CCM wafanya mkutano kanisani, wampiga kiongozi wa kigango

Ni kwaida ya CCM kufanya vurugu hata kwenye nyumba za ibada. Kumbukeni kikundi cha NCHIMBI kilivyovamia kanisani wakati wa uchaguzi mkuu wa 2005, na huyo Nchimbi alivyodiriki kugombana na Askofu Mkuu wake.

CCM ina polisi wake. Ikibidi wanapiga watu risasi kama walivyofanya Pemba na Mwembe Chai. Na polisi wamekuzwa wakielewa kama kuna kutoelewana kati ya CCM na watu wengine, basi hao wengine wamevunja sheria.

CCM imelewa madaraka. Itahodhi madaraka, hata kwa nguvu. Wananchi tufanyeje?
 
Last edited:
Wapumbavu, ndo siasa gani hizo hadi kwenye nyumba za ibada!
Fikiria kabla ya kuandika,kwani waliosema mwenyekiti wa sisieeemu ambaye ndie mkuu wa Tanzania kwamba ni chaguo la Yehova walikuwa wanatoka msikitini au kanisani?Hivyo ujue kuwa Kanisa na sisieeemu ni baba moja mama moja ila tumbo mbalimbali,wana haki ya kufanyia mikutano hapo kanisani mbona mara nyingi tuu mikutano yao ya kampeni inaratibiwa kanisani!.
 
Nyie viongozi wa kanisa si hiki ni chama kilichochaguliwa na Mungu? sasa kwa nini wasifanyie mikutano yao huko kwenye nyumba zenu?
 
Nchi inaelekea kubaya. Ilianza Zanzibar sasa nchi nzima.

Mola ibariki Tanzania
 
Hii ni habari ya kusikitisha sana na kipigo juu?,nashauri kanisa lifungue kesi mahakamani, na wakazi wa Biharamulo fungueni macho na muoneshe kuchukizwa kwenu siku ya kupiga kura.Leo fujo kanisani kesho nyumbani kwetu.
 
Hapo umenena.
 
Kuna mbunge mmoja juzi bungeni alisema kuna chama cha upinzani chenye kufanya fujo. Hakukitaja, lakini alitaka kifutwe kwani sheria za vyama ziko wazi juu ya hilo. Alikuwa mkali kwelikweli kwa msajili wa vyama kuwa hajui kazi yake au anashindwa kutumia madaraka yake vizuri.
Naomba wanaomkumbuka na kuwa na mawasiliano nae, wampe habari hii na tumtake abaki na msimamo wake ili chama chake kinachofanya vurugu hadi kanisani kifutwe.
Kama kuna anayekumbumka jina lake aliweke hapa ili tutafute mawasiliano naye kupitia tovuti ya bunge (wakati huo alikuwa akichangia bajeti ya ofisi ya waziri mkuu)
 
Naomba nijulishwe kwani pamefikia CCM wananyimwa maeneo ya kufanyia mikutano mpaka wakafanye fujo kanisani kweli KIAMA CHA CCM kimeshafikia wameanza kuyaona kwa macho yao mambo yanayotokea wananchi kuwakataa mchana peupeeeeee
 
Kuna mbunge mmoja juzi bungeni alisema kuna chama cha upinzani chenye kufanya fujo. Hakukitaja, lakini alitaka kifutwe kwani sheria za vyama ziko wazi juu ya hilo. Alikuwa mkali kwelikweli kwa msajili wa vyama kuwa hajui kazi yake au anashindwa kutumia madaraka yake vizuri.
Naomba wanaomkumbuka na kuwa na mawasiliano nae, wampe habari hii na tumtake abaki na msimamo wake ili chama chake kinachofanya vurugu hadi kanisani kifutwe.
Kama kuna anayekumbumka jina lake aliweke hapa ili tutafute mawasiliano naye kupitia tovuti ya bunge (wakati huo alikuwa akichangia bajeti ya ofisi ya waziri mkuu)

Ni mbunge wa viti maalum wa nadhani shinyanga, Ester Nyawaza
 
kwani msikitini kuna meza na mabenchi, labda kama wangalikuwa na shida ya mikeka wangeweza kwenda msikitini
Unadhihirisha upeo wa kichwa chako, kumbe chochote chaweza kufanywa kanisani "hata mambo ya aibu kama vikao vya mafisadi" ndio maan wanataka mshiko wa misamaha ya kodi baada ya miaka kumi tutajua mengi kuhusu kanisa!
 
Hivi hadi uwe unarusha matusi ya reja reja hivyo ndio hoja zako zitakuwa na nguvu?
 
-Wanapomuona naibu-katibu taifa wa chama anavishambulia VYOMBO VYA HABARI HADHARANI(kwenye kampeni za busanda)

-Wanapoona katibu wa chama anatamka kauli bila kuzitafakari '........AMEFUNGIWA DUNIANI,NA MBINGUNI AMEFUNGIWA..'-kwenye sakata la Nape

-Wanapoona SPIKA-WA BUNGE(wa chama chao) anamshambulia m'bunge na kumtoa nje kwa staili ya ubabe-ubabe;mh cheyo

WANA CCM WANAAMINI WAO NDIO WANA HAKI YA KUVUNJA UTARATIBU NA SHERIA YOYOTE NCHINI
 
Fikiria wananchi walivyojisikia vibaya kusikia akina mama wa CCM wanaimba mapambio ya chama kanisani.

Walisikika wakiimba:

CCM tieni
Makamba tieni
Malecela tieni
Tieni tieni kwa moyo mmoja
Nambari One eeeh
Nambari ONe ni CCM

Huu winbo uliongeza sana hasira kwa waumini wa RC wa eneo la Nyantakala. Waliona kuwa kama ni najisi hii imevuka mpaka,
 
Kaka acha kupotosha watu,hiki chama sisieeeeem ni chaguo lao hawawezi kupata hasira kwa kusikia eti t n t n!
 
Tunakoelekea si kuzuri. Nadhani ufahamu wa baadhi ya wafuasi wa vyama vya siasa ni mdogo sana
 
duh ......ccm mwisho!
hata kama kanisa lilisema kikwete chaguo la mungu, lilifanya kwa ridhaa yake,haimaanishi kuwa ccm sasa ina nguvu za kuvamia kanisa!
 
Msikitini ? thubutu !!
siyo Biharamulo tu bali nchi nzima ya Tz
hakungekalika Dodoma hadi Dar-es-Salaam
na risasi zingerindima.​

Msikitini ? thubutu !!
hao makafri wangeonja joto la jiwe
hayo yaliyotokea Tunduma yangeonekana
kama mchezo wa kuigiza !​

Kanisani ? rukhsa !!
wanawajua kondoo wao na wanyonge wao
wale ambao wakipigwa shavu la kushoto
hugeuza shavu la kulia.​

Kanisani ? Rukhsa !!
wanawajua kondoo na wanyonge wao
Masikini katibu hakujua nguvu waliyo nayo
wafuasi wa chaguo la Mungu.​

Watanzania ni watu wa ajabu sana! Na kwa kiasi kikubwa sikutegemea (ila sishangai) kuwa udini utaanza kuingizwa kwenye hii topiki. Nadhani ndo maana CCM wanatesa na wataendelea kutesa waTZ hadi kiama!

Yaliyotokea kanisani na kupigwa watu yamekuwa yakiendelea Zenji (hususan Pemba) miaka nenda rudi, hata pale Mwembechai (Dar) miaka ilee, sasa leo nashangaa watu wanaongea kuwa ati hilo haliwezekani misikitini, au kwa waislamu! Watanzania amkeni jama!

Wenye CCM na hao mafisadi wana dini yao ambayo ni tofauti na hizo dini zinazowagawanya ili mtengani humu ndani na hicho ndicho wanachokitaka. Dini na kabila lao ni PESA, bila kujali kama hao mafisadi wanaitwa John, Salum, Nyambisa, Atupele au Katembo! na kanuni yao waitumiayo ni UBINAFSI, na itikadi yao ni DHULUMA, na katiba yao ni KULINDANA!- Yaani kwa sasa Tz kuna Makabila na dini mbili tu Wenye pesa (MAFISADI) na sisi (MASIKINI-Makabwela), ambao watoto wetu wanakaa na kuandikia ardhini mashuleni.

Na mnapoingiza udini kila mahala wao ndo wanashangilia kwani mnajigawanya wanyewe na wao watatia chumvi tu, ili muendelee na huo ujinga!
 
Msikitini ? thubutu !!
siyo Biharamulo tu bali nchi nzima ya Tz
hakungekalika Dodoma hadi Dar-es-Salaam
na risasi zingerindima.

Msikitini ? thubutu !!
hao makafri wangeonja joto la jiwe
hayo yaliyotokea Tunduma yangeonekana
kama mchezo wa kuigiza !

Kanisani ? rukhsa !!
wanawajua kondoo wao na wanyonge wao
wale ambao wakipigwa shavu la kushoto
hugeuza shavu la kulia.

Kanisani ? Rukhsa !!
wanawajua kondoo na wanyonge wao
Masikini katibu hakujua nguvu waliyo nayo
wafuasi wa chaguo la Mungu.

Hivi Mwembechai ilikuwa ni Kanisani?

Pemba huko je wengi ni wakristo?

Ni kauli za viongozi wa CCM na Serikali ambazo zinawafanya wafuasi wao wafikiri kuwa wapo juu ya sheria na kuwa hata wakifanya kosa ili mradi ni kwa niaba ya CCM hawatashtakiwa. Response ya Polisi (kutowakamata wafanyafujo wana-CCM na kuwakamata waliopinga mkutano wa CCM ndani ya kanisa) baada ya uhalifu wa wana-CCM pia inazidi kuwapa imani hiyo.

Hapa kinachotakiwa ni waathirika wa kipigo hicho, mmoja mmoja waende kuandikisha maelezo Polisi (yes! Polisi hukohuko) kisha ifunguliwe kesi Mahakamani ya mashambulizi ya kudhuru mwili yaliyosababisha maumivu makali ya mwili.

Kesi ya namna hii ikinguruma, na watu wakipatikana na hatia kufungwa, watu wataanza kujifunza walau kuheshimu sheria.

Wengi wa washambuliaji hao ni ignorant, wanatakiwa kufundishwa na sheria tu.
 
What a SHAME!!!! Wananchi, Beware the kicks of a dying horse
 
Last edited:
Back
Top Bottom