CCM yabariki waondoke kunusuru chama Wamo Werema, Tibaijuka, Maswi

Na UBUNGE pia.Hatutaki kuwaona wabunge mafisadi.Vinginevyo bunge litaendelea kukosa credibility ya kuwepo.Ama livunjwe kabisa.Pumbavu zao
 
Uongo wa mchana uliotungwa na akili ndogo. CCM haina Kamati ya uongozi bali ina Kamati Kuu tu. Wadanganyeni wajinga wenzenu.

Usibishe ndugu. CCM wana kamati ya uongozi bungeni ambayo ina wajumbe. Mwenyekiti wa wabunge wa ccm na katibu wake wengne ni viongozi wakuu wa chama ambao ni wabunge.
 
Uteuzi wa Profesa muongo na katibu wake, Nishati, utakuwa wa kwanza kutangazwa kusitishwa kwa manufaa ya umma muda wowote kuanzia sasa. Wengine watafuata kutegemeana na muitikio wa hali ya hewa ya Dodoma.

Chanzo: kwa mujibu wa watu ambao wamedokezwa na mamlaka ya uteuzi kabla ya maamuzi.

Kama ni kweli na akwende zake tu,ana dharau wazawa na mitaji ya juice wakati yeye na u Professor wake hata mtaji wa kuuza kashata na visheti hana.
 
Sasa moto unawaka na pa kujificha hakuna. Mkuu wa nchi yuko wapi? Kwanini yeye apone? Angekuwa mzalendo angesharudi immediately. Waungwana watasema ni mgonjwa good. Angeongea chochote basi
 
Tatizo la humu JF ni kuhusu members sijui huwa hawasomi thread zingne maana kila anaye post sasahiv anarudia mambo yaleyale anachokifanya ni kubadilisha heading tu. suala la hawa jamaa kujiudhuru limerudiwa cn. na hivyo ndivyo ilivyo hawatapona wote waliotajwa kwenye sakata hilo sual hapa ni kusubiria hiyo ripot isomwe halafu tujue kitakachoendelea na nimesharudia mara nyingi kwamba hata wakikingiwa kifua na uwingi wa CCM bungeni haitasaidia maana huku raia tutajua tunawahukumu vip.
 
MASIKINI AKICHOKA. Ni kheri tajiri achoke kuliko maskini akicho. Tajiri akichoka, ano uwezo wa kuchagua kuondoka katika mazingiri yaloyo mchosha kwasababu ya uwezo wake kiuchume (Kifedha). Lakini, Masikini akichoka, na kwakuwa hana uwezo wa kuondoka kwenye mazingira yaliyo mchosha (kutokana na hali yake kiuchumi yaani kifedha), basi masikini huyo huamua kusema "Na lolote liwalo, na liwe COME WHAT MAY". Masikini atakapofikia uamuzi wa kutoa kauli kama hiyo, ndipo yanapotokea machafuko katika jamii. 80% ya Watanzania waangukia katika kifungu cha Umasikini, wakati wakitambua bayana kuwa, Inchi yao ya Tanzania, ambayo wamepewa zawadi na Mwenyezi Mungu, imejaa Utajiri ambao hata mataifa yaliyo endele hayana; na kushuhudia jinsi viongozi wao ambao wamewapa dhamana ya kuwaongoza kuidhihirisha Inchi yao iliyojaa Maziwa na Asali hawawajali, bali wanakula na kufuja mali pamoja na pesa ambazo zingeweza kuwaletea mabadiliko ya kuwatoa katika umasikini wao; basi Watanzania hao wanaweza kufikia kikomo cha uvumilivu na kuamua kusema " Na lolote liwalo liwe COME WHAT MAY". NATOA ANGALIZO KWA BUNGE LETU PAMOJA NA WABUNGE WOTE WA VYAMA VYOTE KUWA, ZINGATIENI HAYO NILIYOYASEMA, MFANYE MAAMUZI MAGUMU KWA MANUFAA YA WANANCHI WALIOWACHAGUA ILI KUINISURU INCHI YETU TUSIJE TUKAFIKA MAHALI AMAPO HAWA 80% WAKAFANYA MAAMUZI NILIYOYASEMA. (Discuss).
 
Mawaziri watoswa


  • CCM yabariki waondoke kunusuru chama
  • Wamo Werema, Tibaijuka, Maswi, Muhongo
  • IPTL yaathiri harakati za Mizengo Pinda 2015
23/11/2014 | Na Martin Malera |


KAMATI ya uongozi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imependekeza viongozi waliotajwa kuhusika katika kashfa ya kuchota fedha zaidi ya sh bilioni 321 kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, wajiuzulu.

Tanzania Daima Jumapili, limedokezwa kamati hiyo iliyokutana juzi usiku, ilipendekeza watuhumiwa hao wajiuzulu ili kukinusuru chama pamoja na serikali inayopakwa matope kwa makosa ya watu wachache.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho zilitaja wanaotakiwa kujiuzulu ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Frederick Werema, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Eliachim Maswi na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka aliyepewa sh bilioni 1.6 kutoka kwa mmoja wa wamiliki wa IPTL, James Rugemalila.

Mapendekezo hayo yalitolewa baada ya Kamati hiyo kupewa taarifa fupi kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Deo Filikunjombe.

PAC inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), ndiyo iliyopewa kazi ya kupitia ripoti ya uchunguzi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serrikali (CAG) ambayo sasa iko tayari kuwasilishwa bungeni kujadiliwa.

Watuhimiwa wengine katika kashfa hiyo iliyosababisha wahisani kusitisha misaada yake nchini ya zaidi ya sh trilioni moja ni Gavana wa Benki Kuu (BoT), Benno Ndullu, Waziri wa Fedha na Uchumi, Saada Mkuya na Mkurugenzi wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), Felchesmi Mramba, huku Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitajwa kuhusika kutokana na uzembe wa watendaji wake.

Mapendekezo hayo yatawasilishwa kwenye kikao cha wabunge wa CCM, kinachotarajia kufanyika leo mjini hapa
Habari kutoka ndani ya wabunge wa CCM, zilisema kuwa mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe, atawasilisha taarifa fupi ya kamati yake kuhusu kashfa hiyo ili kutoa mwelekeo kwa wabunge hao kuchangia mjadala wa ripoti ya uchunguzi ya CAG, itakapowasilishwa Bungeni wiki ijao.

Ndugai alaumiwa
Baadhi ya mawaziri na makada wa CCM, wamemlaumu Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai, kwa kuruhusu mjadala wa wiki iliyopita ambapo baadhi ya wabunge kuishambulia mahakama na serikali.

Hata hivyo jana Ndugai alisema haoni kama alifanya kosa bali alikuwa akitaka ushauri wa kuliendesha jambo hilo baada ya kuombwa muongozo wa kuwapo kwa barua ya mahakama inayozuia Bunge lisijadili suala la Escrow
"Ni kweli nimepata lawama kutoka kwa baadhi ya watu lakini mimi nilifanya vile kwa nia njema kwakuwa jambo lenyewe lilikuwa zito sana" alisema.

IPTL yatia doa mbio za Pinda
Katika hatua nyingine, imeelezwa kuwa kashfa ya IPTL, imetoa doa harakati za Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kuwania urais mwakani.
Pinda ambaye hatajwi kuhusika moja kwa moja na kashfa hiyo, lakini anaguswa na uzembe wa watendaji wake, wiki hii alikuwa na wakati mgumu kiasi cha kuzomewa na wabunge.

Pinda alizomewa bungeni pale alipojaribu kuitetea ripoti ya uchunguzi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu Akaunti Escrow isijadiliwe bungeni kwa madai kuwa kuna kesi zaidi ya 10 zinazohusu IPTL na wadau wake hivyo kujadili ni kuingilia uhuru wa mahakama.

Duru za siasa ndani na nje ya Bunge, zinaeleza kuwa kwa jinsi hali ilivyo kashfa hiyo haiwezi kumuacha Pinda salama na hali ikiwa hivyo harakati zake za kutaka kuwania urais kimyakimya, zitakuwa zimekwisha au kupata dosari kubwa.

Wadadavuzi wa mambo ya siasa, wameliambia Tanzania Daima Jumapili, nguzo kubwa ya Pinda katika kuwania urais ni usafi wake kwani hana kashfa wala makando kando ya ufisadi ukilinganisha na baadhi ya makada wanaotajwa ndani ya CCM.

"Ukimsimamisha Pinda na Lowassa na Membe, Lowassa alichafukachafuka kwa kashfa za ufisadi ambazo baadaye zimeonekana sio za kweli. Membe naye alishachafuka. Pinda hana makandokando, na hiyo ndiyo nguzo yake kuu ya kuwania urais. Sasa hii ndio kashfa yake ya kwanza na kibaya zaidi imekuja wakati wa joto la urais na yeye anautaka," alisema waziri mmoja jina limehifadhiwa.

Kutokana na hali hiyo, Pinda ni miongoni mwa viongozi wa juu wa serikali wasiotaka ripoti ya uchunguzi wa kashfa hiyo, iende bungeni kwani madhara yake ni makubwa kwa serikali na kwake
Wakati akichangia kwenye mjadala wa Escrow Akaunti uliotikisa Bunge wiki, bila hata kusoma alama za nyakati kwa wabunge, Pinda alisema kwa hatua iliyofikia, Bunge linahitaji utulivu na busara zaidi katika kufanya maamuzi.

Alisema mihimili mitatu, iliyopo yaani Bunge, Mahakama na Serikali kwa mujibu wa katiba na kila chombo kimepewa eneo lake la kusimamia na namna ya kuendesha shughuli zake,
"Mheshimiwa Spika, Naibu Spika nimeona nisimame niseme jambo kwa ufupi sana, rai yangu kwako na kwa wabunge mnapofika katika hatua ambazo mnataka kidogo utulivu mnataka hekima kubwa ni pale mnapofika hatua kama hii niliyoiona leo.

"Nimeogopa sana kwa baadhi ya kauli zilizotoka kujaribu kuona mahakama kama ni chombo kilichotumika kujaribu kuficha uozo, nadhani si kauli nzuri sana hasa sinapotoka kwenye muhimili kama huu, umepata michango kutoka kwa wabunge na mimi ni mmoja wapo ambaye ningependa haya mambo yaishe lakini lazima tukubali kwamba katika kufanya jambo hili ni lazima tutumie busara kubwa kuhakikisha kwamba maamuzi mtakayoyafanya yawe ni maamuzi ambayo hayataleta ghasia za muingiliano wa majukumu ya chombo kingine chochote," alisema na kusababisha kuzomewa.

Mbali ya Pinda kujitahidi kuepusha mjadala wa ripoti ya CAG isiingie bungeni, baadhi ya wabunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wamepanga kumtetea Pinda asiwajibike kwa makosa ya watendaji wake.

Wakati kundi hilo likiendesha kampeni hizo, kundi linguine ambalo ni kubwa limejipanga kumshughulikia Pinda kwa hoja kwamba kama Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa aliwajibika kwa makosa ya watendaji wake, kwanini Pinda naye akafuata mkondo huo.

Harakati za kuzima kashfa hiyo isifike Bungeni, imepata kufanywa pia na Ikulu kupitia Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue kwamba ripoti hiyo haijakamilika na kuwataka wabunge waache kushinikiza iende Bungeni.
Mgogoro uliosababisha fedha kuwekwa katika akaunti hiyo ya Tegeta ya BoT ulitokana na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kugoma kulipa gharama za uwekaji mitambo (Capacity Charge) kwa IPTL mwaka 2006 kwa vile ilibainika IPTL ilikuwa ikitoza gharama kubwa kuliko iliyopaswa.

Akaunti hiyo ya Tegeta ilianzishwa kwa sababu ya kuhifadhi fedha zote zilizopaswa kulipwa na Tanesco hadi hapo mgogoro baina ya pande hizo mbili umalizike.
Hata hivyo, Septemba mwaka jana, serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, iliagiza BoT kulipa fedha hizo kwa kampuni ya PAP mara baada ya kuridhishwa na uamuzi wa Mahakama Kuu uliosema kwamba mgogoro baina ya wamiliki wa IPTL na Tanesco umemalizika na hivyo Benki Kuu haina sababu ya kuhifadhi fedha hizo.

CC: Tized, Mr Rocky, Fixed Point, lyinga, NATA, Chakaza, Elly B, MziziMkavu, Power to the People, Jasusi, Eiyer, idawa, nguruvi, Mentor, Sikonge, Dingswayo, MANI, tpaul, Bramo, Bulesi Bulldog, Sangarara, MTAZAMO, Erythrocyte, Mag3, Mimibaba, zumbemkuu, Crashwise, amkawewe, Idimi, Ogah, Chakaza, mshana jr, JokaKuu, MWALLA, genekai, PRINCE CROWN, Tuko, Shark, lynxeffect22, samaki2011, MoudyBoka, adolay, Elli, nyabhingi, Janjaweed, S.N.Jilala, MEANDU, Tabby, Candid Scope, Honolulu, August, dyuteromaikota, BONGOLALA, Gefu, Bigirita, Kozo Okamoto, Daudi Mchambuzi, lusungo, Matola



 
Pamoja na kulazimishwa kujiuzuru kwa baadhi ya viongozi hii naona haitoshi.

Wajiuzuru,warudishe fedha za uma mwisho wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.
Japo kwa mahakama zetu wahusika watashinda tu maana waandaa mashitaka na Watoa hukumu wote baba Yao mmoja.

Hayo yote kwa sababu watu wanaokimbilia Uraisi wakati hawauwezi,
 
Na yule jamaa yetu DHAIFU Janga Kubwa hata haijulikani kama matibabu yake yameisha, yanaendelea na atarudi lini nchini. Sakata lote hili yeye yuko kimyaaaa! Sijui alimuachia nchi nani alipopeleka tezi dume lake likatibiwe majuu maana makamu wa Rais naye kimyaaa, Waziri Mkuu ndiye huyo kishadharauliwa kwa kiwango cha juu kabisa mpaka kuzomewa Bungeni, hii inaonyesha haaminiki tena katika nafasi yoyote ya uongozi ndani ya Serikali.

Alieilaani hii nchi inaonekana alishakufa ......

Watu wanachukua fedha bila hata ya aibu .....

Hata Mungu hawezi kutusaidia kwenye hili na mengine!
 
Na yule jamaa yetu DHAIFU Janga Kubwa hata haijulikani kama matibabu yake yameisha, yanaendelea na atarudi lini nchini. Sakata lote hili yeye yuko kimyaaaa! Sijui alimuachia nchi nani alipopeleka tezi dume lake likatibiwe majuu maana makamu wa Rais naye kimyaaa, Waziri Mkuu ndiye huyo kishadharauliwa kwa kiwango cha juu kabisa mpaka kuzomewa Bungeni, hii inaonyesha haaminiki tena katika nafasi yoyote ya uongozi ndani ya Serikali.
Nchi yetu haina serikali ....

Sijui tutaishia wapi!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Umefika muda wa kuhifadh chakula,pesa, Panadol na hata mafuta ya kutosha ya ka usafiri pia kuhakikisha kausafiri kapo sawa 2015 inakuja siielewi elewi
 
Back
Top Bottom