda ukaseme hayo maneno ukiwa nje ya chama, unahoji hata ushindi wa CCM!” aliwaambia wafuasi bila kumtaja mtu.

Kwa mujibu wa barua ambayo Mwananchi limeiona iliyosainiwa na Katibu wa CCM jimbo la Tunguu, Sharifa Maabadi Othman, bila kutaja muda, inaeleza chama kumpa onyo hilo kwa kukiuka maadili.

“Pamoja na mambo mengine kikao kilipokea taarifa kutoka kamati ya maadili ya jimbo kuhusu mahojiano yaliyofanyika juu ya Ali Abeid Karume na kamati ya maadili ya jimbo, pamoja na makosa yake aliomba msamaha katika kikao hicho, kimeamua kukupa onyo kwa kukiuka maadili ya chama chetu,” inaeleza sehemu ya barua hiyo.

Hata hivyo, Mwananchi lilipomtafuta katibu huyo Sharifa kuhusu hatua hiyo, licha ya kusema hawezi kuzungumza chochote kwa sababu yaliyofanyika ni vikao vya ndani, alikiri barua hiyo ni halali.

Balozi Karume alipotafutwa juzi na jana hadi saa 6:50 mchana alisema bado hajapokea barua yoyote kutoka kwenye chama hicho tangu walipomaliza kikao chao.

Hata hivyo, alisema naye ameona barua hiyo kwenye mtandao wa kijamii, akasema ikimfikia atatii maadili ya chama.

Balozi Karume alihojiwa na kamati ya maadili ya tawi la Mwera, kamati ya maadili ya Jimbo la Tunguu na kamati ya maadili ya Wilaya ya Kati.

Barua aliyopewa Karume ni kwa mujibu wa kanunzi za uongozi na maadili za CCM na jumuiya yake toleo la mwka 2021 ibara ya (8) kifungu kidogo (a) (ii).

Nakala ya barua hiyo ilikwenda kwa Katibu wa CCM wilaya ya Kati na Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja.

Kutokana na kanuni hiyo mwanachama anayekiuka maadili ya chama anapewa onyo, onyo kali au kufukuzwa uanachama huku kukiwa na muda maalumu wa uangalizi kuanzia miezi mitatu, sita na mwaka mmoja.

Mmoja wa watu wa ndani ya chama hicho ambaye hakutaka kutajwa alisema iwapo kikipita kipindi cha uangalizi bila kuonyesha maabdiliko, wilaya itatoa mapendekezo kwenda ngazi ya mkoa kwa hatua zaidi.

Mapendekeo hayo yanaweza kuwa kumfukuza uanachama kiongozi huyo.

Akizungumza na gazeti hili mchambuzi wa masuala ya kisiasa Zanzibar, Ali Makame alisema hatua iliyochokuliwa ni sawa kwa sababu lengo la kila chama ni kuishika dola, lakini kuna taratibu za kufuata katika kuzungumza.

“Ukiangalia huyu ni mtoto wa muasisi wa taifa hili na chama chake, kwa hiyo anajua mengi, madhaifu na mazuri ya chama, lakini kutoka hadharani na kuanza kusema vile si uungwana, kama unapinga tumia utaratibu wa chama unapotoka nje unakuwa utovu wa nidhamu,” alisema

Hata hivyo, alisema hatua zilizochukuliwa na chama hicho ni jambo la kujifunza hata kwa watu wengine kwa sababu linaweza kuwagawa wanachama na viongozi, hivyo kuwaondoa kwenye lengo la chama kama kikundi chenye dhamira moja.

MWANANCHI
 
soon atapewa ajira
 
Ukweli ndio huo ccm haijawahi kushinda zanzibar katu na bara uchaguzi wa 2015 lowasa alishinda na 2020 lissu alishinda huku ccm ikishindishwa na dola lakini ipo siku aidha wananchi wataamua lao au dola itawaasi itawatema!!!
Ahahahahaha! Unachekesha kweli! Yaani upate wabunge 70 kati ya zaidi ya 300 halafu ujidanganye eti ulishinda Urais! Au mnafikiri kwa kutumia Masaburi!?
 
Ukweli unauma sana. Tangu mfumo wa vyama vingi urudi CCM haijawahi kushinda Zanzibar.
Hataa mtanzania mjinga anajua tukiweka uccm pembeni chaguzi zote baada mfumo wa vyama vingi CCM hawajashinda tena siyo Zanzibar tu na bara pia,Kazi yao ni kununua wapinzani maarufu ili waseme mabaya ktk na kuzua taharuki Lakini bado wanashindwa kwenye box la kupiga kura.
 
Ahahahahaha! Unachekesha kweli! Yaani upate wabunge 70 kati ya zaidi ya 300 halafu ujidanganye eti ulishinda Urais! Au mnafikiri kwa kutumia Masaburi!?
Wewe naye mbumbu hujui lolote,ulishawahi kusimamia hata chaguzi moja ukaona Mambo yanayofanyika na mifumo ya dola na vyombo vyote ili kuhakikisha CCM anatangazwa. Wewe ZUZU uelewa wako wa kitoto
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimemuweka chini ya uangalizi wa miezi mitatu kada wake Balozi Ali Abeid Karume kutokana na kauli zake za kukidhalilisha chama na viongozi wake.

Hatua hiyo inatokana na onyo alilopewa na kamati ya siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Jimbo la Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja iliyokutana Juni 15, 2023.

Karume aliitwa kuhojiwa na kamati ya maadili ya jimbo hilo kutokana na kauli zake alizozitoa kwenye mitandao ya kijamii akikituhumu chama kuwa hakijawahi kushinda kihalali kisiwani humo na kumkosoa hadharani Rais Hussein Mwinyi kuhusu sera zake za kukodisha visiwa.

Pia alipinga utaratibu wa wananchi wa Kilimani kuondolewa kujenga ukumbi wa kimataifa na ujenzi wa uwanja wa Amani akidai vinakiuka utaratibu.

Juni 11, katika moja ya mikutano yake, Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar, Hussein Mwinyi aliiagiza kamati ya maadili kuwashughulikia makada wanaokwenda kinyume na taratibu huku akihoji kwanini bado wako ndani ya chama.

“Wakati umefika kwa kamati ya maadili kufanya kazi yake, una sababu gani ya kubaki kwenye chama hiki, ikiwa hupendi chama ondoka! Nenda ukaseme hayo maneno ukiwa nje ya chama, unahoji hata ushindi wa CCM!” aliwaambia wafuasi bila kumtaja mtu.

Kwa mujibu wa barua ambayo Mwananchi limeiona iliyosainiwa na Katibu wa CCM jimbo la Tunguu, Sharifa Maabadi Othman, bila kutaja muda, inaeleza chama kumpa onyo hilo kwa kukiuka maadili.

“Pamoja na mambo mengine kikao kilipokea taarifa kutoka kamati ya maadili ya jimbo kuhusu mahojiano yaliyofanyika juu ya Ali Abeid Karume na kamati ya maadili ya jimbo, pamoja na makosa yake aliomba msamaha katika kikao hicho, kimeamua kukupa onyo kwa kukiuka maadili ya chama chetu,” inaeleza sehemu ya barua hiyo.

Hata hivyo, Mwananchi lilipomtafuta katibu huyo Sharifa kuhusu hatua hiyo, licha ya kusema hawezi kuzungumza chochote kwa sababu yaliyofanyika ni vikao vya ndani, alikiri barua hiyo ni halali.

Balozi Karume alipotafutwa juzi na jana hadi saa 6:50 mchana alisema bado hajapokea barua yoyote kutoka kwenye chama hicho tangu walipomaliza kikao chao.

Hata hivyo, alisema naye ameona barua hiyo kwenye mtandao wa kijamii, akasema ikimfikia atatii maadili ya chama.

Balozi Karume alihojiwa na kamati ya maadili ya tawi la Mwera, kamati ya maadili ya Jimbo la Tunguu na kamati ya maadili ya Wilaya ya Kati.

Barua aliyopewa Karume ni kwa mujibu wa kanunzi za uongozi na maadili za CCM na jumuiya yake toleo la mwka 2021 ibara ya (8) kifungu kidogo (a) (ii).

Nakala ya barua hiyo ilikwenda kwa Katibu wa CCM wilaya ya Kati na Katibu wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja.

Kutokana na kanuni hiyo mwanachama anayekiuka maadili ya chama anapewa onyo, onyo kali au kufukuzwa uanachama huku kukiwa na muda maalumu wa uangalizi kuanzia miezi mitatu, sita na mwaka mmoja.

Mmoja wa watu wa ndani ya chama hicho ambaye hakutaka kutajwa alisema iwapo kikipita kipindi cha uangalizi bila kuonyesha maabdiliko, wilaya itatoa mapendekezo kwenda ngazi ya mkoa kwa hatua zaidi.

Mapendekeo hayo yanaweza kuwa kumfukuza uanachama kiongozi huyo.

Akizungumza na gazeti hili mchambuzi wa masuala ya kisiasa Zanzibar, Ali Makame alisema hatua iliyochokuliwa ni sawa kwa sababu lengo la kila chama ni kuishika dola, lakini kuna taratibu za kufuata katika kuzungumza.

“Ukiangalia huyu ni mtoto wa muasisi wa taifa hili na chama chake, kwa hiyo anajua mengi, madhaifu na mazuri ya chama, lakini kutoka hadharani na kuanza kusema vile si uungwana, kama unapinga tumia utaratibu wa chama unapotoka nje unakuwa utovu wa nidhamu,” alisema

Hata hivyo, alisema hatua zilizochukuliwa na chama hicho ni jambo la kujifunza hata kwa watu wengine kwa sababu linaweza kuwagawa wanachama na viongozi, hivyo kuwaondoa kwenye lengo la chama kama kikundi chenye dhamira moja.

MWANANCHI
Makongoro naye aunge mkono hoja ya Ally Karume
 
Mwingine huko bara anafanya yake!!!
 
Attachments

  • B9C38E9D-0AB6-40D6-8095-B8B7DCEF9F6E.jpeg
    B9C38E9D-0AB6-40D6-8095-B8B7DCEF9F6E.jpeg
    81.5 KB · Views: 3

Angalieni huku mtuambie kama yuko sawa kufuatana na chama chao
 
Attachments

  • 4A607D42-9FE2-41B1-9BBB-FA21E6473C9F.jpeg
    4A607D42-9FE2-41B1-9BBB-FA21E6473C9F.jpeg
    115.9 KB · Views: 3
  • F15B20C7-F9F9-49F5-9109-CCB0AEE52678.jpeg
    F15B20C7-F9F9-49F5-9109-CCB0AEE52678.jpeg
    37.8 KB · Views: 4
  • 3EF3FD4C-F6D7-49DD-BF98-A6B8B28B68A1.jpeg
    3EF3FD4C-F6D7-49DD-BF98-A6B8B28B68A1.jpeg
    55 KB · Views: 2
  • 76A4ECA2-61B9-4DA8-A6E8-905CD73A5592.jpeg
    76A4ECA2-61B9-4DA8-A6E8-905CD73A5592.jpeg
    66.2 KB · Views: 2
  • 3F093163-E98C-4E67-92DC-2737950443F0.jpeg
    3F093163-E98C-4E67-92DC-2737950443F0.jpeg
    50.6 KB · Views: 2
  • 91490627-E207-443E-BD07-7E56B84D6C10.jpeg
    91490627-E207-443E-BD07-7E56B84D6C10.jpeg
    140.9 KB · Views: 2
  • 46D74C40-B3D4-4499-BAFA-A3C43804E709.jpeg
    46D74C40-B3D4-4499-BAFA-A3C43804E709.jpeg
    51.3 KB · Views: 2

Similar Discussions

Back
Top Bottom