CCM yango'a bendera ya CHADEMA na kusababisha ghasia Sumbawanga

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Hali ya hewa ilichafuka jana katika ufunguzi wa tawi la CCM la Isesa ambapo nusura vijana CCM na wa Chadema watwangane makonde baada ya vijana wa Chadema kuwatuhumu CCM kwamba wamewaibia bendera ya chama chao.

Mabishano kuhusu bendera hiyo yaliendelea katika kipindi chote ambacho Kinana alikuwa akizungumza na wanachama wa tawi hilo.

"Hawa CCM wameng'oa bendera yetu hapa huo siyo ustaraabu ni lazima mturudishie bendera yetu vinginevyo patakuwa hapatoshi," mmoja wa vijana wa Chadema alisikika akisema.

Hata hivyo, busara za askari polisi waliokuwa katika mkutano huo zilisaidia kuzima hasira za vijana wa Chadema ambao walionekana kuwa wengi kuliko wale wa CCM.

Source: Mwananchi
 
Sasa hawa magamba wanataka tuwashe moto siyo? Ndio mambo ya safu chakavu siyo? patachimbika...
 
Ccm wezi wa kura,wezi wa pembe za ndovu,wezi wa Epe,wezi wa,,,,,,hata na bendera wanaiba ?basi wakaitundike pale lumumba basi kha!
 
Ccm wezi wa kura,wezi wa
pembe za ndovu,wezi wa Epe,wezi wa,,,,,,hata na bendera wanaiba ?basi
wakaitundike pale lumumba basi kha!

CDM mnashindwa siasa mnabaki na propagander zisizo na msingi
 
Tufanye kama Marekani na nchi zingine za Ulaya bendera za vyama ziachwe kupeperishwa wakati wa kampeni au mikutano ya hadhara ya vyama bali itumike bendera ya taifa tu ili kukuza uzalendo.

kwa walioona kampeni za marekani hakuna bendera za vyama bali ya marekani tu na hii inawaunganisha wananchi kujenga nchi.

Tunahitaji pia kuangalia upya sare za vyama kama zinalenga kujenga utaifa au kubomoa utaifa.
 
Sijaamini leo umetoa hoja ya busara sana.
 
CCM wamekosa hekima, busara na subira.
Sijui wana viongozi kweli?
Au viongozi wao ndio wenye akili za kuku wanawaongoza wafuasi wao kung'oa bendera
 
Tufanye kama Marekani na nchi zingine za Ulaya bendera za vyama ziachwe kupeperishwa wakati wa kampeni au mikutano ya hadhara ya vyama bali itumike bendera ya taifa tu ili kukuza uzalendo.

kwa walioona kampeni za marekani hakuna bendera za vyama bali ya marekani tu na hii inawaunganisha wananchi kujenga nchi.

Tunahitaji pia kuangalia upya sare za vyama kama zinalenga kujenga utaifa au kubomoa utaifa.

Umetoa hoja ya msing sana isivyo kawaida yako. Endelea kufunguka Mama Porojo.
 
Sikubaliani kwamba Polisi huwa wanatumia busara kutatua matatizo kati ya CHADEMA na CCM
 
ccm wezi wa kura,wezi wa pembe za ndovu,wezi wa epe,wezi wa,,,,,,hata na bendera wanaiba ?basi wakaitundike pale lumumba basi kha!
hivi kile chama ambacho viongozi weke wa juu hawaoi na wakioa wanaopoa wake za watu ni chama gani kile!
 
nakubaliana na hoja ya Mama Porojo, kuna sbsbu za msingi kwamba ikiwezekana vyama visiwe na bendera kwenye mikutano yao, na labda kama ni muhimu wawe na nazo basi ziishie kwenye ofisi zao tu ili tupunguze misuguano mingine isiyo na maana
 
Tufanye kama Marekani na nchi zingine za Ulaya bendera za vyama ziachwe kupeperishwa wakati wa kampeni au mikutano ya hadhara ya vyama bali itumike bendera ya taifa tu ili kukuza uzalendo.

kwa walioona kampeni za marekani hakuna bendera za vyama bali ya marekani tu na hii inawaunganisha wananchi kujenga nchi.

Tunahitaji pia kuangalia upya sare za vyama kama zinalenga kujenga utaifa au kubomoa utaifa.
Daughter you are growing up now. I will bring you "eat some more" chocolate when I come back!
Now go and finish that assignment!
 
CCM kwenye mabango, Chadema kwenye mioyo yetu.
mtang'oa bendera ila hamtaweza kuyang'oa matumaini tuliyojiwekea juu ya CHADEMA.

HATARI:
Weka mbali na Tembo.
 
Tufanye kama Marekani na nchi zingine za Ulaya bendera za vyama ziachwe kupeperishwa wakati wa kampeni au mikutano ya hadhara ya vyama bali itumike bendera ya taifa tu ili kukuza uzalendo.

kwa walioona kampeni za marekani hakuna bendera za vyama bali ya marekani tu na hii inawaunganisha wananchi kujenga nchi.

Tunahitaji pia kuangalia upya sare za vyama kama zinalenga kujenga utaifa au kubomoa utaifa.

Mama umefanyiwa artificial insermination au stem transplant ndo umekuwa mpya kiasi hiki na kutoa mapoint?
 
tufanye kama marekani na nchi zingine za ulaya bendera za vyama ziachwe kupeperishwa wakati wa kampeni au mikutano ya hadhara ya vyama bali itumike bendera ya taifa tu ili kukuza uzalendo.

Kwa walioona kampeni za marekani hakuna bendera za vyama bali ya marekani tu na hii inawaunganisha wananchi kujenga
tunahitaji pia kuangalia upya sare za vyama kama zinalenga kujenga utaifa au kubomoa utaifa.

hapo umenena! Utaifa kwanza vyama baadae. Kila chama bendera! Ya taifa hatuitumii?
 
Back
Top Bottom