CCM yawaruka Mussa Mkangaa na wenzake

CCM yawaruka Mussa Mkangaa na wenzake

Nafikiri uliyeleta hii thread uliyoyaandika siyo yale aliyoyasema, na kama amesema basi ulimi wake umeteleza.

Mh. Tindu Lissu hana mamlaka yoyote kisheria kuwafunga watu jela. Hii ni kazi ya Mahakama. tusipotoshe umma.

We jamaa vipi?aliyekwambia T.Lissu ni mahakama nani?akili.
 
CCM imeonyesha tabia halisi ya Kijambazi, imewalaghai watu wafungue kesi, sasa kesi wameshindwa inakataa kuwasaidia kulipa gharama za kesi. Ni aibu sana, watanzania wasiojua kitu ndio watakofungwa, mijitu ya CCM inaendelea kutanua. Athari za kupenda kutumika ndo zinaonekana. CCM wamemaliza kula muwa wanatema makapi!

[TABLE="width: 879"]
[TR]
[TD][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD]CCM yawatosa waliofungua kesi kupinga matokeo.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD]CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewageuka wanachama wake waliotumwa kufungua kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi katika majimbo mbalimbali nchini, Tanzania Daima Jumapili limebaini.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa waliofungua kesi kupinga ubunge wa Godbless Lema mkoani Arusha, wametoswa na sasa wanakusudia kumwangukia mbunge huyo kumwomba radhi ili awasamehe deni la uendeshaji wa kesi tangu mwanzo hadi juzi Mahakama ya Rufaa ilipomrejeshea ubunge.

Baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2010, CCM kupitia Katibu Mkuu wake, kwa wakati huo, Yusuf Makamba, iliandika barua yenye kumbukumbu namba CCM/OND/636/VOL.11/122 ya Novemba 9, 2010 kwenda kwa makatibu wake wa mikoa na wilaya kuwaamuru wote walioshindwa katika uchaguzi wapinge matokeo, na kwamba chama kingewasaidia gharama za uendeshaji wa kesi hizo.

Katika barua hiyo, Makamba aliwataka wagombea wa ubunge kufungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, huku wagombea udiwani walioangushwa kufungua kesi katika mahakama za mahakimu wakazi ndani ya siku 30, tangu ulipofanyika uchaguzi huo.

Katika barua hiyo ambayo Tanzania Daima Jumapili ina nakala yake, Makamba aliwaagiza makatibu wa CCM wa mikoa kwa kushirikiana na makatibu wa wilaya na kata kuwasaidia wagombea walioshindwa kwenye uchaguzi kuandaa hoja za malalamiko na vielelezo kwa ajili ya kupeleka mahakamani, huku akisisitiza kuwa "Chama Cha Mapinduzi Makao Makuu kitachangia gharama za mawakili kwa wagombea ambao hawana uwezo kifedha."

Baadhi ya wabunge wa upinzani walioshitakiwa na kesi zao kuhukumiwa na kuibuka kidedea, hawajalipwa gharama za uendeshaji wa kesi hizo.
Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde (CHADEMA) kupitia kwa wakili wake, Benjamin Mwakagamba wa Kampuni ya uwakili ya BM ya jijini Dar es Salaam, alisema kuwa, mdaiwa katika kesi hiyo, Dk. Lucas Siame (CCM) tangu aamriwe na mahakama kulipa, amekuwa haonekani mahakamani au kuonesha dalili zozote za kulipa gharama za uendeshaji wa kesi.
Wakili huyo anasema kuwa, mdaiwa huyo ambaye alipinga matokeo, amekuwa akiishi kwa kujificha maeneno ya Sinza, jijini Dar es Salaam.

Tanzania Daima Jumapili lilimtafuta Dk. Siyame kupitia simu yake ya mkononi akapatikana, ila alisema hajui utaratibu kama alipaswa kulipa au la.
"Mwandishi hizo habari za kulipa ndio nazisikia kwako," alisema lakini alikiri kuwa CCM haikumsaidia uendeshaji wa kesi aliyofungua dhidi ya Silinde.

Silinde, alishinda kesi katika Mahakama Kuu ya Rufaa Kanda ya Mbeya, baada ya kufuta shauri la kesi ya rufaa iliyopelekwa na Siame, aliyekuwa mgombea wa CCM, Mei 2, mwaka huu.

Siame aliyekuwa amekata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa Julai mosi, mwaka jana dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu uliompa ushindi mbunge huyo wa CHADEMA, alilazimika kuomba mahakama kuondoa shauri hilo.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu' (CHADEMA) ambaye naye alishinda kesi ya pingamizi iliyofunguliwa na Benson Mpesya (CCM), alipoulizwa endapo amelipwa fidia kama ilivyoamriwa na mahakama, alisema kuwa amelipwa sehemu ya fedha, na nyingine bado.

Sugu alisema kuwa, hata hivyo Mpesya amekuwa akimtuma wakili wake kuonana na wa kwake ili angalau amwongezee muda wa kulipa. "Nimekuwa mstaarabu sana, ningeweza kutafuta amri ya mahakama ili mali zake zikamatwe, lakini alimtuma wakili wake nimvumilie," alisema Mbilinyi.

Wakati mzigo wa kulipa gharama ukiwaangukia wafungua kesi, waliomshtaki Mbunge wa Singida Mjini, Tundu Lissu (CHADEMA) wanatafuta suluhu. Walalamikaji wawili waliokata rufaa dhidi ya Lissu, ambao kesi yao bado haijaanza kusikilizwa, tayari wameshaanza kumtafuta mbunge huyo ili wafanye utaratibu wa kuondoa kesi Mahakama ya Rufaa.

Akizungumza kwa simu kutoka Muyanji-Makiungu, Singida, mlalamikaji wa kwanza katika kesi hiyo, Shabani Selema alisema: "Natamani sana kuiondoa kesi hiyo mahakamani ambayo Chama chetu Cha Mapinduzi kilishinikiza tukate rufaa, lakini kwa sasa chama hakieleweki, sina haja tena na hiyo kesi, sitaki na ninataka kwenda Dodoma nionane na wakili wetu angalau nichukue hata kitambulisho changu cha mpiga kura kwani kilikuwa ni sehemu ya vielelezo, mimi nakuahidi kuwa nakuja Dar es Salaam wakati wowote na nitamtafuta Lissu tukafute hiyo kesi."

Alipohojiwa inakuwaje ajitoe katika hatua hii ya rufaa, Selema alijibu: "Mwandishi kama kuandika andika tu, mimi hii kesi sina hamu nayo, nimekuwa naiendesha mwenyewe, hata familia yangu, rafiki zangu na wasomi mbalimbali sasa wananishangaa, chama kimeniacha, kwanza wamenivuruga sana."

Kwa upande wake, Lissu alisema taarifa kwamba mlalamikaji wake anamtafuta ili wafute kesi, amezisikia kutoka kwa wanafamilia yake.

Tanzania Daima Jumapili iliwatafuta viongozi wa CCM Makao Makuu kuzungumzia suala hilo, lakini simu zao hazikuweza kupatikana hewani huku simu ya Naibu Katibu Mkuu bara, ikiita muda wote bila kupokelewa.

Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda alipopigiwa simu hakuweza kupokea, lakini baadaye alimpigia mwandishi na kumuuliza: "wewe nani?"
Mwandishi alipojitambulisha kwamba anatoka Tanzania Daima Jumapili, Chatanda alisema: "Kama wewe ni wa Tanzania Daima, nipigie sina haja ya kukupigia." Baada ya kusema hayo akakata simu, na alipopigiwa tena, simu ilikuwa tayari imefungwa - haikupatikana tena.

Source – TANZANIA DAIMA


[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][TABLE="width: 599"]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Pango la mashetani ndio lilivyo, ni umafia kwa kwanda mbele.
 
Hakuna sababu ya kuilaumu CCM, huu ni wakati sasa wa waliodanganywa na tamaa za kutaka fedha bila jasho kujilaumu na kuwa onyo kwa wengine wasifuate mkumbo huo. Watanzania tumekuwa na hulka za ajabu ukiambiwa tu fanya hiki utapata fedha bila kutafakari unaenda kichwa mbele. Sasa waone matokeo yake. Nawashauri wote walioshinda kesi hakuna kusamehe ni lazima walipe gharama za kesi ili iwe fundisho kwa wengine pia.

CCM imeonyesha tabia halisi ya Kijambazi, imewalaghai watu wafungue kesi, sasa kesi wameshindwa inakataa kuwasaidia kulipa gharama za kesi. Ni aibu sana, watanzania wasiojua kitu ndio watakofungwa, mijitu ya CCM inaendelea kutanua. Athari za kupenda kutumika ndo zinaonekana. CCM wamemaliza kula muwa wanatema makapi!
 
images


CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewageuka wanachama wake waliotumwa kufungua kesi za kupinga matokeo ya uchaguzi katika majimbo mbalimbali nchini, Tanzania Daima Jumapili limebaini. Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili, umebaini kuwa waliofungua kesi kupinga ubunge wa Godbless Lema mkoani Arusha, wametoswa na sasa wanakusudia kumwangukia mbunge huyo kumwomba radhi ili awasamehe deni la uendeshaji wa kesi tangu mwanzo hadi juzi Mahakama ya Rufaa ilipomrejeshea ubunge.


Baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2010, CCM kupitia Katibu Mkuu wake, kwa wakati huo, Yusuf Makamba, iliandika barua yenye kumbukumbu namba CCM/OND/636/VOL.11/122 ya Novemba 9, 2010 kwenda kwa makatibu wake wa mikoa na wilaya kuwaamuru wote walioshindwa katika uchaguzi wapinge matokeo, na kwamba chama kingewasaidia gharama za uendeshaji wa kesi hizo.

Katika barua hiyo, Makamba aliwataka wagombea wa ubunge kufungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, huku wagombea udiwani walioangushwa kufungua kesi katika mahakama za mahakimu wakazi ndani ya siku 30, tangu ulipofanyika uchaguzi huo. Katika barua hiyo ambayo Tanzania Daima Jumapili ina nakala yake, Makamba aliwaagiza makatibu wa CCM wa mikoa kwa kushirikiana na makatibu wa wilaya na kata kuwasaidia wagombea walioshindwa kwenye uchaguzi kuandaa hoja za malalamiko na vielelezo kwa ajili ya kupeleka mahakamani, huku akisisitiza kuwa “Chama Cha Mapinduzi Makao Makuu kitachangia gharama za mawakili kwa wagombea ambao hawana uwezo kifedha.”

Baadhi ya wabunge wa upinzani walioshitakiwa na kesi zao kuhukumiwa na kuibuka kidedea, hawajalipwa gharama za uendeshaji wa kesi hizo.


  1. Mbunge wa Mbozi Magharibi, David Silinde (CHADEMA) kupitia kwa wakili wake, Benjamin Mwakagamba wa Kampuni ya uwakili ya BM ya jijini Dar es Salaam, alisema kuwa, mdaiwa katika kesi hiyo, Dk. Lucas Siame (CCM) tangu aamriwe na mahakama kulipa, amekuwa haonekani mahakamani au kuonesha dalili zozote za kulipa gharama za uendeshaji wa kesi. Wakili huyo anasema kuwa, mdaiwa huyo ambaye alipinga matokeo, amekuwa akiishi kwa kujificha maeneno ya Sinza, jijini Dar es Salaam. Tanzania Daima Jumapili lilimtafuta Dk. Siyame kupitia simu yake ya mkononi akapatikana, ila alisema hajui utaratibu kama alipaswa kulipa au la. “Mwandishi hizo habari za kulipa ndio nazisikia kwako,” alisema lakini alikiri kuwa CCM haikumsaidia uendeshaji wa kesi aliyofungua dhidi ya Silinde. Silinde, alishinda kesi katika Mahakama Kuu ya Rufaa Kanda ya Mbeya, baada ya kufuta shauri la kesi ya rufaa iliyopelekwa na Siame, aliyekuwa mgombea wa CCM, Mei 2, mwaka huu. Siame aliyekuwa amekata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa Julai mosi, mwaka jana dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu uliompa ushindi mbunge huyo wa CHADEMA, alilazimika kuomba mahakama kuondoa shauri hilo.
  2. Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (CHADEMA) ambaye naye alishinda kesi ya pingamizi iliyofunguliwa na Benson Mpesya (CCM), alipoulizwa endapo amelipwa fidia kama ilivyoamriwa na mahakama, alisema kuwa amelipwa sehemu ya fedha, na nyingine bado. Sugu alisema kuwa, hata hivyo Mpesya amekuwa akimtuma wakili wake kuonana na wa kwake ili angalau amwongezee muda wa kulipa. “Nimekuwa mstaarabu sana, ningeweza kutafuta amri ya mahakama ili mali zake zikamatwe, lakini alimtuma wakili wake nimvumilie,” alisema Mbilinyi.
  3. Wakati mzigo wa kulipa gharama ukiwaangukia wafungua kesi, waliomshtaki Mbunge wa Singida Mjini, Tundu Lissu (CHADEMA) wanatafuta suluhu. Walalamikaji wawili waliokata rufaa dhidi ya Lissu, ambao kesi yao bado haijaanza kusikilizwa, tayari wameshaanza kumtafuta mbunge huyo ili wafanye utaratibu wa kuondoa kesi Mahakama ya Rufaa. Akizungumza kwa simu kutoka Muyanji-Makiungu, Singida, mlalamikaji wa kwanza katika kesi hiyo, Shabani Selema alisema: “Natamani sana kuiondoa kesi hiyo mahakamani ambayo Chama chetu Cha Mapinduzi kilishinikiza tukate rufaa, lakini kwa sasa chama hakieleweki, sina haja tena na hiyo kesi, sitaki na ninataka kwenda Dodoma nionane na wakili wetu angalau nichukue hata kitambulisho changu cha mpiga kura kwani kilikuwa ni sehemu ya vielelezo, mimi nakuahidi kuwa nakuja Dar es Salaam wakati wowote na nitamtafuta Lissu tukafute hiyo kesi.” Alipohojiwa inakuwaje ajitoe katika hatua hii ya rufaa, Selema alijibu: “Mwandishi kama kuandika andika tu, mimi hii kesi sina hamu nayo, nimekuwa naiendesha mwenyewe, hata familia yangu, rafiki zangu na wasomi mbalimbali sasa wananishangaa, chama kimeniacha, kwanza wamenivuruga sana.” Kwa upande wake, Lissu alisema taarifa kwamba mlalamikaji wake anamtafuta ili wafute kesi, amezisikia kutoka kwa wanafamilia yake.

Tanzania Daima Jumapili iliwatafuta viongozi wa CCM Makao Makuu kuzungumzia suala hilo, lakini simu zao hazikuweza kupatikana hewani huku simu ya Naibu Katibu Mkuu bara, ikiita muda wote bila kupokelewa. Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Mary Chatanda alipopigiwa simu hakuweza kupokea, lakini baadaye alimpigia mwandishi na kumuuliza: “wewe nani?”
Mwandishi alipojitambulisha kwamba anatoka Tanzania Daima Jumapili, Chatanda alisema: “Kama wewe ni wa Tanzania Daima, nipigie sina haja ya kukupigia.” Baada ya kusema hayo akakata simu, na alipopigiwa tena, simu ilikuwa tayari imefungwa - haikupatikana tena.
 
Mussa Mkanga apige mnada ile nyumba yake iliyopo sombetini,akisamehewa NITAKUWA CHADEMA MFU,hii itasaidia kuwapa fundisho wale wote wanaojipendekeza.
 
Nakumbuka mara baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 Makamba Snr alipowa-encourage wale walioshindwa uchaguzi kwenda kufungua kesi mahakamani.. Akiwaahidi kuwapa ushirikiano kwa acilimia 100.. Usanii wa hali ya juu toka kwa vuvuzela..

Ili liwe fundisho kwa wengine wenye tamaa ya kutumika ili kupata wepeci wa maisha.. hao wote waliofungua keci na kushindwa walipe gharama zote za keci.. Hakuna kusamehewa kwani walikuwa na nia ovu mioyoni mwao na njia pekee ya kuiondoa hiyo nia ovu ni kwa wao kuwajibika kwa mujibu wa sheria (ambayo ni kulipa gharama)..
 
CCM ni matapeli na majingili, hasa toka Mwl. Nyerere alipoondoka. CCM ndilo genge kubwa la kimafia kusini mwa Afrika.
 
Siku Moja Shetani alimtembelea Mungu. Mungu akamwambia mbona Unaniharibia watu wangu kwa nguvu na kasi kubwa hivyo. Shetani akamjibu ."Mtukufu uharibifu wote huo unaouona mwingine sio mimi ninayefanya fanya. Hao binadamu wengine wamepituka. hayo hayo mengine ni yao wanayofanya ni yao. Natuma mtu amdhulumu mtu mmoja mmoja. lakini kwa haya ya kudhulumu halaiki ni yao wenyewe wamebuni".Mwisho wa kunukuu. Hao watu type ya Mkangaa walipe hakuna msamaha wamewadhulumu watu wa Arusha kwa miezi tisa sasa. tutafidiaje hiyo huduma tuliyokosa wana arusha? kwa msamaha ? hapana walipe ili wakome. tena mi nashauri baada ya kumaliza shamrashamra lema akakazie hukumu fasta.
 
Tulikwishawaambia ccm inawatumia Kama toilet paper halafu wanatupwa chooni mchezo unakwisha
 
Ingekuwa vyema kukazia hukumu kwa kutoa na time limit ya kulipwa kwa gharama hizo, maana wengine watabweteka na 'MDENI HAFUNGWI'.
 
Hakuna sababu ya kuilaumu CCM, huu ni wakati sasa wa waliodanganywa na tamaa za kutaka fedha bila jasho kujilaumu na kuwa onyo kwa wengine wasifuate mkumbo huo. Watanzania tumekuwa na hulka za ajabu ukiambiwa tu fanya hiki utapata fedha bila kutafakari unaenda kichwa mbele. Sasa waone matokeo yake. Nawashauri wote walioshinda kesi hakuna kusamehe ni lazima walipe gharama za kesi ili iwe fundisho kwa wengine pia.

Na uzuri shauri la Mh. Lema limeweka historia nzuri sana. Kuanzia sasa ni marufuku wanaojiita "wapiga kura" kufungua kesi kwa niaba ya wagombea walioshindwa kama ambavyo imekuwa ikifanywa na CCM muda wote.

Huu ni zaidi ya upuuzi na inaonesha jinsi watanzania tusivyo na kazi za kufanya badala yake tunakubali kutumika. La kufurahisha mwisho wa yote wametupwa kama mipira ya kiume wapuuzi hawa.

Hoja nzuri sana hii kwa vyama vya upinzani kuipeleka kwa wananchi jinsi CCM ilivyowatumia wananchi vibaya kwa muda mrefu tena
kinyume cha sheria. Yapasa wananchi kulijua hili kwa undani na kwa kina - mshindwe wenyewe wapinzani.
 
Back
Top Bottom