CCM yapasuka? Kinana ang'atuka...

mwanaume akiguna jua amekili kosa. Kumbe kweli kang'atuka!. Asante nape. mia
 

Kinana ndiye 'mzee' pekee aliyekuwa mstari wa mbele uchaguzi wa 2010. Angeweza kabisa kuachia ngazi baada ya uchaguzi kuisha maana kila kitu kilienda hovyo na sura ya CCM mpya ilikuwa hadharani. Lakini alibaki kundini na week chache tu alikuwa Marekani na wanachama wa CCM wa huko. Kinachoondelea sasa hivi Dodoma ni 'cheusi chekundu' kwa matumaini kwamba kundi moja litakuwa limekunywa wanzuki ya kutosha na hivyo kutogundua ni kitu gani hasa kinaendelea hadi pale watakapojikuta kwenye tope.

Lakini (LAKINI) kwa bahati mbaya/nzuri wote wanajuana na ndani ya 36 hours all the splinter groups wataanza safari (kwa pamoja lakini different caravan) kuelekea kibla. Hakuna hatua yoyote itakayochochukuliwa Dodoma amabayo haitakuwa na madhara. Hakuna. Wapatane, wapigane ngeu, wajidunge sindano ya ganzi, vyovyote vile watakutana na madhara. Muda wa CCM kujipanga ulishapita, and the only way, and I mean the only way, ni lazima usemi usemao 'hujafa hujaumbike' utimie. Lazima watoke nje ya ulingo wakaanze upya.
 


Kweli mkuu NasDaz,

Speed ya kukimbia jamvini kuweka mambo sawa na muda aliofanya hivyo lazima utupe hints kwamba mambo hayako sawa!!

CCM imezaliwa mikononi mwetu na sasa tunashuhudia jinsi inavyokata roho....Hii aina ya uongozi ya akina Nape haijawahi kuwepo kwenye CCM ya akina Msekwa, Kawawa, Kolimba, Mangula....labda kwa akina Makamba na Mukama!!

Something is very wrong somewhere!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mwita Maranya ishu iliyoko ubaoni ni kujiuzulu kwa Kinana. Wewe kama una yako na Ndungulile fungulia thread tutachangia....
 
KInana amesoma alama za nyakati akaona kheri aliache Jahazi la CCM linaloelekea Nungwi ili yeye abaki kama Mtazamaji!
 
Mkuu NasDaz you cant be seriou my friend. Kinana huyu huyu tunayemfahamu anapambana na ufisadi/mafisadi? Mara hii umeshasahau lundo la tuhuma zake za rushwa, ufisadi na uharamia wake? Zipo thread nyingi tu hapa ukizitafuta utazipata zimeweka wazi kila kitu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Nape, kwanza asante kujitokeza mapema kuujibu ule uzushi!, lakini kusema tuu ni uzushi hakutoshi!. Ile thread unayoiita ya uzushi, inazungumzia barua Kinana aliyoiandika!, wewe unazungumzia maneno Kinana aliyoyatamka, hivyo ni vitu viwili tofauti!.

Sasa ili kanusho lako liwe na maana, tungeshukuru kama ungetufafanulie
  1. Jee Kinana ameandika barua?.
  2. Kwenye barua hayo uliyoyasema wewe ndiyo yaliyomo kwenye hiyo barua?.
  3. Kama ameandika barua, na hayo uliyoyasema ni matamshi ya mdomo, then ile thread still stands mpaka uthibitishe hata kwenye barua, yale hayapo!.
  4. Mode, Nape akithibitisha ule ni uzushi, then funge ile thread na kumpatia muanzisha thread haki yake!.
  5. Nape, tunakushauri, karibu tena na tena sio tuu kukanusha thread za uzushi, bali pia jitokeza kujibu baadhi ya hoja valid kuhusu CCM!.
Asante.

Pasco.
 
Watch And Learn.

Itaandikwa vitabuni kuwa ilikuwa ni Dodoma 2012
 
Nape si uutenge tu huo mzigo wote wa barua ya babu Kinana hapa watanzania tuuchambue wenyewe?? au ni nyaraka ya serikali?? anyways, hata wewe huwezi kuaminika kwa hiyo mistari yako uliyoiweka hapo.

ILA ANGALAU TUMEJUA KUWA KINANA KAAMUA KUKAA KANDO, IWE KWA KHERI AU KWA SHARI. Halafu Nape, haya maneno ya siasa uchwara ndani ya CCM mbona ni ya kawaida sana, kilichokufanya uje haraka haraka kui-neutralize ile thread iliyotangulia ni nini??

MBONA ROSTAM ALIZICHANA SIASA UCHWARA ZA ccm LIVE, NA WEWE BINAFSI UKANYWEA NA HUKUTOA TAMKO?? duh!! Nape bhana una matatizo sana.
 
Wewe nape huwezi sema yote, Mimi nahisi kweli kachoka na siasa uchwara maana yaloelezwa kwenye barua yake ni ya kweli kama siyo kweli tolea ufafanuzi wa familia yote ya mkuu kuingia NEC!
 
Kama kumbukumbu zangu zipo sawa ni kwamba Kinana alikuwa anawachana akina Lowassa live ndani ya vikao.....hilo la ufisadi wa Kinana nafahamu limeshwahi kuibuka hapa JF!
 
Kuhusu kujiuzulu sijui kungatuka kwa kinana bila kufata la nape wala la wanaosema siasa uchwara.

Kama wewe ni greatthinker utajiuliza hivi

Ni juzi tu alikuwa manager wa kampeni, alifungua tawi USA huko, alikuwepo kwenye team ya usuluhishi kwa makundi yasiyopatana CCM, na bado ana umri mzuri tuu kuendesha siasa ukilinganisha historia ya viongozi wengi wa CCM...sasa jiulize why yeye???? na kwanini kwa muda huu? Then utapata jibu na kujua mchele ni upi kati ya nape na wanaodai ni siasa uchwara.
 
Mbona kanusho limetoka haraka hivi? hiyo moja; Pili wapi barua kamili ya kung'atuka? Tatu mbona ile thread hadi sasa iko hewani?.................najaribu kuunganisha mambo


Leo tuko pamoja Elizabeth Dominic,


Hii speed ya mwanga aliyokimbia nayo Nape siyo ya CCM tunayoijua......

Labda kama alitokea kwa Mch Rwakatare kuombewa!
 
Last edited by a moderator:
Ukitaka kufahamu kuwa hili neno 'kupokezana vijiti' linawekwa tu ili kujibu hoja hata kama halina mantiki fikiria haya:
F.Sumaye na E.Lowassa wamefikia katika uongozi wa juu kitaifa (mawaziri wakuu), wamepata fursa ya kufanya yale waliyoyafikiria kwa taifa iwe kwa njia nzuri au mbaya. Hivi kuna sababu gani ya wao kugombea NEC, kwanini wakiwa wameshatoa vijiti wanarudi upande wa pili kulilia vijiti vile vile?

Pili, jiulize muda wa kupokezana vijiti ni miaka mingapi? Kama tutakubali Kinana anatoa kijiti basi wote akina Nape na wengine nao watatumia miaka 25 kama base line. Jiulize kupokezana vijiti kunatokea mtu akiwa katika utumishi wa chama kwa miaka mingapi, na nafasi gani zinazotumika kutoa vijiti?

Fikiria kuwa ndani ya NEC na CC ya sasa kuna watu wangapi wametumikia kwa miaka zaidi ya 15 hadi 20.
The bottom line, ni kigezo gani linatumika kusema huyu kajiuzulu, huyu kakimbia siasa uchwara,huyu katoa kijiti, huyu kaogopa chama kufia mikononi mwake n.k.
 
Izi chaguzi on a seroius note mwisho wa siku zitaleta sintofahamu nyingi ndani ya CCM.
Vitisho toka kwa akina Mkono,na matamko ya kila leo ya akina SITTA ni wazi kwamba hao watu watapigwa chini na we never know hasira zao witawatuma wachague karata ipi ndani ya chama au waende upinzani.
Na kuhusu kungatuka kwa Mzee wetu Kinana mengi yatasemwa na wengi wanaweza mfuata kwa mtindo wa kungatuka
 
Pasco,

Mimi sio Nape na siye uliyeniuliza swali, lakini naomba nitoe ufafanuzi kidogo.
Kinana hajagombea nafasi za uongozi katika uchaguzi. Hii ni tofauti na mtu aliye madarakani anapoyaacha madaraka hayo. Madaraka ya Kinana yamemalizwa kwa mujibu wa katiba ya chama na sasa ni uchaguzi ambao angeweza kuamua kugombea au kutogombea.
Katika hali kama hiyo hakuna sababu ya kuandika barua.
Sijasema kuwa hakuna barua iliyoandikwa ila sioni umuhimu wa kuchimbachimba na kutafuta barua iwapo mtu ameamua kutogombea nafasi fulani ya uongozi.
 
Last edited by a moderator:
Kuna uwezekano kuwa hii issue ikawa picked kwenye mainstream media kesho. Of course kila mmoja wetu anao wajibu wa kucrosscheck kuthibitisha taarifa hii. Binafsi nimefanya. Nimetafuta hapa na pale kwa sources zangu huko Dodoma. Sijapata sana kitu tangible, lakini pia kwa maelezo niliyopata siwezi kumbishia aliyeanzisha hoja hii. Maana swali ambali wengi wanajiuliza ndani ya magamba in uamuzi wake wa kutowania nafasi yoyote ndani ya chama chao cha magamba aka chama cha mabwepande, katika uchaguzi wao we ndani unaoendelea. It has been found to be unusual thing.

Ofcourse jamaa wameshindwa kukaa CC leo kama walivyopanga. Wamelazimika kuahirisha mara mwili, asubuhi na jioni ya leo. Vikao vya maadili, ulinzi na usalama vimeshindikana kumalizika kwa muda Kama ilivyotakiwa. Makundi yanaparurana. Magamba yameshika hatamu. Yamekomea kiunoni. Hayavuki tena. Nani wa kumfunga paka kengele. Unakumbuka kamati yao hiyo eti ya maadili, ulinzi na usalama iliwahi kuongozwa na mmoja wa watuhumiwa sugu wa ufisadi nchini. Kisha eti ikapewa kazi ya kusimamia uchunguzi wa tuhuma za Nape juu ya jengo la UVCCM.

Sasa CC ya Chama Cha Mabwepande inawezekana ikakutana kesho.
 

Mkuu Mwita. Hapa tunajadili ishu ya kinana. Wewe kama una yako na Ndungulile anzisha thread tutachangia
 
Last edited by a moderator:
Pasco,

Ndugu hapa Nnauye Jr harudi. Hili chama halijielewi na halieleweki. Na hapa ndio tutaona umuhimu wa Mwanahalisi, hawa wengine watapiga tu propaganda.
 
Last edited by a moderator:

Kinana ana umri gani? Umri wa kustaafu ni miaka mingapi?

Tambua kuwa watu hufanya shughuli za siasa kwa purpose fulani sio kwa mazoea. Mtu anapoona ile purpose imetimia au haiwezi kutimia hana sababu ya kuendelea kung'ang'ania madarakani. Hizo siasa za kugombea tu ili mradi aonekane yuko madarakani ni siasa za mazoea na huu siyo wakati wake.

Kumbuka uchaguzi huu ungempa Kinana majukumu kwa miaka mingine mitano. Je, yuko tayari kubeba majukumu kwa miaka hiyo mitano?

Unajua daktari wake amemshauri vipi?

Unajua familia yake ina msimamo gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…