CCM yaweza kutawala kwa miaka 100 ikiwa tu...

CCM yaweza kutawala kwa miaka 100 ikiwa tu...

Mkuu mbona Kiswahili chako kina walakini namna hii?




Na hapa chini uandishi wako una walakini.
Nakubaliana nawe.Niliandika haraka bila ku proof read. Nashukuru kwa kunisaidia mkuu.
Ahsante nitarekebisha.
 
Wacha kuidanga ccm, hizi mbinu ulizopendekeza hapa wakiamua kuzitumia wanaondoka madarakani mapema sana. Sio kwamba hawajui hizi mbinu ila haziwafanyi kushinda. Njia pekee ni kutumia Tiss kubaki madarakani. Hiyo ccm ni kama mwanamke mzee, hata ajipake wanja, avae nguo za vijana bado havutii na ukiona mwanamke mzee vijana wanamfuata ni hela zake ndio zinawavutia na sio urembo wake.
Mkuu Tindo siwadanganyi bali nawapa tips tu.
 
Mwenye akili ya mushkeli KAMWE hawezi kuvumiliwa. Wahi hospitali kabla hujaanza kuokota makopo.

Dah.Umenipatia bonge la tusi. Sina Mshkeli ila akili n inywele kila mtu ana zake.
Ila uzuri ume comment na hii ni kusema imekuingia na kukufurahisha na pengine kukukasirisha,
Tuvumilianae tu mkuu,
Toa sababu kwa nini umeona mshkeli?
 
CCM ni chama ambacho kimekuwa katika utawala wa taifa hili kwa miaka mingi sana. Na kina mizizi hadi mashinani tofauti na vyama vingine vya upinzani. Na kwa ujio wa vyama hivi pia kumeipa CCM changamoto si haba.

Kuwa na wanachama mpaka mashinani si jambo ambalo linaweza kudumu ikiwa CCM haitabadilisha mbinu zake katika ku maintain/Kushikilia na hata kuongeza wananchama wengine.

CCM inaweza kutawala hata zaidi ya miaka 100 ikiwa itafanya MABADILIKO katika mbinu zake bila hata kutumia NGUVU/MABAVU katika kushindana na WAPINZANI.
Baadhi ya mbinu hizo ni kuwa:

1. ili CCM izidi kukubalika na kudumu ni lazima iwe na kitengo chake maalumu kitakachohusika hasa na mambo ya UTAFITI/Research- CCM POLITICAL STRATEGY RESEARCH. Kitengo hikikiwe na WATAAALAMU mbali mabali wengine waliosomea POLITICAL SCIENCE NK
.Na kazi yake kuu iwe ni kufanya UTAFITI MASHINANI ili kujua
Ni nini WANACHAMA na Wananchi kwa ujumla HAWAKIPENDI ama WANGETAKA kifanywe .
Both katika:
KUINUA MAISHA ya wananchi,
Katika KUKIBORESHA chama cha CCM.

2. MALALAMIKO hayo ama MAPENDEKEZO yawe analyzed na YAFANYIWE KAZI.
Maisha ya Mtazanaia Mashinani YAKIBOREKA CCM itatawala zaidi ya miaka 100.

Lakini ikijiona na kusema "TUTASHINDA TU Sisi ni chama kikubwa" inaweza kuangushwa vibaya sana.

Anaweza AKAINUKA jamaa yeyote tu na akawa VERY CHARISMATIC leader MUHAMASISHAJI wa ajabu kutoka chama kingine na pengine akawa hana hata hela lakini ana MDOMO wa ASALI na kujikuta AMEITEKA mioyo ya Watanzania WENGI NA HATA WANA CCM . Huku aki MAJOR kuhusu udhaifu wa CCM na hivyo kubadili mkondo wa kisiasa nchini kabisa.

3.CCM POLITICAL STRATEGY RESEARCH IAJIRI vijana wasomi wanaojua SCIENTIFIC RESEARCH na mambo ya STATISTICS /TAKWIMU.
Kwa kufanya hivi CCM itajua MALALAMIKO,VILIO na MAHITAJI na MAPENDEKEZO ya watu na KUJARIBU kadri ya uwezo wao KUYATATUA ama kuwapa MATUMAINI.

4.VIONGOZI wa CCM wawe WASIKIVU wazuri sana.
Na Mtu akitoa maoni mbadala yaliyotofauti asionekane na kuwa ni mpinzani maana DEMOKRASIA ni lazima IWEMO NDANI ya CHAMA chenyewe cha CCM..

5..WAZEE waliochoka wapumzike tu polepole na kutoa ushauri bali si utafiti.

6.Mambo ya CCM yasiachiwe TISS. Acha TISS ishughulikie usalama wa Taifa letu.
Na mambo ya SIASA yaachiwe wanasiasa.

Na ikiwa ni ku chip in iwe ni kidogo kidogo sana. Maana wanatakikana kuwa APOLITICAL ENTITY/ WASIOEGEMEA chama chochote kulingana na kazi yao.
CCM kwa sasa inatumia Marungu, mapanga, jela, polisi, hongo kupata ushindi. Kwa mtaji huu itatawala milele.
 
Mwenye akili ya mushkeli KAMWE hawezi kuvumiliwa. Wahi hospitali kabla hujaanza kuokota makopo.
Haitatokea hata siku moja.
CCM walikufanyiaga nini Mkuu?
walikunyima teuzi?
hivyo NDO SABABU una hasira kali namna hii?
Maana hata sababu yako huielezi, bali ni kufyatua tu maneno yasiyo na heshima.
Labda unahitaji msaada wa kushauriwa kimawazo./Pyschological counselling!!!!!!
 
Tupo pamoja mkuu
sawa mkuu ni kubadilishana mawazo ma hoja tu kiistaarabu.
Sijui kwa nini wengine badala ya kijibu hoja ama kutoamaoni yeye ni matusi tu.
mara nyingi huwa sielewi ni kwa nini. Je unaweza kujua ni nini hasa huwa ni tatizo la watu kama hao?
 
Back
Top Bottom