CCM yaweza kutawala kwa miaka 100 ikiwa tu...

CCM yaweza kutawala kwa miaka 100 ikiwa tu...

Maisha magumu aisee
Nakuelewa. Ila si kwa kila mtu, Naona anayefaanya kabiashara ama kazi ama kamradi kokote mbona naona watu wako sawa kimaisha? Ama mimi sioni?
 
CCM ni chama ambacho kimekuwa katika utawala wa taifa hili kwa miaka mingi sana. Na kina mizizi hadi mashinani tofauti na vyama vingine vya upinzani. Na kwa ujio wa vyama hivi pia kumeipa CCM changamoto si haba.

Kuwa na wanachama mpaka mashinani si jambo ambalo linaweza kudumu ikiwa CCM haitabadilisha mbinu zake katika ku maintain/Kushikilia na hata kuongeza wananchama wengine.

CCM inaweza kutawala hata zaidi ya miaka 100 ikiwa itafanya MABADILIKO katika mbinu zake bila hata kutumia NGUVU/MABAVU katika kushindana na WAPINZANI.
Baadhi ya mbinu hizo ni kuwa:

1. ili CCM izidi kukubalika na kudumu ni lazima iwe na kitengo chake maalumu kitakachohusika hasa na mambo ya UTAFITI/Research- CCM POLITICAL STRATEGY RESEARCH. Kitengo hikikiwe na WATAAALAMU mbali mabali wengine waliosomea POLITICAL SCIENCE NK
.Na kazi yake kuu iwe ni kufanya UTAFITI MASHINANI ili kujua
Ni nini WANACHAMA na Wananchi kwa ujumla HAWAKIPENDI ama WANGETAKA kifanywe .
Both katika:
KUINUA MAISHA ya wananchi,
Katika KUKIBORESHA chama cha CCM.

2. MALALAMIKO hayo ama MAPENDEKEZO yawe analyzed na YAFANYIWE KAZI.
Maisha ya Mtazanaia Mashinani YAKIBOREKA CCM itatawala zaidi ya miaka 100.

Lakini ikijiona na kusema "TUTASHINDA TU Sisi ni chama kikubwa" inaweza kuangushwa vibaya sana.

Anaweza AKAINUKA jamaa yeyote tu na akawa VERY CHARISMATIC leader MUHAMASISHAJI wa ajabu kutoka chama kingine na pengine akawa hana hata hela lakini ana MDOMO wa ASALI na kujikuta AMEITEKA mioyo ya Watanzania WENGI NA HATA WANA CCM . Huku aki MAJOR kuhusu udhaifu wa CCM na hivyo kubadili mkondo wa kisiasa nchini kabisa.

3.CCM POLITICAL STRATEGY RESEARCH IAJIRI vijana wasomi wanaojua SCIENTIFIC RESEARCH na mambo ya STATISTICS /TAKWIMU.
Kwa kufanya hivi CCM itajua MALALAMIKO,VILIO na MAHITAJI na MAPENDEKEZO ya watu na KUJARIBU kadri ya uwezo wao KUYATATUA ama kuwapa MATUMAINI.

4.VIONGOZI wa CCM wawe WASIKIVU wazuri sana.
Na Mtu akitoa maoni mbadala yaliyotofauti asionekane na kuwa ni mpinzani maana DEMOKRASIA ni lazima IWEMO NDANI ya CHAMA chenyewe cha CCM..

5..WAZEE waliochoka wapumzike tu polepole na kutoa ushauri bali si utafiti.

6.Mambo ya CCM yasiachiwe TISS. Acha TISS ishughulikie usalama wa Taifa letu.
Na mambo ya SIASA yaachiwe wanasiasa.

Na ikiwa ni ku chip in iwe ni kidogo kidogo sana. Maana wanatakikana kuwa APOLITICAL ENTITY/ WASIOEGEMEA chama chochote kulingana na kazi yao.
Nguvu ya Risasi za Lisu "inaweza " kutawala milele
 
Nakuelewa. Ila si kwa kila mtu, Naona anayefaanya kabiashara ama kazi ama kamradi kokote mbona naona watu wako sawa kimaisha? Ama mimi sioni?
Utakuwa na matatizo wewe, watu wanafunga biashara zao wewe unasema kuna unafuu?
 
Utakuwa na matatizo wewe, watu wanafunga biashara zao wewe unasema kuna unafuu?
Mkuu nakuelewa sana na ninakupata. Hata hivyo si wote wanaofunga biashara.
 
Huko tunakoenda hapatabiriki, nchi imetawaliwa na siasa kila kona. Ukienda ofisi za umma si viongozi si wafanyakazi wengi ni makada wa CCM. Matamko ndio yametawala kila mahali. Katika hali kama hii tujiandae kudumbukizwa kwenye mdororo wa kila kitu
 
Huko tunakoenda hapatabiriki, nchi imetawaliwa na siasa kila kona. Ukienda ofisi za umma si viongozi si wafanyakazi wengi ni makada wa CCM. Matamko ndio yametawala kila mahali. Katika hali kama hii tujiandae kudumbukizwa kwenye mdororo wa kila kitu
Ni sisi wananchi ndo tunaoweza kubadilisha tabia hiyo. Badala ya kuwa wanasiasa maofisini watu wafanye kazi.
 
Almost all opposition parties in Tanzania are like family NGO’s. The leaders for the same are there for their personal interests, they are making money. They are not intending to outset the ruling party simply because they are weak and most of them are big cheaters.
 
Hapo number 6 ndo roho ya ccm ilipoegemea, hiyo ndo engine ya umafya was ccm, tiss ni ccm na ccm ni tiss, tembelea mikoani majengo yote ya ccm ndimo walimo tiss hata hapo lumumba tiss wamo wengi tu, huu mwingiliano was tiss na ccm ndo uliotufikisha hapa na unatupeleka kuzimu maovu yote ya serkali yanafichwa wadadisi wanashughulikiwa, tiss in return wanapewa vyeo na nafasi za kazi kwenye taasisi zote za serkali matokeo yake taasisi hazina ufanisi maana fisadi ni tiss anaetakiwa kumchunguza takukuru nae ni tiss, kesi ikienda mahakamani Jaji nae ni tiss, it is a vicious circle
Hata ingekuwa kuna ka ukweli kuhusu hao TISS kuwa kwenye majengo ya CCM basi si umewauza mkuu?USIRI wa kazi utakuwa wa
Ni lazima basi walazimike kubadili makao ya ofisi zao maana watakuwa VULNERABLE/Hatarini.
Kama ni kweli na si propaganda..
Mambo mengine MEZEA hii ni nchi yako mkuu.
 
Almost all opposition parties in Tanzania are like family NGO’s. The leaders for the same are there for their personal interests, they are making money. They are not intending to outset the ruling party simply because they are weak and most of them are big cheaters.
Nothing could be further from the truth.
NONE of these leaders I know has Tanzania at heart except having hegemony attitudeon how to make money minting schemes while hiding undercover of "LEADERS of OPPOSITION parties"
While at the same time hoodwinking Tanzanians that they are fighting for their live's wellbeing.
Which is a big lie.
 
Back
Top Bottom