CCM yabariki waondoke kunusuru chama Wamo Werema, Tibaijuka, Maswi

Hawa watu ni Kweli kabisa walimuua Julius Kambarage Nyerere.
Bado kidogo wataanza kuuwana wenyewe kwa wenyewe
 
Mkuu hii nchi ukifikiria kwa undani unaweza kuwehuka.
Lakini tusikate tamaa kila kitu kinamwisho.

Ni kweli,lakini safari hii naona Bibi amekuja juu,shamba lake kumegwa kila wakati.
 
Uongo wa mchana uliotungwa na akili ndogo. CCM haina Kamati ya uongozi bali ina Kamati Kuu tu. Wadanganyeni wajinga wenzenu.
haijalishi nani kautunga, uongo au ukweli ukihusu mchuzi wa IPTL unanoga tu! hatuna haja ya kuuponda maana kila mtu ana hasira zake hapa!
 
Kwa sasa hivi Tanzania hatuna kiongozi mwenye kauli ya mwisho, mtu kama pinda hata hajui madaraka ya PM.

Bilali ndio kabisa yupo kama jino bandia ni show tu hana lolote.

ha! Huyo mzee haeleweki kabisa! Yeye anachoweza ni sherehe, kuzindua v2 vya ovyoovyo,mara mabomba, dini, na kutunuku vyeti wahitimu. Makamu wa rahisi ni kula bata tu!..
 
Alieilaani hii nchi inaonekana alishakufa ......

Watu wanachukua fedha bila hata ya aibu .....

Hata Mungu hawezi kutusaidia kwenye hili na mengine!

Isijekuwa laana ya Mwalimu. Najaribu ku-refer statement ya Vicent kule arumeru
 
  • CCM wataka wang'oke kukinusuru chama

  • CHADEMA, CUF wamtaka JK asiwakingie kifua

MACHO na masikio wiki hii yataelekezwa zaidi mjini Dodoma, kujua hatma ya watuhumiwa wanaodaiwa kuchota zaidi ya sh bilioni 300, zilizohifadhiwa kwenye Akaunti Maalum ya Tegeta Escrow katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Wiki hii, Bunge linatarajia kutumia siku mbili kujadili ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), iliyochunguza kashfa hiyo.

Habari kutoka ndani ya kikao cha wabunge wa CCM mjini hapa, zilibainisha kuwa wabunge wengi wameridhia watuhumiwa katika kashfa hiyo wawajibike kwa kuachia nafasi zao na kuhakikisha wanarejesha fedha hizo za umma. Watuhumiwa katika kashfa hiyo waliotajwa bungeni na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), ni pamoja na Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, Katibu Mkuu wake, Eliachim Maswi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema ambao wiki itakuwa chungu sana kwao.

Wengine ni Waziri wa Fedha Saada Mkuya, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Benno Ndulu na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Mhandisi Felchesmi Mramba, huku Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitajwa kuhusika kutokana na uzembe wa watendaji wake kushindwa kusimamia rasilimali za taifa.

CHADEMA: JK usimbebe Pinda

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kutomkingia kifua Waziri Mkuu Mizengo Pinda katika sakata la kuchota fedha kwenye Akaunti ya Escow, zilizohofadhiwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA Bara, John Mnyika wakati akifungua mkutano wa siku mbili kwa mkatibu na viongozi mbalimbali wa mikoa wa Baraza la Vijana wa CHADEMA, (BAVICHA). Alisema CHADEMA imenasa taarifa kwamba Rais Kikwete anashinikiza kutowajibishwa kwa Waziri Mkuu kuhofia Serikali yake kuanguka na ndio ameendelea kufumbia macho na kukaa kimya juu ya kashfa hiyo.

Mbali na Pinda, Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo, pia alimtaka Rais Kikwete kutokingia kifua watuhumiwa wengine katika kashfa hiyo kama watalazimika kuwajibika. Alisema kashfa hiyo imetokana na udhaifu wa Rais Kikwete na Serikali, ambao umeisababishia taifa hasara kwa baadhi ya watu wachache kuchota fedha hizo bila kuchukuliwa hatua yoyote.

Huku akishangiliwa na makada wa CHADEMA, Mnyika alisisitiza hakuna sababu hata chembe ya kumkingia kifua Waziri Mkuu Pinda, Werema, Maswi na wengine, kwani kiasi cha fedha kilichochotwa ni kikubwa na kingeweza kusaidia hata ujenzi wa maabara kwa nchi nzima badala ya kuwachangisha wananchi sasa.

Akizungumzia uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Mnyika aliwataka viongozi hao wa vijana kuhakikisha wanajipanga kukabiliana na hujuma zinazofanywa na Serikali kwa ajili ya kuhujumu uchaguzi huo pamoja na uchaguzi mkuu ujao. Alisema kuwa, hivi sasa kuna hujuma za baadhi ya wagombea wa vyama vya upinzani wanafanyiwa urasimu wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu za uchaguzi ili waonekane wameshindwa kufuata sheria.

Naibu Katibu Mkuu huyo, pia alilaani kauli za Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye, kwamba CHADEMA imesambaza waraka wa kutaka wagombea wote wawe wa CHADEMA badala ya Ukawa, jambo ambalo sio sahihi. Alisema makubaliano ya Ukawa ni kusimamisha mgombea mmoja mwenye nguvu kwenye kila nafasi ya uchaguzi hadi urais ili kuing'oa CCM.

Mnyika, aliwataka vijana hao kufanya kampeni ya kuikataa Katiba pendekezwa kwani ikipitishwa ni sawa na kurejesha ufisadi zaidi nchini. Jijini Dar es Salaam, Chama cha Wananchi (CUF), kimewataka Waziri Mkuu Pinda, Mwanasheria Mkuu Jaji Werema, Waziri wa Nishati na Madini Prof.

Muhongo pamoja na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Maswi, wajiuzulu au kufukuzwa mara moja. Pia kimeitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), iwachunguze haraka kama wamehusika na rushwa katika kuwezesha kampuni ya Pan African Power (PAP), ambayo imeshirikiana na viongozi wa serikali kuitapeli na kuibia fedha serikali kwa kuzichukua kutoka akaunti ya Tegeta Escrow.

Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, alisema viongozi hao moja kwa moja wanahusika katika kashfa hiyo, kwa kuwa hata Benki Kuu ilikuwa na wasiwasi kuwa fedha za Tegeta Escrow zilikuwa zinachukuliwa kinyume na utaratibu, lakini wao waliruhusu na kukaa kimya. Alisema Mwanasheria Mkuu, alivunja sheria kwa kuelekeza kuwa kodi ya ongezeko la thamani kwenye tozo la uwekezaji ‘capacity charges' isilipwe na kusababisha serikali kupoteza mapato ya sh bilioni 21.

Aliongeza kuwa, Waziri Mkuu kwa kushirikiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, hawakufanya uhakiki kuhusu uhalali wa umiliki wa kampuni ya IPTL na kusaini kutoa fedha za Escrow bila ya kuhakikisha fedha za Tanesco zinarudi, hivyo kulipotezea shirika zaidi ya sh bilioni 321.

Pia, alisema Mkurugenzi wa Shirika la Umeme (Tanesco), na Bodi ya shirika hilo, hawakutimiza wajibu wao wa kulinda maslahi ya shirika wanaloliongoza na kugeuza maamuzi yake yenyewe na kulikosesha sh bilioni 321, hivyo nao wanatakiwa kuachie ngazi. Alisema Waziri Mkuu ambaye ndiye kiongozi wa Serikali bungeni na Msemaji Mkuu, alilipotosha Bunge, aliposema bungeni mwezi Mei kuwa fedha hizo sio za umma isipokuwa kodi.

Prof. Lipumba, alisema BoT iliwahi kuandika barua kwa viongozi hao ili kujiridhisha pia anaamini hata Rais Kikwete analifahamu suala hilo na aliamua kukaa kimya bila kuchukua hatua zozote. "Hivyo tunamtaka Rais Kikwete aueleze umma kwa nini serikali yake ilishindwa kuzuia fedha za Tegeta Escrow zisiporwe wakati Benki Kuu ilionyesha wazi wasiwasi wake kuhusu uhalali wa kuhamisha fedha hizo," alisema Prof. Lipumba.

Aidha, alisema sakata la Tegeta Escrow linaonyesha umuhimu wa Bunge kuisimamia Serikali na Wabunge kutokuwa mawaziri kama ilivyopendekezwa katika Rasimu ya Katiba na Tume ya Jaji Warioba kabla ya kuondolewa kwenye katiba inayopendekezwa. Aliiongeza kuwa, baada ya ripoti ya CAG kukamilika, Waziri Mkuu amekuwa akitafuta visingizio vingi ili ripoti hiyo isijadiliwe bungeni .

Lipumba, alisema kuwa taarifa za vigogo wengi kupewa fedha kutoka akaunti inayomilikuwa na James Rugemalira inaonesha umuhimu wa kifungu kilichopendekeza zawadi za viongozi zirejeshwe serikalini, ambacho kimechakachuliwa ili kuruhusu viongozi wa serikali kuendelea kujichotea mali za Watanzania kwa njia ya hongo za zawadi.
 
Yego masika kinuki wasu abhanu abhaloma wasu nuje ika wasu masika.
 
Mbona wote wachafu tu!!WM ni MBUZI wa kafara alitakiwa Prof wa Kichina aanze kubwaga manyanga,sababu kama kiongozi lazima atakuwa amepelekewa issue nzima ,na kuelezwa vyema hali halisi,lakini hakuchanganya za kwake alichukua za kuambiwa na Werema tu,hivyo na yeye ajiondoe tu.:sad::sad::hatari:
 
NI vema kwa hekima za nchi pinda ukapumzika na ukajibu mashitaka ya jaribio na hatimaye kukwapua fedha mali ya umma
 
Fredrick-Werema-November22-2014.jpg

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema

Wakati mbivu na mbichi kuhusu sakata la uchotaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 za Escrow akaunti iliyopo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zikitarajia kujulikana wiki hii, habari za kina zaidi zinazowafanya wakubwa serikalini wakose usingizi zimezidi kubainika.

Taarifa ambazo NIPASHE imezikusanya kwa muda mrefu kutoka vyanzo mbalimbali, zinaonyesha kuwa sakata hilo linawatesa wakubwa katika kipengele cha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), mkataba ulivyofikiwa kati ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na IPTL, kukiukwa kwa taratibu na jinsi fedha hizo zilivyotolewa BoT.

Sababu nyingine ni jinsi Tanesco na IPTL walivyoingia katika mgogoro kuhusiana na ukokotoaji wa kiwango cha malipo ya uwekezaji na hatimaye mgogoro huo kuwasilishwa katika Mahakama ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICSID).

TANESCO ILIVYOINGIA MKATABA NA IPTL
Taarifa kutoka vyanzo mbalimbali zinaeleza kuwa Mei 26, 1995 , Tanesco iliingia katika makubaliano ya ununuzi wa umeme (Power Purchase Agreement – PPA), uliokuwa unazalishwa na IPTL Tegeta, jijini Dar es Salaam.

Makubaliano haya ambayo yalikuwa ni ya miaka 20, Tanesco ilitakiwa kulipa IPTL malipo ya manunuzi ya umeme (Energy Purchase Price) na malipo ya kiwango cha malipo ya uwekezaji (Capacity Purchase Price au Capacity Charge).

Hata hivyo, baada ya miaka kadhaa, IPTL na Tanesco waliingia katika mgogoro mkubwa kuhusiana na ukokotoaji wa kiwango cha malipo ya uwekezaji na suala hilo kuwasilishwa katika Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa (ICSID).

Uchunguzi wa NIPASHE unaonyesha kuwa kutokana na mgogoro huo kufikishwa mahakamani, Tanesco walitumia haki yao chini ya PPA kutoa notisi ya pingamizi la malipo (Invoice Dispute Notice), sambamba na kuomba kufunguliwa kwa Akaunti Maalum (Escrow Account), ili malipo yote yalipwe kwenye akaunti hiyo hadi pale migogoro hiyo itakapotatuliwa.

AKAUNTI YA ESCROW ILIVYOFUNGULIWA
Uchunguzi umebaini kuwa Julai 5, 2006, Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, IPTL na BoT waliingia katika makubaliano ya kufungua Akaunti Maalum (Escrow Account) ambayo serikali ingetekeleza Makubaliano ya Utekelezaji chini ya PPA kwa kuweka fedha katika akaunti hiyo.

Chini ya makubaliano hayo, fedha hizo zingeendelea kushikiliwa na BoT mpaka pale IPTL na serikali wangekuwa wamemaliza tofauti zao kuhusu viwango vya malipo ya uwekezaji.

Kwa mujibu wa Kifungu 7.7 cha Makubaliano ya Ufunguzi wa Akaunti (Escrow Agreement), fedha zilizomo kwenye akaunti hiyo zingeendelea kuwapo na kuwa katika mamlaka ya "Escrow Agent" ambaye ni BoT, na zingetolewa tu kama kuna hukumu ya Mahakama inayoamuru kutolewa kwake au kama pande mbili za Makubaliano (IPTL na Serikali) zitawasilisha makubaliano yanayoridhia kutolewa kwa fedha hizo kwa upande uliotajwa katika Makubaliano hayo.

MGOGORO ULIVYOAMLIWA NA MAHAKAMA
Uchunguzi wa NIPASHE umeendelea kubaini kuwa Mahakama Kuu ya Tanzania ilitoa uamuzi Septemba 5, 2013 uliogusa umiliki wa fedha zilizopo katika Akaunti ya Escrow iliyokuwa chini ya udhibiti wa BoT.

Kutolewa kwa uamuzi kulitokana na maombi yaliyokuwa yamefanywa na mmoja wa wanahisa wa IPTL –VIP Engineering & Marketing Limited (VIP) ambaye aliiomba mahakama iridhie kufutwa kwa shauri ambalo VIP walikuwa wamelifungua Mahakamani (Misc. Civil Application No. 49/2002 & Misc. Civil Application No. 254/2003).

Maombi hayo yalitokana na makubaliano ya mauzo ya hisa za VIP katika IPTL kwenda kwa kampuni ya Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP).

Uchunguzi unabainisha kuwa katika uamuzi huo, Mahakama pamoja na mambo mengine iliridhia kufutwa kwa mashauri hayo na kuelekeza kwamba mali zote za IPTL, kikiwamo kiwanda cha kufua umeme zikabidhiwe kwa mmiliki mpya wa IPTL ambaye ni PAP.

Baada ya uamuzi huo, BoT ilipokea mawasiliano mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Madini (MEM) na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao walikuwa na maoni kwamba fedha zilizopo kwenye Akaunti ya Escrow zitolewe baada ya masharti kadhaa kutekelezwa.

MASHARTI YALIYOTOLEWA KABLA KUTOLEWA FEDHA BOT
Taarifa zinaonyesha kwamba kabla ya kutolewa fedha hizo, kulitolewa masharti kadhaa kwamba utolewe ushahidi kama PAP ndiyo wamiliki wa hisa za Mechmar katika IPTL, kufikiwa kwa muafaka wa mgogoro wa ukokotoaji wa kiwango cha Malipo ya Uwekezaji kati ya IPTL na Tanesco.

Sharti jingine lililowekwa ni kwamba kuwapo na hakikisho baada ya kulipwa kwa fedha hizo, IPTL hawatadai chochote kuhusiana na tozo zinazobishaniwa.

WIZARA YA NISHATI NA MADINI ILIVYOSHIRIKI
Uchunguzi unaonyesha kuwa baada ya kuwekwa masharti hayo, Septemba 24, 2013, Wizara ya Nishati na Madini iliitisha mkutano kwa ajili ya kujadili maombi ya Serikali ya kuruhusu kutolewa kwa fedha za Escrow. Katika mkutano huo uliomshirikisha Gavana wa BoT, Katibu Mkuu Hazina, Mwakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) na wawakilishi wa Tanesco, BoT ilitoa hoja tano ambazo ilitaka zizingatiwe kabla ya kutolewa ridhaa ya kutoa fedha hizo.

Hoja hizo zilikuwa ni kupata ushahidi kama hisa za Mechmar zinamilikiwa na PAP na ushahidi kwamba umiliki huo umesajiliwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na ushahidi wa suluhu ya mgogoro kuhusu tozo kati ya IPTL na Tanesco.

Hoja nyingine zilizotolewa na BoT ni kujua iwapo IPTL na serikali wako tayari kusamehe riba inayotolewa kwa dhamana za Serikali ambako fedha za "Escrow" zimewekezwa; kauli ya Wizara ya Fedha na Uchumi kuhusiana na uamuzi wa kutolewa kwa fedha hizo na iwapo viongozi wa kitafa wana taarifa juu ya suala hilo.

Nyingine ni iwapo serikali imejihami dhidi ya uwezekano wa madai yanayoweza kufunguliwa na wadai mbalimbali, wakiwamo Standard Chartered Bank (Hong Kong) ambao wanadaiwa kuidai IPTL.

Uchunguzi zaidi unaonyesha kuwa kufuatia hoja hizo za BoT, iliundwa timu ya wataalam ili kuzifanyia kazi hoja hizo zilizoibuliwa na kujadiliwa, na kuwasilisha ripoti kwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishatri na Madini kwa hatua zaidi.

Taarifa zinaeleza kuwa ripoti hiyo ilikamilika na kuwasilishwa Septemba 30, 2013, ikiwa na mapendekezo yaliyohitaji kufanyiwa kazi kabla ya kutekelezwa kwa uamuzi wa mahakama kuhusu kutolewa kwa fedha. Mapendekezo hayo yalishabihiana na hoja zilizokuwa zimetolewa na BoT.

USHIRIKI WA AG NA KATIBU MKUU NISHATI
Taarifa zinaonyesha kuwa baada ya kuwasilishwa kwa ripoti hiyo, BoT ilipokea nakala ya barua ya Oktoba 7, 2013, iliyotoka kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali akielezea msimamo wake kuhusiana na yale yaliyoelezwa na timu ya wataalamu.

Katika ushauri wake, AG alishauri kwamba, baada ya kufikia muafaka kuhusu mgogoro wa tozo kati ya IPTL na Tanesco, fedha zilizomo katika Escrow Account zilipwe kwa IPTL kama uamuzi wa Mahakama ulivyoelekeza.

Aidha, Oktoba 15, 2013, BoT ilipokea nakala ya barua iliyoelekezwa kwa Katibu Mkuu Hazina, ikinukuu ushauri uliotolewa na AG na kushauri kwamba uamuzi wa Mahakama utekeleze ili kuiondolea Serikali madhila ya mashauri yanayoweza kuepukika. Barua iliandikwa na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini.

JINSI FEDHA ZILIVYOTOLEWA BoT
Taarifa zaidi zinaonyesha kuwa ilipofika Oktoba 21 mwaka 2013, Serikali ya Tanzania na IPTL walisaini makubaliano ya kutoa fedha zilizomo katika Escrow Account ili zilipwe kwa IPTL makubaliano yaliyojulikana kama "Agreement for Delivery of Funds to Independent Power Tanzania Limited".

Makubaliano hayo yaliambatana na muhtasari wa kikao cha pamoja cha uhakiki wa malipo ya tozo kati ya IPTL na Tanesco, pamoja na barua ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini ikiwasilisha makubaliano hayo na kuiomba BoT iliruhusu malipo hayo kwenda IPTL kama uhakiki ulivyobainisha.

Hata hivyo, habari zinasema kabla ya kufanyika kwa malipo hayo, BoT ilimuandikia barua Katibu Mkuu Hazina ikimuomba kuchukua hatua kadhaa kuhusiana na malipo ya IPTL. Miongoni mwa mambo yaliyoshauriwa na BoT ni ufungaji wa Escrow Account uzingatie kwamba mamlaka ya kufanya hivyo yako kwa Mlipaji Mkuu wa Serikali (Paymaster General) na kutokana na unyeti wa suala hilo na ukubwa wa malipo husika, Waziri wa Fedha apate fursa ya kuwajulisha viongozi wakuu wa kitaifa.

Pia BoT ilitoa ushauri kuwa serikali iombe kutolewa kwa kinga itakayoikinga dhidi ya madai yanayoweza kujitokeza baada ya malipo hayo kufanyika.

Kutokana na ushauri huo, vyanzo mbalimbali vinaonyesha kwamba Oktoba 27, 2013, IPTL ilitoa hati ya Kinga (Indemnity) ambayo iliikinga BoT pamoja na serikali dhidi ya madai yote, ya sasa na ya baadaye, mashauri ya kisheria, pamoja na kuahidi kuzifidia BoT na serikali gharama na tozo zozote ambazo zitawagharimu au zitakazotokana na uamuzi wao wa kuruhusu kuchukuliwa kwa fedha za Escrow au sehemu ya fedha hizo, kwa mujibu wa Makubaliano ya Kutoa Fedha.

USHAURI WA AG ULIVYOSABABISHA SERIKALI KUKOSA KODI
Taarifa zinaonyesha kuwa Mamlaka ya Mapato (TRA) iliomba msaada wa Katibu Mkuu Hazina katika kukata kiasi cha Sh. bilioni 26.9 kama VAT kwa malipo ambayo yaliwekwa kwenye akaunti ya Escrow ambazo zilikokotolewa kutoka katika kiasi cha Sh. 176,649,195,314.00 ambazo zilikadiriwa kuwapo katika akaunti hiyo. Hata hivyo, katika ushauri ambao ulitolewa na AG Novemba 18, 2013, ilielezwa kwamba malipo ya Capacity Charge hayakuhusisha VAT na kwamba kiasi chote kilichokuwamo katika Escrow Account kilikuwa ni malipo ya IPTL pasipo na VAT.

Vyanzo vinaeleza kwamba ushauri huo wa AG ulitokana na barua ya BoT na ya Katibu Mkuu Hazina ambazo ziliomba ufafanuzi kuhusu suala hilo kabla ya uhamishaji wa fedha kwenda IPTL.

UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA KUHAMISHA FEDHA
Taarifa zinazidi kueleza kuwa utekelezaji wa maagizo ya kuhamisha fedha za capacity charge zilikuwa katika makundi mawili, ambayo ni katika fedha za Kitanzania, wakati kiasi kingine kilikuwa katika dola za Marekani.

Makundi hayo mawili ya fedha yalikuwa yamewekezwa katika uwekezaji wa ndani na wa nje, kwa kuzingatia kifungu 3.4 cha Escrow Agreement na kiasi kilichokuwa kimewekezwa nje ya nchi kilikuwa ni Dola za Marekani 22 milioni, wakati fedha za Kitanzania ziliwekezwa katika hati fungani za siku 182.

Uchunguzi huo umebaini kuwa malipo ya fedha taslimu, yaani dola za Marekani 22,198,544.60 na Sh. 8,020,522,330.37 yalilipwa Novemba 28, 2013, uhamisho wa hati fungani ulifanywa Desemba 5, 2013, hatua ambazo zilihitimisha jukumu la BoT kama wakala wa akaunti ya Escrow.

Baada ya kuhitimishwa kwa malipo hayo Desemba 19, 2013, BoT ilimuandikia Katibu Mkuu Hazina kuomba kufungwa rasmi kwa akaunti hiyo, kwa vile madhumuni ya kufunguliwa kwake yalikuwa yamefikia tamati.

Chanzo: Nipashe
 
jamaa wanajua kuchukua hela huko BOT. jasho la watanzania hilo jamaa wanatafuna. baada ya hili kutakuja a/c nyingine tena. haziishi hizi a/c za kuchota hela hapo BOT. sasa hv na mm natafuta chanel tu niwe kwenye mrija.:A S-rap:
 
Mbona LUKUVI simsikii akitajwa wakati ndio ambae yupo kimbelembele kutetea na pia yumo katika ile orodha ya waliokwapua fedha hizo? yaani kamegewa 2.6 Billion.
 
Tulishalalamika ubadilishaji wa umiliki wa mahoteli kama iliyokuwa Royal Palm kuwa Serena, iliyokuwa Kilimanjaro Hotel kuwa Kempinski kisha kuwa Hyatt Regency ni mbinu za wawekezaji kuiibia serikali, yaani Tanzania imekuwa kama Chifu Mangungo.

Nimesoma report hii ya escrow japo haijatoka yote nimegundua kuwa viongozi wetu ni mbumbumbu sana kwani huu mtindo wa kubadili jina la kampuni wakati mmiliki wake ni yule yule ni UFISADI huu wa escrow unaanzia pale IPTL ilipojibatiza jina jipya na kuwa PAP yaani Pan African Power na wakati huo suala la IPTL na Tanesco likiwa bado mahakamani.

Nyie viongozi wetu mbona hata m.j.i.n.g.a anaelewa kuwa mlifanya ufisadi kwa kuhamisha umiliki toka IPTL kwenda Pan-Africa Power wakati kesi ya msingi kati ya Tanesco na IPTL haijaisha.
 
Back
Top Bottom