CCM yaweza kutawala kwa miaka 100 ikiwa tu...

CCM yaweza kutawala kwa miaka 100 ikiwa tu...

Ni ushauri mzuri. Jambo jingine muhimu ni: kuhakikisha kwamba viongozi wanakuwa na uadilifu na wenye kuishi yale wanayoyasema! Aidha wawe na mpango wa kuandaa vijana kushika nafasi (succession Plan).
Ushauri mzuri lakini wengi sijui kwa nini wanakichukia chama hiki?
Unakuta mtu badala ya kujibu hoja anatoa tusi. Why?
 
Hata atokee charismatic leader kutokea mbinguni hawezi kuishinda CCM kwa kutumia tume hii ya uchaguzi.
 
there are countless ways of skinning a cat.

ZANU PF, KANU, Siade Barre, Gadafi, Wahutu, Hosni Mubarak, etc, etc.
Please give us some examples on how to execute your skinning techniques.
 
Hata atokee charismatic leader kutokea mbinguni hawezi kuishinda CCM kwa kutumia tume hii ya uchaguzi.
Naamini kabisa uchaguzi ulio FREE/Huru Fair/Haki and Transparent/Uwazi ndo kitovu cha amani cha taifa lolote lile.
Bila hayo nchi nyingi zimeingia vurugu ambazo zingeweza kuepukikaikiwa mambohayoyangezingatiwa.. Tufikirie hilo kwa makini sana.
 
Kuhamia kijanj kumuunga mkono mh katika jitihada zake za kuleta maendeleo
Kama Watanzania tuna jukumu la kumuunga mkono kiongozi aliyeko madarakani ili kuleta maendeleo.
Siasa za shari nan ugomvi hudumaza maendeleo.
 
Kama Watanzania tuna jukumu la kumuunga mkono kiongozi aliyeko madarakani ili kuleta maendeleo.
Siasa za shari nan ugomvi hudumaza maendeleo.
Sawa, kupanga ni kuchagua
 
Hiy

Hiyo nguvu ya risasi kivipi tena mkuu, Nauliza tena ndugu Retired
Shige kwani unaishi wapi ndugu yangu? Kama uko nje nitakueleza, kama unaishi hapa, unanikejeli. Nambie
 
Shige kwani unaishi wapi ndugu yangu? Kama uko nje nitakueleza, kama unaishi hapa, unanikejeli. Nambie
Mkuu niko area. Hapa hapa.
Pole sikuwa na nia mbaya kuuliza swali hilo bali ni katika kuendeleza mjadala tu. Samahani mkuu
 
Hata atokee charismatic leader kutokea mbinguni hawezi kuishinda CCM kwa kutumia tume hii ya uchaguzi.
Naamini CCM si waizi bali wako sanaMashinani pia hili ni lazima tujue.Vyama hivi vingine viko zaidi mijini
 
Huko tunakoenda hapatabiriki, nchi imetawaliwa na siasa kila kona. Ukienda ofisi za umma si viongozi si wafanyakazi wengi ni makada wa CCM. Matamko ndio yametawala kila mahali. Katika hali kama hii tujiandae kudumbukizwa kwenye mdororo wa kila kitu
Kutabadilikatu kama nilivyosema jana.
 
CCM ni chama ambacho kimekuwa katika utawala wa taifa hili kwa miaka mingi sana. Na kina mizizi hadi mashinani tofauti na vyama vingine vya upinzani. Na kwa ujio wa vyama hivi pia kumeipa CCM changamoto si haba.

Kuwa na wanachama mpaka mashinani si jambo ambalo linaweza kudumu ikiwa CCM haitabadilisha mbinu zake katika ku maintain/Kushikilia na hata kuongeza wananchama wengine.

CCM inaweza kutawala hata zaidi ya miaka 100 ikiwa itafanya MABADILIKO katika mbinu zake bila hata kutumia NGUVU/MABAVU katika kushindana na WAPINZANI.
Baadhi ya mbinu hizo ni kuwa:

1. ili CCM izidi kukubalika na kudumu ni lazima iwe na kitengo chake maalumu kitakachohusika hasa na mambo ya UTAFITI/Research- CCM POLITICAL STRATEGY RESEARCH. Kitengo hikikiwe na WATAAALAMU mbali mabali wengine waliosomea POLITICAL SCIENCE NK
.Na kazi yake kuu iwe ni kufanya UTAFITI MASHINANI ili kujua
Ni nini WANACHAMA na Wananchi kwa ujumla HAWAKIPENDI ama WANGETAKA kifanywe .
Both katika:
KUINUA MAISHA ya wananchi,
Katika KUKIBORESHA chama cha CCM.

2. MALALAMIKO hayo ama MAPENDEKEZO yawe analyzed na YAFANYIWE KAZI.
Maisha ya Mtazanaia Mashinani YAKIBOREKA CCM itatawala zaidi ya miaka 100.

Lakini ikijiona na kusema "TUTASHINDA TU Sisi ni chama kikubwa" inaweza kuangushwa vibaya sana.

Anaweza AKAINUKA jamaa yeyote tu na akawa VERY CHARISMATIC leader MUHAMASISHAJI wa ajabu kutoka chama kingine na pengine akawa hana hata hela lakini ana MDOMO wa ASALI na kujikuta AMEITEKA mioyo ya Watanzania WENGI NA HATA WANA CCM . Huku aki MAJOR kuhusu udhaifu wa CCM na hivyo kubadili mkondo wa kisiasa nchini kabisa.

3.CCM POLITICAL STRATEGY RESEARCH IAJIRI vijana wasomi wanaojua SCIENTIFIC RESEARCH na mambo ya STATISTICS /TAKWIMU.
Kwa kufanya hivi CCM itajua MALALAMIKO,VILIO na MAHITAJI na MAPENDEKEZO ya watu na KUJARIBU kadri ya uwezo wao KUYATATUA ama kuwapa MATUMAINI.

4.VIONGOZI wa CCM wawe WASIKIVU wazuri sana.
Na Mtu akitoa maoni mbadala yaliyotofauti asionekane na kuwa ni mpinzani maana DEMOKRASIA ni lazima IWEMO NDANI ya CHAMA chenyewe cha CCM..

5..WAZEE waliochoka wapumzike tu polepole na kutoa ushauri bali si utafiti.

6.Mambo ya CCM yasiachiwe TISS. Acha TISS ishughulikie usalama wa Taifa letu.
Na mambo ya SIASA yaachiwe wanasiasa.

Na ikiwa ni ku chip in iwe ni kidogo kidogo sana. Maana wanatakikana kuwa APOLITICAL ENTITY/ WASIOEGEMEA chama chochote kulingana na kazi yao.
Wao enzi hizo walijinadi kutawala miaka elfu.
Lakini historia hakuna himaya iliotawala miaka elfu.Wamebakia miaka minane tu.
 
Wao enzi hizo walijinadi kutawala miaka elfu.
Lakini historia hakuna himaya iliotawala miaka elfu.Wamebakia miaka minane tu.
Vipi China mkuu. Chao chao ni cha miaka mingi sana.
 
Hakijatawala miaka 100,wametwaa madaraka baada ya vita kuu ya pili (WW2)
Mkuu si hiyo bado si ni miaka mingi sana zaidi ya miaka 60 tangu Mapinduzi yajulikanayo kama China Cultural Revolutions?
 
Wao enzi hizo walijinadi kutawala miaka elfu.
Lakini historia hakuna himaya iliotawala miaka elfu.Wamebakia miaka minane tu.
Ninejibu hapo chini hope umejisomea mkuu.
 
Hapo number 6 ndo roho ya ccm ilipoegemea, hiyo ndo engine ya umafya was ccm, tiss ni ccm na ccm ni tiss, tembelea mikoani majengo yote ya ccm ndimo walimo tiss hata hapo lumumba tiss wamo wengi tu, huu mwingiliano was tiss na ccm ndo uliotufikisha hapa na unatupeleka kuzimu maovu yote ya serkali yanafichwa wadadisi wanashughulikiwa, tiss in return wanapewa vyeo na nafasi za kazi kwenye taasisi zote za serkali matokeo yake taasisi hazina ufanisi maana fisadi ni tiss anaetakiwa kumchunguza takukuru nae ni tiss, kesi ikienda mahakamani Jaji nae ni tiss, it is a vicious circle
Could that be true? Pole nimerudia kuuliza tu maana nimerudia rudia kuusoma uzi na mchango wako kadhaaa hivi ili nitafakari vizuri. Ila neno MAFIA si zuri. Tumia nenolaupole kidogo tu.Ahsante.
 
Nilivyoambiwa na mwingine kuwa TISS hausiani na VISIASA SIASA. Hilo nalo ni jipya sijalisikia
Ni lini Mkurugenzi wao alishawahi kutoa tamko kwa niaba ya CCM?

Ukinikibu hapo labda sasa nitakuelewa. Zingine ni dhana tu nafikiri,
Na inawezekana nikawa sina ufahamu kama wewe, Nisaidie kupanua uelewa wangu na ufahamu wangu katika hilo
Akili zako hazikotoshi hata wewe mwenyewe.
Uliwahi kusikia TISS wakitoa matamko au waraka wa hata hizo kazi zao walizopangiwa kisheria.
 
Back
Top Bottom