CCM wakata rufaa Igunga kupinga Kafumu kuvuliwa ubunge

CCM wakata rufaa Igunga kupinga Kafumu kuvuliwa ubunge

kazi ipo kwa ccm maana kila kona wanabanwa unajua kwa mtu makini na unapenda haki na kama pia umepata mafundisho ya dini hii ndio tamati ya ccm au mwisho umefika wa utawala zalimu wa ccm mungu mkubwa na anaweza kuifanya 1 ikawa 2 tusubiri na tumuombe mungu atupe maisha marefu tuikombe tanzania kabla ss vijana hatujatangulia mbele ya haki tuwe tumeiacha uhuru tanzania
 
Aliyekuwa Mbunge wa Igunga,Dr.Dalaly Peter Kafumu, amedai kuwa kwasasa yeye hataki Ubunge lakini CCM inamlazimisha kukata na kuishughulikia rufaa yake dhidi ya kuvuliwa Ubunge huo na Mahakama Kuu. Nikizungumza naye hivi punde, Dr.Kafumu ameilalamikia CCM kwa kuwakosesha Mbunge wana-Igunga kwa kung'ang'ania rufaa ya Ubunge isiyo na tija.

'Sikia Ndugu yangu,mimi kwasasa nimejielekeza kwenye 'profession' yangu.Sitaki hata kusikia Ubunge wala nini sijui. Washauri Viongozi wetu wakubali Jimbo litangazwe wazi na uchaguzi ufanyike upya ili wana-Igunga wawe na Mbunge. Nilishakubali matokeo ya Mahakama.' alisema Dr.Kafumu

'Niliandika kuwafahamisha viongozi wangu. Sasa kwanini hawataki kunielewa? Kwanini wananilazimisha? Kwanini wanang'ang'ania jambo hili? Hawa watu sijui wakoje?!' alisikika Dr.Kafumu kwa sauti ya kukwazika.

Jambo gani liko nyuma ya Jimbo hili la Igunga?
 
Chama cha magamba kwa sasa kinaogopa sana kuingia katika uchaguzi mdogo baada ya kipigo cha Arumeru mashariki. Hivyo kinachofanyika ni kujifanya kukata rufaa ili kuchelewesha uchaguzi mdogo.
 
Mwambieni Kafumu kuwa tatizo la CCM ni akili ndogo kutawala akili kubwa. Atajuliza sana na hataelewa,
 
Rufaa ikikatwa Dr Kafumu atarudishiwa ubunge.

wasahau rufaa rage alitoa bastola na kuifyetua hadharani igunga badala ya msimbazi, mwigulu alitoa rushwa kwa walimu, mahindi waligaiwa igunga wakati baa la njaa likiwa halipo
 
@vuta nkuvute aka Mzee tupatupa tunashukuru kwa taarifa.
 
Last edited by a moderator:
@vuta nkuvute aka Mzee tupatupa tunashukuru kwa taarifa.
Pamoja Mkuu.Vile vikao vya kutafuta adhabu kwa wana-MTWARA vimeahirishwa kwa muda usiojulikana.Tunasubiri maelekezo mengine.Tupo humo kwa ajili yenu nyinyi mliopo nje mjue mnavyoongozwa. Hadi kieleweke.Sijui kwa nini wamsakame Dr.Slaa wakati hata sisi makada maarufu wa CCM tumekichoka chama....chama ni kibovu,viongozi wabovu
 
Maccm saiz yapo bize kupambana na dk slaa hayataki kuskia uchaguzi tena
 
Mwenyekiti wao si amesema anaishangaa hukumu ya kumuondolea Ubunge!!!!! Kwa maana nyingine ni kwamba, Mkulu anajuwa sheria kuliko Jaji aliyetoa hukumu ya kumuondokea Ubunge. Ukuzingatia kila taarifa mpaka asomewe na kina Silva. Maana hana hata muda wa kujisomea. Anawaza safari tu.
 
Kama ni kweli anaamini hivyo mbona ni kazi rahisi sana. Hawawezi kumlazimisha kama hataki. Na njia rahisi ya kukataa kulazimishwa na kuwarudishia watu wa Igunga nafasi ya kumchagua Mbunge wao ni kwa yeye kuamua kujiunga na chama kingine cha siasa - anaweza akaamua kujiunga na ADC au CCK!

Veri Simpo!!
 
watakuwa na macho il hawataona,watahitaji kufa ila hawatakufa.
 
Back
Top Bottom