CCM wamemtelekeza Wastara, ameoza miguu

CCM wamemtelekeza Wastara, ameoza miguu

Sio kila sehemu ni za kupigia siasa kama una chuki sana na chama fulani tafuta sehemu inayo faa kutoa tuhuma zako na sio kuhusisha watu wanohitaji msaada kutoka kwa kila mtanzania wa kila kada bila kuzngatia chama
 
d60e04959a58504a8cd34b7818e65bfd.jpg
497dd7dd70a59eac103cd37292bb6f45.jpg
244de6f98d88953a3f68cda7ef2b7c32.jpg
bb9bfe21a5ac3166ea95fc67981ad7a9.jpg


Chama cha mapinduzi ccm kimemtelekeza mwanachama wake na Msanii wao Wastara Sajuki ambae aliokuwa kwenye kikundi cha Mama Ongea na Mwanao.

Msanii huyo Licha ya kuwa Mlemavu aliamua kupambana ili ccm ishinde mpaka kupelekea kudondoka jukwaani ambapo ilipekea pingiri za mgongo kuhama na mguu kuanza kuoza.

Tokea aumie mpaka sasa yuko ndani hana msaada wowote mguu wake unaoza anahitaji milioni 30 ya matibabu viongozi wa ccm hawapokei namba yake.

Anahitaji msaada wa kila Mali ili asije kufa kwa sababu ya kuoza maana itapelekea kupata kansa ccm hawana kazi nae tena amekuwa karai hana kazi tena asubiri 2020 sasa kazi yao ni kununua wapinzani tu.

Yaani nimejaribu kumfatilia unaweza kulia hakuna hata kiongozi wa ccm ambae anataka kumuona yaani wanasubiri msiba wake wakapige picha hawa watu hawana utu.

Tumsaidieni wastara Namba zake ni 0713666113
0768666113
Kwakwambia nani ccm ina fungu la kutibia wanachama wake?
 
sisiemu waliwatelekeza wahanga wa tetemeko kagera pamoja na kula rambirambi zao sasa mnashangaa nini kumtelekeza WASTARA??
 
Daah huyu binti anatia huruma anapitia mambo magumu sana,si alikuwa mke wa msanii marehemu aitwa Sajuki
 
Mboba naskia kwenye kampeni za 2015 walilipwa mamilioni wengine wakajenga nyumba hadi wakamiliza maana kuna waliokuwa wanalipwa milioni 90 atii
 
CCM ni nani huyo, taja mtu specifically..; either way, tatizo lake linaweza kutibiwa Muhimbili kwa teknolojia ya telemedicine bila kulazimika kwenda nje. Ila Ahsante kwa kuweka namba zake, binafsi nitashiriki kwenye hii crowd funding kwa kutoa chochote.
 
Mnataja ccm....ccm...kwani wao ndio walio mvunja huo mguu...[emoji16] [emoji16] [emoji16]
 
" .. ameoza miguu ..."
Hiyo kauli sio nzuri. Huyo Wastara ni binadamu sio kuku au ng'ombe.
Ungeweza kufikisha ujumbe kwa lugha nzuri tu. Mfano: ".. anasumbuliwa sana ugonjwa lakini CCM wamemtelekeza .."
 
ccm kueni na utu basi embu mtibuni mtoto wa watu ,na yeye atulie sio apone tena aanze kurukaruka kwenye kampeni,
 
Jamani hakuna alie mkamilifu.Na ndio maana wengi wetu tunaamini Mwenyezi Mungu ni mwingi wa REHEMA na HURUMA.Hivyo basi hakuna aijuae kesho yake,au hata baadae yake.Na ndio maana wapo wanaoamka wakiwa bukheri wa afya,lakini matatizo huwakuta kabla hata siku kuisha.Si vyema kumdhihaki mwenzako,kwa sababu uzima ni wake Maulana.Tofauti zote zilizopo kati yetu ni vyema tusiwe tunazihusisha katika mambo ya msingi hasa yanapohusisha utu wa mtu.Mimi katika maisha yangu kama binadamu huwa ninapitia changamoto nyingi pia.Lakini mara zote,huwa kila nikimtafakari Mungu huwa ninamwambia ASANTE.LEO NI WASTARA,WEWE JE NI LINI?ULISHAJIULIZA KUHUSU HATIMA YAKO?NI VYEMA KWA ATAKAEWEZA KUMSAIDIA AMSAIDIE.MWENYEZI MUNGU ATUPE WEPESI SOTE,MIMI,WEWE NA WENGINE WOTE WANAOHITAJI WEPESI KATIKA YANAYOWASIBU AMINA.HERI YA MWAKA MPYA 2018,YALIYOPITA SINDWELE,TUGANGE YAJAYO.ALUTA CONTINUA!
 
Kwanini tusiende kwenye page yake insta kwa uhakika ili apate kusaidika?

Naamini wanajf tukijiunga na kumchangia atafanikiwa matibabu!....ngoja nione kama kuna uwezekano
 
Kwa nchi nyingi (almost zote), ukiamua kujipambanua na chama tawala, lazima uwe Tayari kwa lolote mbele ya safari. It is so unfortunate but that is the truth. Unaonekana msaliti. Ndo maana nawaasa vijana wengi kabla hamjafanya maamuzi ya kisiasa! (Siwaambii kwamba muingie upinzani-Far from that). Lakini kuweni makini sana. Siasa zetu za kibongo ni za kinafiki sana. Unaweza kuharibu future yako kwa mambo ya kipumbavu.

Lazima tukubali hata CCM ingefanya mangapi mazuri, kuna ambao wanaichukia kwenye damu zao (and in some cases rightly so)! na wanawachukia wale wote wenye any kind of association na hicho chama. Kwa hiyo sishangai, Ingawa inawezekana hata huyu dada alikuwa anashabikia CCM kwa ajili ya kupata mkate wake wa kila siku...But there are those who will hate her no matter what! na sana sana watamkejeli tuu kama kwenye hii thread... just because alikuwa karibu na CCM.

Kama ambavyo siasa zimesaidia wengi 'kutoka', zimeua ndoto za wengi pia. Kijana huna haja ya kuvaa mashati ya kijani kusudi uonekane mwaminifu kwa chama. Wapo ambao hata kadi hawana Lakini hicho hicho chama kinawategemea! It all depends what you bring on the table!
 
Kwani huku ndo makao ya chama jaman? Mwenye dukuduku lake moyoni apeleke kwenye ofisi au makao ga chama
 
Tokea aumie mpaka sasa yuko ndani hana msaada wowote mguu wake unaoza anahitaji milioni 30 ya matibabu viongozi wa ccm hawapokei namba yake.


Mwenyekiti wetu ana taarifa hizi!!!? Hawa ndiyo wanyonge anaowatafuta naamini soon atafika huko amini usiamini
 
Na ateseke sana mpka akome. Hawa ndio waliiweka CCM madarakani wakijali maslahi yao binafsi kuliko watanzania wasio na maji na elimu vijijini. Na afe kabisa huyu


Hapana naomba tumuuombee, kila binadamu ana haki ya kupenda akionacho, maradhi ni mpango wa Mungu, hakuna ajuaye siri iliyomo ndani yake, tumuombee tumchangie aweze kufurahia maisha kama wewe na wengine wote
 
Muda mwingi uliotumia kupiga siasa za kishamba ungeutumia kueleza matatizo yake na watu wakajitoa kumsaidia, vijana wa ufipa sijui akili zenu zikoje, sijui ni kwa sababu makao makuu ya chama chenu yapo karibu na mtaro wa kinyesiiii. Kila kitu mnapiga siasa hata ktk uhai wa mtu siasa, ukiondoa u ccm ya huyo dada anabakia kuwa Mtanzania ambaye ni ndugu wa Mtanzania yeyote hata asiye na chama....acha kuonyesha wehu wako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom