Hali ya hewa ilichafuka jana katika ufunguzi wa tawi la CCM la Isesa ambapo nusura vijana CCM na wa Chadema watwangane makonde baada ya vijana wa Chadema kuwatuhumu CCM kwamba wamewaibia bendera ya chama chao.
Mabishano kuhusu bendera hiyo yaliendelea katika kipindi chote ambacho Kinana alikuwa akizungumza na wanachama wa tawi hilo.
"Hawa CCM wameng'oa bendera yetu hapa huo siyo ustaraabu ni lazima mturudishie bendera yetu vinginevyo patakuwa hapatoshi," mmoja wa vijana wa Chadema alisikika akisema.
Hata hivyo, busara za askari polisi waliokuwa katika mkutano huo zilisaidia kuzima hasira za vijana wa Chadema ambao walionekana kuwa wengi kuliko wale wa CCM.
Source: Mwananchi