Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 61
Kuna Mwanaccm hapa anapenda sana kusifia ushindi wa ccm katika chaguzi zote kuanzia mwaka 1995 hadi leo kama dalili ya kuwa chama hicho kinapendwa na watanzania.
Nilikuwa Tanzania uchaguzi wa mwaka 95 na 2000 ambako nilishuhudia mamilioni ya pesa yakitolewa na wagombea uchaguzi wa ccm. Nilishuhudia kanga na vitenge vyenye picha za Mkapa vikitolewa kama Njugu kwa wananchi wa Mwanza na Bukoba bure.
Mwanachama wa CCM mzee Butiku alilalamika kwa Mkapa mwaka 2005 jinsi ambavyo baadhi ya wana ccm (Kikwete akiwemo) walivyokuwa wanatumia mamilioni (ya Rostam Azizi) kufanya kampeni za kumpata mgombea wa ccm
Report iliyovuja toka BOT inaonyesha jinsi ambavyo mabilioni ya pesa yalichotwa benki kuu ili kugharimia uchaguzi wa mwaka 2005.
Nadhani imefika wakati CCM ikaweka wazi vyanzo vya mapato ya pesa ambazo zimetumia na wagombea wake kwa chaguzi zote tatu.
Inabidi pia taarifa ya pesa na matumizi hayo iwekwe wazi kila mwezi au kila miezi mitatu ili wananchi wote waisome.
Hapa Marekani, kuna udhibiti mkubwa sana kwa wanasiasa kuhusu mapato na matumizi ya pesa kwenye chaguzi. Haijalishi chama gani kiko madarakani lakini vyama vyote vinatakiwa kutoa report kila miezi mitatu ya matumizi na mapato yanayotumika kwenye uchaguzi.
Nina hakika kuwa hili likifanyika, huyo anayesifia ushindi wa ccm hapa atakosa cha kusifia muda si mrefu.
Asante.