Lu-ma-ga kuna wakati nilitoa ushauri kwa CHADEMA kupitia upya Katiba yake kwani naamini matatizo yake yamelalia hapo watu hawakunielewa. Kwa nini Slaa alikwenda Mwanza? Hii ni hoja ya kikatiba na wala si suala la Slaa kutaka kuonyesha kwamba yeye ana uwezo wa kufanya kila kitu kwenye CHADEMA.
Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA mambo yakiamuliwa ngazi ya Jimbo au Wilaya (yenye Jimbo moja) ngazi inayofuatia ni Makao Makuu. Kwa maana nyingine Mgogoro wa Chagulani hauwezi kujadiliwa na Uongozi wa Mkoa wa Mwanza kwa sababu katiba haitambui hivyo, badala yake baada ya Chagulani kushindana na Kamati tendaji ya Wilaya ngazi iliyofuatia ilikuwa ni Makao Makuu.
Kama Katiba ingeelekeza mambo ya udiwani na madiwani kuishia au kupitia kwanza kwenye ngazi ya Mkoa kabla ya kwenda Makao makuu, basi bila shaka Slaa angekuwa ni mtu wa mwisho kwenda Mwanza kwenye uchaguzi wa Meya. Lakini kwa sababu watu wa wilaya ya Mwanza hawaelewani basi ngazi inayofuatia kimadaraka (siyo kiprotokali) ni Makao Makuu na hapo ndipo Katibu Mkuu anapoingia, Lakini kwa nini iwe hivyo? Hivi haya si mambo madogomadogo kwa Katibu Mkuu kuyashughulikia!!?