CCM wakata rufaa Igunga kupinga Kafumu kuvuliwa ubunge

CCM wakata rufaa Igunga kupinga Kafumu kuvuliwa ubunge

Nilipata kuzungumza hapa jamvini kwamba maamuzi ya kesi ya lema ktk mahakama kuu hayakuwa haki,hivyo kuna namna ya kujaribu kuweka ulinganifu wa hukumu kwani wenye maamuzi ndio wenye hatamu!siyo mbaya tusubiri hoja za kitaalam kadri ya muda.
 
Naona kuna dalili ya kutaka kusawazisha bao la Lema, yetu macho.

Majaji kwa sasa wanasimamia taaluma maana wanamuogopa sana Lissu. Kuitwa vilaza (wasio na sifa) sio jambo dogo! Jiulize kwa nini serikali imeshindwa kujibu tuhuma za TL?! Udhani majaji wengine watataka kuaibishwa.
 
Sina hakika kama Dr. Kafumu ametafakari kwa makini! Vielelezo vilivyoko mahakama kuu kuvipangua ni sawa na ngamia kupenya tundu la sindano!

Hiki kilichofanyika ni kumlazimisha Kafumu kukata hii Rufaa haikufanyika kwa matakwa yake na jinsi hali ilivyo sidhani kama anahitaji tena Ubunge kwani ni fedheha mtu na elimu yako unazomewa mbele za umati wa watu kisa siasa.
 
Naona kuna dalili ya kutaka kusawazisha bao la Lema, yetu macho.

Hawawezi kusawazisha kwani Lema kuingia Bungeni CDM imeongeza vichwa kama 20 vya wabunge wa CCM na Kafumu akirudi CCM watakuwa wameongeza kichwa 1
 
yeaah! jamaa ni mtaalamu wa madini, atakuwa anafundisha jinsi ya kuiba au kusaini mikataba feki ya madini kwenye shule za kata........... and he is not defending the public welfare at all, ila nadhani atakuw anafundisha kwa remote manake he is residing in singida


Mkuu Mungi, wakati mwingine zionee huruma mbavu zangu. We mama mbavu zangu! We mama mbavu zangu, he, hee, heee, heeee! Ah!
Hiyo remote ya kufundishia ki-tekelinalotujia wanaita eti video conferencing. UDOM kumbe ni shule ya Kata, sikujua.
 
Mkuu Mungi, wakati mwingine zionee huruma mbavu zangu. We mama mbavu zangu! We mama mbavu zangu, he, hee, heee, heeee! Ah!
Hiyo remote ya kufundishia ki-tekelinalotujia wanaita eti video conferencing. UDOM kumbe ni shule ya Kata, sikujua.

hahaaaaaa sasa nawe ndo ushaanza kuniumiza mbavu zangu................ mkuu hata dogo langu limepangiwa udom, nimemtahadharisha kuwa ni chuo cha kata so lazima awe makini!
 
Mbona ushindi uko wazi kisheria, kwa kuwa mwigulu nchemba alitoa rushwa kwa walimu hadhari, ccm igunga walisambaza mahindi ya bure kwenye vijiji kama ibologelo, choma, ziba, bado msomali waccm ilitoa bastola hadharani
 
Naona kuna dalili ya kutaka kusawazisha bao la Lema, yetu macho.


Watasubiri sana huyu jaji hana longo longo anafuata sheria kuna mtu alikata rufaa Dodoma kupinga hukumu na huyu mama ndo akatoa hukumu ya hiyo rufaa yani jamaa alizimia masaa matatu so let's wait and see
 
Wakuu. Ccm wamekata rufaa kupinga kuvuliwa ubunge kwa Dr Peter Kafumu, habari ni kama inavyosomeka hapa chini. Simba aliliambia NIPASHE kuwa rufaa ya Dk. Kafumu ilikatwa kupitia Wakili wake, Kamaliza Kayaga, takriban wiki tatu zilizopita, na tayari taarifa kuhusu rufaa hiyo zimekwisha andaliwa kwa ajili ya kupelekwa Mahakama ya Rufani ili kupangiwa tarehe ya kusikilizwa.“Wameshafaili na kulipia kila kitu. Notisi (taarifa) zao zimekwisha andaliwa. Tunasubiri kupeleka Mahakama ya Rufaa, ambayo ndiyo itapanga taratibu lini vikao vitafanyika,” alisema Simba.*Uamuzi uliotengua ubunge wa Dk. Kafumu ulitolewa na Jaji wa mahakama hiyo, Mary Shangali, Agosti, mwaka huu, baada ya kuridhika na pingamizi la mlalamikaji katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, uliofanyika Oktoba 2, mwaka jana. Akisoma hukumu hiyo, Jaji Shangali alisema kuwa Mahakama imeridhika na hoja saba za upande wa mlalamikaji, ambazo alisema zinathibitisha na kuonyesha kuwa uchaguzi huo mdogo wa Jimbo la Igunga haukuwa huru na haki.Alizitaja baadhi ya kasoro zilizosababisha kutenguliwa kwa matokeo ya uchaguzi huo ni pamoja na ahadi iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi,* Dk. John Magufuli, kuhusu ujenzi wa daraja la Mbutu ambalo wakati wa kampeni alidai kwamba kama wananchi hawataichagua CCM, daraja hilo halitajengwa. Waziri huyo alitoa ahadi hiyo katika kipindi hicho ambacho kulikuwa na shida kubwa ya usafiri katika eneo hilo.Jaji Shangali alisema kuwa pia Waziri Magufuli alitumia nguvu* na kuwatisha wapiga kura kwamba kama hawatamchagua mgombea wa CCM, watawekwa ndani, kitu ambacho alisema kilitishia uchaguzi huo kuwa huru na wa haki.Jaji Shangali alisema kitendo kilichofanywa na Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage (CCM), kwamba mgombea wa Chadema amejitoa katika uchaguzi huo, hakikuwa cha kiungwana kwani alitumia lugha ya uongo kwa lengo la kupotosha wapiga kura. Alisema pia Rage alihusika katika vitendo vya kujenga hofu kwa wapiga kura baada ya kupanda jukwaani na bastola, hali ambayo iliwafanya wapiga kura kuhofia na hivyo kuleta dosari katika uchaguzi huo. Jaji alisema kuwa hoja hiyo imezingatiwa na Mahakama.Jaji huyo alioonyesha kusikitishwa na kitendo kilichofanywa na Imamu wa Msikiti wa Ijumaa wa Igunga, Sheikh Swaleh Mohamed, kutangaza msikitini akiwataka waumini wa dini ya Kiislamu wasikichague Chadema kwa madai kuwa viongozi wake walihusika kumdhalilisha aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatma Kimario. Kadhalika, Jaji Shangali aliithibitisha kuwa kauli iliyotolewa na Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama, kuwa Chadema kimeingiza makomandoo katika wilaya ya Igunga kwa lengo la kuvuruga uchaguzi huo mdogo, ilikuwa na madhumuni ya kupeleka vitisho kwa wananchi. Kuhusu madai ya kugawa chakula wakati wa kampeni, Jaji Shangali alisema kitendo cha serikali kugawa mahindi ya msaada kwa wakazi wa Igunga katika kipindi cha kampeni kimeleta fedheha kubwa kwa wapiga kura. Alihoji, je; ni nani aliyekufa njaa katika kipindi hicho na kwamba kulikuwa na umuhimu gani kugawa mahindi katika kipindi cha kampeni?Kesi hiyo ilifunguliwa na Kashindye, ambaye aliwakilishwa na wakili maarufu nchini, Profesa Abdallah Safari, akipinga matokeo ya uchaguzi huo kwa kulalamikia ukiukaji wa sheria ya uchaguzi. CHANZO: NIPASHE
Mtoi hujacheka kwanza kabl ya kupost haya ?Hawa jamaa sijui wanafikiri watachezesha kwa simu ya ikulu na promo ya judge huku waki blackmail watanzania na CDM kwa kutaka linganisha na ushindi wa Lema. JK is second to non-kwa kublack mail watu wanaomzunguka, na mara kadhaa kafanya majaribio y akublack mail wapiga kura anaposhindw akabisa ku deliver.Kwa karibu anafuatiw ana Zitto.wao huwa wanachukiwa tuu, wao huwa wanhujumiwa tuu, wao ni wajuaji tuu, wao ndio wapo sahihi tuu,wao ndio wazalendo tuu, wao ndio wanaon atime inakimbia sana kuliko wengine ila wao ndio wantenda mambo binafsi tuu. Moh Mtoi nakuhaikikishiwa CCM wanakwenda ibika tena kwa kulazimisha tena ushindi halafu wasingizie Kuwa mbona kwa Lema walishindwa na wakakubali.prof Safari atang`aa sana ktk hili.
 
Mkuu Mungi, wakati mwingine zionee huruma mbavu zangu. We mama mbavu zangu! We mama mbavu zangu, he, hee, heee, heeee! Ah! Hiyo remote ya kufundishia ki-tekelinalotujia wanaita eti video conferencing. UDOM kumbe ni shule ya Kata, sikujua.
Yaani wasomi wetu kwa kutaja termilogies halafuhawajui kategory za hayo mambo.HUwa napata kichefuchefu sana.hapo kun akina mulugo wengi sana.
 
Wakate tu! Lakini linapofika suala la gharama za kesi asiachiwe Dr Kafumu.
Teh teh teh! Umeona eeh? Kafumu mwenyewe kasema hataki kuendelea na siasa, sijui wanakata rufaa ili iweje
 
Hiki chama twawala kinapoteza rasilimali bure, hivi ile kesi ya Mahalu mmeshakata rufaa pia? Na ile ya Dowans kuamuliwa ilipwe na TANESCO imefikia wapi? Serikali ya ccm na ccm ni kama kikopo na kifuniko vile wanashindwa kutabiri mbio za panya huku wanaona sakafu.Mwacheni Dr.Kafumu akafaidi madini kabla ya kurudishwa kwa wanyonge 2015.
 
hayo ni natumizi mabovu ya fedha za walipa kodi kwa kesi ya wazi kiasi hicho.
hizo pesa kama zinawawasha wapeleke kuendeleza visima vya maji kwenye baadhi ya vijiji humo jimboni igunga!!!! waache kutapatapa !!!!
 
Mbona hili zuri tu? Tusubiri hiyo orodha ya mashahidi patakuwa patamu!
katika hatua ya rufani huwa hakuna kuita mashaidi bali mawakili hujadili makosa ya hukumu kulingana na ushahidi uliotolewa mahakama kuu period na majaji huamua kwa kutumia mabishano hayo a kiasheria
 
Kwa kweli kwa kesi hii ccm nimeamini ni mafisadi wa wazi kabisa. Hahitajiki mtaalamu wa sheria kujua kuwa igunga ccm na serikali walicheza rafu mbaya wakati wa uchaguzi mdogo. Tatizo la ccm ni kupuuza ushauri wa wataalamu wake,huo ni ulevi wa madaraka. Ccm ni zaidi ya uijuavyo!
 
Huku ni kupoteza muda na pesa, hukumu iko wazi kabisa.
CCM tulicheza rafu za wazi kabisa kwenye uchaguzi ule.

Sioni namna ambavyo CCM tunaweza kushinda kwenye rufaa hii tena kwenye jopo la majaji watatu.
 
Back
Top Bottom