Kuna conflict of interest ya wazi kabisa Chama tawala kinapokuwa na biashara na serikali. Si halali serikali kutoa tenda au kutoa contract kwa chama chake. Serikali yetu ni Serikali ya CCM. Ni kosa serikali ya CCM iingie mikataba ya kiuchumi na CCM.
Siku za nyuma kulikuwa na SUKITA. Tunajua mapesa ya uma yalimalizikia pale. Inafilisiwa kwa sasa, na nadhani bado inameza, kwa siri kubwa, fedha za serikali
.
Huko nyuma, wakati wa chama kimoja, kuna wakati watu waliuliza iweje CCM itengewe fedha nyingi hivyo za uma. Mzee Kawawa alijibu zilikuwa ni fedha za consultancy. Yaani serikali ilibidika kulipa consultancy fees kwa chama chake.
Fedha zilizochukuliwa na CCM kupitia BoT ni kama shilingi moja kati ya kila shilingi 10 za bajeti. Zilikuwa fedha nyingi kiasi cha kutisha. Kwa hivyo, hizo hongo nyingi walizopewa wananchi kama alivyosema Mwafrika wa Kike, zilitokana na fedha za wananchi. Yaani CCM inachukua kwa nguvu (au kwa njia za wizi) fedha za wananchi kisha inazitumia kununua kura za wananchi.
Kumbukeni kwamba kuna wakati hata viwanja vikuu vya michezo vilidaiwa na CCM kwamba ni mali yake. CCM ina historia ya kupora mali ya wananchi. Haiwezekani kabisa CCM ikubali kuwatangazia wananchi, kwa ukweli, mapato na matumizi yake. Mapato ya kuchota kiasi cho chote upendacho Hazina utayatangazaje?
Hatuwezi kutegemea msaada toka kwa Msajili wa Vyama kwenye jambo hili. Kwani anachaguliwa kwa ushirikiano na vyama vyote? Kwa mpango uliopo, Msajili wa Vyama lazima awe mwana CCM (overtly or covertly).
Mwafrika wa Kike: well done. Lakini jua kabisa hali ya Tanzania itabaki kuwa ya mipango mibaya hadi CCM watakapowekwa upinzani kwa angalau kipindi kimoja au viwili. Mawazo yako mazuri lakini umegonga mwamba.