CCM wafanya mkutano kanisani, wampiga kiongozi wa kigango | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM wafanya mkutano kanisani, wampiga kiongozi wa kigango

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng'wanza Madaso, Jun 30, 2009.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  CCM wafanya mkutano kanisani, wampiga kiongozi wa kigango

  Na Frederick Katulanda, Biharamulo

  WAFUASI wa CCM juzi walivamia Kanisa Katoliki, Kigango cha Nyantakara kilicho Kata ya Lusahunga na kufanya mkutano wao, huku wakimshambulia na kumjeruhi katibu wa kanisa hilo baada ya kuwaamuru watoke.

  Tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 3:00 asubuhi wakati wafuasi hao wa wanawake wa CCM, wakiongozwa na mtu mmoja aliyejulikana kwa jina moja la John, walipoingia kanisani humo kwa madhumuni ya kuchukua viti kwa ajili ya mkutano wao. Badala ya kuchukua viti, waliamua kutotoka na kufanyia mkutano huo kanisani.

  Akizungunza na Mwananchi katekista wa kigango hicho ambacho kipo katika parokia ya Kaniha, jimbo la Kahama, Faustine Damas alisema wafuasi hao wa CCM waliingia kanisani na kuchukua meza ya kuendeshea ibada na kuigeuza kuwa meza ya wageni wao na baadaye kuendesha mkutano wao.

  Alieleza kuwa alipofika kanisani alistaajabu kusikia nyimbo wa 'Tieni, tieni' ukiimbwa na baada ya kuingia ndani alikuta wakiwa wanaendelea na mkutano wao huku wakitumia meza kuu ya ibada, jambo ambalo lilimfanya ampigie simu katibu wa kigango hicho, Festus Masumbuko ambaye baada ya kuwaomba waondoke na kuwanyang'anya meza hiyo ya ibada, wafuasi hao wa CCM walianza kumpiga.

  "Waliamua kugoma kuondoka na ndipo alipowanyang'anya meza ya ibada, lakini wakamvamia na kumpiga mateke na ngumi. Wamemjeruhi vibaya na pia wamemchania shati," alieleza katekista huyo.

  Alisema kutokana na hali hiyo alilazimika kupiga kelele na ndipo wananchi walipofika na kumwokoa. Lakini wakati hali hiyo ikiendelea, mfuasi mmoja wa CCM alipiga simu polisi na kuwaeleza kuwa walikuwa wakifanyiwa vurugu na ndipo polisi walipoenda eneo hilo na kuwakamata wananchi waliokuwa wanataka kumuokoa katibu.

  Wananchi hao wanashikiliwa na polisi kwa kufanya vurugu katika mkutano huku wana CCM wakiachiwa huru na kuondoka zao.

  Kutokana na hali hiyo paroko wa parokia ya Kaniha, Padri Isaya Bahati ambaye pia ni msaidizi wa askofu wa jimbo la Kahama, alisema muda mfupi baadaye akiwa polisi kuwa amesikitishwa na vurugu hizo na kusisitiza kuwa kanisa kama nyumba ya ibada inapaswa kuheshimika kwa vile si uwanja wala ukumbi wa mikutano.

  Alipoulizwa kuhusu suala hilo, naibu katibu mkuu wa CCM, George Mkuchika alisema hana taarifa ya vurugu za wafuasi wake kanisani na kwamba kwa kuwa amepokea taarifa hizo, atazifuatilia kwa kina.

  “Ngoja nifuatilie kwa kina kujua ni nini kimetokea,” alieleza Mkuchika.

  Kamanda wa polisi mkoa wa Kagera Henry Salewi alisema kuwa hakuwa kwenye eneo la uchaguzi na kumtaka mwandishi awasiliane na kamishina Telesphol Anaclet ambaye ndiye amekuwa akishughulikia masuala hayo. Hata hivyo, kamishna huyo alisema jeshi la polisi linaendelea na masuala yake hivyo lipewe nafasi ya kufanya kazi.

  “Naomba mtuache tufanye kazi yetu sina cha kukueleza kwa sasa,” alisema kamishina huyo wa oparesheni maalumu ya uchaguzi na akakata simu.

  Waliokamatwa na jeshi hilo la polisi wametajwa kuwa ni Evarist Dotto, Semen Elias, Mosha Makoye, Batista na Timetheo ambao walitambulika kwa jina moja.


  SOURCE: Mwananchi
   
 2. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Sasa Wamefika mpaka Makanisani, Duh ni Hatari sana, Je wangekuwa kwenye msikitini wangeambiwa nini?? Hivyo hizi operation ambazo kila wakati wa uchaguzi ndio zinaendeshwa ni za nani?? Naombeni Jibu jamani??Mara zote CCM ndio huwa wanaanzisha Vurugu katika Chaguzi zote
   
 3. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Duh tumeshafika huko aisee?
   
 4. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Ni bora waliingia kanisani nafikiri ingekuwa msikitini wangesomewa albadiri.
   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Nilishawahi kusema kwamba siku CCM wakishindwa bara watafanya kama Zanzibar ama watapindua Nchi. Kuna kila dalili kwamba CCM na polisi wana kazi moja tu na si demokrasia kufanya kazi. Hii ni hatari wacha tusikie wakubwa wa CCM na Serikalini watasema nini .
   
 6. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  huo ndio mwanzo wa mwisho wa CCM mikoani na vijijini, haya mambo ni watu wa mjini tu ndio walikuwa wanayaona na kwa mtaji huu CCM inajiangusha yenyewe taratibu, kwa kweli mpinzani wa kweli wa CCm yupo ndani ya chama chenyewe
   
 7. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280

  Msikitini ? thubutu !!
  siyo Biharamulo tu bali nchi nzima ya Tz
  hakungekalika Dodoma hadi Dar-es-Salaam
  na risasi zingerindima.

  Msikitini ? thubutu !!
  hao makafri wangeonja joto la jiwe
  hayo yaliyotokea Tunduma yangeonekana
  kama mchezo wa kuigiza !

  Kanisani ? rukhsa !!
  wanawajua kondoo wao na wanyonge wao
  wale ambao wakipigwa shavu la kushoto
  hugeuza shavu la kulia.

  Kanisani ? Rukhsa !!
  wanawajua kondoo na wanyonge wao
  Masikini katibu hakujua nguvu waliyo nayo
  wafuasi wa chaguo la Mungu.

   
 8. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  kwani msikitini kuna meza na mabenchi, labda kama wangalikuwa na shida ya mikeka wangeweza kwenda msikitini
   
 9. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #9
  Jun 30, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Wapumbavu, ndo siasa gani hizo hadi kwenye nyumba za ibada!
   
 10. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Rhodesia (Zimbabwe) walianza kama hivyo matokeo yake ulimwengu umeshuhudia
   
 11. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  e bwana wee hilo neno wapumbavu ni matusi kwa upande wapili huwezi kulitumia baada ya kwisha pita chumbe kutojea unguja
   
 12. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hivi ndo viroja vyenyewe, walio pigwa wanashitakiwa, wapigaji wanapeta mtaani, nyumba ya ibada inageuzwa ukumbi wa mikutano, dola kigugumizi!

  Hivi kitu ambacho huwa sielewi, askari akiambiwa tatizo yeye huwa ahoji na kuuliza ama walau kutumia ubongo wake kidogo akafikiri anafika na kubeba hata asiye husika? mpaka lini jamani watanzania tutaheshimika na kuishi kwa misingi ya haki?
   
 13. GM7

  GM7 JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 492
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Jamani! jamani! jamani! mambo gani tena hayo? Hivi hao waliovamia hilo kanisa, je baadhi yao si wakatoliki? Kwa kweli cha hiki, ngoja niishie hapo.
   
 14. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Naona kuwa CCM wanatafuta visingizio kibao na kutaka kujua itakuaje, Maana CCM ndio zao, Huko wamekabwa Koo
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  tetetetetetetetehhhhhhhhhh
   
 16. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #16
  Jun 30, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Msikitini wangekiona cha moto ,naamini waumini wangetangaza jihadi tu,na kuwatoa baru na magwanda yao ya kijani.si mliona yule aliezabuliwa kibao kwa kuchanganya ugali na bamia wakati hakutakiwa kuchanganya bali kutowea.
   
 17. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #17
  Jul 1, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,844
  Likes Received: 1,110
  Trophy Points: 280
  CCM wanatafuta laana sasa
   
 18. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #18
  Jul 1, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Unajua kuna msemo mmoja kuwa "mtoto ukimdekeza sana atakutia aibu mbele ya wageni" Siku atakapokutuma ukamletee maji ya kunywa haraka huku umekaa na wageni waheshimiwa kwenye kochi utabakia kucheka na kusema huku umeinamisha kichwa cini, enhe wewe bwana enhe acha utani bwana, na yeye anakuja na tusi la f...n si nimekutuma unacheka cheka nini? pu..b..v.u. Ndiyo haya ya CCM na wanachama wao ilitarates na bado wanazidi kuwajaza ujinga ili wapate kura.

  Vingozi wakuu wa CCM wanapopita na kusema kuwa serikali ni yao na dola ni yao watafanya lolote watakalo, ni signal mbaya waliopo chini wengine hata uwezo wa kufanya analysis hawana, hawa ndiyo wanavunja sheria makusudi kwa kisingizio kuwa polisi wapo upande wao. Na kwa wakubwa wa polisi wao ukubwa huo wanaona ni kama favour waliyopewa na watawala badala ya kuona kama ni dhamana ya kuwatumikia wananchi pasi na unaguzi wa aina yoyote. Hii ni hatari kwa umoja wetu kwani tunajenga matabaka ambayo huko mbele itakuwa kazi kukabiliana na outcomes zake.
   
 19. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #19
  Jul 1, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wapate mara ngapi?
   
 20. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #20
  Jul 1, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani mbona kila mara wanazichapa ngumi misikitini wenyewe kwa wenyewe tena wakiwa wamevaa makanzu, niliwahi kushuhudia pale Msikiti mmoja Mabibo, na kwingine kule Morogoro wa Msikiti wa Mahita hapakutosha!!
   
Loading...