CCM wakata rufaa Igunga kupinga Kafumu kuvuliwa ubunge

CCM wakata rufaa Igunga kupinga Kafumu kuvuliwa ubunge

Chama cha magamba kwa sasa kinaogopa sana kuingia katika uchaguzi mdogo baada ya kipigo cha Arumeru mashariki. Hivyo kinachofanyika ni kujifanya kukata rufaa ili kuchelewesha uchaguzi mdogo.
Ndio zao hata Sumbawanga wanazidi ku-manipulate sheria ili kumpa Aeshi nafasi ya kurudi japo wanasumbawanga na mahakama zilishamtema. Hawa maCCM kwa nini hawa-accept defeat!!
 
achana naye huyo anatapatapa tu. kama hataki ubunge mwanzoni nani alimwambia aende pale? anaona amekosa kote, alichokuwa anakifuata hakukipata, uwaziri wa nishati na madini au walau unaibu waziri, sasa kakosa cheo chake kikubwa cha ulaji kule madini, na ubunge hana....anatapatapa tu. aende igunga akalime mpunga, nafasi hiyo kachukua jembe prof na hatutaki mwingine. uyo jamaa hana maana.

Umegusa ukweli wa kinachomfanya mpaka sasa ajutie kuingia siasa. Kudanganywa. Na hii nilifanikiwa kuinasa baada ya kujipenyeza kiuandishi 'karibu' na familia yake nilipokwenda Igunga kwenye mkutano wa kuwashukuru wana Igunga. Kudanganywa.
 
CCM kweli imekufa!!
hila zote hozo kwa cdm, kutumia polisi, Uwt, Geshi, na matakataka mengine ya kuifitinisha CDM.....lkn bado wanaiogopa namna hiyo!!!!!

RIP CCM!

Hofu. Mkuu Mzizi wa Mbuyu, wanasumbuliwa na hofu. Ni matokeo au dalili za wazi kuwa wameshaanza kuoneshwa exit. Mlango wa kutokea.

Kwa mtazamo wangu, hakuna wakati CCM imekuwa na hofu ya kuondoka madarakani kama wakati, miaka 20 baada ya kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi. CCM wana hofu sana. Muda wote wanakimbia kivuli cha CHADEMA. Kila wanachofanya au wanafikiria CHADEMA wata react au watanufaika vipi. Hofu hii haiwezi kuwaacha salama, no wonder hawawezi tena kufikiria na kutenda sawasawa. Kila wanachofanya au kusema, wanajikuta wanakosea zaidi. HOFU.
 
Hii ishu ni serious iwapo source ni reliable tu.
Lkn inanishangaza kuona mtu msomi wa aina ya Kafumu kulalamika kwa kauli ya kusikitisha kiasi hicho, yani hadi bibi yangu wa kijijini atasikitika sn akisoma kauli ya Kafumu!

Je huu ndiyo mwisho wa Usomi na wasomi? Weledi wetu unatusaidia wapi? Endapo Kafumu hana option zaid ya kulazimshwa kukata rufaa, hali hii inatisha!
 
kama kweli dr kafumu kasema hivo basi hii kali ya mwaka. sababu ni nyingi. najiuliza alikuwa hatak tangia mwanzo kugombea ubunge au ni kwasasa baada ya kunyanganywa na mahakama? any way watu kama dr kafumu ni watu tunaowahitaj. fanya kaz uipendayo na unayojiamin zaid kuwa unaiweza. kama ni kweli safi kafumu
 
Wanachoogopa CCM kukubali uchaguzi mdogo ni kwamba Chadema itashinda kwa vyovyote vile! Na ikishinda maana yake itajiongezea umaarufu hivyo kuiweka CCM katika hali mbaya kwenye uchaguzi mkuu 2015,Sana sana wanaogopa kupoteza Urais kama walivyopoteza 2010 na kulazimika kuzuia matokeo vituoni!CCM bhana.
 
Rufaa si alikata yeye. Hizi ni akili ndogo sana maana kulazimishwa ukakubali hata hicho ulichosomea hakikufai. Ni sawa na kutenda kinyume cha maumbile, si unakubali
 
Kama ni kweli anaamini hivyo mbona ni kazi rahisi sana. Hawawezi kumlazimisha kama hataki. Na njia rahisi ya kukataa kulazimishwa na kuwarudishia watu wa Igunga nafasi ya kumchagua Mbunge wao ni kwa yeye kuamua kujiunga na chama kingine cha siasa - anaweza akaamua kujiunga na ADC au CCK!

Veri Simpo!!
Mzee Mwanakijiji CCM wanajuana mpaka wanakoingiziwa pesa za madili yao........huyu wanafahamu anahazina ya kutosha hawawezi kumwachie na akijiondoa wanaye kwa kutumia vyombo vyao
 
Last edited by a moderator:
Hii ni ajabu! Hivi kuna mwana CCM anayekataa ubunge siku hizi? Hii habari ya Bw Vuta nikuvute source yake mbona sioni? Hapa kweli inabidi Nape aje atoe majibu!
 
Aliyekuwa Mbunge wa Igunga,Dr.Dalaly Peter Kafumu, amedai kuwa kwasasa yeye hataki Ubunge lakini CCM inamlazimisha kukata na kuishughulikia rufaa yake dhidi ya kuvuliwa Ubunge huo na Mahakama Kuu. Nikizungumza naye hivi punde, Dr.Kafumu ameilalamikia CCM kwa kuwakosesha Mbunge wana-Igunga kwa kung'ang'ania rufaa ya Ubunge isiyo na tija.

'Sikia Ndugu yangu,mimi kwasasa nimejielekeza kwenye 'profession' yangu.Sitaki hata kusikia Ubunge wala nini sijui. Washauri Viongozi wetu wakubali Jimbo litangazwe wazi na uchaguzi ufanyike upya ili wana-Igunga wawe na Mbunge. Nilishakubali matokeo ya Mahakama.' alisema Dr.Kafumu

'Niliandika kuwafahamisha viongozi wangu. Sasa kwanini hawataki kunielewa? Kwanini wananilazimisha? Kwanini wanang'ang'ania jambo hili? Hawa watu sijui wakoje?!' alisikika Dr.Kafumu kwa sauti ya kukwazika.

Jambo gani liko nyuma ya Jimbo hili la Igunga?

na yeye alitokana wapi na hao freemasons? hataweza kuwatoka kiurahisi hao watu, wanaweza wakammalizia mbali. mnajiingiza ili mpate favour kwenye kazi na biashara zenu, angalia sasa yanamshinda anahangaika, songa mbele fanya maamuzi magumu kafumu, zaidi hapo huna jinsi, watakutoa kafara.
 
This is too much now jamani! Hata ningekuwa mimi mwenye Kashahada kangu kamoja ningeamua jambo jema kwangu
 
Kama ni kweli anaamini hivyo mbona ni kazi rahisi sana. Hawawezi kumlazimisha kama hataki. Na njia rahisi ya kukataa kulazimishwa na kuwarudishia watu wa Igunga nafasi ya kumchagua Mbunge wao ni kwa yeye kuamua kujiunga na chama kingine cha siasa - anaweza akaamua kujiunga na ADC au CCK!

Veri Simpo!!
Mkuu Dk Kafumu amenukuliwa kutaka kurudi kwenye kazi yake ya zamani serikalini, sasa akienda ADC au CCK sio ndio itakuwa mwisho wa kuwa Mtumishi wa Umma? Kumbuka kujitangaza kuwa mwanachama wa Upinzani Tanzania maana yake wewe sio mtumishi tena.
 
Alipokufa Chacha Wangwe, Profesa Samwel Wangwe aliamua kuuweka U-profesa wake pembeni na kuzungumza habari za kijiweni ili aifurahishe Mi-CCM, leo hii yuko hoi kitandani kapigwa na Kiharusi, sintoshangaa akikurupuka na kudai kwamba ni "kazi" ya CDM! Hao ndio aina ya Wasomi tulionao.

Prof wangwe mzee wa kuarakisha umoja wa africa mashariki yupo hoi kwa ki-wedding?
 
cheki avatar yangu navomchekaaaaaaaaaaaaaaaa hahahahaha
 
Hii ni ajabu! Hivi kuna mwana CCM anayekataa ubunge siku hizi? Hii habari ya Bw Vuta nikuvute source yake mbona sioni? Hapa kweli inabidi Nape aje atoe majibu!
Hii ni ajabu pia kwamba hata aliposema yeye @Vutanikuvute ameongea na Dk Kafumu bado haiwezi kuwa source? Ulitaka aseme source ni ITV au gazeti la Mwananchi au @ Nnauye Jr
 
Gharama ya kufanya uchaguzi ni kubwa kuliko kukata rufaa.
 
Dr. Kafumu umeshameza ndoano yenye chambo, huna jinsi tena. Jiandae kulipa gharama za kesi kama wale jamaa wa Arusha, maana CCM watakukana soon utakaposhindwa mahakama kuu ya rufani.
 
Sauti ya wengi ni sauti ya MUNGU ... wasijali, kama kawaida yetu; Tunaanza na MUNGU na tutamaliza na MUNGU vile vile ...
 
Back
Top Bottom