Zanzibar 2020 CCM Zanzibar kama ni kweli mmependekeza iwe hivi basi mnaenda kutengeneza Makundi na Mpasuko baina yenu

Mzukulu

JF-Expert Member
Feb 14, 2020
1,412
2,000
Akina Mzukulu tupo pale mlipo na tutaendelea kuwepo hadi Jumapili ijayo huko Dodoma ila nimesikitishwa mno na Mapendekezo yenu ya Kiuwoga kuwa Mmekubaliana na uliokuwa pia Mtazamo wangu kuwa Profesa Makame Mbarawa awe Isles next CCM Flag bearer kwa mwaka 2020 lakini eti kwa Kumpoza Mzee Mwinyi (Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili) mmeamua kuwa Profesa Makame akiapishwa tu basi amteue Dkt. Hussein Mwinyi kuwa Makamu wa Pili wa Rais huko Kisiwani Zanzibar.

Nimesema kuwa mnaenda kutengeneza mpasuko mkubwa sana ndani ya CCM huko Kisiwani Zanzibar kama kweli mtalazimisha Profesa Mbarawa amteue Dkt. Hussein Mwinyi kuwa Makamu wa Pili wa Rais kwani nina uhakika hata Watoto wa waliokuwa Viongozi huko Zanzibar wa akina Karume na Jumbe nao watahisi Kutengwa kama pia si Kudharauliwa hali ambayo inaweza kutengeneza Uhasama na Mpasuko mkubwa wa Kichama na Kiuongozi ambao utakithiri kabisa Chama cha Mapinduzi huko.

Ushauri wangu Kwenu ni kwamba nimefurahi kuwa Prof Makame Mbarawa atakuwa Rais ila naomba Dkt. Mwinyi asiwe Makamu wa Pili wa Rais.
 

Mzukulu

JF-Expert Member
Feb 14, 2020
1,412
2,000
Mchucho tiyar top 05
Ndiyo Mchujo ni tayari na Wote wawili hawa wapo katika Kikosi cha Top Five lakini kama kuna Kosa ambalo CCM watafanya ni Kumwomba Rais Mtarajiwa wa Zanzibar Profesa Makame Mbarawa amteue Dkt. Hussein Mwinyi kuwa Makamu wa Pili wa Rais huko ili tu Kumpoza Baba yake ambaye amekuwa ni Mpiga Debe mkubwa kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
 

owomkyalo

JF-Expert Member
Dec 26, 2017
4,216
2,000
Ndiyo Mchujo ni tayari na Wote wawili hawa wapo katika Kikosi cha Top Five lakini kama kuna Kosa ambalo CCM watafanya ni Kumwomba Rais Mtarajiwa wa Zanzibar Profesa Makame Mbarawa amteue Dkt. Hussein Mwinyi kuwa Makamu wa Pili wa Rais huko ili tu Kumpoza Baba yake ambaye amekuwa ni Mpiga Debe mkubwa kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.


Sawa niwekee Top 05 nione km jecha yumo then kuhusu coalition government according to Zanzibar constitution haifanyi Nazi.
 

Mzukulu

JF-Expert Member
Feb 14, 2020
1,412
2,000
Mkuu wewe ulitaka iweje labda hiyo top5 tuanze hapo kwanza!
Najua na nilishasema hapa mapema tu kuwa Profesa Makame Mbarawa atakuwa Mrithi wa Rais anayemaliza muda wake huko Kisiwani Zanzibar Dkt. Shein na ninamkubali na nitawasifu mno CCM wakimpitisha kwa Nguvu moja. Ila sitaki na wala sipendelei Mtoto yoyote wa waliowahi kuwa Viongozi wa Zanzibar kuanzia Karume, Jumbe na Mwinyi wawe sehemu ya Uongozi wa Juu huko. Kama Mimi ningekuwa Profesa Mbarawa nikiapishwa tu kuwa Rais basi Makamu wangu wa Pili wa Rais ningemteua Masauni. Zanzibar ya sasa inahitaji Sura mpya kabisa na zisizo na Mizizi wala Makundi ya Kifamilia.
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
35,347
2,000
Hivi kwanini siri za ccm zinavuja kibwege sana ? Halafu hilo unalolisena halitoweza kutimia kwa vile ccm itashindwa vibaya sana kwenye uchaguzi huu
Yaani ccm ni mazwazwa kwelikweli, yaani yameanza hadi kujipangia vyeo?
Eti makamu wa pili sijui awe fulani, Mara hapana awe Fulani hivi wamesahau kuwa chaguzi zote huwa wanashindwa Ila ustaarabu wa Wazenji tuu ndio ulio sababisha kukubali yaishe?
Sasa safari hii ACT ya Maalim Seif sio ya kukubali yaishe!
 

Mzukulu

JF-Expert Member
Feb 14, 2020
1,412
2,000
Yaani ccm ni mazwazwa kwelikweli, yaani yameanza hadi kujipangia vyeo?
Eti makamu wa pili sijui awe fulani, Mara hapana awe Fulani hivi wamesahau kuwa chaguzi zote huwa wanashindwa Ila ustaarabu wa Wazenji tuu ndio ulio sababisha kukubali yaishe?
Sasa safari hii ACT ya Maalim Seif sio ya kukubali yaishe!
Kumbe Mzukulu ni CCM Ndugu? Nilikuwa sijui / silijui hili. Ngoja kuna Uzi naunzisha hivi punde wa CHADEMA sijui pia utasema ni wa huko tena!
 

THOMASS SANKARA

JF-Expert Member
Nov 13, 2014
1,730
2,000
Acha ramli chonganishi..!!

Unazijua vizuri siasa za Zanzibar wewe!!??Siasa za Upemba na Uunguja?
Atoke Mpemba aje Mpemba??
Hili halitoweza tokea asilani abadani.

Prof Mbarawa ni kiongozi mzuri sana kiutendaji ila CCM itampitishaje mtu ambaye hajawahi chaguliwa na watu hata kwa nafasi ya ubalozi wa Nyumba kumi ama usheha??
 

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
9,365
2,000
Akina Mzukulu tupo pale mlipo na tutaendelea kuwepo hadi Jumapili ijayo huko Dodoma ila nimesikitishwa mno na Mapendekezo yenu ya Kiuwoga kuwa Mmekubaliana na uliokuwa pia Mtazamo wangu kuwa Profesa Makame Mbarawa awe Isles next CCM Flag bearer kwa mwaka 2020 lakini eti kwa Kumpoza Mzee Mwinyi ( Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili ) mmeamua kuwa Profesa Makame akiapishwa tu basi amteue Dkt. Hussein Mwinyi kuwa Makamu wa Pili wa Rais huko Kisiwani Zanzibar.

Nimesema kuwa mnaenda kutengeneza mpasuko mkubwa sana ndani ya CCM huko Kisiwani Zanzibar kama kweli mtalazimisha Profesa Mbarawa amteue Dkt. Hussein Mwinyi kuwa Makamu wa Pili wa Rais kwani nina uhakika hata Watoto wa waliokuwa Viongozi huko Zanzibar wa akina Karume na Jumbe nao watahisi Kutengwa kama pia si Kudharauliwa hali ambayo inaweza kutengeneza Uhasama na Mpasuko mkubwa wa Kichama na Kiuongozi ambao utakithiri kabisa Chama Cha Mapinduzi huko.

Ushauri wangu Kwenu ni kwamba nimefurahi kuwa Prof Makame Mbarawa atakuwa Rais ila naomba Dkt. Mwinyi asiwe Makamu wa Pili wa Rais.
Atakaebisha mapendekezo hayo atashugulikiwa mpaka achakae. Hiki sio chama tena ni genge la wahuni.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom