CCM wakata rufaa Igunga kupinga Kafumu kuvuliwa ubunge

CCM wakata rufaa Igunga kupinga Kafumu kuvuliwa ubunge

'Sikia Ndugu yangu,mimi kwasasa nimejielekeza kwenye 'profession' yangu.

Mwanzoni Profession alikuwa amemwachia nani? Mambo ya mfa maji hayo. Jamaa alikuwa na nafasi nzuri..Kamishina wa Madini, Mteule wa Rais. Sasa amekosa mwana na maji ya moto!

Pole lakini.
 
amesahau Rostam alifanya nini? Ni rahisi afuate njia ile ile ya Rostam
 
ukizungumza nae wewe nani, mwandishi? Habari kamba tupu hii...

ni kweli anachokisema mkuu kwani hii si mara ya kwanza kusema hivyo kwani alishasema mara tu baada ya hukumu kutoka aliwaeleza ccm hataki tena ubunge anataka kurudi kwy profesional yake lakini ndiyo hivyo tena CCM hawasikii wameweka siasa mbele kuliko maslahi ya wananchi. huyu jamaa labda nikuibie kafumu alikosa watu wazuri wakumshauri kuacha ukurugenzi wa madini kwa sababu ya utumishi wake mzuri wa kukataa ujinga kwahiyo ubunge ulipokuja waliutumia kama mtego kumtoa kwenye nafasi ile sasa ndiyo amestuka too late.
 
Lema alisema mkulu aliingilia kesi yake kule Arusha watu wakamwona Lema mwongo, si mmemsikia mwenyewe anasema amemshangaa hakimu aliyetoa hukumu wakati wanatekeleza ilani ya chama chao, hivi rais wetu ni mbumbumbu wa sheria kiasi cha kutoona kosa la Magufuli aliposema kuwa hawawezi kujengewa daraja la Mbutu kama watachagua mbunge wa upinzani, wakati akijua pesa za kujengea daraja hilo ni za walipa kodi wote bilatéraux kujali itikadi zao za siasa??!!
 
ccm hovyo sana. Wanaweza mpa mtu kiharusi hivihivi kwa mashinikizo ya kijinga kama haya. Si wamuache aendelee na maisha yake?
 
Jamani kafumu ameshafumuliwa tayari, sasa kwa nini magamba wameng'ang'ana na rufaa iliyoshindwa kabla ya kusikilizwa!!! Au ndiyo mbinu ya ku-buy muda ili filimbi ya uchaguzi mdogo isipulizwe!! Bila shaka magamba yakikumbuka mechi ya Arumeru yatakuwa hayalali hata usingizi.
 
Amepigwa jini kimnyung'unyu huyo!ukipigwa hilo hata ukipewa mamilioni hupokei
 
Asilete hadithi za sizitaki mbichi hizi kama alikuwa hautaki ubunge mbona aligombea?. Wanaomlazimisha wanajua kama kawaida yao watafanya hila arudishiwe ubunge wake.
 
Asilete hadithi za sizitaki
mbichi hizi kama alikuwa hautaki ubunge mbona aligombea?.
Wanaomlazimisha wanajua kama kawaida yao watafanya hila arudishiwe
ubunge wake.

alikuwa akiuota uwaziri!
 
Aliyekuwa Mbunge wa Igunga,Dr.Dalaly Peter Kafumu, amedai kuwa kwasasa yeye hataki Ubunge lakini CCM inamlazimisha kukata na kuishughulikia rufaa yake dhidi ya kuvuliwa Ubunge huo na Mahakama Kuu. Nikizungumza naye hivi punde, Dr.Kafumu ameilalamikia CCM kwa kuwakosesha Mbunge wana-Igunga kwa kung'ang'ania rufaa ya Ubunge isiyo na tija.

'Sikia Ndugu yangu,mimi kwasasa nimejielekeza kwenye 'profession' yangu.Sitaki hata kusikia Ubunge wala nini sijui. Washauri Viongozi wetu wakubali Jimbo litangazwe wazi na uchaguzi ufanyike upya ili wana-Igunga wawe na Mbunge. Nilishakubali matokeo ya Mahakama.' alisema Dr.Kafumu

'Niliandika kuwafahamisha viongozi wangu. Sasa kwanini hawataki kunielewa? Kwanini wananilazimisha? Kwanini wanang'ang'ania jambo hili? Hawa watu sijui wakoje?!' alisikika Dr.Kafumu kwa sauti ya kukwazika.

Jambo gani liko nyuma ya Jimbo hili la Igunga?

Kauli hiyo ni nzito, aliisema kwenye taarifa rasmi au kirafiki tu? Nisingependa kuiendekeza taarifa isiyo rasmi hala kesho tunaona kinafanyika kitu kingine kinyume cha mada ulivyoileta. Vinginevyo uthibitisho wa kauli hii unahitajika kutiliwa maanani.
 
Alitumia pesa nyingi sana kushinda ubunge, sasa mahakama kuu ilivyotengua ushindi wake amevurugikiwa sana kiasi kwamba hataki tena siasa.
Muacheni Kafumu ajipumzikie hali si shwari kwa upande wake lakini ccm hawataki kumuachia sijui hawana mwanachama mwingine huko Igunga?
 
CCM kweli imekufa!!
hila zote hozo kwa cdm, kutumia polisi, Uwt, Geshi, na matakataka mengine ya kuifitinisha CDM.....lkn bado wanaiogopa namna hiyo!!!!!

RIP CCM!
 
achana naye huyo anatapatapa tu. kama hataki ubunge mwanzoni nani alimwambia aende pale? anaona amekosa kote, alichokuwa anakifuata hakukipata, uwaziri wa nishati na madini au walau unaibu waziri, sasa kakosa cheo chake kikubwa cha ulaji kule madini, na ubunge hana....anatapatapa tu. aende igunga akalime mpunga, nafasi hiyo kachukua jembe prof na hatutaki mwingine. uyo jamaa hana maana.
 
Alipokufa Chacha Wangwe, Profesa Samwel Wangwe aliamua kuuweka U-profesa wake pembeni na kuzungumza habari za kijiweni ili aifurahishe Mi-CCM, leo hii yuko hoi kitandani kapigwa na Kiharusi, sintoshangaa akikurupuka na kudai kwamba ni "kazi" ya CDM! Hao ndio aina ya Wasomi tulionao.
 
Kauli hiyo ni nzito, aliisema kwenye taarifa rasmi au kirafiki tu? Nisingependa kuiendekeza taarifa isiyo rasmi hala kesho tunaona kinafanyika kitu kingine kinyume cha mada ulivyoileta. Vinginevyo uthibitisho wa kauli hii unahitajika kutiliwa maanani.

Mkuu Candid Scope

Unakumbuka kauli yake siku ile tu baada ya hukumu? Kumbuka alichosema na walichosema CCM kupitia kwa Nape. Zilikuwa kauli mbili tofauti kbs. Nilifika Igunga siku chache tu baada ya hukumu iliyotengua ubunge wa Kafumu, kwa kutumia mbinu za uandishi wa habari niliweza kujipenyeza kwenye mazungumzo ya usiku karibu na 'familia' ya Kafumu. Ziko kauli tata sana baada ya hukumu ile.

Lakini pia kauli hii, kama mwanzisha thread ana uhakika nayo, unaweza kuiunganisha na kilichotokea pale kwenye kesi ya Ubungo ambapo Hawa Ng'humbi hakukata rufaa dhidi ya John Mnyika baada ya ile kesi ya awali. Hawa hakukata rufaa. Waliokata rufaa ni CCM na the so called system. Jinanla Hawa lilitumika tu.

Mwenyewe alisema kuwa baada ya kesi ya msingi alikuwa ameridhika kuwa ameshindwa na hakuona sababu ya kukata rufaa, hivyo akakitaarifu chama chake, CCM hivyo. Lakini hawakukubali. Wakatumia jina lake kukata rufaa, wakisema imekatwa na Hawa Ng'humbi.
 
nani anatakiwa kukata rufaa?

Mungi

Sheria inazungumzia mgombea na mpiga kura (ambaye bila shaka anaweza kuwa mwanachama wa chama husika). Chama hakina nafasi. Ndiyo maana mwanzoni kbs walipoingia chaka kwa kusema CCM kitakata rufaa baada ya Kafumu kuwa ameridhika na hukumu pale mahakamani, Dkt. Slaa akawaambia wamepotea, hakuna kitu kama hicho (chama kukata rufaa) kwenye kesi ya uchaguzi.

Kwa sababu walikurupuka kuzungumza, no wonder sasa wanamlazimisha Kafumu...
 
Back
Top Bottom